Huyu mwanamke anafaa kuwa mke kweli?

Akili 2

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
1,221
1,829
Habari Wakuu,

Bila kupoteza mda niende Moja kwa Moja kwenye mada.

Nilikuwa na mpenzi ambaye ndiyo nilikuwa nategemea kumuoa, kilichofanya nije niulize hapa ni hili tukio. Mimi Niko mkoa mwingine na mpenzi wangu alikuwa anafanya kazi mkoa mwingine.

Siku moja nikawa nimeenda kumsalimia na nikaa naye kama siku tatu hivi ,baada ya hapo nikarudi mkoa ninaoishi kwa ajili ya kazi, basi ijumaa ya wiki hiyo niliyorudi akaniambia kutakuwa na ugeni ofisin kwao hivyo atakuwa busy maan yeye anafanya kazi hotel.

Basi kuanzia siku ya jumatatu hakuwahi pokea simu yangu wala kujibu text zangu Wala kanipigia yani nikawa nampigia simu inaita weee bila kupokeleea na namtumia text hajibu mpaka wiki ikaja kuisha siku ya jumapili ndiyo akaja pokea simu baada ya kumuuliza kwann hupokei simu wiki nzima na hata text hujibu, akanijibu vimajibu vya kitoto sana basi nikakaa kimya.

Siku hiyo hiyo baada kama ya lisaa limoja hivi nikapokea text kutoka number mpya ikiwa inanitaka nitoe ushirikiano wa kuwa huyu GETU unamfahamu? Na nina yako, maana Mimi nilikuwa naye wiki nzima na simu nilikuwa nazo Mimi.

Basi nikamuelekeza jamaa naye akamaindi sana, kumbe jamaa naye alikuwa katoka zenzibar kamfata Getu, basi kama wanaume tukaongea pale yakaisha ikaonekana demu anatuchanganya wote, basi mie nikaona hapa hamna mwanamke

Baada ya tukio hilo baada ya mwezi mmoja akaanza kunitafuta na kuniomba msamaha Sana na alinifata hadi ninakoishi mkoa mwingine lakini nilimfukuza alilia Sana ila nilikaza na baadaye akasema Akili mbili Nina Mimba na hii Mimba ni yako.

Ishu kubwa inayonitesa je hii Mimba inaweza kuwa yangu kweli au nimpotezee tu nisubiri akija jifunguwa ndiyo nione mtoto Kama anafanana na Mimi au laa?

Maana Toka tukio Lile sinaga hisia naye kabisa na namchukia sana.
 
Asee hili swala nalo lina hitaji tujibu ?yahee Mbona majibu yaako waziiii bwanaaa, mimba ampelekeea mpembaa
 
Hahahah wewe unatuonaga wajinga na mafala sisi tunaokataaga Mumbai,wanaume tumeumbwa na akili sana.Hatuoi mwanamke mpumbavu wala kulea mimba za wanaume wengine https://jamii.app/JFUserGuide what they say Karma...kimbia huna chako hapo kata mawasiliano yote
 
box_awards_knockouts_01.jpg
 
Mabinti bwana. Sasa kuna situations kama hizi. Anafanya matukio kama haya halafu anakuwa anaendelea kubembeleza jamaa aendelee kuwa nae.

Wakishaingia ndoani na kuzaa jamaa yule shetani wa hasira ya wivu, na matukio aliyofanyiwa na mwanamke vinakuja kumvaa tena. Anaanza kumbadilikia mwanamke na kuanza kumpa kichapo, matusi na kila aina ya udhalilishaji.

Wakati huo binti umri umeshaenda hana tena mvuto wa kuwa na mwanaume mpya na yeye ndio anajifanya amestaarabika na ameacha umapepe.

Jamii ikitazama tukio wanasema jamani wanaume ni makatili na ni wanyanyasaji. Kumbe hawajui kuwa mkorofi na ABUSER namba moja ni mwanamke. Sababu kipindi jamaa akiwa na mapenzi ya ukweli juu yake yeye alikuwa anamfanyia matukio ya kiudhalilishaji na kumletea msongo wa mawazo mwanaume wake sababu enzi hizo za usichana attention ya wanaume ilikuwa kubwa sana. Na yeye aliitumia vibaya.

Maswala ya unyanyasaji wa kijinsia huwa yanatazamwa kinafiki sana. Na siku zote mwanamke huonekana mstaarabu na hajasababisha chochote. Ila mwanaume anaonekana mwehu kakurupuka tu ghafla na kuanza kuchukia mke wake.
 
