SOLOGWIGABA
Member
- Aug 9, 2011
- 22
- 0
Jamani kuna mdogo wangu amemaliza Form six HGL mwaka juzi akapata Division 3 akiwa na principle tatu.Hata hivyo kulingana hali ya maisha kuwa ngumu niliamua kumtafutia kibarua amudu kujikimu mahitaji yake.Kwa sasa anaendelea na kibarua na nimemshauri mwaka huu ameomba Open University na amepata Mass Communication.Sasa tatizo kuna rafiki zake walioko vyuo mbalimbali kama UDOM,UDSM na kwingineko wanamshauri asisome Open eti kuwa kiwango cha elimu inayotolewa haikidhi kiwango cha kimataifa na kuwa OUT ni wasumbufu na hawaratibu vizuri Programs zao.Ndogo amekata tamaa na mimi napenda asome huku akifanya kazi kwa ajili ya kujikimu.Naomba ushauri wenu wakuu na ukweli kuhusu Open kwa wanaofahamu kwa kina hasa waliosoma au wanaoendelea kusoma OUT.