Dini na Mungu ni vitu viwili visivyokubaliana mkuu.
Mahusiano ya Mungu ni kwa mtu binafsi na kamwe haijawahi kuwa kwa kundi la dini au dhehebu fulani.
Fuatilia watu wote wanaogombewa kuwa Icon za dini zote. Wao hawajawahi kuwa sehemu ya hiyo mifumo ya kidini tofauti na mmoja tu aliyejinasibisha kwa dini ya kiisilamu.
Mwangalie Nuhu hajawahi kuwa na kundi lililojiita kitu fulani zaidi ya uhusiano wake binafsi na Mungu.
Halikadhalika Ibrahimu, Isaac, Yakobo, Musa, Eliya, Isaya, Daudi , Ezekiel, Yeremia, Daniel , Malaki nk, hawakuwahi kujinasibisha na dhehebu lolote kuwapa uhalali wa haki kutoka kwa Mungu.
Hata wanafunzi wa Yesu hawakujulikana kwa dhehebu lolote ila waliitwa wanafunzi wa Kristo yaani Yesu kwa maana ya mkristo akiwajibika kibinafsi kwa Mungu nje ya dhehebu liwalo lote.
Hawa wapigaji wa mwilini kwa kigezo cha dini au dhehemu haina maana yoyote kuwawekea usikivu maana dhawabu yao ni katika fahari ya dunia tu.
Hata Yesu shetani mwenye kuimiliki Babylon system aliwahi kumtega akimwambia ikiwa utanisujudia nitakumilikisha utajiri wa hii dunia. Lakini Yesu alimkatalia kwa hoja kwamba wakuabudiwa ni Mungu peke yake .
Hizi dini na vikundi vyote vya kisiri vimeridhia kumsujudia yule jamaa yaani shetani na amewamilikisha utajiri wa nchi kijinai.