Umeandika ukiwa unamawazo mazito sana. Kama unajiona ukimuacha utaumia zaidi msamehe mlee akishajifungua utamzalisha mtoto wako wa uhakika
 
Anafaa sana kuwa mke hiyo jomba. Kama hujaanza mchakato fanya ujitambulishe kaka. Oa mke mwema huyo. Jitahidi kabla hujachelewa, wa hivyo kuwapata inasumbua sana
 
Achana nae huyo malaya bro. Hizo story za mimba mwambie sii atajifungua yatajulilana. Kama mtoto atakuwa wako still usilete ujinga wakumsamehe na use uishi nae. Wee toa mahataji ya mtoto basi
 
Mabinti bwana. Sasa kuna situations kama hizi. Anafanya matukio kama haya halafu anakuwa anaendelea kubembeleza jamaa aendelee kuwa nae.

Wakishaingia ndoani na kuzaa jamaa yule shetani wa hasira ya wivu, na matukio aliyofanyiwa na mwanamke vinakuja kumvaa tena. Anaanza kumbadilikia mwanamke na kuanza kumpa kichapo, matusi na kila aina ya udhalilishaji.

Wakati huo binti umri umeshaenda hana tena mvuto wa kuwa na mwanaume mpya na yeye ndio anajifanya amestaarabika na ameacha umapepe.

Jamii ikitazama tukio wanasema jamani wanaume ni makatili na ni wanyanyasaji. Kumbe hawajui kuwa mkorofi na ABUSER namba moja ni mwanamke. Sababu kipindi jamaa akiwa na mapenzi ya ukweli juu yake yeye alikuwa anamfanyia matukio ya kiudhalilishaji na kumletea msongo wa mawazo mwanaume wake sababu enzi hizo za usichana attention ya wanaume ilikuwa kubwa sana. Na yeye aliitumia vibaya.

Maswala ya unyanyasaji wa kijinsia huwa yanatazamwa kinafiki sana. Na siku zote mwanamke huonekana mstaarabu na hajasababisha chochote. Ila mwanaume anaonekana mwehu kakurupuka tu ghafla na kuanza kuchukia mke wake.
Umedadavua vizuri sana. Unamuoa mtu ukiwa na makovu ya kisaikolojia halafu unategemea muwe na ndoa yenye amani na furaha. Ngumu sana!
 
Mabinti bwana. Sasa kuna situations kama hizi. Anafanya matukio kama haya halafu anakuwa anaendelea kubembeleza jamaa aendelee kuwa nae.

Wakishaingia ndoani na kuzaa jamaa yule shetani wa hasira ya wivu, na matukio aliyofanyiwa na mwanamke vinakuja kumvaa tena. Anaanza kumbadilikia mwanamke na kuanza kumpa kichapo, matusi na kila aina ya udhalilishaji.

Wakati huo binti umri umeshaenda hana tena mvuto wa kuwa na mwanaume mpya na yeye ndio anajifanya amestaarabika na ameacha umapepe.

Jamii ikitazama tukio wanasema jamani wanaume ni makatili na ni wanyanyasaji. Kumbe hawajui kuwa mkorofi na ABUSER namba moja ni mwanamke. Sababu kipindi jamaa akiwa na mapenzi ya ukweli juu yake yeye alikuwa anamfanyia matukio ya kiudhalilishaji na kumletea msongo wa mawazo mwanaume wake sababu enzi hizo za usichana attention ya wanaume ilikuwa kubwa sana. Na yeye aliitumia vibaya.

Maswala ya unyanyasaji wa kijinsia huwa yanatazamwa kinafiki sana. Na siku zote mwanamke huonekana mstaarabu na hajasababisha chochote. Ila mwanaume anaonekana mwehu kakurupuka tu ghafla na kuanza kuchukia mke wake.
Natamani ku-like hii comment zaidi ya mara moja, tatizo hiyo option haipo
 
Leo tarehe 13 april 2022, nasema kuwa nimepata somo kidogo kuhusu unyanyasaji wa hawa wanawake na inakuja kidogo kama inakataa ila ngoja ntarudi kuthibitisha hilo.
 
Mapenzi n hisia pia kama humpendi achana nae usimuonee huruma itakukost baadae itakua kaachwa n yule jamaa ikabidi aje kukupumzkia wewe..subiri mtoto azaliwe umtunze km atakua wako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom