Je, huyu anafaa kuolewa

tafuta mwanamke huko huko ulipo achana na longdistance relationship utaja lea mtoto si wako
 
Kashapata bwana mwingine huyo kinacho mfanya asikuache ni kwasababu bwana yake Hana pesa labda ni mwanafunzi mwenzake kwahiyo anakutumia ww Kama accnt yake ya akiba
 
Hahitaji uwe lofa kiwango cha standard gauge kujua kwamba hakupendi anakutumia. Vibinti vya chuo na long distance relationship wapi na wapi? We unatoa pesa wengine wanajimegea tu ndo ukweli mchungu.
Achana naye utawekeza sana na utalia ishia uwekezaji wako hapo, kwani mbona serikali imetosa miradi mingapi we unafail wapi
 
Kashapata bwana mwingine huyo kinacho mfanya asikuache ni kwasababu bwana yake Hana pesa labda ni mwanafunzi mwenzake kwahiyo anakutumia ww Kama accnt yake ya akiba
Take this piece of advice and work on it.
Inauma sana kumuacha sijui naanzaje sasa
 
Inauma sana kumuacha sijui naanzaje sasa
Najua ni ngumu lakini yanini kuendelea na biashara yenye hasara.
Ninaandika kwa herufi kubwa, ACHANA NAYE ANAKUCHUNA TU HAKUPENDI NA ANAONA UNAMBOA NA MIMESEJI YAKO ANAKULILIA KWASABABU ANAONA ATAKOSA PESA ZAKO
 
Asanteee! Ila kwani siwezi kumroga na akanipenda?
Unaenda kuuza future yako, roho yako, sadaka zako, future ya watoto wako, ukoo wako kwa mganga kisa demu, by the way penzi la kuroga halina raha, kuna siku utatatakiwa kwenda ku update uchawi wako huko, ili penzi lianze kunoga tena.

Mbona wanawake ni wapo wengi kuliko wanaume? Au unajiweka sehem moja ndio maana huwaoni.

Acha mentality ya kuku, akikuta mchele au pumba akala hata zikiisha atachimba chimba hapo hapo, akidhani ndio sehemu pekee kwenye chakula.kumbe kuna shamba lina mahindi tele,na ghala lenye pumba tele.

Wadada wenye kazi zao wazuri wapo wengi, wanaohitaji mwenza, utakuta huyo hana ishu na anakupeleka.
 
Jamaa hamuwezi huyo demu kwanza hajiamini kabisa ndio maana anapelekeshwa hata akibahatika kumuoa huyo demu bado hatamuweza, sisi wanaume tupo duniani kumiliki kila kilichomo humu na kijione kipo Salama chini yetu ,jamaa ameyumba since day one yaelekea alimtongoza kiuwogauwoga demu akaona huyu mwamba hajiamini.
 
Mtreat mtu namna anavyotaka au kupenda. Sasa mtu hajibu ujumbe wako it means hapendi kuwasiliana na wewe, sasa kwann usimpe anachotaka...?!

Mkalie kimya, wacha apambane na habari zake...... Wewe tafuta ambaye usipomtext anakosa hamu ya kula na anasikia kama figo zinataka kutoka........

Mapenzi ni two way street. Ukiona unalazimisha penzi, basi jitafakari sana.
 
Inauma sana kumuacha sijui naanzaje sasa
Ebu tuondolee ujinga hapa
1. Uliwezaje kuacha ziwa la mama yako?
2. Uliwezaje kuiacha nchi ya Tanzania na kwenda kuishi Kenya?
3. Uliwezaje kuwaacha baba na mama yako na kwenda kujitegemea?

Tumia njia hizo hizo kumsahau huyo demu ambaye ameshakuacha ila wewe ndio unashindwa kukubali matokeo
 
Kitu nilichojifunza ni kuwa wanawake wengi ukianza naye tu mahusiano anabadili tabia yake ya asili,inawezekana ulipomuona mwanzoni hakuwa hivyo,ila pindi mkianzisha anakuwa tofauti,sasa sijajua inakuwa ni ushauri anaopewa na marafiki au ni nature yao,utakuta anaanza katabia ka kununa,au kutopokea simu mara moja ni mpaka urudie,au tabia ya kuzila/kususa,au kuomba hela kwenye kila kitu hata vile ambavyo mwanzoni aliweza kujimudu,inakuwa ni kama amepata benki ya kujipatia pesa ya kutatua kila shida yake,au kukufokea hata mbele za watu n.k. n.k....
 
Hawa ndio wale vijana wanao jiua kisa toto halimtaki halafu yeye ndio kakolea vibaya mno, ndio maana ana mtusi sometimes.
definitely hajiamini .
Kwa post hii nina mashaka na umri wako na kama umeshapevuka basi nina mashaka na akili zako
Nashukuru kwa ushauri wenu
 
Dada anahofu yasije mkuta kama ya shishimbi akakosa pote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…