Je, El Chapo ametoroka jela tena?

Primier

Member
Dec 16, 2015
86
14
160109052437_guzman_arrest_640x360_afp_nocredit.jpg
Image copyright AFP
Image caption El Chapo ametoroka jela mara mbili
Kuanzia jana jioni, habari zilienea kwenye mitandao ya kijamii na hasa Twitter kwamba mlanguzi hatari wa dawa za kulevya Joaquin Guzman, maarufu kama EL Chapo alikuwa ametoroka jela tena.


Je, zilikuwa za kweli?

La hasha. Habari hizi zilitokana na tovuti ya habari za kubuni ya abcnews.com.co ambayo imefanywa kuonekana kana kwamba ni ya shirika tajika la habari la Marekani la ABC News ambalo tovuti yake halisi ni abcnews.go.com.


Habari hizo za kubuni, zilieleza jinsi walinzi wawili wa gereza walivyoonekana wakiwa wamemshika El Chapo, kana kwamba wanamhamisha kutoka seli moja hadi nyingine, mwendo wa saa nane usiku na baadaye ikadaiwa kwamba ametoweka pamoja na walinzi hao.

160109044504_mexico_chapo_guzman_640x360_reuters.jpg
Image copyright Reuters
Image caption Watu sita walifariki wakati wa operesheni ya kumkamata tena El Chapo
Muda mfupi baadaye, habari hizo zinasema gari la gereza lilipatikana likiwa limeachwa umbali wa maili moja hivi kutoka gerezani.

Wengi waliamini habari hizo na wakaanza kujadili kutoroka kwake jela kana kwamba ni tukio lililokuwa limefanyika.

Hilo lilifanya jina lake kuvuma sana katika mitandao ya kijamii.

Baadhi walisema iwapo El Chapo alikuwa amefanikiwa kutoroka jela mara ya tatu, basi hata akienda jehanamu atafanikiwa kutoroka.

160201104401_el_chapo_tweet.jpg

Ukweli ni kwamba El Chapo, aliyekuwa kiongozi wa genge la walanguzi la Sinaloa, bado anazuiliwa katika gereza la Altiplano nchini Mexico chini ya ulinzi mkali.

Alikamatwa tarehe 8 Januari baada ya kuwa mtoro kwa zaidi ya miezi sita.

Kwa sasa, utaratibu wa kumhamishia Marekani akajibu mashtaka unaendelea.

El Chapo alikuwa ametafutwa sana baada ya kutoroka jela tarehe 11 Julai mwaka 2015, akipitia shimo lililochimbwa chini ya gereza hadi kufikia seli yake gerezani.

Marekani ilikuwa imeahidi zawadi ya $5m kwa mtu ambaye angetoa habari za kuwezesha kukamatwa kwake.

160109060208__84710590_2s2d5xbk.jpg
Image copyright Other
Alikamatwa mara ya kwanza Guatemala mwaka 1993 lakini akatoroka jela ya Puente Grande 2001, akiwa amefichwa kwenye kapu la kubeba nguo za kwenda kuoshwa, baada yake kuwahonga maafisa wa gereza.

Alikaa mafichoni mwa miaka 13 kabla ya kukamatwa na kufungiwa Altiplano mwaka 2014.

Tovuti hiyo bandia imewahi kutoa habari za uongo awali ambazo watu walizisambaza na kudhani ni za kweli. Mfano ni habari kwamba Rais Obama alikuwa ameidhinisha sheria ya kuwataka watu wanaomiliki silaha wawe wakiruhusiwa kumiliki bunduki tatu pekee.

Wakati mmoja, walitangaza pia kwamba Donald Trump alikuwa amemtangaza Sheriff Joe Arpaio kuwa mgombea mwenza wake.
 
Hata kama ingekuwa kuizoea serikali lakini isingekuwa sio kihivyo.
 
Back
Top Bottom