Je, inawezekana kupata GPA 5.0 chuo?

Je, inawezekana kupata GPA 5.0 chuo?

Inawezekana.

Ila ukishaipata utaifanyia nini?... Huo mda unaotumia kusoma kwa ajili ya kutafuta 5.0 GPA,ungetumia kusoma + kuthubutu biashara ndogo ya kuanza nayo au kusoma + kutengeza network ya watu watakaokusaidia.

Hakuna ajira,hivyo msiweke nguvu nyingi kwenye GPA,mwisho wa siku una 5.0 GPA unaishia kuwa bodaboda.

Usingizi umekugomea mkuu?
Shule tunakwenda ili kusoma kufaulu na kupata kile umekusudia, ikiwemo g.p.a kubwa.. Kwani ukipata 5.0 utashindwa kujiajiri?
Kikubwa kufahamu umekwenda shule kufanya nini na kubalance mambo. Mana hata waliofeli walitamani kupata first class pia.
 
Habarini wanajamvi,
Je inawezekana kupata GPA tajwa hapo juu, na ukitoa mfano hai itapendeza,karibuñi (kwa level ya chuo kikuu)
Inategemea unaenda kusoma chuo gani!

Mfano UDSM ukiwa na A zote wewe una 5.0 ila SUA (na mzumbe kama sikosei), ukiwa na A zote unaweza kuta una 4.5 au 4.6!!

Kwanini?

SUA and the alike hawaangalii tu A wanaangalia una A ya ngapi!! So mtu mwenye A ya 70 au 80 ni tofauti na mtu mwenye A ya 90 au 100!!

Ila kwa UDSM ukiwa na A tu basi hata kama una A ya 80 basi utakua sawa na mtu mwenye A ya 100!!
 
Hiyo GPA ya 5.0 siyo ya mchezo,Maana hata Chegele sidhani kama aliipata hiyo.Maana ndiyo nasikia T.O wa StdVII,Form II,IV,VI& Chuo kikuu.Lakini nadhani Msuli wake siyo wa mchezo na lazima uambatane na Utabe flani hivi.Nashukuru mie niliambulia 4.40 japo shughuli haikuwa ndogo
 
Hongera sana ase, ulifanya kitu kikubwa mno. Bosi embu tupe technique uliwezaje kufanikisha hilo?
Soma dogo ......hakuna techniques kweli hilo vimba na desa......wewe na desa desa na wewe ila kupata GPA ya 5.0 kamili sahau.....kuanzia 4.4-4.9 it's possible
 
Sisi wengine tuna unclassified degrees-hakuna kitu kama GPA. Lakini GPA ya tano inawezekana tatizo wachumi wanakuambia kuna "law ya dimishing marginal returns" kwa wengi wetu tukifika hiyo 2.7 marginal returns inashuka hivyo hata 3 huwa ni issue kubwa achilia mbali 5.
 
Inategemea unaenda kusoma chuo gani!

Mfano UDSM ukiwa na A zote wewe una 5.0 ila SUA (na mzumbe kama sikosei), ukiwa na A zote unaweza kuta una 4.5 au 4.6!!

Kwanini?

SUA and the alike hawaangalii tu A wanaangalia una A ya ngapi!! So mtu mwenye A ya 70 au 80 ni tofauti na mtu mwenye A ya 90 au 100!!

Ila kwa UDSM ukiwa na A tu basi hata kama una A ya 80 basi utakua sawa na mtu mwenye A ya 100!!
Yaani SUA mnapenda kufanya maisha magumu. Kila score band ina fomula yake ya kukokotoa grade point unazopata kwenye somo. Hivyo GPA ya 5 lazima ule 100% kila somo. LoL
 
Yaani SUA mnapenda kufanya maisha magumu. Kila score band ina fomula yake ya kukokotoa grade point unazipata kwenye somo. Hivyo GPA ya 5 lazima ule 100% kila somo. LoL
Na huwezi pata 100% masomo yote...

Kuna kipindi nikiwa mwaka wa pili nilikomaa kweeeli nikaishia 4.01!! Ningekua udsm ningekua na 4.8 or something close to that!!
 
Back
Top Bottom