Je, huu ni uungwana kweli?

Ntuzu

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
17,424
2,000
Unakuta mtu ana wafanyakazi wa ndani yani (House girls) wawili na watoto wake. Anatoka nao kwenda kwenye mgahawa kupata chakula na kinywaji kidogo!

Kwanza anapofika ktk mgahawa haongozani na hao wafanyakazi wake! Anatangulia yeye na mke wake na watoto wake wa kuzaa then hao wafanya kz wanakuja wanachungulia chungulia kwa woga na kukaa pembeni umbali wa hatua 30 kutoka meza ya mabwana zao! Na hawaruhusiwi kuagiza chochote mpaka agizo litoke kwa Bwana.

Na wanakaa wametulia na kujalibu kuwatuliza watoto wa Boss wao ambao wanaonekana ni watundu na wanaokimbiakimbia hovyo ktk mgahawa!

Then baada ya hapo Bwana na bibi wanaagiza chakula na kinywaji na kula wao tu peke yao huku wale wafanyakazi wamekaa pembeni tena ktk viti vya wageni ktk mgahawa huku hawatumii chochote!

Je huu ni uungwana kweli kwa mtu anaekutunzia na kukuangalizia watoto wako wakati wewe ukiwa ktk mapilika ya maisha yako? Na hii mpaka nje km kwenye migahawa mtu anaweza kuwafanyia hivi wafanyakazi wake wazi wazi, je huko ktk familia yake majumbani si ndio balaa kabisa?!!

Maana huko inaonekana ni marufuku mfanyakazi kula chakula km anachokula bwana! Bwana km anakula chips kuku, mfanyakazi anakula ugali Dagaa au maharagwe. Boss km anakunywa maji ya kwenye Fridge yaliyopowa basi mfanyakazi anakunywa ya kwenye ndoo! Na huenda ni marufuku kukaa sebuleni kuangalia Tv au kuwasha tv na redio!

Nauliza jee huu ni UUNGWANA KWELI?
 
Wapoti

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
2,822
2,000
Unajua mkuu haya mambo yana pande mbili house girl anapothamini kazi yake hata mwajiri atamthamini lakini kuna wengine akiingia kwako tu matumizi utadhani umenunua magari 4 yanayokunywa mafuta hasa kwa uharibifu wa makusudi kukosa uaminifu kazi zenyewe hazifanyiki vizuri. House girl wa namna hii hata mwajiri hatamthamini.lakini kuna wengine huwezi jua kama ni house girl
 
Ntuzu

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
17,424
2,000
Unajua mkuu haya mambo yana pande mbili house girl apothamini kazi yake hata mwajiri atamthamini lakini kuna wengine akiingia kwako tu matumizi utadhani umenunua magari 4 ya cc 22000

Hoja sio ktk matumizi Mkuu! Hoja hapa ni namba gani unaishi Na Hawa watu. Unawapenda km unavyojipenda Wewe? Unawapa haki Vzr?

Wewe ndio unaepanga matumizi ya nyumbani kwako, km sio Wewe basi mkeo! Sasa kwanini matumizi yazidi?
 
Wapoti

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
2,822
2,000
Hoja sio ktk matumizi Mkuu! Hoja hapa ni namba gani unaishi Na Hawa watu. Unawapenda km unavyojipenda Wewe? Unawapa haki Vzr?

Wewe ndio unaepanga matumizi ya nyumbani kwako, km sio Wewe basi mkeo! Sasa kwanini matumizi yazidi?

Matumizi yanazidi kutokana na hasara wanazoleta kwa makusudi. Pia mwingine hajithamini mwenyewe anakaribishwa kwenye chumba cha watoto kitanda shuka na godoro safi lakini haogi mchafu ukimfundisha ni ugomvi tuu. Wangekuwa wanajithamini na kufanya kazi kwa uaminifu wangependwa tu. Mbona wengine wanasomeshwa kabisa
 
Daata

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
4,516
2,000
Familia yenye mahouse girl wawili kuna haja gani ya kwenda wote mgahawani kula chakula ....kwanini wasipike nyumbani?
 
