Mada hailalamiki.
Inaeleza historia ya Waislam na mambo yaliyojiri katika nchi yetu.
Wahindu na Wapagani hawajapata kuwa tatizo Tanzania.
Kuelezea mambo ya kuonewa kudhulimiwa na kusema mfumo uliopo unakandamiza tabaka fulani kama sio kulalamika ni kufanya nini ?, umekatazwa au haujapewa fursa ya kutafuta kile unachosema unayimwa ?, hivi na wengine wakianza kuja juu kuhusu historia ya nchi yetu, utumwa na jinsi waarabu walivyowakandamiza na kukiambia kizazi cha sasa kwamba walionewa na waarabu hii inajenga au kuharibu ?, ni kweli historia inabidi isomwe na iwepo ila sio kujenga hoja kwa present na future.., hata kama ni kweli usemayo Nyerere alikuwa anawanyanyasa waislamu Je hii inasaidia nini ya sasa na yajayo.., waarabu waliowatesa mababu zetu.., je hii dhambi ni ya wajukuu na watoto zao pia tunaoishi nao vizuri sasa ?
Chukua wakati kujielimisha kiasi unapoandika watu wapende kukusoma.
Ondokana na vitu visivyo na maana katika kujenga hoja zako.
Jifunze kufikiri kwa ubongo wako usiupe moyo nafasi.
Ukifanya hivyo mengi yatakupita.
Sasa kati yangu mimi na wewe hapo juu ni nani anayoongea yasiyo na maana
Mada hii na nyingine nilizoandika mfano wa hizi zimehifadhiwa kwingi
na ni rejea kwa wanafunzi wa African history katika vyuo vingi.
Huwezi kufahamu lakini wajuzi wanasema sehemu ambayo inaweza kulipuka katika Afrika ni
Tanzania.
Wenzetu washaziona dalili.
Hayo ya wewe kuandika mengi na mengine kuhifadhiwa mimi hayanihusu mimi nilichofanya ni kujibu post yako uliyotoa hapa, Ni kweli Tanzania inaweza kulipuka.., na huku kutasababishwa na watu wanaoleta mbegu za chuki kama wewe.., watu wanaotumia historia kusema kwamba tabaka fulani halifai au kuingiza serikali katikati wakati serikali haina dini wala hakuna anaekatazwa kutafuta au kuamini anavyotaka kwa wakati wake.., kwahio ni kweli serikali inabidi ifanye kazi yake kuhakikisha hakuna watu wanaopanda mbegu za chuki ambapo hapo mwanzo zilikuwa hazipo
Askari polisi na JWT weshaingia mitaani kupambana na Waislam.
Magari ya deraya, helikopta zinaruka kuwadhibiti Waislam...
Tumefika vipi hapa?
Sasa wewe unataka watu wakikiuka mamlaka na sheria waachiwe tu wafanye wanachotaka ?, tumefika hapa sababu ya kuchekeana kwa muda mrefu.., tumefika hapa sababu ya kuacha huu ugonjwa sasa umekua na unatuumbua (to put it plainly sasa mchicha ushakua mbuyu) inabidi kukata mizizi kabla hali haijawa mbaya zaidi
Kwa nini mada yangu inaogopesha kwa hiyo inatolewa JF isisomwe?
Mkuu sio mada yako tu ni nyingi huwa zinafutwa kutokana na Mods wenyewe kuona kwamba hii habari either inapotosha au inaleta chuki au mada nzuri lakini wachangiaji wanaleta matusi..., mkuu hio ndio kazi ya Mods kama unaona hawafanyi kazi yao au wanachemsha nadhani jaribu labda kuomba kazi ya kuwa Moderator na wewe au anzisha blog yako where everything goes..
Kwa nini kitabu "Mwembecha Killings..." kinawatisha watawala na hivyo
kukipiga marufuku kisisomwe?
Kama walikipiga marufuku lazima waliona either kuna upotoshaji au kinaweza kuleta fujo / chuki (binafsi sijui sababu sijakisoma wala sijawahi kukisikia) nadhani hata leo nikiandika kitabu kuhusu waarabu walivyo wabaya au walivyotesa babu zetu hivyo kupelekea wananchi wengine kuwachukia waarabu serikali ikikifungia itakuwa imefanya vyema.., nadhani ndio sababu hata vitabu kama Satanic Verses vilifungiwa.., au unataka kuniambia vitabu vyako kufungiwa ndio inaonyesha conspiracy dhidi ya uislamu ?
Jiulize anaetishwa na maandishi haya ni nani na kwa nini?
Maandishi kama haya ndio yanatufikisha hapa tulipo chuki dhidi ya sisi na sisi kwa imani ambayo Babu zetu hata walikuwa hawazitambui, hata kama sio wewe uliechoma makanisa au kufanya fujo au kupelekea watu waone waislamu ni wafanya fujo lakini indirectly maneno kama yako ndio yanayoleta chuki, hakuna tofauti na mimi kuanza kupiga debe na kuandika uovu wa waarabu zamani au labda wahindi wananyonya watu.., ni hizi hizi propaganda alizotumia Hitler against Jews..
Baada ya uhuru wametaka kujenga Chuo Kikuu lakini kikahujumiwa na
Nyerere na Kanisa Katoliki.
Miaka ya 1990 Waislam wametaka kujenga Chuo Kikuu cha Kiislam serikali ikahujumu chuo hicho
kikajengwa Mbale, Uganda.
Ndio yale yale unaleta historia za kuunga unga.., wewe ungetaka kufanya cha maana hizo nguvu unazotumia ungekusanya watu wenye imani kama wewe mkachanga pesa na kutafuta msaada na kujenga hata vyuo vikuu hata mia mbili au kila kata uone kama kuna mtu angekukataza
PS:
Nimekuona unatia maneno ya Kiingereza katika uandishi wako.
Mimi nina Merit Pass (First Class) English Oral, Cambridge Examination.
Nimetihaniwa lugha ya Kiingereza nazungumza na kusikilizwa na walimu wa Kiingereza.
Wamenipasisha ngazi ya kwanza.
Again who cares ?, wewe elimu yako au kujua kwako mimi kunanihusu nini?, you are just a mere comment in this forum siangalii ni nani kasema nini bali ni nini kimesemwa.., wala huwa siangalii mchangiaji ni comment zake.., siangilii sura bali character ya mtu.., ninajibu comment na sio mtu.., kwahio your personal status has no merit whatsoever if your comments leave a lot to be desired