Je, inawezekana kupata GPA 5.0 chuo?

Je, inawezekana kupata GPA 5.0 chuo?

Mijitu iliyofeli na kupata gpa ndogo inatoa motivation speech tu hahahahaha. Acheni kuwadanganya watoto wasisome. Mimi nilipata first class degree na wala haikuwa kazi ngumu. Ukiwa genius hiyo gpa wala sio kazi ngumu kabisa
 
Mkuu we nenda unyooshe msuli uipate hiyo GPA ya 5.0 kwanza. Masuala ya ajira na kutoka hayo ni mbele ya safari Mungu atatengeneza mwenyewe. Kipindi sisi tunasoma wale waliokuwa na good grades chuo walipata kazi fasta sana hasa kwenye auditing firms mara tu tulipomaliza chuo. Asikuambie mtu mkuu, kazi hakuna lakini kuna kazi selective ambazo wanachukua creme ya briliant guys kama wewe (utakapopata hiyo grade).

Kajinyooshe mkuu yote yanawezekana.

Kajitume kamanda. Kila la kheri.
Pamoja sana Mkuu
 
Tena hatari SUA wanajifanya hawako nyuma
kuna kitu ambacho ukiangalia yu matokeo ya wanafunzi wa chuo husika utagundua ubora wa elimu wa chuo husika
kuna utafiti nilisoma ulisema kwenye kundi kubwa la watu, watu wenye akili sana ni wachache , wenye akili za wastani ndo wengi na wenye akili kidogo nao ni wachache.
kwahio chuo (course ) hawezi kuwa na watoto 500 alafu first class ziwe 200 na hao wanaobaki wawe ni secondo class hapo inamana elimu inayotolewa hapo ni hovyo kabisa au kusiwe na fist class wala second class kuwe na pass na sup ata hapo elimu inayotolewa ni hovyo kabisa
 
Kaulize SUA ili upate hiyo 5 lazima upate 100% masomo yote wanatumia maksi sio A,B n.k ndo mana mnapata A wengi lakin GPA hazitafanana kamwe kwa SUA
Sasa ulichoandika kina tofauti gani na nilichoandika kwenye comment ya #24?
 
GPA 5 wewe ni John Kisamo Sana Ila First Class kuipata kawaida ata ya 4.6 japo nazo ni ngumu uwe ume make opportunity cost sana mostly social activities
 
Inategemea chuo na kozi unayosoma. Aina ya walimu pia inachangia. Kuna wahadhiri wanakuambia kabisa huwezi pata A somo lake.
Mambo ya gpa yalikuwa zamani wakati watanzania walikuwa wachache. Kama huamini muulize DAB.
 
Inategemea unaenda kusoma chuo gani!

Mfano UDSM ukiwa na A zote wewe una 5.0 ila SUA (na mzumbe kama sikosei), ukiwa na A zote unaweza kuta una 4.5 au 4.6!!

Kwanini?

SUA and the alike hawaangalii tu A wanaangalia una A ya ngapi!! So mtu mwenye A ya 70 au 80 ni tofauti na mtu mwenye A ya 90 au 100!!

Ila kwa UDSM ukiwa na A tu basi hata kama una A ya 80 basi utakua sawa na mtu mwenye A ya 100!!
Ila kwenye kupata best student ni tofauti hapo
 
Back
Top Bottom