Je, huu ni uungwana kweli?

Wapoti Mimi Si km nakupinga ktk Hoja zako! Mimi nitakaa nao meza moja ata kwa kuwalazimisha! Km nikiwa Na mazungumzo Na mke wangu Na tuko kwa mgahawa, watoto wote Na mfanyakazi, nitawatoa Na kuwaweka meza ya karibu pembeni kidogo wale wanywe chochote na mimi ntabaki Na mke wangu tunakumbushia ile siku ya kwanza tulipoonana! Lkn sio Mtu unawaacha wafanyakz kwenye viti vya mapokezi Alafu Wewe Na mke wako ndo mnaingia kwa mgahawa Na hauwanunulii chochote!

Hata mimi nataka wajithamini wanapokuwa kwa watu. wasidhani kuwa kufanya kazi za ndani ni umaskini au shida wajipende waishi kwa kuwaangalia wenyeji wao wajiweke kwenye hadhi ya juu ili mwenye nyumba mwenyewe ajue kwamba wao pia ni binadamu tena wafanye na mabadiliko ya vitu ambavyo haviko sawa kama usafi mapishi kwani wake wengine balaa tu.hata mwenye nyumba atapenda uendelee kuwepo..
 
Last edited by a moderator:
Unakuta mtu ana wafanyakazi wa ndani yani (House girls) wawili na watoto wake. Anatoka nao kwenda kwenye mgahawa kupata chakula na kinywaji kidogo!

Kwanza anapofika ktk mgahawa haongozani na hao wafanyakazi wake! Anatangulia yeye na mke wake na watoto wake wa kuzaa then hao wafanya kz wanakuja wanachungulia chungulia kwa woga na kukaa pembeni umbali wa hatua 30 kutoka meza ya mabwana zao! Na hawaruhusiwi kuagiza chochote mpaka agizo litoke kwa Bwana.

Na wanakaa wametulia na kujalibu kuwatuliza watoto wa Boss wao ambao wanaonekana ni watundu na wanaokimbiakimbia hovyo ktk mgahawa!

Then baada ya hapo Bwana na bibi wanaagiza chakula na kinywaji na kula wao tu peke yao huku wale wafanyakazi wamekaa pembeni tena ktk viti vya wageni ktk mgahawa huku hawatumii chochote!

Je huu ni uungwana kweli kwa mtu anaekutunzia na kukuangalizia watoto wako wakati wewe ukiwa ktk mapilika ya maisha yako? Na hii mpaka nje km kwenye migahawa mtu anaweza kuwafanyia hivi wafanyakazi wake wazi wazi, je huko ktk familia yake majumbani si ndio balaa kabisa?!!

Maana huko inaonekana ni marufuku mfanyakazi kula chakula km anachokula bwana! Bwana km anakula chips kuku, mfanyakazi anakula ugali Dagaa au maharagwe. Boss km anakunywa maji ya kwenye Fridge yaliyopowa basi mfanyakazi anakunywa ya kwenye ndoo! Na huenda ni marufuku kukaa sebuleni kuangalia Tv au kuwasha tv na redio!

Nauliza jee huu ni UUNGWANA KWELI?

Aisifuye mvua ujue imemnyea....kwa namna ulivyoandika hakika nawe ni mtendaji wa huo mtindo.
 
Mheshimiwa Ntuzu, suala la wadada wa kazi linachangamoto sana. Binafsi, sipendi kuwachikulia kama wafanya kazi, ni zaidi ya mfanyakazi.
Mtu anaekuamngalizia watoto na kubaki na dhamana ya nyumba unapokua haupo ni wa muhimu sana.

Tatizo linakuja baadhi yao ukimuweka karibu sana kama, ndugu anakuona mteremko na anaanza vitimbi.
Ukiamua kwenda nae kama mfanyakazi, (yaani hakuna mahusiano zaidi ya yeye kufanya kazi na wewe kumlipa pesa yake) haiwi uungwana.

Kuna rafiki yangu nilienda kwake, yeye dada wa kazi ni marufuku kukaa sebuleni. Big NO. Lakini cha ajabu ndio anampikia chakula, iliniuma sana.

Hitimisho, kama umeamua kuwa na msaidizi, jitahidi siku akiondoka hapo akukumbuke huko atakapoenda katika maisha yake.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kadiri ulivyoelezea huu si uungwana hata chembe, ni aina fulani ya ukandamizaji na muendelezo wa matabaka yasiyo ya lazima.
 
