Je, huu ni uungwana kweli?

Je, huu ni uungwana kweli?

Unakuta mtu ana wafanyakazi wa ndani yani (House girls) wawili na watoto wake. Anatoka nao kwenda kwenye mgahawa kupata chakula na kinywaji kidogo!

Kwanza anapofika ktk mgahawa haongozani na hao wafanyakazi wake! Anatangulia yeye na mke wake na watoto wake wa kuzaa then hao wafanya kz wanakuja wanachungulia chungulia kwa woga na kukaa pembeni umbali wa hatua 30 kutoka meza ya mabwana zao! Na hawaruhusiwi kuagiza chochote mpaka agizo litoke kwa Bwana.

Na wanakaa wametulia na kujalibu kuwatuliza watoto wa Boss wao ambao wanaonekana ni watundu na wanaokimbiakimbia hovyo ktk mgahawa!

Then baada ya hapo Bwana na bibi wanaagiza chakula na kinywaji na kula wao tu peke yao huku wale wafanyakazi wamekaa pembeni tena ktk viti vya wageni ktk mgahawa huku hawatumii chochote!

Je huu ni uungwana kweli kwa mtu anaekutunzia na kukuangalizia watoto wako wakati wewe ukiwa ktk mapilika ya maisha yako? Na hii mpaka nje km kwenye migahawa mtu anaweza kuwafanyia hivi wafanyakazi wake wazi wazi, je huko ktk familia yake majumbani si ndio balaa kabisa?!!

Maana huko inaonekana ni marufuku mfanyakazi kula chakula km anachokula bwana! Bwana km anakula chips kuku, mfanyakazi anakula ugali Dagaa au maharagwe. Boss km anakunywa maji ya kwenye Fridge yaliyopowa basi mfanyakazi anakunywa ya kwenye ndoo! Na huenda ni marufuku kukaa sebuleni kuangalia Tv au kuwasha tv na redio!

Nauliza jee huu ni UUNGWANA KWELI?

Hii sijakutana nayo lakini nikikutana nayo, hawatokula hapo hao ma boss au mimi ntafukuzwa kwenye hiyo restaurant.
 
Ndivyo mabwenyenye wa dunia hii walivyo na walaaniwe na pesa zao za wizi!
 
Huo sio uungwana aisee....bad manners,si muwaagizie tu,au mngewaacha home wajipikie wale watosheke
 
Familia yenye mahouse girl wawili kuna haja gani ya kwenda wote mgahawani kula chakula ....kwanini wasipike nyumbani?

Kubadilisha mazingira... and kuwapa off nao wa enjoy, wawe served na wao sio kila siku kupika. Kama unaenda nao mgahawani na unawa treat vizuri sioni tatizo maana hata wanafamilia si huwa kuna siku mnatoka? Issue ambayo sio fresh ni kuwa treat vibaya na kuwabagua
 
Hapana si ungwana hata kidogo, umenikumbusha Leonard Mambo Mbotela enzi hizo akiwa KBC radio alikuwa anaendesha kipindi cha je huu ni ungwana?????
 
Katika familia yetu ukitoa swala la Mzee Lyamber kua mkali sana sema niliexperience kitu cha tofauti..siku akirudi home na furaha mixa amepata faida alikua kama anatoa hela anawapa nyumba nzima kuanzia bi.mkubwa mpaka dada wa kazi ingawa itifiaki ilikua ikizingatiwa..ukiwa mkubwa unapata hela nyingi...Over..!!
 
kumbe familia iliyofanya hivyo ni ya kiarabu sishangai hata kidogo wana ubaguzi wa hali ya juu watu wa jamii hiyo

Umeona eeh....hata waafrika.wanaoenda kufanya kazi kwao nasikia wananyanyaswa sana sana hivyo sio.ajabu
Ntuzu sio.uungwana kabisa..mimi wa kwangu namtreat kama binti yangu tu kama.mwanafamilia..mtoko kwa wote kula meza moja pamoja nk
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom