Je, tatizo la wananchi ni kutokuwepo kwa Sheria ya Huduma za Afya au gharama za kuhudumiwa? (Jicho langu)

Mathayo Fungo

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
319
510
Jicho Langu linaona kwamba, Serikali imefanya mambo mengi katika kuboresha huduma za afya hapa nchini tangu tupate uhuru mwaka 1961. Miaka ya 1960 hadi 1990 Serikali ilikuwa inatoa huduma za kijamii bure ikiwemo huduma za afya. Ilipofika miaka ya 1990 kama ilivyo katika mataifa mengine duniani Tanzania ilijiondoa kwenye kutoa baadhi ya huduma za kijamii na kuruhusu sekta binafsi kuwekeza katika kutoa huduma hizo.

Ni katika maboreso hayo, mwaka 1990 serikali iliandaa sera ya kwanza ya afya ambayo pamoja na mambo mengine ilianzisha namna bora ya wananchi kuchangia huduma za afya. Sera hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2007. Katika marekebisho hayo, Sera ilitoa maelekezo na matamko ya jinsi huduma za afya zitakavyotolewa hapa nchini, ikiwemo wananchi kuchangia gharama za matibabu kwa fedha taslimu yaani malipo ya papo kwa papo, njia ya msamaha na mfumo wa Bima.

Baada ya serikali kuruhusu sekta binafsi kushiriki katika kutoa huduma za kijamii ikiwemo afya, tumeshuhudia maboresho makubwa katika sekta ya afya. Kumekuwepo na maboresho makubwa katika utoaji wa huduma za afya ndani ya sekta binafsi.

Aidha, Serikali kwa upande wake imefanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha miundo mbinu ya kutolea huduma za afya ikiwa ni pamoja na kutekeleza Sera ya Zahanati kila Kijiji, kituo cha afya kila kata na Hospitali katika kila Wilaya na Mkoa. Uwekezaji mkubwa pia tumeuona katika vifaa tiba, watumishi na upatikanaji wa dawa. Hadi sasa, kuna jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya vipatavyo 10,067 nchini ikijumuisha vya serikali na binafsi. Kutokana na uwekezaji huu changamoto iliyokuwa inawakabili wananchi ilikuwa ni nanma ya kuchangia katika kupata hizo zilizoboreshwa na kusogezwa katika maeneo wanayoishi.

Aidha, katika kuwawezesha wananchi kuzipata huduma za afya zilizoboreshwa, Bunge lilitunga sheria ya Mfuko wa Afya ya Jamii – CHF mwaka 1999. Mfuko huu ulilenga kutafuta namna bora ya wananchi hasa walioko katika sekta isiyo rasmi kuchangia huduma za matibabu kabla ya kuugua.Tangu kuanzishwa kwa Mfuko huu hadi mwaka 2022 ni Asilimia 6 tu ya Watanzania wamejiunga na kunufaika na Bima ya CHF.

Vilevile, katika kuhakikisha watumishi wa Umma wanapata huduma za afya pasipo kikwazo cha fedha, Bunge lilitunga sheria ya kuanzisha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mwaka 2001. Lengo la mfuko huu ilikuwa ni kuwahudumia watumishi wa umma pamoja na wategemezi wao. Kupitia sheria hii kila mtumishi alilazimika kuchangia asilimia 3 ya mshahara wake na mwajiri kuchangia asilimia 3. Kutokana na sheria kutokuwa na dhana ya uhiari mfuko huu uliweza kuimarika na kuwahudumia watumishi na wategemezi wao kwa ufanisi.

Kutokana na kukua kwa uhitaji wa bima ya afya, bunge lilifanya maboresho katika Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mwaka 2015 kwa kuruhusu makundi mengine ya wananchi wasio watumishi wa umma kujiunga kwa hiari. Maboresho hayo yaliwezesha asilimia 8 ya watanzania kunufaika na bima ya afya kufikia mwaka 2022.

Tangu utaratibu wa bima ya afya ulipoanzishwa kupitia CHF (dhana ya uhiari) na NHIF (dhana ya ulazima kwa watumishi wa umma na uhiari kwa makundi mengine) ni asilimia 14 tu wa watanzania wamenufaika na bima ya afya katika kipindi cha miaka 24. Kutokana na uwepo wa uhiari katika kujiunga na mifuko hii miwili, taarifa toka NHIF inaonesha kwamba asilimia kubwa ya wanachama waliojiunga kwa uhiari walikua tayari ni wagonjwa.

