Je hii ingetokea kwetu angepona mtu kweli??

Je hii ingetokea kwetu angepona mtu kweli??

Perfectz

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2017
Posts
9,576
Reaction score
29,713
Ndege ya abiria imeanguka baharini baada ya kukosa barabara ya ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chuuk International huko Micronesiam kulingana na maafisa wa uwanja huo wa ndege.
Ndege hiyo kutoka kampuni ya ndege ya Air Niugini kutoka taifa la Papua New Guinea ilionekana ndani ya maji ya kina kifupi karibu na pwani ya eneo hilo.
Wakaazi wa eneo hilo walichukua hatua ya haraka kupitia kuifuata ndege hiyo wakiwa wameabiri maboti na kuweza kuwasaidia abiria wake 36 pamoja na wafanyika zi 11.
INGEKUWA KWETU NAHISI UOKOZI UNGESUBIRI KWANZA KUTAFUTA NYENZO ZA UOKOZI
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    24.9 KB · Views: 42
Kwetu tungesubiri kwanza tutengeneze kamati ya uokoaji na baadae kesho yake ndio zoezi zima lingeanza baada ya kualika vyombo vya habari
 
Habari hii ingekuwa pouwa kwa kuwa destination ni zahanati 3+
 
Kwa sababu zilizotajwa na wachangiaji wa thread hii, tungekuwa tunafanya uopoaji.
 
Unajitahidi kuwa mpotoshaji na kujiweka mbali na uzalendo wa nchi yako matukio ya ajali ni mengi sana duniani na kila aina ya ajali ina asili yake ina mtindo wake unalinganishaje watu walio zama na watu wanaoelea!!!?hayo ndiyo mazingira yetu hata wewe ungekuwa Rais hali hiyo ingetokea.
 
Huku kwetu wangepona bhana mbona ile pale arusha kisongo walipona
 
Kua mzalendo sio kuogopa kusema au kuponda mapungufu ya kwenu.Dhambi yakutokuambiana ukweli nakupenda kusifia tu ata katika madudu haitatusaidia.Wenzetu wamefanikiwa kuendelea kwasababu waliacha unafiki nawakathubutu kuitaja dhambi kwa jina kisha wanajirekebisha.Nahuo ndio uzalendo wa kweli sio huo wakwako wakinafiki.
Mkuu acha uzandiki kua mzalendo kuponda nyumbani kwako wakati ndipo unapoishi sio poa..kama vipi hamia huko unakosifia..
 
Mkuu ungehamia huko ukakae nao utuachie unafiki wetu hapa
 
Mkuu acha uzandiki kua mzalendo kuponda nyumbani kwako wakati ndipo unapoishi sio poa..kama vipi hamia huko unakosifia..
Lazima ukweli usemwe hatuwezi kukaa kimya kwa kuogopa kuwasema wazembe, UZEMBE NI UZEMBE TUU TUACHE UNAFIKI
 
Back
Top Bottom