Je, huyu anafaa kuolewa

Nyavinene

Senior Member
Jul 28, 2020
164
174
Habari wadau

Jamani naomba mnishauri kuhusiana na haya mahusiano yangu kwani ni zaidi ya mwaka sasa bila kuyaelewa. Binafsi Mimi naishi Kenya ila kwetu ni Tanzania.

Ilikuwa ni mwaka jana nilipokuwa nafanya kazi za tiba ya asili mkoani Simiyu ndipo nilikutana na binti mmoja hivi, nikamueleza yaliyopo moyoni mwangu na yeye akanielewa sana. Kwa vile yeye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo cha Kati hapa nchini tulikaa pamoja Kama miezi 2.

Alisafiri kwenda huko Dodoma na mimi nikaenda zangu huko Kenya baada ya kumaliza kazi iliyonileta. Mwanzoni mawasiliano yakuwa bomba sana but baada ya muda yalianza kupungua.

Ila tatizo lake hawezi kunitafuta kama hana shida ya hela. Wakati mwingine namtumia text hata WhatsApp namuona yupo Online lakini hajibu isipokuwa anaisoma tu na kupotezea. Kuna wakati napata hasira namtusi ndipo anaanza kujibu kwa kujitetea.

Jamani naumia sana nikifikiria namna nilivyowekeza pesa nyingi kwake kweli naishiwa nguvu kabsa. Mfano sasa hivi nimetuma text WhatsApp ila hajajibu japo kaisoma. Hivi hapo kuna tumaini la ndoa kweli.

Mbaya zaidi nikilalamika ananiambia kuwa anaumia ninapolalamika nipeni ushauri ila tatizo kubwa lipo kwenye kuishi naye mbali na kutonitafuta mpaka nimtafute au awe na shida ya pesa.
 
Weka picha ya demu mkaliii kwenye dp yako WhatsApp.

Then post picha nyingine Kali ya demu huyo huyo, halafu andika "aksante Mungu" Kisha baada ya dk 15 zifute hizo picha Kisha zima simu.

Nakuhakikishia utarudi na mrejesho.
 
Mkuu hapo hujui tyu. Yan hii mbinu niliitumia tukawa vzr kwa muda ila badaye tukavurugana tena
 
Ili kupata majibu kama ni wa ndoa ama ni mpita njia points ni zile zile
Kuanzia sasa usimtafute....usipige,usitume sms
Akiomba pesa usitoe

Sikilizia kama atakutafuta unatake over mahusiano,yani unamgeuzia kibao cha yeye kuanza kukubembeleza
Asipokutafuta jua huitajiki hapo,fanya mambo mengine

Life iko too short kuumizwa na mtu,tulia fanya mambo yako utapata mtakayependana
Sometimes unatakiwa kuchukua maamuzi magumu kwa usalama wa moyo wako kwa badae

Pendana na anayekupenda
 
Mzee baba ,
Kweli sikio la kufa halisikii dawa, na huyo mwanamke kwako Ni zimu likujualo hivyo halikukuli likakwisha.

#Kwani kuoa lazima.? Huo uwekezaji uliofunya kwake Ni wakujitakia.
 
Mzee baba ,
Kweli sikio la kufa halisikii dawa, na huyo mwanamke kwako Ni zimu likujualo hivyo halikukuli likakwisha.

#Kwani kuoa lazima.? Huo uwekezaji uliofanya kwake Ni wakujitakia. Ukija kupata akili nakusihi wekeza kwa mwanamke unayezaa naye na mtoto wako huko kwengine acha serikali iwekeze.
 
Ili kupata majibu kama ni wa ndoa ama ni mpita njia points ni zile zile
Kuanzia sasa usimtafute....usipige,usitume sms
Akiomba pesa usitoe

Sikilizia kama atakutafuta unatake over mahusiano,yani unamgeuzia kibao cha yeye kuanza kukubembeleza
Asipokutafuta jua huitajiki hapo,fanya mambo mengine

Life iko too short kuumizwa na mtu,tulia fanya mambo yako utapata mtakayependana
Sometimes unatakiwa kuchukua maamuzi magumu kwa usalama wa moyo wako kwa badae

Pendana na anayekupenda
Asanteee! Ila kwani siwezi kumroga na akanipenda?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom