Je, hii ndio asili ya mtu mweusi?

Je, hii ndio asili ya mtu mweusi?

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
24,237
Reaction score
39,807
Habari za asbuhi great thinkers.

Moja kwa moja niende kwenye topic kuhusu nilichotafiti kwangu binafsi kwa kuconnect dots ya source mbalimbali nilizosoma naweza conclude kwamba weusi wetu ulitokea kwa CAIN kwa kupita binti yake EGYPTUS au Neitamuk kisumeria aliyeolewa na Baba wa waafrika HAM

Biblia inaeleza kwamba Cain aliwekewa ALAMA

Mwanzo 3
15 BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.

Ingawa biblia haijaeleza hiyo alama ina maana gani ila nikakusanya dots kwenye kitabu cha jasher

Jasher 2:26-30

27 And Tubal Cain told his father to draw his bow, and with the arrows he smote Cain, who was yet far off, and he slew him, for he appeared to them to be an animal.

Huu mstari ulinifanya niamini kwamba huenda alama aliyowekewa ilimfanya Cain awe mweusi ambapo kwa kuwa rangi hiyo haikuwa imezoeleka wakahisi mnyama ndio maana wakamuua

NB: Wengine mtasema book of jasher hakipo kwenye biblia hivyo sio reliable.... Ushahidi wa kwamba lamech alimuua Cain upo pia kwenye biblia maana Mungu alisema atakayemuua kain atalipia kisasi mwanzo 4:15

15 BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga

Na unabii huu unatimia kwa lamech kuonyesha ni yeye aliyemuua Cain maana anairithi ahadi ile

Mwanzo 4
23 Lameki akawaambia wake zake,Sikieni sauti yangu, Ada na Sila;Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu;Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha;Kijana kwa kunichubua;
24 Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba,Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba.

Hivyo basi kwakuwa Cain alikuwa mweusi hivyo naamini kizazi chake chote kilikuwa cheusi na hata binti yake egyptus ndio aliekuja kuolewa na Ham ambaye alikuwa mtoto wa Nuhu.

NB: kuna watu wanadai ham alikuwa mweusi ila cha kujiuliza kama alikua mweusi kivp baba yake yani Nuhu awe mweupe azae mweusi??

Baada ya gharika tunaambiwa na kitabu cha Abraham kwamba misri ilivumbuliwa na binti wa ham na egyptus (binti wa cain )

Book of Abraham

23 The land of Egypt being first discovered by a woman, who was the daughter of Ham, and the daughter of Egyptus, which in the Chaldean signifies Egypt, which signifies that which is forbidden;

24 When this woman discovered the land it was under water, who afterward settled her sons in it; and thus, from Ham, sprang that race which preserved the curse in the land

Ushahidi zaidi kwamba misri ilivumbuliwa na binti wa ham ipo pia kwenye biblia wanapoita misri kma HEMA LA HAM au biblia ya kiingereza LAND OF HAM soma mistari hii
Zaburi.78:51; 105:23,27; 106:22; Nyakati 1 4:40

Kitabu cha Moses ambacho kinatumika na baadhi ya makanisa duniani kinaenda mbali zaidi na kueleza rangi ya uzao wa ham ilikuaje

Book of moses 7:8

8 For behold, the Lord shall curse the land with much heat, and the barrenness thereof shall go forth forever; and there was a blackness came upon all the children of Canaan, that they were despised among all people.

Pia mstari wa 8 wa kitabu hiki unaonyesha kwamba Cain alikua mweusi na hata uzao wake ulikua wa watu weusi

Moses 7:22

22 And Enoch also beheld the residue of the people which were the sons of Adam; and they were a mixture of all the seed of Adam save it was the seed of Cain, for the seed of Cain were black, and had not place among them

Je kutokana na ushahidi huu wa vitabu vya kihistoria vya dini na nje ya dini kuna ukweli kwamba asili ya mtu mweusi ni CAIN ?? Ya kwamba alilaaniwa ndio akawa mweusi ndio maana na sisi tumekuwa weusi???

