Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,861
18,282
Makabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Hapa Tanzania, kwa mfano, kuna mambo fulani ambayo ni mwiko kufanyika katika jamii na ikitokea mmoja wa wanajamii akaenda kinyume na mwiko huo anaweza kupata balaa au kuwasababishia wanajamii wengine balaa.

Baadhi ya mambo/matendo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Jogoo akiwika usiku kabla ya mapambazuko huchukuliwa kuwa ni laana ama uchuro. Adhabu yake ni kuchinjwa na kufanywa kitoweo.

2. Bundi akilia usiku karibu na maskani ni balaa. Ili kuepukana na hiyo balaa, unatakiwa kuamka ukoke moto na kuchoma punje za mtama kwenye moto huo hadi punje hizo zilipuke.

3. Kwa kabila letu, hairuhusiwi mtu kutupa tula (Sodom apple) kumvuka msichana au mvulana ambaye bado yupo jandoni. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kifo au kuleta balaa kwa mhusika.

4. Ukiwa unapita porini na kukuta uyoga (edible mushroom) usiuache hapo ulipo. Hata kama huutaki au hujisikii kuula, ungo’e na kuuweka sehemu iliyoinuka ili mtu mwingine anayeuhitaji akipita auchukue akale. Kuuacha bila kuung’oa inaweza kukusababishia matatizo au mikosi.

5. Maisha ya kijijini ni ya kijamaa na watu huishi kwa kusaidiana. Kuna wakati unaweza kukosa unga ukaenda kuomba kwa jirani. Hata kama huyo jirani uliyemuendea naye hana unga wa kukugawiwa, chombo ulichoenda nacho hakirudi bure. Angalau akuwekee unga kisoda kimoja kwenye chombo hicho ili kisirudi tupu. Ni mwiko chombo hicho kurudi tupu.

6. Ukitembelewa na mgeni ambaye hajakutembelea baada ya muda mrefu hata kama huna chakula mmegee ukoko kutoka kwenye sufuria atafune au hata fundo la maji anywe. Ni mwiko mgeni huyo kuondoka kwako bila kula chochote.

Hii ni baadhi ya miiko ninayoweza kukumbuka kwa haraka haraka. Nitaongezea mingine wasaa mwingine. Je, wewe kwenye kabila lako au mahali ulipokulia, ni miiko gani umewahi kuishuhudia na mpaka sasa inaheshimiwa? Tupia mmoja hapa tujifunze kitu.

Nawasilisha.
 
Makabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Hapa Tanzania, kwa mfano, kuna mambo fulani ambayo ni mwiko kufanyika katika jamii na ikitokea mmoja wa wanajamii akaenda kinyume na mwiko huo anaweza kupata balaa au kuwasababishia wanajamii wengine balaa.

Baadhi ya mambo/matendo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Jogoo akiwika usiku kabla ya mapambazuko huchukuliwa kuwa ni laana ama uchuro. Adhabu yake ni kuchinjwa na kufanywa kitoweo.

Hiyo si kwa wote. Kuna (baadhi ya Waislam) nimewashudia ambao anapowika jogoo, katika mida ambayo si kawaida ya jogoo kuwika, huwa wanasoma dua na wanasema "malaika anapita".
 
- kujichokonowa pua mbele za watu. Ni tabia ambayo kwetu haijwahi kukubalika kuanzia kwa watoto wadogo mpaka watu wazima. Kwetu Pwani.

Imefikia mpaka mimi siikubali kabisa na nashindwa kujizuwia mtu akijichokonowa mbele yangu, nampa wazi, nendachooni jichokonowe mpaka uchoke kisha nawa mikono yako kwa sabuni, usije kuwapa watu mkonoau kutushikia vitu na mauchafu yako.

Kinyaa.
 
Makabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Hapa Tanzania, kwa mfano, kuna mambo fulani ambayo ni mwiko kufanyika katika jamii na ikitokea mmoja wa wanajamii akaenda kinyume na mwiko huo anaweza kupata balaa au kuwasababishia wanajamii wengine balaa.

Baadhi ya mambo/matendo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Jogoo akiwika usiku kabla ya mapambazuko huchukuliwa kuwa ni laana ama uchuro. Adhabu yake ni kuchinjwa na kufanywa kitoweo.

2. Bundi akilia usiku karibu na maskani ni balaa. Ili kuepukana na hiyo balaa, unatakiwa kuamka ukoke moto na kuchoma punje za mtama kwenye moto huo hadi punje hizo zilipuke.

3. Kwa kabila letu, hairuhusiwi mtu kutupa tula (Sodom apple) kumvuka msichana au mvulana ambaye bado yupo jandoni. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kifo au kuleta balaa kwa mhusika.

4. Ukiwa unapita porini na kukuta uyoga (edible mushroom) usiuache hapo ulipo. Hata kama huutaki au hujisikii kuula, ungo’e na kuuweka sehemu iliyoinuka ili mtu mwingine anayeuhitaji akipita auchukue akale. Kuuacha bila kuung’oa inaweza kukusababishia matatizo au mikosi.

5. Maisha ya kijijini ni ya kijamaa na watu huishi kwa kusaidiana. Kuna wakati unaweza kukosa unga ukaenda kuomba kwa jirani. Hata kama huyo jirani uliyemuendea naye hana unga wa kukugawiwa, chombo ulichoenda nacho hakirudi bure. Angalau akuwekee unga kisoda kimoja kwenye chombo hicho ili kisirudi tupu. Ni mwiko chombo hicho kurudi tupu.

6. Ukitembelewa na mgeni ambaye hajakutembelea baada ya muda mrefu hata kama huna chakula mmegee ukoko kutoka kwenye sufuria atafune au hata fundo la maji anywe. Ni mwiko mgeni huyo kuondoka kwako bila kula chochote.

Hii ni baadhi ya miiko ninayoweza kukumbuka kwa haraka haraka. Nitaongezea mingine wasaa mwingine. Je, wewe kwenye kabila lako au mahali ulipokulia, ni miiko gani umewahi kuishuhudia na mpaka inaheshimiwa? Tupia mmoja hapa tujifunze kitu.

Nawasilisha.
Kwetu ni mwiko kutahiriwa
 
- kujichokonowa pua mbele za watu. Ni tabia ambayo kwetu haijwahi kukubalika kuanzia kwa watoto wadogo mpaka watu wazima. Kwetu, pwani.

Imefikia mpaka mimi siikubali kabisa na nashindwa kujizuwia mtu akijichokonowa mbele yangu, nampa wazi, nendachooni jichokonowe mpaka uchoke kisha nawa mikono yako kwa sabuni, usije kuwapa watu mkonoau kutushikia vitu na mauchafu yako.

Kinyaa.
Aisee moja ya Tabia ambazo sizipendi Duniani Ni moja wapo hiyo ndio maana siku hizi Mimi sisalimiani na watu kwa kushikana mikono ukija kunipa Mkono nakupa tano imeisha hiyo
 
Back
Top Bottom