Umeanza vibaya jibu lako.
Hebu soma ufunguzi wa kauli yako.
Namna hii haipatikani tija na mjadala unakosa umakini.
Kukosolewa ni kitu asichoweza kukiepuka yeyote yule anaeingia katika mjadala.
Mimi hilo halijapata kunitisha.
Nina uwezo wa kusimama na yeyote kwa hoja na nimefanya hivyo kwingi tu.
Isome historia ya Waislam na nini kilitokea baada ya uhuru kupatikana.
Kwa muhtasari nimeeleza katika post ambayo hapa JF imeondolewa.
Mada hii kwa namna tofauti nimeizungumza kwingi duniani na kwa hakika imeleta
changamoto kiasi nitakufahamisha kuwa nilipomaliza kuiwasilisha pale ZMO Berlin
niliombwa nikazungumze University of Humburg.
Nyinyi ndiyo mnatishika na historia hii.
Kwa wenzetu ni kitu kipya ambacho watafiti
wa historia ya Afrika wanathamini.
Insha Allah natayarisha mada "The Reversion of History and the Dangers of Fallacy."
Mungu akipenda nitaiweka hapa JF kuonyesha maradhi yanayowasibu watu wanapoletewa
mashujaa wapya katika historia iliyofutwa.
Angalia hofu na hamaki iliyoingia baada ya kubainika kuwa si Nyerere aliyeasisi TANU bali
ni rafiki yake Abdulwahid Sykes.
Hadi leo bado watu wamechanganyikiwa hawajui la kufanya.
Sheikh Mohamed Said Ahsante sana kwa darasa unalolitoa humu ndani. naona wamechanganyikiwa sasa ati wanaleta habari za yesu...... Na hiyo mada uliyoitaja hapo juu tunaisubiri kwa hamu. Ama kweli, ukweli ukidhihiri uongo hujitenga! Uongo haudumu. wameshatudanganya sana hawa watu kuhusu historia ya nchi hii, lakini sasa umeshawaacha uchi.
muungwana akivuliwa nguo huchutama sasa naona wao wanakimbia wanazidi kujifedhehasha. Bravo sheikh! endelea kutoa darasa.