Je? Fomu hii ya PF3, Imeshasababisha Mauti kwa Watanganyika Wangapi mpaka sasa??

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,057
1,371
Mtu anapata ajali, au anapigwa vibaya katika hali yoyote ile, Wasamaria (Wema), wanamuokota na kumpeleka hospitali au kituo cha afya ili kupata huduma ya kwanza na matibabu akiwa bado yupo hai. Akifika huko, anarudishwa akalete Fomu ya PF3, kutoka kituo cha polisi kabla ya huduma. Wakati urasimu huu unatekelezwa mpaka unakamilika Mgonjwa anakata roho.

Je? Utaratibu huu unamaslahi kwa mwanachi kweli?? Au ni nini?
 
Kwa mfano kama yule mtoto alipigwa na baba yake na kufariki dunia, kama ilivyo ripotiwa na gazeti la AMANI la tarehe 10-10-2013, inaonekana huenda uhai wake ungeokolewa kama wasingerudishwa kufata PF3.
 
Mbona cku hizi hospital nyingi wamepunguza,kuihitaji hiyo pf 3!wanakutibu kwanza then,unafuatilia hiyo form,mi kuna jamaa wiki iliyopita aliwamia na wahuni akajeruhiwa vibaya,2lichofanya ni kumkimbiza hospital kwanza,ndio palikuwa karibu,akapata matibabu then,akaambiwa ataleta pf3,labda ni ukosefu wa uelewa tu kwani jeshi la polisi walishatoa maelekezo kuwa kuna matukio m2 akipata apelekwe kwanza hospital,ndio utaratibu mwingine ufuate.
 
Back
Top Bottom