Karibuni mtiririke wana jukwaa :

Cc:
Malcom Lumumba Wick Indundu Eiyer MSEZA MUKULU Kiranga Al watan Hearly Da'Vinci Izzo mshana jr Palantir n.k

kwa maoni yako vitabu hivi vya kihistoria vinapotosha ukweli halisi hivyo basi mtazamo wako kuhusu asili ya mweusi ni ipi??
mimi wa kizazi hichi ni vigumu kutambua kwa urahisi asili ya mwafrika kwani kwa kiwango kikubwa na karne nyingi historia yetu imeharibiwa ......
ndiyo maana kuna mitazamo miwili kuhusu historia ya Afrika
-Afrocentric thought
-Eurocentric thought

angalau kina WalterRodney mamejaribu kutoa mwanga historia yetu
 
Mkuu zitto junior
nasikitika kuwa biblia inakuacha njia panda unapojitazama na kujiona kuwa mweusi wakati kichwani una wazo kuwa wazazi wetu wa kwanza walikuwa weupe!

Ni kweli kwamba watu wa kwanza kuumbwa walikuwa wawili tu, mwanaume na mwanamke walioitwa Adamu na Eva. Na ukweli wa jambo hilo unathibitishwa kwanza katika biblia hasa katika kitabu cha mwanzo ile sura ya 1:27-28a. Inasomeka hivi,
“Mungu akaumba mtu kwa mfano wa Mungu alimwumba mwanaume na mwanamke”

Katika Agano Jipya Bwana wetu Yesu Kristo kusisitiza kuwa walioumbwa kwanza ni watu wawili tu yaani Adamu na Eva, alisema hivi,
“Hamkusoma ya kuwa yeye aliyeumba mwanzo, aliwaumba mume na mke?” mwisho wa kunukuu. Mt 19:4.

Ushahidi mwingine ni wa kuenea kwa dhambi ya asili, dhambi ambayo walioifanya walikuwa wazazi wetu wa kwanza yaani Adamu na Eva. Dhambi hiyo imeenea kwa kila binadamu wote. Ndiyo kusema, kama Mungu angekuwa ameumba watu zaidi ya Adamu na Eva, wenye kuambukizwa dhambi hiyo wangekuwa ni wale tu wa uzao wa Adamu na Eva.

Uthibitisho mwingine wa kwamba hapo mwanzo Mungu aliumba watu wawili tu yaani Adamu na Eva na kutokana na hao wawili sisi tumepatikana (yaani binadamu wote) ni jina letu. Watu wote duniani wanaitwa binadamu. Maana yake bin-Adamu, hakuna anayeitwa binjiwe. Hiyo ni ishara wazi kwamba watu wote shina lao ni Moja tu yaani Adamu na Eva kama baba na mama yao.

Hizo ni baadhi tu ya thibitisho la imani yako kuwa hapo mwanzo Mungu aliumba kwanza watu wawili tu, Adamu na Eva na kutokana na hao, binadamu wote wamepata kuwepo duniani. Hivyo hilo unaloamini ndilo unalopaswa kulishika na kuwaambia wengine.

Katika swali linauliza kuwa hao Adamu na Eva ndiyo wazazi wa wayahudi na hao Adamu na Eva walikuwa weupe kama walivyo wayahudi, je sisi kama binadamu, yaani wa uzao wa Adamu hivyo mbona tu weusi? Sasa huo weusi tumeupata wapi? Kabla ya kukupa jibu la swali lako, naomba kwanza nikuweke sawa kwa jambo hili,
Ni kweli kuwa wayahudi ni weupe kama ulivyosema katika swali lako na ni kweli kuwa wayahudi wametokana na Adamu na Eva kwa sababu wayahudi ni watu na watu wote wametokana na Adamu na Eva hivyo lazima Adamu na Eva wawe ndiyo asili ya wayahudi, kama ilivyo kwa binadamu wengine kama vile wazungu, waasia, wachina waafrika n.k.
Lakini naomba nikuondoe hisia kwamba Adamu na Eva walikuwa weupe kama wayahudi. Najua utashtuka sana kwa maneno hayo, lakini baada ya muda si mrefu utanielewa ninachotaka kukuambia.

Ni hivi Biblia haisemi lolote juu ya rangi waliyokuwa nayo Adamu na Eva kama vile ambavyo haisemi kuwa watu hao wa kwanza walikuwa wafupi au warefu, wanene au wembamba. Na kama haisemi na leo hii sisi tunawaona waiskimo, watu walio wafupi kabisa duniani –wao wametoka wapi? Au tunawaona watu warefu kama waingereza –na wao wametoka wapi. Au tunawaona wachina watu wanene kama baadhi ya wachina-wao wametoka wapi. Leo hii tunawaona watu wembamba kama waingereza hata tukawaita English figure wao nao wametoka wapi. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kama vile ambavyo hatujui kama Adamu na Eva walikuwa warefu au wafupi, wanene au wembamba ndivyo ambavyo hatuwezi kusema kwa uwazi kuwa Adamu na Eva walikuwa weupe kama walivyo wayahudi.

