Hajakosea kabisa hata kidogo, usijaze chochote ndio ukweli wenyewe?????? Lakini kuvuta bangi na kuibia maskini kipi afadhali, halafu elewa kuwa wanaovuta bangi wote ni shauri ya umaskini ili kupoteza mawazo ya kuonewa kunyanyaswa na kudhulumiwa. Wengine nanapoteza mawazo kama ifuatavyo Baada ya wavuta bangi wanafuata wanywa gongo na pombe za kienyeji baada ya hao wale wanokunywa bia kwenye kontainer, halafu hivyo hivyo upwards mpaka wale ambao wanatuibia na wakifurahia na kusherehekea kuiba huenda kujitakasa sehemu huku wakicheza gofu, kuvua samaki na maboti yao yenye baa ndani na au kunywa bia ya shs 4000/=, hela ambayo ambao ukimpa mvuta bangi ataenda kununulia watoto utumbo wa kuku ili wanae wasuuze matumbo yao yaliyochoka dagaa , mchunga na mnyavu.Lakini kabla ya wavuta bangi kuna wale wavuta petroli ambao hawana hamu ya kuishi wao wanatafuta njia ya mkato ya kwenda jehanamu na wako wengine wa unga hawa labda nisaidiwe nashindwa kuwaweka kwenye kundi muafaka.
Jina linajieleza. Niliamua kutumia jina hilo ili, kwanza kuuonesha umma kuwa hata katika nchi ambayo imejaa watu corrupt, bado tupo waadilifu wachache, na nimekuwa nikijitahidi siku zote (kwa msaada wa Mungu) kuishi sawa sawa na jina langu. Pili kuleta ladha ya tofauti, maana nimekuwa nikishuhudia majina yanayopendwa sana siku hizi, ni Fisadi(mtoto), Shetani, "mwaga ugali nimwage mboga"..etc. Tanzania yenye uadilifu inawezekana, usisubiri wawepo wengi, anza wewe wengine watafuata.
It sounds Utopian...kwakuwa tu Watanzania hawakotayari...kabisaaa...nionavyo.Naam ndugu yangu, Tanzania yenye uadilifu na isiyo na mafisadi inawezekana kabisa.
All my children have their first names beginning with J.Ndivyo ninavyofahanika kule uswahilini kwetu.