Je, inakuwaje wanawake wasiotulia huopoa wanaume wenye muafaka...?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
couple-PF-378x414.jpg

Kuna jambo moja huwa linawaacha wanawake wengi na maswali yasiyo na majibu na wengi huwa wanajiuliza maswali bila ya kupata majibu.

Kuna baadhi wanawake ambao hawajatulia, vijana wa mjini huwa wanawaita "utulivu ziro" yaani sio kwamba ni makahaba, hapana, lakini wanakuwa na tabia ya kutotulia na kuonekana kama wana vurugu kichwani. Kwa wanawake wengi huwa wanawaona wanawake wa aina hii kama sio wife material, yaani hawako katika kundi la wanawake wanaofaa kuolewa kutokana na tabia zao hizo za kutotulia.
roaming-eyes-153x153.jpg

Lakini jambo ambalo huwa linawaacha wanawawake wengi na mwaswali ni pale wanapowaona wanawake wa aina hii wakiopoa wanaume wenye muafaka, yaani wanaume wenye sifa zinazowavutia wanawawake wengi kuolewa nao. Hapo ndipo yanapoibuka maswali mengi kwa baadhi ya wanawake wakijiuliza.

"Ni kitu gani kimemvutia huyu mwanaume kwa mwanamke yule.....!"

Ciara-153x153.jpg

Lakini jambo la kushangaza zaidi ni kwamba uhusiano wao unaweza kukua hadi kufikia kufunga ndoa, na usije ukadhani kwamba yule mwanamke atabadilika tabia, la hasha, anaweza kubaki na tabia yake hiyo hiyo ya kutotulia na bado akamudu kumshika huyo mwanaume barabara. Mwanaume huyo anaweza kujikuta amenasa na hawezi kuchomoka, na hata ikitokea wakitengana, haitapita muda wararudiana pamoja na uhusiano wao kutawaliwa na vurugu fulani fulani.

amber-rose-wiz-khalifa-feat-153x153.jpg

Wapo baadhi huwa wanabadilika na kujenga uhusiano imara hata kuwashanganza watu wengi, lakini huwa ni wachache sana, narudia kusema, mara nyingi huwa ni wachache sana, lakini wengi wao pamoja na kutotulia na kuonekana kuwa na vurugu kichwani, lakini humudu kuwashika wanaume wenye muafaka na kuwaacha wanawake wenzao vinywa wazi.

Je ni jambo gani linatokea?

Naomba mchango wenu.

CC: cacico, Paloma, snowhite, Lisa, lara 1, King'asti, Preta, KOKUTONA, Madame B, Nivea, BADILI TABIA, miss wa kinyaru, sister, marejesho, AshaDii, Kongosho, Fixed Point, gfsonwin, Mwali, mwallu
 
Mtambuzi umenifikirisha sana kwa hili jambo, ila ninachoona kuna mahusiano ya ufahamu wa mambo ya ndani zaidi katika utundu wa chumbani kuliko hao wanaitwa wife material.
mara nyingi wanapenda kujiachia, sasa na wanaume wanapenda vitu kama hivyo....
 
Uzuri umeshatuhabarisha si kahaba, yawezekana anaonekana hajatulia na sio wife materials but akawa tofauti katika maswala ya mapenzi yaani akawa msikivu, mwelewa kwa mpenzi wake jambo ambalo halionekani nje na kwa watu wengine, na nafikiri hyo ndo sababu ya wanaume kubaki kwa watu wa design hii......

ni hayo tu Bro Mtambuzi
 
Kiukweli hata mim hili jambo uwa silielewi...kuna mdada tulikuwa tunasoma nae chuo alikuwa hajatulia kama unavyosema...lakini tumemaliza tu chuo akaolewa...
 
Hivi kuna wanaume "viwembe" hawajaoa!!!?????

Kwa hili la wanawake wanaoitwa hawajatulia nadhani ni wale wanaojitambua sana nini cha kufanya na wapi pa kufanya hivyo ila tatizo they are not there to kiss nobodys azz hata kama ni mume!!!!!!

Sasa kwa mfumo dume huyu lazima abatizwe mapepe au hajatulia sababu hupenda kuishi vile atakavyo,labda ndio maana pia hupata wanaume wa kitasha kwa urahisi sababu wanaweza kuelewana kirahisi kuliko sie tuliolelewa kibongo!!!!!!

Ila what i know for sure ni kuwa ni machizi kwa bed na game zao ni tight,wanapika mbaya(wakiamua),akiwa na kipato mi gift sio issue na wanajua taste sana,wanaishi leo hawana hofu ya kesho kama mama mzazi,sharp minded ila hawajali!!!!!!!

Sasa mwanaume mwenye msimamo wa kimaisha anahitaji kampani na hiyo ni zaidi ya inatosha kwake as uchumi sio ishu sasa kwa nini asinase???!!!!!

Na wengi akishakuwa na watoto huwa wanazima mapepe yoote na kuwa poa kabisaa mpaka watu hushangaaa!!!!!
 
Na mimi nasubiri majibu hapa, maana nina mdogo wangu nae ameoa hawa "wanawake wasiotulia" bahati mbaya siri za mke huyu zimenza kuvuja inafika wakati mdogo wangu anona aibu hata kuongozaa nae.
 
Ni kweli mara nyingi wanawake wanaonekana hawajatulia hupata wanaume wa maana kirahisi kwa sababu zifuatazo
1. free minded na wanajiamini
2. very funny and unpredictable kitu ambacho wanaume wanaojiamini wengi wanakipenda.
3. Mapenzi ya kitandani na nje ya kitanda wanayamuduuu.
4.wana upeo mpana wa kutoa ushauri na kufanya jambo bila kuelekezwaaa.
5. wanajuaa kumiliki hisiaa za wanaume wao kirahisii.
 
Kwa sababu wana wengi ina maaana katika hao wengi lazima at least mmoja anakuwa Mwanaume wa maana.
 
Na mimi nasubiri majibu hapa, maana nina mdogo wangu nae ameoa hawa "wanawake wasiotulia" bahati mbaya siri za mke huyu zimenza kuvuja inafika wakati mdogo wangu anona aibu hata kuongozaa nae.

Kama kaoa kicheche hapa majibu yatakuwa tofauti!!!!!
 
sijawahi kuelewa ni kwa nini
maana kuna watu wanakua hawajatulia kabisaaaa lakini wanaolewa na wanaishi vizuri tu
 
Good girls aint no fun,wapole nje hadi ndani,hao wasiotulia are a type of bad girls ,they r not ass kissers at all,adventurous and men love that..wanajua kusumbua a guy akiwa anamfukuzia and know maujanja every angle ya relationship,tatzo ndo wanaweza wakawa wanagawa kw wengi
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom