Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Kuna jambo moja huwa linawaacha wanawake wengi na maswali yasiyo na majibu na wengi huwa wanajiuliza maswali bila ya kupata majibu.
Kuna baadhi wanawake ambao hawajatulia, vijana wa mjini huwa wanawaita "utulivu ziro" yaani sio kwamba ni makahaba, hapana, lakini wanakuwa na tabia ya kutotulia na kuonekana kama wana vurugu kichwani. Kwa wanawake wengi huwa wanawaona wanawake wa aina hii kama sio wife material, yaani hawako katika kundi la wanawake wanaofaa kuolewa kutokana na tabia zao hizo za kutotulia.
Lakini jambo ambalo huwa linawaacha wanawawake wengi na mwaswali ni pale wanapowaona wanawake wa aina hii wakiopoa wanaume wenye muafaka, yaani wanaume wenye sifa zinazowavutia wanawawake wengi kuolewa nao. Hapo ndipo yanapoibuka maswali mengi kwa baadhi ya wanawake wakijiuliza.
"Ni kitu gani kimemvutia huyu mwanaume kwa mwanamke yule.....!"
Lakini jambo la kushangaza zaidi ni kwamba uhusiano wao unaweza kukua hadi kufikia kufunga ndoa, na usije ukadhani kwamba yule mwanamke atabadilika tabia, la hasha, anaweza kubaki na tabia yake hiyo hiyo ya kutotulia na bado akamudu kumshika huyo mwanaume barabara. Mwanaume huyo anaweza kujikuta amenasa na hawezi kuchomoka, na hata ikitokea wakitengana, haitapita muda wararudiana pamoja na uhusiano wao kutawaliwa na vurugu fulani fulani.
Wapo baadhi huwa wanabadilika na kujenga uhusiano imara hata kuwashanganza watu wengi, lakini huwa ni wachache sana, narudia kusema, mara nyingi huwa ni wachache sana, lakini wengi wao pamoja na kutotulia na kuonekana kuwa na vurugu kichwani, lakini humudu kuwashika wanaume wenye muafaka na kuwaacha wanawake wenzao vinywa wazi.
Je ni jambo gani linatokea?
Naomba mchango wenu.
CC: cacico, Paloma, snowhite, Lisa, lara 1, King'asti, Preta, KOKUTONA, Madame B, Nivea, BADILI TABIA, miss wa kinyaru, sister, marejesho, AshaDii, Kongosho, Fixed Point, gfsonwin, Mwali, mwallu