Je huu ni utapeli kwa hisani ya Serikali?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,154
TCRA, BENKI KUU na idara zingine zinazohusika.

Huu ni utapeli kwa hisani ya serikali kwasababu hawa watu wana vibali vya huduma hii toka BENKI KUU na idara zingine husika.

Ukikopa wakati wa marejesho utaona pesa imekatwa VAT kama kawaida kuthibitisha kuwa serikali ndiyo iliyobariki uhuni huu.

Mkopo wa ndani ya siku 5 inakuwaje uwe na riba kubwa kiasi hichi?

Sijacalculate vizuri lakini naona ni kama 70% hivi.

Je, serikali inawasaliti wananchi kwa vipande vya fedha?

Najua wajinga watasema ni nani kakulazimisha kukopa. Issue sio kukopa issue ni pale serikali inapobariki haramu kiasi hichi.

Kulingana na picha hapo chini mkopo huu ni wa siku 6 lakini uhalisia ni siku 5 tu.

Yaani siku ya tano au siku moja kabla ya tarehe ya makusanyo unapigiwa simu asubuhi mapema kuwa tayari unapaswa kurudisha fedha.

Hapo ndipo ugomvi hutokea kati ya mdai na mdaiwa na mwisho wa siku unaaibishwa.

Serikali hii ndio inawataka Watanzania wawe wazalendo?
Watanzania wana hali ngumu kila sekta.

Labda suala la amani pekee labda.

Screenshot_20240316-185731.jpg
Screenshot_20240316-185842.jpg
 
Mkuu katika biashara ya fedha kila taasisi huwa na vigezo na masharti yake ambayo mkopaji hupaswa kuyaelewa kwa kina. Pindi uyasomapo na kuyaelewa vyema, una hiyari ya kuyakubali ama kuyakataa, kabla ya kufanya uamuzi wa kujifunga rasmi na mkataba

Sasa kama uliuridhia mkataba, na pia ulinufaika na fedha, huna namna zaidi ya kulipa deni lako lote mpaka ulimalize. Kuuanza kuelekeza lawama kwa taasisi ya kifedha iliyokukopesha, na kutafuta visingizio visivyokuwa na mashiko, si jambo la kiungwana hata kidogo!
 
Kwahiyo ukimtapeli mtu si kosa kwakuwa alikubali mwenyewe?

Wizi na unyang'anyi ni tofauti na utapeli.

Utapeli lazima watu wawili au zaidi wafikie muafaka.
Mkuu katika biashara ya fedha kila taasisi huwa na vigezo na masharti yake ambayo mkopaji huyaridhia. Uyasomapo na kuyaelewa vyema, una hiyari ya kuyakubali ama kuyakataa kabla ya kujifunga na mkataba...
 
Acha mambo ya kukopa ni utapeli
Hapana mkuu kuna wakati vitu lazima Serikali kupitia mamlaka husika iingilie na kuregulate. Malalamishi ya mleta mada ni sahihi. Nchi tajiri kama Norway Serikali na bunge mwaka juzi ilibidi iingilie kati kusaidia wananchi kupitia hizi online quick loans. Kwasababu riba ni kubwa na terms zao confusing. Mteja anapohitaji mkopo yupo desperate muda wa kusoma terms na condition hana ni confirm tu.

Bora betting na gambling kuliko hawa wahuni wa mikopo online.
 
Sijawahi kukopa mtaani ila kwa uhalisia riba zosizo na mrengo wa kumsaidia mtu ni chanzo cha taifa kupoteza kodi nyingi kwa kuwa anayekopeshwa akifeli kulipa akapoteza mali zake vilevile maana yake biashara imekufa na kodi na ushuri navyo vimepotea kwa serikali.

Umaskini hautaondoshwa haraka bila serikali kuwa na mikakati ya kuingilia vitu kama hivi
 
acha kupiga mayowe yaani kuanzia uk hadi poland wana mkoloni wao USA wewe ni nani usiwe chini ya mkoloni tanzania hii jipige kifua halafu sema mimi mtumwa ndani ya taifa langu over.
 
Hapana mkuu kuna wakati vitu lazima Serikali kupitia mamlaka husika iingilie na kuregulate. Malalamishi ya mleta mada ni sahihi. Nchi tajiri kama Norway Serikali na bunge mwaka juzi ilibidi iingilie kati kusaidia wananchi kupitia hizi online quick loans. Kwasababu riba ni kubwa na terms zao confusing. Mteja anapohitaji mkopo yupo desperate muda wa kusoma terms na condition hana ni confirm tu.

Bora betting na gambling kuliko hawa wahuni wa mikopo online.
Hawa wakopeshaji wanatumia mwanya ulioachwa wazi na uzembe/kutowajibika kwa serikali. Kama serikali ingejenga mazingira bora ya ukopaji kupitia mabenki, hakuna mtu angeenda kukopa kwa watu binafsi.

Kwahiyo ni makosa kuwalaumu. Kama huridhishwi na huduma zao ni vema ukaenda benki.
 
Hapana mkuu kuna wakati vitu lazima Serikali kupitia mamlaka husika iingilie na kuregulate. Malalamishi ya mleta mada ni sahihi. Nchi tajiri kama Norway Serikali na bunge mwaka juzi ilibidi iingilie kati kusaidia wananchi kupitia hizi online quick loans. Kwasababu riba ni kubwa na terms zao confusing. Mteja anapohitaji mkopo yupo desperate muda wa kusoma terms na condition hana ni confirm tu.

Bora betting na gambling kuliko hawa wahuni wa mikopo online.
Mifumo ya bank yote ndio yale yale,mifumo tunayotumia yote ni ya riba ,utawezaje kuzuia😂😂.Makali ya mikopo hao wa online na banks ni yale yale.

sasa hivi hata mitandao ya simu wanakopesha bundle ni hatari yaani ,watu wanajali faida si wateja wao.

Ukielewa michezo ya banks zote ni kandamizi ili mradi wapige pesa ,wao kazi kutangaza faida ila watu wanaumia .

Chukulia mfano wakopaji ni walimu mpaka wanazeeka wanakuwa na deni
 
Back
Top Bottom