Habari wadau
Jamani naomba mnishauri kuhusiana na haya mahusiano yangu kwani ni zaidi ya mwaka sasa bila kuyaelewa. Binafsi Mimi naishi Kenya ila kwetu ni Tanzania.
Ilikuwa ni mwaka jana nilipokuwa nafanya kazi za tiba ya asili mkoani Simiyu ndipo nilikutana na binti mmoja hivi, nikamueleza yaliyopo moyoni mwangu nayeye akanielewa sana. Kwa vile yeye alikuwa ni Mwanafunzi wa chuo cha Kati hapa nchini tulikaa pamoja Kama miezi 2.
Alisafiri kwenda huko dodoma na Mimi nikaenda zangu huko Kenya baada ya kumaliza kazi iliyonileta. Mwanzani mawasiliano yakuwa bomba sana but baada ya muda yalianza kupungua.
Ila tatizi lake hawezi kunitafuta Kama hana shida ya hela. Wakati mwingine namtumia text hata WhatsApp namuona yupo Online lkn hajibu isipokuwa anaisoma tu na kupotezea. Kuna wakati napata hasira namtusi ndipo anaanza kujibu kwa kujitetea.
Jamani naumia sana nikifikiria namna nilivyowekeza pesa nyingi kwake kweli naishiwa nguvu kabsa. Mfano saivi nimetuma text WhatsApp ila hajajibu japo kaisoma. Hivi hapo kuna tumaini la ndoa kweli.
Mbaya zaidi nikilalamika ananiambia kuwa anaumia ninapolalamika nipeni ushauri ila tatizo kubwa lipo kwenye kuishi naye mbali na kutonitafuta mpaka nimtafute au awe na shida ya pesa