Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga, Kutasaidia?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,669
119,300
Wanabodi,

Naendelea na zile mada zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", zikijikita kwenye uzalendo Kwa taifa Letu huku nikisisitiza ukweli na uwazi, ( truthfulness and transparency)
ukiwa mkweli na muwazi,
, ukweli utakuweka huru!. Hili ni swali, "Jee hizi terorizing ziara za kushtukiza, hakutajenga nidhamu ya woga?!. Jee, kutasaidia?!.

Hiki nilichokishuhudia leo Eapoti jamani sio!. Tufike mahali watu wanaommudu, wamshauri, that is not the right way.

Leo nimemshuhudia kwenye kipindi maalum cha TV jinsi Ngosha anavyoterorize wale maofisa pale Eapoti, tangu lini kwenye arrival abiria wanapita kwenye scanner?!, akashauri eti kwa nini hao abiria wasizungukie kule kwenye scanner za depature ndipo waingie nchini!, kiukweli watu wenye akili zao, wanaanza kumuona huyu jamaa kama sio!, kiukweli ile ni terorising tuu!, nitamshauri yule Mama Makamu, amsaidie Bosi wake, na huyu Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya mawasiliano, vitu vingine viishie kwenye habari tuu na sio kuviingiza kwenye kipindi maalum wakidhani wanamjenga kumbe ndio kwanza wana mdhalilisha bure kwa kumuaibisha kwa waelewa!. Lakini na sisi jamaa zenu wa Kanda ile tunavyopenda masifa mbele ya kamera!, kiukweli huu ushamba wetu sometimes unachekesha!.

Nasisitiza naunga mkono tumbua tumbua na kinachofanyika kuisafisha nchi yetu na serikali yetu kwa madudu yaliyokithiri, the man is doing the right thing but sometimes in a wrong way!.

Every human being deserves to have dignity!. Pamoja na yote jamani, ka human dignity japo kadogo, kawepo!, na sio huu udhalilishaji mbele ya kadamnasi ya watu zikiwemo kamera za TV, halafu wanarusha kwenye kipindi maalum!. Please wajemeni!.

Hata hivyo, leo namshukuru sana Mzee wa Tumbua Tumbua, japo kashtukiza lakini leo hakutumbua zile za papo kwa papo, labda sauti zetu zinaanza kusikika and to make sense, ila hizi ziara za kushtukiza zinaweza kusababisha nidhamu ya woga na kujikombakomba, mnaweza kushuhudia utumbuaji majipu ukifuatia ziara hii pale Eapoti leo Jumamosi, au siku ya Jumatatu, kisa jamaa kapita pale kashuhudia na kadanganywa!.

Tanzania inachohitaji sasa sio a one man show, na movie za ze comedy!, tunahitaji kujenga mifumo, systems, kama hakuna scanner kwenye arrival zote duniani, bali kuna declaration forms, kila mzigo unaofikia arrival ulikuwa scanned kule ulikotoka na ukawa cleared ni majangili mataahira tuu ndio wataua tembo wetu kisha wabebe pembe za ndovu na kuingia nazo kupitia arrival! wakati mipaka yetu yote ni very porous!. Vitalu vyote vya uwindani vina private air strips midege inaingia na kutua na kujichukulia chochote na kuishia zao juu kwa juu, kwa kisingizio ni vitalu vya uwindaji!, ni kichaa tuu mwenye uwezo wa kutua porini kubeba nyara na kuja nazo arrival!.

Kila ndege kabla haijaingia Tanzania lazima ipate clearance toka TCAA, tuweke watu kwenye every private air stripe na kujenga mfumo toka TCAA kuwa hakuna ndege itakuwa cleared kutua kwenye shamba la bibi, bila bibi kutuma mjukuu ashuhudie hiyo ndege imeleta nini, na hakuna clearance kupaa hadi mjukuu athibitishe imebeba nini!.

Kiukweli hii ya leo kwangu ilikuwa Ze Comedy!, hatuwezi kwenda hivi jamani!.

Namalizia kwa lile swali la msingi, "Jee Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga, Kutasaidia?!".

Nawatakia Jumamosi Njema.

Paskali
 
Wewe unaita Ze comedy lakini wataalam wa masuala ya Management watakiona kinachofanyika ni serious stuff.

Kinachofanywa na Rais Mgufuli wataalam wa masuala ya management wanaita management by wandering around ambayo mwasisi wake alikuwa Rais wa America, Abraham Lincoln wakati wa American civil war.