Wataalam wa kanuni za Bima wanatuambia, ili kuwa na huduma za bima ya afya ambazo ni endelevu lazima wananchi wajiunge wakiwa wazima na wachache ndiyo wawe wagonjwa ndipo mfuko unaweza kuwahudumia kwa ufanisi. Kwa mantiki hiyo lazima tuwe na mfumo wa kisheria ambao utawawezesha kuongeza msukumo kwa wananchi kujiunga katika mfumo wa Bima ya Afya kabla ya kuugua ili wanapopata changamoto ya kiafya waweze kuzitumia bila kikwazo cha fedha na kuwezesha uendelevu wa skimu za bima ya afya kutoa huduma.

Jicho Langu linaona kuwa ni ukweli usiopingika kuwa Serikali imefanya jitihada kubwa kuhakikisha huduma za matibabu zimeboreshwa katika ngazi zote kwa maana ya zahanati hadi hospitali ya Taifa. Lakini pia huduma za matibabu ni gharama kwa wananchi wengi kuzilipia kwa mfumo wa malipo ya papo kwa papo. Tunahitaji mfumo ambao ni jumuishi utakao wawezesha wananchi kugharamia huduma za matibabu.

Jicho langu linaona kuwa changamoto siyo kukosekana kwa sheria ya kusimamia huduma za afya kwani eneo hili tayari seriakali imefanya uwekezaji mkubwa. Eneo ambalo bado linahitaji msukumo wa kisheria ni katika kuwawezesha wananchi kujiunga katika Bima ya Afya ili waweze kunufaika na uwekezaji uliofanywa na serikali katika sekata ya afya.

AFYA BORA INA GHARAMA ZAKE NA LAZIMA SASA WANANCHI TUJE NA NAMNA YA KUTATUA MFUMO HUU. VITUO VIPO, CT SCANS ZIPO, MAABARA ZIPO, MRI ZIPO.

JE SASA TUNAZIGHARAMIAJE?
JE TUACHE BIMA YA AFYA KWA WOTE NA BADALA YAKE TUANZE KUJADILI SHERIA YA HUDUMA ZA AFYA?

HIVI TANZANIA IMEZALIWA LEO MPAKA TUWEKEANE SHERIA KATIKA KUJENGA VITUO, KUNUNUA VIFAA, KUPATA DAWA?

JE HILI NDO HITAJI LA WANANCHI KWELI AU MAMLUKI WA KISOMI WAMEAMUA KUTUMIKA VIBAYA?

Ni dhahiri kuwa endapo dhana ya uhiari wa kujiunga na bima ya afya itaondolewa wananchi wengi zaidi wataweza kuwa na uhakika wa matibabu yao pasipo kuwa na kikwazo cha fedha kabla ya kuugua.

JICHO LANGU LINAONA KUWA CHA MUHIMU NI KUWAWEZESHA KUGHARAMIA HUDUMA ZILIZOPO NA SIYO KUZITUNGIA SHERIA , HIVYO BIMA YA AFYA KWA WOTE NDO MUDA WAKE NA NDO HITAJI LA WANANCHI KWA SASA.

NAWASILISHA
 
Umesema sahihi ndugu. Huduma za matibabu kwa sasa zipo ila sasa gharama zake kubwa. Tupate tu hiyo bima ya afya itakuwa nafuu. Kwa sisi wenye magonjwa yasiyoambukiza tunahitaji bima kama jana. Ila muangalie na uwezi wetu kuchangia.
 
Kwa hakika nimesoma andiko hili lipo vizuri saana kwa sasa Bima ya Afya kwa wote ni jambo muhimu zaidi
 
Bima ya Afya inampa mwananchi uhakika wa matibabu kabla ya kuugua ,kwani ugonjwa haubishi hodi
 
Kwa kweli mimi naipongeza sana serikali kwa hatua hii kubwa ya kuboresha na kuhakikisha huduma za afya kwa wote kupitia bima ya Afya kwa wote ,wabunge na wizara wakamilishe utaratibu tuanze kujiunga
 
Bima ya afya kwa wote ni Mwarubaini wa changamoto zote za Kiafya hususani upande wa Gharama
 
Back
Top Bottom