Je, kama heater inatumia umeme kuzalisha joto, ni kwanini freezer halizalishi umeme, na badala yake nalo linatumia umeme?

Hii imekaaje kaaje hii? Nakaribisha maoni
Hivi ni vitu viwili tofauti,heater ina coil ya waya wenye ukinzani mkubwa,ambapo ukipitisha mkondo wa umeme,unazalisha joto,kanuni inayotumika hapa ni,mkondoXmkondoXResistance=nguvu joto(WATTS).
Freezer inatengenezwa kwa kuunga vitu kadhaa,kuna evaporator(copper coil tube zinazonyonya joto ndani ya jokofu),condenser(copper pipe,zipo nje zinatupa joto nje).Compressor(hii ni pump inayosukuma gas ndani ya condenser na evaporator,hii gesi ndio inayotumika kuamisha joto kutoka ndani.
 
Unaamini sifahamu hivyo? Nauliza kwa general logic, ni kama ambavyo motor inatumia umeme kuzalisha mzunguko, na motor hiyo hiyo ikibadilishwa polarity inaweza kutumia mizunguko kuzalisha umeme (alternator)
 
hmmm inapatikana ila umeme mdogo mno

peltier effect zina apply hasa kwa thermocouple

inatoa umeme mdogo mno, kwa heating/cooling effect kubwa
 
Si wa la saba B tunabaki wasoma comments tu hapa, mara sijui condenser, mara compressor maro ooh sijui madude gani huko!! Sie tunajua kuna kinywaji baridii kinasubiri mtu akikunywe basi! Haya ya kuanza kuchunguza sijui hii inafanyaje kazi hayo hayatuhusu.
 
Terminology ngeni, fafanua
unawezapata umeme kwa sumaku, kemikali, joto au mwanga

kwenye joto unapata umeme japo ni mdogo
hata kwenye friji/friza upo ila huweziendeshea mota/kompresa

badala yake effect iyo (peltier effect=current effect of heating) inatumika kwenye vifaa vinaitwa thermocouple

vimejaa viwandani uko, wana apply joto kupata umeme (nakazia tena mdogo sio wa kuendesha kompresa ya friza)
 
Utafiti wa kina zaidi ufanyike kuongeza ufanisi wa ‘Thermoelectric generators’, umeme mwingi sana hupotea katika mfumo wa joto
 
Unaamini sifahamu hivyo? Nauliza kwa general logic, ni kama ambavyo motor inatumia umeme kuzalisha mzunguko, na motor hiyo hiyo ikibadilishwa polarity inaweza kutumia mizunguko kuzalisha umeme (alternator)
Hamna shida papaa,kama unataka kubadirisha nishati ya umeme iwe nishati ya mwendo/mechanical utaipa motor(DC motor)umeme,na yenyewe itakupa mzunguko.
Au ukitaka umeme kutoka kwenye motor unaizungusha na yenyewe inakupa umeme.
Sasa wewe ulikuwa unataka kujua freezer itazalisha vipi umeme?Ili upate nishati fulani,inabidi ubadilishe nishati nyingine,sasa hapa kwenye freezer,nishati gani unayobadilisha?
 
Si joto au?
 
Si joto au?
Dah....usiwaze sana...umeambiwa tayari...heater na freezer Ni vitu tofauti...vinavyofanya kazi misingi tofauti... Heater inatoa joto kutokana na athari ya mkondo wa umeme kupita kwenye kikinzani.....na freezer linanyonya joto ndani yake na kulitoa nje kwa athari ya migandamizo ya vimimika au gesi inayozunguka full stop 🤭
 
Hii imekaaje kaaje hii? Nakaribisha maoni

Electrical energy is converted into Heat energy in a heater, the later acts as a medium in which the whole process of heat generation is undertaken, you can say that the conservative law of enegy takes place in the heater unlike a refrigerator in which Electrical energy is converted into Rotational Enegy of its motor/compressor which inturn circulates refrigerant/gas through a tube which passes via a built- in cold chamber in which heat exchange takes place, heat of stuffs stored in a refrigerator is exchanged with Coldness of the refrigerant, in other words you can say a fridge is a heat exchange unit.

For more detailed explanations you can read a book.
 
Unaamini sifahamu hivyo? Nauliza kwa general logic, ni kama ambavyo motor inatumia umeme kuzalisha mzunguko, na motor hiyo hiyo ikibadilishwa polarity inaweza kutumia mizunguko kuzalisha umeme (alternator)
Boss, ukibadili polarity ya power supply kwenye motor ya namna gani inaweza kuzalisha umeme?
 
Motor ya Ndalilo. Nilichomaanisha ni motor ni opposite ya alternator, motor inatumia umeme kuzalisha mizunguko, Alternator/ Dynamo / Generator inatumia mizunguko kuzalisha umeme. Details za how tafuta
 
Back
Top Bottom