King Octavian

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
403
250
hili jambo kwanza vitendo kama hivyo tunavi group kuwa neno moja UNYANYASAJI hii tabia ni inate au ni kasumba ambayo watu wanazaliwa nayo, na mtu anayemfanyia hivi house girl hata kwa ndugu yake huwa anafanya hivi hivi, ni kama ile kauli ya yesu Mti mbichi na mti mkavu
 
Ntuzu

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
17,424
2,000
Matumizi yanazidi kutokana na hasara wanazoleta kwa makusudi. Pia mwingine hajithamini mwenyewe anakaribishwa kwenye chumba cha watoto kitanda shuka na godoro safi lakini haogi mchafu ukimfundisha ni ugomvi tuu. Wangekuwa wanajithamini na kufanya kazi kwa uaminifu wangependwa tu. Mbona wengine wanasomeshwa kabisa

Bado sikubaliani Na swala lako la matumizi kwasababu mimi au mke wangu ndio tunao panga budget ya nyumbani Na viwango km vile Kg ngapi kwa siku au mlo Mmoja zipikwe! Kwahiyo ktk Hilo sikuelewi!

Swala la usafi ni jukumu la mke kumuelimisha kiustaraabu taratibu mpk ataelewa tu! Huwezi kumuelimisha Mtu kwa kumfokea au kumshambulia hapo utakua unajenga chuki tu!

Alafu ni vema kila Mmoja akawa na sehemu Yake ya kulala ata watoto Wa kuzaa Kwani kila Mmoja awe anawajibika kutunza malazi Yake ata kwa kutandika kitanda tu kulikoni kuwachanganya wote sehemu moja wanakua wanajiachia tu Na lawama anaangushiwa mfanyakazi!

Bado nasimama pale pale tunatakiwa kuishi Na wafanya kz wetu Vzr km watoto wetu kwa kuwaonesha upendo Na kuwajali!
 
Ntuzu

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
17,424
2,000
Familia yenye mahouse girl wawili kuna haja gani ya kwenda wote mgahawani kula chakula ....kwanini wasipike nyumbani?Mkuu Mtu anakwenda nao wote wawili Na hawanunulii chochote kile Yani ata kukaa nao meza moja ni marufuku!
 
Wapoti

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
2,822
2,000
Unajua kila mtu anapanga bajeti na huwezi kuficha kama unaishi na mwizi .pia suala la malazi kila mtu na kitanda chake ila chumba ni kimoja hata ukambembeleza hawaelewi utamnunulia na nguo nzuri na kumpa za kwako nakwambia utazikuta chafu na zimetupwa nje hazithamini. Mimi nahisi wakitaka wathaminiwe wahithamini wao kwanza na wathamini vitu vya waajiri wao mkuu siku ukiishi nao utawajua au kama unayezuri mshukuru mungu na kaa. Nae vizuri
 
Ntuzu

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
17,424
2,000
hili jambo kwanza vitendo kama hivyo tunavi group kuwa neno moja UNYANYASAJI hii tabia ni inate au ni kasumba ambayo watu wanazaliwa nayo, na mtu anayemfanyia hivi house girl hata kwa ndugu yake huwa anafanya hivi hivi, ni kama ile kauli ya yesu Mti mbichi na mti mkavu

Tena ni unyanyasaji mkubwa!
 
SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,255
2,000
Unakuta mtu ana wafanyakazi wa ndani yani (House girls) wawili na watoto wake. Anatoka nao kwenda kwenye mgahawa kupata chakula na kinywaji kidogo!

Kwanza anapofika ktk mgahawa haongozani na hao wafanyakazi wake! Anatangulia yeye na mke wake na watoto wake wa kuzaa then hao wafanya kz wanakuja wanachungulia chungulia kwa woga na kukaa pembeni umbali wa hatua 30 kutoka meza ya mabwana zao! Na hawaruhusiwi kuagiza chochote mpaka agizo litoke kwa Bwana.

Na wanakaa wametulia na kujalibu kuwatuliza watoto wa Boss wao ambao wanaonekana ni watundu na wanaokimbiakimbia hovyo ktk mgahawa!

Then baada ya hapo Bwana na bibi wanaagiza chakula na kinywaji na kula wao tu peke yao huku wale wafanyakazi wamekaa pembeni tena ktk viti vya wageni ktk mgahawa huku hawatumii chochote!

Je huu ni uungwana kweli kwa mtu anaekutunzia na kukuangalizia watoto wako wakati wewe ukiwa ktk mapilika ya maisha yako? Na hii mpaka nje km kwenye migahawa mtu anaweza kuwafanyia hivi wafanyakazi wake wazi wazi, je huko ktk familia yake majumbani si ndio balaa kabisa?!!

Maana huko inaonekana ni marufuku mfanyakazi kula chakula km anachokula bwana! Bwana km anakula chips kuku, mfanyakazi anakula ugali Dagaa au maharagwe. Boss km anakunywa maji ya kwenye Fridge yaliyopowa basi mfanyakazi anakunywa ya kwenye ndoo! Na huenda ni marufuku kukaa sebuleni kuangalia Tv au kuwasha tv na redio!

Nauliza jee huu ni UUNGWANA KWELI?
Hii thread ni purely mahusiano.Tafadhali Active, ihamishie mmu.
 
Last edited by a moderator:

Tized

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
4,025
2,000
Mkuu Ntuzu nakushukuru sana kwa kuliona hili. Binafsi yangu huwa namna yoyote ya ubaguzi isipokuwa ya mdogo kumbagua mkubwa huwa inaniumiza sana kaka.

Najiulizaga HIVI UKIKAA VIZURI NA MHUDUMU WAKO/DEREVA WAKO AU NA WALE WASIO NA UWEZO, UTAPUNGUKIWA NA NINI kwani ukimjali si ndio ndio atakujali wewe na wanao? si ndio atakuletea baraka na furaha zaidi? si atajitahidi kila siku kufanya mema kuwapendezesha?

Umenikumbusha kisa flani kiliwatokea jamaa zangu, walikua wanaendeshwa na dereva wao, then wakaenda mahali wakala nyama za kutosha, dereva walimuacha tu kwenye gari.. walioporejea kwa gari dereva akendesha gari hadi kwenye matope mengi, akakorofisha kitu akawaambia gari haiendi tena inabidi hao jamaa wasukume angalao liwake.. yaani jamaa walihangaishwa hadi ile nyama waliokula ikawatokea puani.

Tena unakuta ni vitu vidogo sana lakini vinawauma watu roho vibaya sana.

FURAHA YETU IPO KWENYE VILE TUNAVYOTOA KWA WENGINE NA TUNAVYOJITOA KWA WENGINE.
 
Last edited by a moderator:

Ntuzu

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
17,424
2,000
Unajua kila mtu anapanga bajeti na huwezi kuficha kama unaishi na mwizi .pia suala la malazi kila mtu na kitanda chake ila chumba ni kimoja hata ukambembeleza hawaelewi utamnunulia na nguo nzuri na kumpa za kwako nakwambia utazikuta chafu na zimetupwa nje hazithamini. Mimi nahisi wakitaka wathaminiwe wahithamini wao kwanza na wathamini vitu vya waajiri wao mkuu siku ukiishi nao utawajua au kama unayezuri mshukuru mungu na kaa. Nae vizuri

Mkuu Mimi naishi Na binti Wa kz, Lkn jinsi ninavyoishi nae km mtoto wng! Yani ata kwenda Kwao hataki! Anakwenda kusalimia tu nakurudi! Ukija kwangu Huwezi fahamu km Huyu ni binti Wa kz!

Mkuu sikupingi swala la usafi Lkn anapaswa kufundishwa taratibu Na kwa kauli nzuri mpk ataelewa! Tusione Kua unakaa nae Na labda unamlipa basi kila unalomuelekeza unamuelekeza kwa ukorofi, kufoka n.k. Sio Vzr!
 
Wapoti

JF-Expert Member
Aug 28, 2013
2,822
2,000
Mkuu Mtu anakwenda nao wote wawili Na hawanunulii chochote kile Yani ata kukaa nao meza moja ni marufuku!

Hilo la kutowanunulia chochote ni kosa kubwa sana lakini kutokaa nao meza moja ni sawa labda wasichana wenyewe haeajithamini kujiona kama binadamu
 
Ntuzu

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
17,424
2,000
Mkuu Ntuzu nakushukuru sana kwa kuliona hili. Binafsi yangu huwa namna yoyote ya ubaguzi isipokuwa ya mdogo kumbagua mkubwa huwa inaniumiza sana kaka.

Najiulizaga HIVI UKIKAA VIZURI NA MHUDUMU WAKO/DEREVA WAKO AU NA WALE WASIO NA UWEZO, UTAPUNGUKIWA NA NINI kwani ukimjali si ndio ndio atakujali wewe na wanao? si ndio atakuletea baraka na furaha zaidi? si atajitahidi kila siku kufanya mema kuwapendezesha?

Umenikumbusha kisa flani kiliwatokea jamaa zangu, walikua wanaendeshwa na dereva wao, then wakaenda mahali wakala nyama za kutosha, dereva walimuacha tu kwenye gari.. walioporejea kwa gari dereva akendesha gari hadi kwenye matope mengi, akakorofisha kitu akawaambia gari haiendi tena inabidi hao jamaa wasukume angalao liwake.. yaani jamaa walihangaishwa hadi ile nyama waliokula ikawatokea puani.

Tena unakuta ni vitu vidogo sana lakini vinawauma watu roho vibaya sana.

FURAHA YETU IPO KWENYE VILE TUNAVYOTOA KWA WENGINE NA TUNAVYOJITOA KWA WENGINE.

Mkuu Tized nashukuru sn kwa Hoja yako! Tena umetanua mada mpk kwa madreva! Ni Kweli Mkuu mdreva Na wao wanapata shida sn! Unakuta wanawapeka maboss zao ktk mambo Yao binafsi wanabaki kulala Na kusinzia kwenye Gari weeee huku boss akijilewea mipombe Na vimada au akifanya michepuko Na bila kuja Driver amekula au amekunywa chochote Na wakati huo huo Hawa madriver ndio wanaotunza siri nyingi za maboss wao!

Si uungwana ata kidogo!
 
Last edited by a moderator:

Suprise

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
2,697
1,195
na hapo wamewabeba ili wawasaidie kubeba watoto wao maana ingekua amri yao wangewaacha home wawe walinzi
 
Ntuzu

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
17,424
2,000
Hilo la kutowanunulia chochote ni kosa kubwa sana lakini kutokaa nao meza moja ni sawa labda wasichana wenyewe haeajithamini kujiona kama binadamu

Wapoti Mimi Si km nakupinga ktk Hoja zako! Mimi nitakaa nao meza moja ata kwa kuwalazimisha! Km nikiwa Na mazungumzo Na mke wangu Na tuko kwa mgahawa, watoto wote Na mfanyakazi, nitawatoa Na kuwaweka meza ya karibu pembeni kidogo wale wanywe chochote na mimi ntabaki Na mke wangu tunakumbushia ile siku ya kwanza tulipoonana! Lkn sio Mtu unawaacha wafanyakz kwenye viti vya mapokezi Alafu Wewe Na mke wako ndo mnaingia kwa mgahawa Na hauwanunulii chochote!
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom