Wewe una utaalamu gani wa Management? Au ni wataalamu gani hao.Kwenye theory ipi ya management? Unaona sasa....
Hicho kitabu "In Search of Excellence ,A lesson From Americas Best-Run Companies" Cha Robert Waterman na Tom kiliandikwa karibia miongo mitatu iliyopita,1980s.
Nimekisoma na wewe ni aidha hujakisoma au umekisoma hujakielewa.
Yeye Mwenyewe alisema System and structures are the only tools for organizational Change. Acha uongo kisome tena au kama huna nakala nikuazime ukisome tena.Hakuna anachofanya Magufuli kinachofanana na hicho au anafanya in a twisted way
Nirudi kwenye mada sasa,
Mkuu
Pasco,
Jana niliwaambia kwenye ule uzi waliokuja nao kwa Mbwembwe wakasema nina wivu ninamkejeli Rais
Hakuna Leadership Style ya Namna hii iliyowahi kufanikiwa Duniani
Hata Kim Jong-Un wa Korea ya Kaskazini anafanya vizuri zaidi ya hivi anavyofanya
Rais anafanya kazi ya Meneja wa uwanja wa Ndege au Security Manager
Tunahitaji atengeneze Chain of accountability.Ndio mfumo wa kitaasisi
Anavyofanya hivi akiwa hayupo watu wataanza kumtafuta Magufuli mwingine
Cha ajabu kuna wasomi(Sijui kama ni wasomi wenye viwango vya ukwelikweli) wanashabikia kama mazuzu.Hawana tofauti na wale walioenda Loliondo na wale walioliwa kwenye Upatu wa DECI
Rais anatangaza kutoa amri ya kuzuia kuagiza sukari wanashangilia "weweeee ...wewe ndio Jembe letu.Hakuna kama wewe.Yaani weee ndio Sokoine uliyefufuka"
Baada ya Mwezi Sukari hakuna au iliyopo inauzwa 3000-4000 .Wanakaa kimya
Rais anatoa Tamko kuwa "tutaagiza sukari Tani 70,000 kutoka nje .
Watu walewale wanashangilia weweeee.Wewe ndio mkombozi wetu,Wewe ni mchapakazi .Kweli nchi ilikua imeoza sasa unawanyoosha.Wewe huna tofauti na Nyerere"
Hawa ndio watakaokushambulia katika huu uzi
Kuna ule utafiti wa Nottingham University kuwa tu vinara wa unafiki Duniani bado unaendeleea kudhihirika
Kuna ule wa PEW Research kuwa Tunaongoza kwa kuamini katika Miujiza,Ushirikina duniani.Siwezi kuupinga maana hata hapa tunaamini katika Muujiza wa Magufuli kama Magufuli kushinda hata muujiza ambao ungeletwa na Rasimu ya Katiba ya Warioba au hata chain of accountability ambayo ingejengwa.Tunaamini muujiza wa Rais kuwa kila mahali kufanya kila shughuli
Kwa fikra na imani hizi kwanini tusichanjwe chale kwa waganga wa kienyeji au kutapeliwa makanisani.Kwanini tusifurike Loliondo na kuachana na tabibu za kisayansi mahospitalini(Hata Magufuli aliamini na akapata uzoefu kule na anapita njia ile ile ya Babu kwa kuwa watanzania ni wale wale walofurika kwa babu),Kwa nini DECI wasivune fedha nyingi kwetu ?
Nyerere alisema adui mkubwa kwetu ni ujinga.Ukimshinda tu umeshinda umaskini,Maradhi na hata ufisadi maana maadili yatakuwepo na uwezo wa kuwajibishana utakuwepo kwa kuwa hata ethics and principles of good governance zitakuwepo.
Ukute Rais kafanya tukio lile kupotezea sekeseke aliloliunda mwenyewe la Sukari na sakata la Lugumi. Kama kawaida watu wapo "Weweee huyu ndio Jembe,Hakuna kama wewe.UKAWA sidhani kama wangeweza hivi"
Halafu Sukari ni 3000 ,Asubuhi kama ya Leo wanaamka alfajiri zaidi ili kuikwepa familia na kujifanya kuwahi kwenye shughuli.