Je, jogoo kuwika mapema kuna uhusiano wowote na mikosi?

manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
5,070
11,897
Za asubuhi wakuu,

Kwa wataalam wa mambo ya asili kama mshana jr, Jichawi , mzizimkuu1 na wengineo naomba kueleweshwa kama kuna uhusiano wowote kati ya jogoo kuwika mapema kama saa moja, saa mbili au saa tatu usiku na mikosi na mabalaa.

Imani hii nimeikuta karibu Tanzania nzima na jogoo akiwika nyakati hizo haki yake ni kuchinjwa.

Je kuchinjwa kunaondoa balaa au mikosi hiyo ?
 
Ngoja akuje atwambie maana wiki iliyopita jogoo aliwika midaa ya saa tatu uck na juz tumefiwa na bibi sasa cjui mahusiano yaliyopo hapo
 
Ndege wanaweza kutoa ishara za kitu fulani kama vile mvua,msiba nk
Mfano bundi akiashiria msiba anajulikana hata njiwa,jogoo ambaye huwa anawika asipowika sikuhiyo kama ilivyokawaida hapo uwezekano mkubwa wa kusomwa historia ya mtu unakuepo

Ndio maana hata wachawi wanawatumia sana ndege hao
 
hakuna uhusiano wowote acheni imani za kishirikina
Ndo maana nimeuliza mkuu kwani hii imani imesambaa sana karibu nchi nzima. Nyumbani kwangu kuna kuku chotara ambae anawika wakati wowote ila kila anapowika majirani wananigongea na kuniambia nimchinje sasa sielewi ana uhusiano gani na mabalaa.
 
Sidhani mi nahisi ni kuwika tu kwa kawaida.Hawezi patia masaa kila mara
 
Back
Top Bottom