Inafaa tufahamu kwamba, wayahudi –ni kweli kuwa ni weupe, lakini wayahudi kama taifa lisihesabiwe kuwa ndilo uzao wa moja kwa moja wa Adamu na Eva na hivyo tukitaka kujua rangi ya Adamu na Eva basi tuwatazame wayahudi, la hasha! Kwa taarifa tu, taifa la wayahudi lilianza kupata historia yake baada ya mwito wa Abrahamu ambaye aliishi miaka zaidi ya maelfu baada ya kuumbwa kwa Adamu na Eva. Hilo urejee Mwanzo. 5-12. ninachotaka kusema hapa ni kwamba, baada ya Adamu na Eva hadi kipindi cha Noah yaani kipindi cha gharika kuu iliyoangamiza watu wote duniani, kulikuwa na watu wengi sana duniani kwani tayari ilikwishapita miaka zaidi ya elfu mbili. Tena baada ya gharika kuu iliyomnusuru Noah tu na wana hadi Abraham ambaye wayahudi wanamhesabu kama ndiye babu yao aliyechaguliwa miongoni mwa mataifa mengi, ilipita miaka zaidi ya elfu moja na hivyo kulikuwa na watu wengi duniani wakiwemo weusi-kama kwani wakati huo bara la Afrika lilikuwapo.

Kuthibitisha kuwa wakati huo, yaani kabla ya kuitwa kwa Abrahamu tayari dunia ilikuwa na watu wa rangi mabalimbali, kutajwa kwa majina ya watoto wa Hamu ambaye alikuwa mmoja kati aya watoto wa Noah. Watoto hao ni Misri na Kushi. Kumbe Misri ni sehemu ya Afrika hali kadhalika Kushi ni eneo la Ethiopia ya sasa ambako watu wake ni weusi. Rejea Mwanz. 10:6. Hapo zamani majina ya watu ndiyo pia yalikuwa yanachukua majina ya mahali. Miaka mingi baadaye ndipo Abrahamu ambaye alitokana na ukoo wa Shemu aliyekuwa mmoja wa wana wa Noah alipopata kuwapo. Rejea Mwanzo. 11:10-31.
Kuhusu Agano kati ya Mungu na Abrahamu rejea kitabu cha Mwanzo 17:1-24.

Mpaka hapa bado sijakupa jibu la swali lako la kuwa wewe au watu weusi wametoka wapi. Kama umenifuata vizuri wewe mwenyewe unaweza kubaini kwamba watu wa rangi zote wametokana na Adamu na Eva kama vile ambavyo watu wa maumbile mbalimbali wametokana na wazazi hao wawili. Sasa, walikujaje? Hapa sasa uniruhusu nikupe hoja za kisayansi. Lakini kabla ya kukupa hoja hiyo naomba ukubali kwamba kama vile ambavyo biblia haisemi kuwa mtu wa kwanza alikuwa wa rangi gani, nami nakuambia kuwa inawezekana mtu wa kwanza yaani Adamu na Eva si lazima kuwa walikuwa weupe na inawezekana wazazi hao walikuwa weusi kuliko weupe kama wanavyodhani watu wengi na wewe pia. Nasema walikuwa weusi kwa sababu, kinachofanya watu watofautiane katika rangi ni mazingira. Watu wengi wanaoishi katika ukanda wa Ikweta ni weusi kwani sehemu hiyo ina jua kali sana, hivyo rangi hiyo nyeusi ni muhimu katika kuwalinda watu hao dhidi ya magonjwa ya ngozi kama kansa yanayotokana na mionzi ya jua.

Weusi huo hutaokana na muunganiko wa chembechembe hai iitwayo melanini iliyopo katika vishina vya vinyoleo ambavyo huwa ni vyeusi. Lakini kadiri watu wanavyoishi mbali na ukanda wa Ikweta ambako jua hupungua makali yake, melanini pia hupungua na hata kutoweka kabisa na hivyo mtu aishiye maeneo hayo yenye jua hafifu huwa mweupe kwa sababu ya kukosa chembechembe hizo kwa sababu hawazihitaji katika mazingira yale ya jua hafifu. Ndiyo maana watu wanaoishi Kongo katika Afrika ni weusi zaidi kuliko wale wanaoishi Afrika kusini na Afrika ya Kaskazini ambako makali ya jua yamepungua. Au ukienda India, wahindi wanaoishi upande wa kusini si weupe kama wale wa Kaskazini, wao ni wekundu au weusi kabisa kwa sababu upande huo umepitiwa na Ikweta hivyo kuna joto na jua kali. Au ukienda Amerika ya kusini kama vile Brazil. Watu wa kule wengi ni weusi sababu si tu kwamba weusi hao walitoka Afrika kipindi kile cha utumwa, la hasha! Historia inatuambia kwamba wakazi wa asili wa Amerika ya kusini ni wahindi wekundu ambao nimekuambia kuwa wapo pia upande wa kusini wa India.

Ninachosema hapa ni kwamba, Mungu aliumba watu wawili tu Adamu na Eva, lakini watu walivyoongezeka mno duniani na kwenda kuishi sehemu mbalimbali duniani zenye mazingira na hali ya hewa tofauti zikawafanya watu hao wawe na rangi inayotofautiana kadiri ya mazingira waliyoishi na kuzaliana. Kwa mfano, watu walioenda kuishi mazingira kama ya Ulaya ambako melanini haihitajiki walipata kuwa weupe kama wayahudi, wale waliokwenda kuishi katika mazingira ambayo kuna jua kali na hivyo melanini inahitajika wakawa rangi yao nyeusi kama unavyowaona waafrika sababu katika Afrika kuna jua kali na hivyo melanini inatakiwa.

Hapo awali nilidokeza kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba Adamu na Eva walikuwa weusi na si weupe kama watu wengi wanavyodhani. Tena wapo watu wanaosema kuwa watu weusi walitokana na uzao wa Hamu mtoto wa Noah ambaye baba yake alimlaani baada ya kuutazama uchi wa baba yake. Mwanzo 9:20-27. Habari hizo ni za uwongo zilizotungwa na wazungu wa karne ya kumi na tisa waliotaka kuhalalisha biashara halamu ya utumwa kwa kusema kuwa waafrika ni uzao wa Hamu ambaye alilaaniwa na hivyo waafrika wamelaaniwa ndiyo maana ni halali kuwa watumwa.
Hoja ya kwamba huenda wazazi wetu wa kwanza yaani Adamu na Eva walikuwa weusi inatolewa na wanasayansi wengi wakitoa hoja kwamba ni rahisi kwa mtu kubalika kutoka weusi kwenda rangi nyingine kuliko kutoka weupe kuja weusi. Kwa hoja hiyo, wanadai kwamba kama Adamu na Eva wangekuwa weupe basi watu weusi wasingepatikana. Hata katika mazingira ya kawaida watu waliozaliwa weupe hawawezi kujifanya weusi ila weusi wanaweza kujifanya weupe.

Ni kweli kwamba wayahudi ni weupe, na ni kweli kwamba Adamu na Eva walikuwa wazazi wa kwanza wa watu wote pamoja na wayahudi. Ni kweli pia kwamba hapa duniani kuna watu weusi kama walivyo waafrika. Utofauti au asili ya rangi hizo tofauti umetokana na mabadiliko ya kimazingira ambamo watu wamekuwa wakiishi. Lakini biblia haituambii kuwa watu hao wa kwanza yaani Adamu na Eva walikuwa wa rangi gani; yawezekana walikuwa weupe au pia yawezekana walikuwa weusi kama wanasayansi wengi wanavyosema wakitoa hoja zao za kisayansi. Hivyo usidhani kuwa wayahudi au watu weupe wataanza kuwahodhi Adamu na Eva wakidai kuwa ndiyo wazazi wao halisi na sisi watu weusi tumepatikana kwa ajali tu. Siyo hivyo hata kidogo.

Kuelewa kwamba biblia haikuwa na lengo la kuweka rekodi ya namna gani kitu kilivyoanza. Kitabu cha Mwanzo kinatoa masimulizi ya namna gani binadamu na ulimwengu kwa jumla ulivyoanzishwa kwa mkono wa Mungu. Kwa namna ya pekee, kitabu hicho kinatoa masimulizi ya namna gani binadamu alianza na si namna watu walivyoanza. Watu wote weusi kwa weupe wote ni binadamu walioumbwa na Mungu wakianzia kwa wazazi wao Adamu na Eva. Mabadiliko ya kimazingira ndiyo yaliyowafanya waonekane tofauti baada ya miaka ya miaka min
 
Asee mkuu Da'Vinci ahsante kwa nondo zako nzito za kushibisha ubongo ila naona kama umepanua sasa mjadala wa kisayansi kuhusu uwezekano wa mtu kubadilika rangi kutokana na mazingira je niulize kivipi aborigines wa Australia bado ni weusi tii angali wamekaa huko karne kibao mkuu??

Ila hoja zingine zote nimekuelewa kwamba kwakuwa biblia haikusema origin ya rangi ya Adam na eva hivyo ni makosa kuamini kuwa walikuwa weupe!!

Ila swali linakuja tumeshuhudia vizazi vya shem na japhet vimezaa watu wa ulaya na asia na vile vile vizazi vya HAM ambaye kwa kiaramaic inamaanisha MWEUSI amezaa makabila yaliyotajwa kwenye biblia ambayo kwa sasa tunaona mengi yao ni ya watu weusi ya cush-ethiopia, Mizraim-wasudan/wanubi, put- libya n.k je inawezekana vipi yeye awe na watoto weusi alafu kaka zake wawe na watoto weupe ?? Mfano sudan wameishi na waarab kwa miaka zaidi ya 1000 sasa ila waarabu ni weupe na wasudan bado weusi tiiiii!!!

Je hakuna uwezekano Asili ya rangi ya hamu ina ukakasi kidogo au labda kweli kuna uwezekano alioa mwanamke mweusi hivyo kusababisha kizazi cha rangi nyeusi kupatikana??

Embu tuwekane sawa kidogo hapo kwa faida ya wengi
 
mbna quran hujatoa ?
Mkuu habari za Cain kwa kirefu zipo kwenye vitabu vya kiyahudi ndio maana nimeviquote mfano jasher , book of abraham na book of moses havitumiwi na wakristo bali wayahudi wa kale indio maana nmezungukia kwenye hizi dini mbili ila kama una source kupitia quran inayoweza kuelezea Nature ya watu weusi funguka utuelemishe

Ahsante
 
Mkuu zitto junior
nasikitika kuwa biblia inakuacha njia panda unapojitazama na kujiona kuwa mweusi wakati kichwani una wazo kuwa wazazi wetu wa kwanza walikuwa weupe!

Ni kweli kwamba watu wa kwanza kuumbwa walikuwa wawili tu, mwanaume na mwanamke walioitwa Adamu na Eva. Na ukweli wa jambo hilo unathibitishwa kwanza katika biblia hasa katika kitabu cha mwanzo ile sura ya 1:27-28a. Inasomeka hivi,
“Mungu akaumba mtu kwa mfano wa Mungu alimwumba mwanaume na mwanamke”

Katika Agano Jipya Bwana wetu Yesu Kristo kusisitiza kuwa walioumbwa kwanza ni watu wawili tu yaani Adamu na Eva, alisema hivi,
“Hamkusoma ya kuwa yeye aliyeumba mwanzo, aliwaumba mume na mke?” mwisho wa kunukuu. Mt 19:4.

Ushahidi mwingine ni wa kuenea kwa dhambi ya asili, dhambi ambayo walioifanya walikuwa wazazi wetu wa kwanza yaani Adamu na Eva. Dhambi hiyo imeenea kwa kila binadamu wote. Ndiyo kusema, kama Mungu angekuwa ameumba watu zaidi ya Adamu na Eva, wenye kuambukizwa dhambi hiyo wangekuwa ni wale tu wa uzao wa Adamu na Eva.

Uthibitisho mwingine wa kwamba hapo mwanzo Mungu aliumba watu wawili tu yaani Adamu na Eva na kutokana na hao wawili sisi tumepatikana (yaani binadamu wote) ni jina letu. Watu wote duniani wanaitwa binadamu. Maana yake bin-Adamu, hakuna anayeitwa binjiwe. Hiyo ni ishara wazi kwamba watu wote shina lao ni Moja tu yaani Adamu na Eva kama baba na mama yao.

Hizo ni baadhi tu ya thibitisho la imani yako kuwa hapo mwanzo Mungu aliumba kwanza watu wawili tu, Adamu na Eva na kutokana na hao, binadamu wote wamepata kuwepo duniani. Hivyo hilo unaloamini ndilo unalopaswa kulishika na kuwaambia wengine.

Katika swali linauliza kuwa hao Adamu na Eva ndiyo wazazi wa wayahudi na hao Adamu na Eva walikuwa weupe kama walivyo wayahudi, je sisi kama binadamu, yaani wa uzao wa Adamu hivyo mbona tu weusi? Sasa huo weusi tumeupata wapi? Kabla ya kukupa jibu la swali lako, naomba kwanza nikuweke sawa kwa jambo hili,
Ni kweli kuwa wayahudi ni weupe kama ulivyosema katika swali lako na ni kweli kuwa wayahudi wametokana na Adamu na Eva kwa sababu wayahudi ni watu na watu wote wametokana na Adamu na Eva hivyo lazima Adamu na Eva wawe ndiyo asili ya wayahudi, kama ilivyo kwa binadamu wengine kama vile wazungu, waasia, wachina waafrika n.k.
Lakini naomba nikuondoe hisia kwamba Adamu na Eva walikuwa weupe kama wayahudi. Najua utashtuka sana kwa maneno hayo, lakini baada ya muda si mrefu utanielewa ninachotaka kukuambia.

Ni hivi Biblia haisemi lolote juu ya rangi waliyokuwa nayo Adamu na Eva kama vile ambavyo haisemi kuwa watu hao wa kwanza walikuwa wafupi au warefu, wanene au wembamba. Na kama haisemi na leo hii sisi tunawaona waiskimo, watu walio wafupi kabisa duniani –wao wametoka wapi? Au tunawaona watu warefu kama waingereza –na wao wametoka wapi. Au tunawaona wachina watu wanene kama baadhi ya wachina-wao wametoka wapi. Leo hii tunawaona watu wembamba kama waingereza hata tukawaita English figure wao nao wametoka wapi. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, kama vile ambavyo hatujui kama Adamu na Eva walikuwa warefu au wafupi, wanene au wembamba ndivyo ambavyo hatuwezi kusema kwa uwazi kuwa Adamu na Eva walikuwa weupe kama walivyo wayahudi.

Inafaa tufahamu kwamba, wayahudi –ni kweli kuwa ni weupe, lakini wayahudi kama taifa lisihesabiwe kuwa ndilo uzao wa moja kwa moja wa Adamu na Eva na hivyo tukitaka kujua rangi ya Adamu na Eva basi tuwatazame wayahudi, la hasha! Kwa taarifa tu, taifa la wayahudi lilianza kupata historia yake baada ya mwito wa Abrahamu ambaye aliishi miaka zaidi ya maelfu baada ya kuumbwa kwa Adamu na Eva. Hilo urejee Mwanzo. 5-12. ninachotaka kusema hapa ni kwamba, baada ya Adamu na Eva hadi kipindi cha Noah yaani kipindi cha gharika kuu iliyoangamiza watu wote duniani, kulikuwa na watu wengi sana duniani kwani tayari ilikwishapita miaka zaidi ya elfu mbili. Tena baada ya gharika kuu iliyomnusuru Noah tu na wana hadi Abraham ambaye wayahudi wanamhesabu kama ndiye babu yao aliyechaguliwa miongoni mwa mataifa mengi, ilipita miaka zaidi ya elfu moja na hivyo kulikuwa na watu wengi duniani wakiwemo weusi-kama kwani wakati huo bara la Afrika lilikuwapo.

Kuthibitisha kuwa wakati huo, yaani kabla ya kuitwa kwa Abrahamu tayari dunia ilikuwa na watu wa rangi mabalimbali, kutajwa kwa majina ya watoto wa Hamu ambaye alikuwa mmoja kati aya watoto wa Noah. Watoto hao ni Misri na Kushi. Kumbe Misri ni sehemu ya Afrika hali kadhalika Kushi ni eneo la Ethiopia ya sasa ambako watu wake ni weusi. Rejea Mwanz. 10:6. Hapo zamani majina ya watu ndiyo pia yalikuwa yanachukua majina ya mahali. Miaka mingi baadaye ndipo Abrahamu ambaye alitokana na ukoo wa Shemu aliyekuwa mmoja wa wana wa Noah alipopata kuwapo. Rejea Mwanzo. 11:10-31.
Kuhusu Agano kati ya Mungu na Abrahamu rejea kitabu cha Mwanzo 17:1-24.

Mpaka hapa bado sijakupa jibu la swali lako la kuwa wewe au watu weusi wametoka wapi. Kama umenifuata vizuri wewe mwenyewe unaweza kubaini kwamba watu wa rangi zote wametokana na Adamu na Eva kama vile ambavyo watu wa maumbile mbalimbali wametokana na wazazi hao wawili. Sasa, walikujaje? Hapa sasa uniruhusu nikupe hoja za kisayansi. Lakini kabla ya kukupa hoja hiyo naomba ukubali kwamba kama vile ambavyo biblia haisemi kuwa mtu wa kwanza alikuwa wa rangi gani, nami nakuambia kuwa inawezekana mtu wa kwanza yaani Adamu na Eva si lazima kuwa walikuwa weupe na inawezekana wazazi hao walikuwa weusi kuliko weupe kama wanavyodhani watu wengi na wewe pia. Nasema walikuwa weusi kwa sababu, kinachofanya watu watofautiane katika rangi ni mazingira. Watu wengi wanaoishi katika ukanda wa Ikweta ni weusi kwani sehemu hiyo ina jua kali sana, hivyo rangi hiyo nyeusi ni muhimu katika kuwalinda watu hao dhidi ya magonjwa ya ngozi kama kansa yanayotokana na mionzi ya jua.

Weusi huo hutaokana na muunganiko wa chembechembe hai iitwayo melanini iliyopo katika vishina vya vinyoleo ambavyo huwa ni vyeusi. Lakini kadiri watu wanavyoishi mbali na ukanda wa Ikweta ambako jua hupungua makali yake, melanini pia hupungua na hata kutoweka kabisa na hivyo mtu aishiye maeneo hayo yenye jua hafifu huwa mweupe kwa sababu ya kukosa chembechembe hizo kwa sababu hawazihitaji katika mazingira yale ya jua hafifu. Ndiyo maana watu wanaoishi Kongo katika Afrika ni weusi zaidi kuliko wale wanaoishi Afrika kusini na Afrika ya Kaskazini ambako makali ya jua yamepungua. Au ukienda India, wahindi wanaoishi upande wa kusini si weupe kama wale wa Kaskazini, wao ni wekundu au weusi kabisa kwa sababu upande huo umepitiwa na Ikweta hivyo kuna joto na jua kali. Au ukienda Amerika ya kusini kama vile Brazil. Watu wa kule wengi ni weusi sababu si tu kwamba weusi hao walitoka Afrika kipindi kile cha utumwa, la hasha! Historia inatuambia kwamba wakazi wa asili wa Amerika ya kusini ni wahindi wekundu ambao nimekuambia kuwa wapo pia upande wa kusini wa India.

Ninachosema hapa ni kwamba, Mungu aliumba watu wawili tu Adamu na Eva, lakini watu walivyoongezeka mno duniani na kwenda kuishi sehemu mbalimbali duniani zenye mazingira na hali ya hewa tofauti zikawafanya watu hao wawe na rangi inayotofautiana kadiri ya mazingira waliyoishi na kuzaliana. Kwa mfano, watu walioenda kuishi mazingira kama ya Ulaya ambako melanini haihitajiki walipata kuwa weupe kama wayahudi, wale waliokwenda kuishi katika mazingira ambayo kuna jua kali na hivyo melanini inahitajika wakawa rangi yao nyeusi kama unavyowaona waafrika sababu katika Afrika kuna jua kali na hivyo melanini inatakiwa.

Hapo awali nilidokeza kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba Adamu na Eva walikuwa weusi na si weupe kama watu wengi wanavyodhani. Tena wapo watu wanaosema kuwa watu weusi walitokana na uzao wa Hamu mtoto wa Noah ambaye baba yake alimlaani baada ya kuutazama uchi wa baba yake. Mwanzo 9:20-27. Habari hizo ni za uwongo zilizotungwa na wazungu wa karne ya kumi na tisa waliotaka kuhalalisha biashara halamu ya utumwa kwa kusema kuwa waafrika ni uzao wa Hamu ambaye alilaaniwa na hivyo waafrika wamelaaniwa ndiyo maana ni halali kuwa watumwa.
Hoja ya kwamba huenda wazazi wetu wa kwanza yaani Adamu na Eva walikuwa weusi inatolewa na wanasayansi wengi wakitoa hoja kwamba ni rahisi kwa mtu kubalika kutoka weusi kwenda rangi nyingine kuliko kutoka weupe kuja weusi. Kwa hoja hiyo, wanadai kwamba kama Adamu na Eva wangekuwa weupe basi watu weusi wasingepatikana. Hata katika mazingira ya kawaida watu waliozaliwa weupe hawawezi kujifanya weusi ila weusi wanaweza kujifanya weupe.

Ni kweli kwamba wayahudi ni weupe, na ni kweli kwamba Adamu na Eva walikuwa wazazi wa kwanza wa watu wote pamoja na wayahudi. Ni kweli pia kwamba hapa duniani kuna watu weusi kama walivyo waafrika. Utofauti au asili ya rangi hizo tofauti umetokana na mabadiliko ya kimazingira ambamo watu wamekuwa wakiishi. Lakini biblia haituambii kuwa watu hao wa kwanza yaani Adamu na Eva walikuwa wa rangi gani; yawezekana walikuwa weupe au pia yawezekana walikuwa weusi kama wanasayansi wengi wanavyosema wakitoa hoja zao za kisayansi. Hivyo usidhani kuwa wayahudi au watu weupe wataanza kuwahodhi Adamu na Eva wakidai kuwa ndiyo wazazi wao halisi na sisi watu weusi tumepatikana kwa ajali tu. Siyo hivyo hata kidogo.

Kuelewa kwamba biblia haikuwa na lengo la kuweka rekodi ya namna gani kitu kilivyoanza. Kitabu cha Mwanzo kinatoa masimulizi ya namna gani binadamu na ulimwengu kwa jumla ulivyoanzishwa kwa mkono wa Mungu. Kwa namna ya pekee, kitabu hicho kinatoa masimulizi ya namna gani binadamu alianza na si namna watu walivyoanza. Watu wote weusi kwa weupe wote ni binadamu walioumbwa na Mungu wakianzia kwa wazazi wao Adamu na Eva. Mabadiliko ya kimazingira ndiyo yaliyowafanya waonekane tofauti baada ya miaka ya miaka min

Cc.
Palantir MONG'ONYO @Zainab002
Mkuu umeshiba kwelikweli! Ila naomba nichangie kidogo.
Hoja ya kwamba biblia haijaweka wazi kuwa Adam na Eva hawajulikani ni rangi gani ni sawa, pia katika vitabu vyengine kama Quran haijaweka was (watanisahihisha kama nimekosea).

Lkn turudi katika mfumo wa uumbaji, wote tunakunaliana kwamba muumbaji alitumia udogo kuumba. Ila kuna maandiko kuwa Adam aliumbwa kwa aina tofauti za udongo (kuna taarifa zinasema ni aina saba ila Sina uhakika).

Hivyo kutokana na huo mchanganyiko wa udongo ndio kunakosekana ushahidi wa rangi halisi ya Adam. Inasemakana hakuwa mweupe wala mweusi ila muonekano wa rangi yake ulikua unakuja kutoka kwenye muono wako. Ukihisi mweusi unaona hivyo kweli na ukihisi mweupe, mwekundu au rangi yoyote utakayo hisi unamuona hivyo kweli.

Kwahiyo kutokana na kutokujulikana rasmi kwa rangi ya Adam ila tunajua asili yake ni udongo wa aina tofauti ndio maana tunaona leo kuna watu weusi, weupe na wekundu.
Wote tumetokana na vinasaba (genetics) moja.

Na kuhusiana na kimo chake, Adam alikua na urefu wa futi 60.

Katika Quran kuna maneno Mungu anasema.

"Enyi wanadamu kwa hakika Tumekuumbeni wote kutokana na mwanaume mmoja (Adamu) na mwanamke mmoja, (Hawwa).
Na Tumekufanyeni Mataifa na Makabila mbalimbali ili mjuane. Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni Yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini, Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari za mambo yote.” Quran (49:13)
 
6ECA9B1F-9909-4145-B54B-6E55861C759D.jpeg
 
Back
Top Bottom