Tofauti yake ni kuwa, hii style ya management ilifanywa na Rais Abraham Lincoln wakati Marekani ikiwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati Tanzania tuko kwenye vita dhidi ya ufisadi, uvivu, wezi, rushwa na ubadhilifu wa mali za umma.

Kwa msaada zaidi kama hufahamu maana ya Management by wandering around unaweza kusoma kitabu kinachoitwa, In Search of Excellence: Lessons From America's Best-Run Companies kilichoandikwa na wataalam wa masuala ya management ambao wanaitwa Tom Peters na Robert H. Waterman.

Haishangazi kusoma hoja kama hizi kwa sababu kuna wengine pia walipoambiwa dunia ni oblate spheroid walicheka na kusema hiyo ni Ze comedy.

Kuna wengine walipoambiwa unaweza ukaiba wanyama twiga wazima Tanzania na kuwasafirisha nje ya nchi kupitia kwenye uwanja wa ndege wa kimataifaTanzania, walicheka na kusema hiyo ni the comedy.

Kinachofanywa na Rais Magufuli ni kugawa shock therapy kwenye management na watazamaji kama huyu mleta mada ambao kwa mabandiko yao wanaonekana hawakuwahi kushuhudia style ya management by wandering around.
 
Ni afadhali kuwa na nidhamu ya woga kuliko kukosa nidhamu kabisa.

Go Magufuli.

Naam dadangu, aidha watu wana nidhamu au hawana. Na hakuna kitu kama "nidhamu ya woga". Ukiwa mtumishi wa umma ni lazima uogope; uogope kuvunja sheria, uogope kutumia madaraka yako vibaya, uogope kukutwa unavuruga! Unatakiwa utende kazi kwa kujiamini, kwa weledi na kwa ufanisi unaotakiwa kutokana na nafasi yako. Sasa bosi wako akitokea na kukuta umekunja nne ukaruka juu na kujimwagia chai na kuanza kujifanya unafanya kazi manake ni kuwa hukuwa mwoga in the first place! Ungekuwa unaogopa ungekuwa huna wasiwasi. Hivyo, woga wa kinidhamu unahitajika na viongozi waendelee kuwashtukiza na kuwatumbua hasa kama watumishi hawawaogopi mabosi wao au viongozi wao wajuu.

Tulidekezwa mno hadi tukadeka na kuamini tunatakiwa kudekezwa.
 
Ni afadhali kuwa na nidhamu ya woga kuliko kukosa nidhamu kabisa.

Go Magufuli.
Ni afadhali kukosa nidhamu kuliko nidhamu ya woga. Nidhamu ya woga ni sawa na unafiki, lakini kwa vile watanzania wote ni wanafiki heri yako wewe ume declare kuwa bora kuwa mnafiki. Taifa la wanafiki haliendelei hata siku moja, tutapiga mark time miaka mitano.

Mfano siku ile Wilson Kabwe anatumbuliwa nikajua mikataba yote ya makusanyo ya mapato kwenye vyanzo vikuu kama stendi na masoko ya nchi nzima vitaangaliwa na kuwatumbua wengine. Cha ajabu utumbuaji uliishia pale kwa vile ulimlenga mtu na sio mfumo.

Ili kumsaidia raisi wetu tumpatie ushauri mzuri, yeye ni mkubwa sana kuhojiana na mkaguzi wa airport, angeangalia kazi inafanyikaje anaenda kujadiliana na waziri wake na mkuu wa airport anaelezwa procedure na kushauri njia bora. Yaani tuanze tena kukaguliwa mizigo yetu tukifika tunakoenda kwa ajili ya kumfurahisha mtu mmoja JPM. Ama kweli upele umepata mkunaji
 
Wewe unaita Ze comedy lakini wataalam wa masuala ya Management watakiona kinachofanyika ni serious stuff.

Wataalam wa masuala ya management wanaita management by wandering around ambayo mwasisi wake ni Abraham Lincoln wakati wa American civil war.

Kwa msaada zaidi kama hufahamu maana ya Management by wandering around unaweza kusoma kitabu kinachoitwa, In Search of Excellence: Lessons From America's Best-Run Companies kilichoandikwa na wataalam wa masuala ya management ambao wanaitwa Tom Peters na Robert H. Waterman.
Dah umenichekesha sana mkuu!! Kwa huyo huyu jamaa ni supervisor au manager na sio President...

Wazungu hawakuwa wajinga kuweka manager, then mkurugenzi, then vice president na hata senior vice president na mwishoooooooooooni anakuwepo president. Leo hii unamtaka mzee wangu wa Chato John Makufuli kuWANDA Tanzania nzima, kilomita za mraba 945,000 ili kuongoza nchi!!!! Ama kweli watanzania tumerogwa. Kama hata wewe uko nafasi ya 15 chini katika washauri wa raisi basi tumekwisha. Kwa upeo wako huu mdogo inatakiwa uwe nafasi ya mia huko chini ushauriane na wafagiaji wenzako
 
Maajabu ya Mussa....kwa nini asingempigia katibu Mkuu au waziri badala ya kuongea na junior staff tena kwenye makamera?mawaziri wake wanajisikiaje? Hoja ya lissu ya instrument za mawaziri inapata nguvu,hoja ya lissu kwamba nchi inaongozwa na mtu mmoja kama Mali yake binafsi inapata nguvu
 
Naam dadangu, aidha watu wana nidhamu au hawana. Na hakuna kitu kama "nidhamu ya woga". Ukiwa mtumishi wa umma ni lazima uogope; uogope kuvunja sheria, uogope kutumia madaraka yako vibaya, uogope kukutwa unavuruga! Unatakiwa utende kazi kwa kujiamini, kwa weledi na kwa ufanisi unaotakiwa kutokana na nafasi yako. Sasa bosi wako akitokea na kukuta umekunja nne ukaruka juu na kujimwagia chai na kuanza kujifanya unafanya kazi manake ni kuwa hukuwa mwoga in the first place! Ungekuwa unaogopa ungekuwa huna wasiwasi. Hivyo, woga wa kinidhamu unahitajika na viongozi waendelee kuwashtukiza na kuwatumbua hasa kama watumishi hawawaogopi mabosi wao au viongozi wao wajuu.

Tulidekezwa mno hadi tukadeka na kuamini tunatakiwa kudekezwa.
Hovyo kabisa
 
Kwani akiwa Rais anakatazwa kushughulikia mambo yaliyoko chini kabisa; au hata Katiba hamuisomi?
 
Naam dadangu, aidha watu wana nidhamu au hawana. Na hakuna kitu kama "nidhamu ya woga". Ukiwa mtumishi wa umma ni lazima uogope; uogope kuvunja sheria, uogope kutumia madaraka yako vibaya, uogope kukutwa unavuruga! Unatakiwa utende kazi kwa kujiamini, kwa weledi na kwa ufanisi unaotakiwa kutokana na nafasi yako. Sasa bosi wako akitokea na kukuta umekunja nne ukaruka juu na kujimwagia chai na kuanza kujifanya unafanya kazi manake ni kuwa hukuwa mwoga in the first place! Ungekuwa unaogopa ungekuwa huna wasiwasi. Hivyo, woga wa kinidhamu unahitajika na viongozi waendelee kuwashtukiza na kuwatumbua hasa kama watumishi hawawaogopi mabosi wao au viongozi wao wajuu.

Tulidekezwa mno hadi tukadeka na kuamini tunatakiwa kudekezwa.
Braza achana na haya mambo jilindie heshima yako kidogo uliyobakia nayo kwa kukaa kimya kwa vile tunajua huwezi kumkosoa Magufuli, unafukuzia ukuu wa wilaya.

Kwa kulinda heshima usingekubaliana na kitu inaitwa nidhamu ya woga. Heri ukose nidhamu kwa vile utafukuzwa kazi na atawekwa mtu mwingine kazi ikafanyika kuliko kuwa na nidhamu ya woga ukakiuka maadili ya kazi yako kumfurahisha boss kuwa YES SIR tutatunga utaratibu mpya wa kumfurahisha raisi Magufuli na kuweka civil aviation protocals mpya za kukagua mizigo kwa arrivals. Tena braza ulikuwa unakaa Houston, Texas!!! Ama kweli njaa ni mbaya.

Jamani watanzania tusiwafuate hawa waganga njaa, nidhamu ya woga haitakiwi kokote. Inatakiwa nidhamu kamili na kufuata SOPs za kazi husika. Kama hakuna SOPs ndio wakati huu Magufuli atusaidie kuweka kuwe na objectivity kwenye kila idara ya serikali
 
Ni afadhali kukosa nidhamu kuliko nidhamu ya woga. Nidhamu ya woga ni sawa na unafiki, lakini kwa vile watanzania wote ni wanafiki heri yako wewe ume declare kuwa bora kuwa mnafiki. Taifa la wanafiki haliendelei hata siku moja, tutapiga mark time miaka mitano.

Mfano siku ile Wilson Kabwe anatumbuliwa nikajua mikataba yote ya makusanyo ya mapato kwenye vyanzo vikuu kama stendi na masoko ya nchi nzima vitaangaliwa na kuwatumbua wengine. Cha ajabu utumbuaji uliishia pale kwa vile ulimlenga mtu na sio mfumo.

Ili kumsaidia raisi wetu tumpatie ushauri mzuri, yeye ni mkubwa sana kuhojiana na mkaguzi wa airport, angeangalia kazi inafanyikaje anaenda kujadiliana na waziri wake na mkuu wa airport anaelezwa procedure na kushauri njia bora. Yaani tuanze tena kukaguliwa mizigo yetu tukifika tunakoenda kwa ajili ya kumfurahisha mtu mmoja JPM. Ama kweli upele umepata mkunaji
Soma historia ya Rais Abraham Lincoln!

Nimetoa mfano wa Rais Abraham Lincoln kwa sababu wakati anafanya kazi katika style ya management by wandering alikuwa ni Rais wa Marekani.

Kikubwa zaidi, Kwani anachokifanya Rais Magufuli ni nje ya mipaka yake ya kazi? Au mnajaribu kumpangia mipaka ya kazi nje ya Katiba ya Tanzania.
 
Kwa hiyo ni afadhali ukose huduma hospitalini (mfano) kwa sababu kuna mkubwa mmoja ameamua kuuza dawa kwa kuwa haogopi?
Ukikosa nidhamu unafukuzwa kazi anawekwa mtu mwingine mwenye nidhamu kazi inaenda. Ni kitu rahisi, nidhamu ya woga ni yule nesi anayenyenyekea wakati yuko na boss wake halafu boss akiondoka anapiga vibao wajawazito. Hatutaki nchi ya namna hii, tunataka nchi ya watu wenye nidhamu ya kumwambia Magufuli kuwa hata ukienda JFK airport mizigo ya arrivals haipiti kwenye ukaguzi tena kwa vile ilikaguliwa ilikopita unless iwe imetiliwa mashaka. Na jibu la namna hiyo anatoa mkurugenzi wa shirika au taasisi husika na sio ATTENDANT kama yule aliyekuwa anahojiwa na JPM. Mtu mwingine anaweza kuwa na furaha isiyo na kifani kukutana uso kwa uso na mkuu wa nchi akajibu maswali kwa ufasaha na mwingine anaweza kutetemeka akashindwa kuongea au akaongea kumfurahisha mkuu. Suluhisho ni raisi kupita na kuangalia systems and procedures akikuta kuna shida anawaita wahusika anatumbua au anaunda timu ya uchunguzi
 
Soma historia ya Abraham Lincoln!

Nimetoa mfano wa Abraham Lincoln kwa sababu wakati anafanya management by wondering alikuwa ni Rais.

Kikubwa kabisa, Kwani anachokifanya Rais Magufuli ni nje ya mipaka yake ya kazi? Au mnajaribu kumpangia mipaka ya kazi nje ya Katiba ya Tanzania.
Naijua historia ya Abraham Lincoln na sijaona popote alipozunguka marekani nzima kukagua kazi. Lincoln anasifika leo hii Marekani nzima kwa vile aliweka mifumo na misingi imara ambayo ilipelekea hadi kufanyika THE SECOND AMENDMENT ambayo Leo hii baadaye sana watu wa Marekani wanafaidi matunda. Kila sehemu kuna systems, procedures na regulator. Mfano mzuri wana vyombo kama NTSB, hata ukiingizi guta lako barabarani likaua watu hawasubiri Obama atoe amri, kesho yake watu wanaingia kazini
 
Hujaona Rais Abraham Lincoln anazunguka wapi wakati nimekupa aina ya utendaji wake wa kazi ambao mpaka leo Taifa la Marekani linamkumbuka.

Tatizo lenu mnataka Tanzania ya leo iwe kama Marekani ya leo bila kufahamu kuwa hata Marekani ya 1860 ilikuwa kama Tanzania ya leo ndiyo maana watu kama Rais Abraham Lincoln wakaja na aina ya utawala ambao ulijenga misingi ambayo umeifanya Marekani kuwa Taifa lenye nguvu kiuchumi na kisiasa.

Sisi tunataka Rais Magufuli afanye kama anavyofanya Rais Obama wakati taasisi zetu ni kama za Marekani ya miaka ya 1860 iliyokuwa chini ya Rais Abraham Lincoln.
 
Kama umenielewa nimesema nataka raisi Magufuli aweke misingi ambayo hata akikaa ofisini au yuko nyumbani na mama yetu Janet, huku chini kila mtu anatimiza wajibu. Asiye timiza wajibu na mwenye nidhamu ya woga anatumbuliwa huko huko na mkubwa wake. Hii itamsaidia sana raisi na misingi hii iko kwenye katiba ya Warioba
 
Back
Top Bottom