kama tatizo ni mila za kiafrika, mwanaume hawezi kulala kwenye nyumba inayomilikiwa na mwanamke, nenda kakope, mrudishie hela zake, badilisha jina la hati na gharama zote za ujenzi utoe wewe. otherwise na wewe tafuta kiwanja chako ujenge.
siku hizi it doesn't matter kama me au ke ndio mwenye uwezo. kinachotakiwa ni kuaminiana, kuongea na kupanga kwa pamoja. trust me, maisha yana vipindi tofauti, kuna wakati wewe utakuwa nazo nyingi, na kuna wakati yeye pia atakuwa nazo kuliko wewe. kama mke humuamini, kwa nini ulimuoa? kama huamini wanaotoka mlimani, kwa nini hukuoa kijijini kwenu?
nyie wanaume mnatakiwa muelewe kwamba nyakati hizi wanawake wana uwezo wa kipesa kama nyie, wana opportunities nyingi za kutengeneza pesa/ kupata ajira nzuri kama nyie. shule wote tunaenda na degree wote tunapata, sometimes kwa grades nzuri kuliko zenu.
so kuna mawili, tafuteni wake ambao hawana uwezo wa kipesa kabisa ili wawe wanawategemea kwa kila kitu na nyie muwe na amani ya moyo, au jifunzeni kuishi na wake zenu wanaoweza kuingiza kipato kama nyie