Je, juhudi za kuondoa plastiki isiyooza zitafanikiwa na kusafisha kabisa taka za plastiki duniani?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111342983986.jpg


Pili Mwinyi

Mkutano wa tano wa Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira (UNEA-5), uliomalizika katika makao makuu ya UNEP jijini Nairobi, umeshuhudia kupitishwa kwa agizo la kihistoria linalotaka kuanzishwa kwa mkataba wa kimataifa wa plastiki.

Kwa mujibu wa agizo hilo, mkataba huo utajadiliwa ifikapo 2024, na timu itakayoshughulikia mkataba huo ambayo itaweka ajenda ya mazungumzo imepangwa kuanzishwa katikati ya mwaka 2022.

Matumizi ya plastiki isiyooza, limekuwa tatizo kubwa linalokabili mazingira duniani, kwani kuongezeka kwa kasi kwa uzalishaji wa bidhaa za plastiki, kumekuwa mzigo unaoendelea kuelemea ulimwengu katika kukabiliana nazo.

Shirika la UNEP linasema kuwa uchafuzi wa plastiki katika Afrika unaongezeka kutokana na ukusanyaji duni wa takataka na ukosefu wa vifaa vya kuchakata tena. Nini kifanyike ili kuzuia Afrika kuwa eneo kubwa zaidi la kutupa plastiki duniani?

Tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, mataifa mengi ya Afrika yaliyo kusini mwa Sahara yalianza taratibu kupitisha sheria inayokataza uzalishaji, uagizaji, uuzaji, matumizi na uhifadhi wa mifuko ya plastiki. Lakini sheria hii mara kwa mara imekuwa ikipuuzwa au hata kutumika vibaya.

Kenya, nchi ambayo iko mstari wa mbele kuhakikisha matumizi ya plastiki yanakwisha, ilipiga marufuku mifuko hiyo mnamo 2017 na kuorodheshwa miongoni mwa mataifa 50 yaliyochukuwa hatua hiyo katika ripoti ya Umoja wa mataifa, ambayo inapendekeza kuwa serikali duniani zinahitaji kufikiria kupiga marufuku au kuidhinisha kodi kubwa kwa watengenezaji mifuko hiyo ya plastiki.

Kufuatia mkutano huu wa UNEA-5 mwanamazingira wa Kenya Joseph Kiragu anasema kuwa ni vigumu kumaliza plastiki zote duniani. Lakini pia ameshauri mataifa kubuni plastiki ambazo zinaweza kutumika tena.

Nchini Tanzania ambako pia matumizi ya mifuko ya plastiki yamepigwa marufuku, kumekuwa na njia mbadala ya kutumia mifuko ya karatasi au wengine kutumia vikapu madukani na sokoni.

Sio mbaya kutumia mifuko ya karatasi kwani kama tunavyofahamu kuwa karatasi ni rahisi kuoza ikilinganishwa na mifuko ya plasitiki. Je hizi zinaweza kuwa ni hatua ndogo na za awali ambazo zitaliokoa bara la Afrika lisizame kwenye bahari ya plastiki isiyooza?

Takriban tani milioni 300 za taka za plastiki huzalishwa duniani kote kila mwaka, na karibu 80% hutupwa ardhini au moja kwa moja kwenye mazingira ya asili na kusababisha uharibifu mkubwa usioweza kurekebishwa kwenye udongo na mazingira ya baharini, huku chini ya 10% tu ya plastiki ndio huchakatwa na kutumiwa tena.

Ili kuondoa tatizo la madhara ya mifuko ya plastiki, viwanda vya uzalishaji mifuko ya plastiki vya China sasa vimekuja na teknolojia na mbinu mpya ya kutengeneza mifuko ya plastiki inayoozaa kwa urahisi na kutoleta madhara kwenye ardhi.

Zhang Haoqian, mwanzilishi mwenza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza mifuko ya plastiki inayooza kirahisi Azurite Microorganisms, anasema wateja wao wanategemea kutumia tani 1 ya plastiki inayoweza kuoza (PHA) ambayo wanatengeza kama mbadala wa plastiki ya zamani isiyooza kirahisi. Hivi sasa ukitembelea karibu supermaket zote za China utakuta mifuko hii ya plastiki inayooza kirahisi na ile ya zamani kwa sasa imekuwa adimu.

China pia haikuishia kwenye mifuko ya plastiki pekee bali imebadilisha hata vitu vingine vinavyotengezwa kwa plastiki, mathalan mirija ya kunyweya vinywaji, sasa inatengezwa kwa mianzi badala ya plastiki ile tuliyoizoea.

Julai 10 2020, idara 9 za China ikiwemo Tume ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi na Wizara ya Ikolojia na Mazingira kwa pamoja zilitoa "Angalizo la Kuimarisha Udhibiti wa Uchafuzi wa Plastiki", ambalo limeitaka miji iliyo katika ngazi ya mkoa au juu ya mkoa kuchukua hatua kali kwa maduka makubwa, Supermarket, maduka ya dawa na maeneo mengine, pamoja na shughuli mbalimbali kama huduma za upishi, kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki isiyooza kuanzia Januari 1, 2021.

Kutokana na kuanzishwa kwa katazo la matumizi ya plastiki kitaifa na sera za kupiga marufuku, maeneo yote ya nchi yaliitikia vizuri na kupiga marufuku kabisa mifuko isiyooza. Sasa hivi mifuko ya plastiki inayooza imezoelekea na kubadilisha maisha ya watu wa China, lakini pia imesaidia kufanya mazingira yawe safi zaidi.
 
Plastic kuisha ni ad ipatikane maligafi itakayo kua mbadala wa plastic ila km akutakua na mbadala wa plastic apo ni kudanganyana tu
 
Back
Top Bottom