Mkuu Uko sawa ktk hitimisho lako!

Mkuu ata Mimi kuna familia moja hivi rafiki zangu Na wao mfanyakazi ni marufuku kukaa sebuleni au kula chakula cha bosi wao japo wao ndio wanaokipika Na kuaandaa kila kitu!
 
Last edited by a moderator:
Kwa kadiri ulivyoelezea huu si uungwana hata chembe, ni aina fulani ya ukandamizaji na muendelezo wa matabaka yasiyo ya lazima.

Mkuu hichi kitu nimekiona Jumapili tu kwa macho Yangu nilipokua nimeenda kutenbea mitaa Fulani Na kupata chakula cha Mchana!

Ghafla ikaingia familia moja ya kiarabu mume Na mke Na watoto wawili Na mabinti kazi wawili Na yakatokea km nilivyoeleza hapo juu! Watoto wao wenyewe walikua watundu wanakimbia kimbia hovyo mpk watu kwenye mgahawa wanashangaa! Na ukiwatizama hao waarabu ni watu wanaoonekana Kua Na uwezo mkubwa tu! Lkn kwanini wawatreat mabinti kz namna hiyo?

Si uungwana hata kidogo!
 
Aisifuye mvua ujue imemnyea....kwa namna ulivyoandika hakika nawe ni mtendaji wa huo mtindo.

Mke wangu Na watoto wangu Na binti Yangu Wa kz wameondoka Jana kwenda Rikizo Mwanza mpk Bariadi! Na binti Yangu Kwao ni Iringa!
 
Heh!! Hii kali.
Binafsi nikiamua kutoka na familia yangu nazichanga kabisa na tukifika tuendako kila mtu ataagiza atakacho na hakuna atakayeulizwa kwa nini umeagiza hiki.
Kwanza hao wafanyakazi wataagiza nini kikubwa cha kumtoa mtu imani? Hebu tupunguze ubinafsi jamani.
Kama mnataka kula wawili tu si mtoke wawili tu? Kwa nini muwabebe waje kung'atwa na mbu wakiwatazama nyie mlavyo?
Kama unaepuka gharama kubwa basi nendeni hotel zenye gharama nafuu.
Sio uungwana hata kidogo Ntuzu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Uko sawa ktk hitimisho lako!

Mkuu ata Mimi kuna familia moja hivi rafiki zangu Na wao mfanyakazi ni marufuku kukaa sebuleni au kula chakula cha bosi wao japo wao ndio wanaokipika Na kuaandaa kila kitu!

Hapo mfanyakazi akiamua kuongeza sumu kwenye ingredients za chakula ataambiwa ana roho mbaya?
 
Familia yenye mahouse girl wawili kuna haja gani ya kwenda wote mgahawani kula chakula ....kwanini wasipike nyumbani?

hivi kula nje ya nyumbani kwako ni mpaka uwe huwezi kupika nyumbani??!!
 
Mkuu hichi kitu nimekiona Jumapili tu kwa macho Yangu nilipokua nimeenda kutenbea mitaa Fulani Na kupata chakula cha Mchana!

Ghafla ikaingia familia moja ya kiarabu mume Na mke Na watoto wawili Na mabinti kazi wawili Na yakatokea km nilivyoeleza hapo juu! Watoto wao wenyewe walikua watundu wanakimbia kimbia hovyo mpk watu kwenye mgahawa wanashangaa! Na ukiwatizama hao waarabu ni watu wanaoonekana Kua Na uwezo mkubwa tu! Lkn kwanini wawatreat mabinti kz namna hiyo?

Si uungwana hata kidogo!

haya mi nimeyashuhudia mara nyingi tu hasa familia za kihindi na kiarabu.....lakini hawa wahindi na waarabu wanambagua mtu mweusi yoyote je unategemea nini kwa mfanyakazi wao wa ndani!!!
 
haya mi nimeyashuhudia mara nyingi tu hasa familia za kihindi na kiarabu.....lakini hawa wahindi na waarabu wanambagua mtu mweusi yoyote je unategemea nini kwa mfanyakazi wao wa ndani!!!

Mkuu hizi Jamii zinaonekana baguzi sn! Kwanini waarabu Na wahindi wako hivi?
 
Ila kwa sababu maovu yake hayatangazwi siku mfanyakazi akishindwa kuvumilia akaamua kumtanguliza bosi kwa sumu kila mtu atamuona mbaya!

Ni Kweli Ennie Yani sijui tufanyeje kujaribu kuyapunguza haya mambo!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom