Je, dunia inahitaji dini mpya?

Je, dunia inahitaji dini mpya?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,505
Reaction score
872,359
Naandika haya nikiwa kitandani nagonjeka. Mwili wote unauma sana!

Ni wazi maisha yamebadilika sana, dunia imebadilika sana na wanadamu nao wamebadilika sana, vitu karibia vyote vimerahisishwa mno, yaliyokuwa ya sirini mengi yamewekwa bayana.

Maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yamebadili mitazamo ya wengi hasa kwenye mambo yahusuyo Mungu, dini na imani.. Na ndio maana kuna kundi kubwa linalokuwa kwa kasi na kuongezeka linalohoji uwepo wa Mungu ama ambalo haliamini tena katika Mungu.

Kwenye nyumba zote za ibada za imani mbalimbali wamebaki na mapokeo, hakuna ubunifu mpya kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia
Mafundisho ni yaleyale
Mahubiri ni yaleyale
Dua ni zilezile
Mifano ni ileile na mingi ikiwa ni ya uongo ama ya kutunga

Uwezo wa watumishi na viongozi wa dini zote umekuwa na kikomo mno.. Wengi wao wanahubiri wasichoamini na wanaamini wasichohubiri
Mahubiri yamejaa mambo ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia..
Hawana suluhisho ya matatizo yanayowakabili waumini wao

Huwezi kumhubiria mtu kwenda mbinguni wakati
Hana Kazi
Hana hela ya kula
Ana vinyongo na visasi kutokana na dhuluma mbalimbali anazofanyiwa na wenye nguvu
Anamwangalia kiongozi wake wa dini kama tapeli tu, ameshiba, amenona ana siha njema tofauti kabisa na yeye.. Huku mahubiri kwa asilimia 90 yakihubiri utoaji

Viongozi wengi wana migongano na viongozi wenzao ama na waumini wao
Viongozi wengi wana kashfa za rusha
Viongozi wengi wana kashfa za ngono na ushoga
Viongozi wengi wana tuhuma za uchawi na kurogana nknk

Kuna baadhi walichungulia fursa baada ya kuona haya madhaifu, wakaja na option ya dini mbadala za kiroho
Kuhubiri miujiza ya uponyaji
Kuhubiri utajiri kwa njia za miujiza
Kuhubiri kupata kazi kwa njia za miujiza
Kuhubiri ndoa, mahusiano, kupata watoto nknk
Hawa wamevuna mabilioni ya pesa toka kwa waumini na waamini waliochoshwa na mahubiri ya mapokeo.. Lakini kwa bahati mbaya sana nao wameanza kushtukiwa janja janja yao maana nao hawakujipanga vema!

Kuna imani hizi za kishirikina.. Zina wateja kwenye imani zote za dini, viongozi watumishi na hata waumini wao. Ni imani zilizobeba usiri mkubwa na wateja bado wapo.. Hizi uwepo wa maendeleo ya sayansi na teknolojia haujaziathiri sana

Kuna hizi dini mbili kongwe sana.. Viongozi wake wameweza kudhibiti kwa kiasi kikubwa maudhui yake! Ni dini kwa ajili ya wachache wanaochaguliwa kwa umakini mkubwa sana. Sio dini za kila mtu hizi.. Na hizi ndio zinaendesha dunia kwa sasa nazo ni Freemason na Satanism. Hawa wako vizuri sana kwenye pesa elimu na fursa za kiuchumi

Hawa wanatamani sehemu kubwa ya wajinga waamini dini zingine waangamie ili wabaki wao tuu.. Na kuna tetesi za wao kufadhili miradi ya siri kwa ajili yakufanikisha hili

Sasa dini mpya ya ulimwengu ujao ni ipi? Hii inaweza kuja kuwa ni mchanganyiko wa hizi dini zinazomuabudu Mungu mmoja, dini zinazoabudu miungu Satanism na The masons. Na hili litatokea baada ya kuona hakuna upande utaweza kuitawala dunia peke yake bila msaada wa mwenzake.

Penye werevu panahitajika na wapumbavu ili mambo yasonge na ndipo hapo dini mpya itakapozaliwa.

37479a72f893e731cd53551c705099a0.jpg
 
Dini nyingine si ipo mkuu inaitwa new world order imeanza karne ya 20 for more information about the future world utaipata kwenye kitabu cha new world order mkuu wameelezea kila kitu kuna kitu kinaitwa noble era kwa waliosoma chemistry wanaelewa maana ya noble the noble era will be the ultimate goal of the new world order.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chini ya hili jua hakuna kipya kitakachokuja kuwa tofauti na hivi tunavyoviona katika maisha yetu.

Haya tunayoyaona na mengine mengi ambayo bado hatujayaona yalikuwepo tangu enzi hizo,yaani kama ni movies tunaweza kusema maisha tunayoishi;iwe raha,manyanyaso na taabu zote ni kama marudio tu na huwenda kuna taabu zaidi hizi tunazoziona wakipitia watu wengine,raha wanazopata wengine na hata manyanyaso wanayopitia wengine hapo baadae.

Dini nyingine hakuna,zaidi tu ya ujio wa mwokozi hapo siku ya mwisho kuja kutuokoa kwenda mbinguni kama baadhi tuvyoamini.Amen🙏🙏
 
Dini nyingine si ipo mkuu inaitwa new world order imeanza karne ya 20 for more information about the future world utaipata kwenye kitabu cha new world order mkuu wameelezea kila kitu kuna kitu kinaitwa noble era kwa waliosoma chemistry wanaelewa maana ya noble the noble era will be the ultimate goal of the new world order.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii itapita na kuja hiyo niliyozungumzia


462c0035e074f59ba422eb6938320587.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena waafrika ndio kabisa hawapaswi kuendelea kukumbatia madawa ya kulevya ya dini maana akili zenyewe ndogo ukichanganya na madawa ya kulevya dini tafrani tupu.
Marx alielezea dini kama 'kasumba ya umati' kwani inapotosha ukweli na kutuliza maumivu ya ukandamizaji wa watu. Anabainisha baadhi ya njia muhimu ambazo dini huthibitisha hilo tena kwa kuunda na kuahidi uzima wa milele mbinguni kwa wale wanaofuata na kushikamana na imani katika dini.

719f61d2324dc6e4d8a02e44d2dff85e.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marx alielezea dini kama 'kasumba ya umati' kwani inapotosha ukweli na kutuliza maumivu ya ukandamizaji wa watu. Anabainisha baadhi ya njia muhimu ambazo dini huthibitisha hilo tena kwa kuunda na kuahidi uzima wa milele mbinguni kwa wale wanaofuata na kushikamana na imani katika dini.View attachment 2753641

Sent using Jamii Forums mobile app
Alikuwa sahihi kwa zaidi ya asilimia mia moja
 
Sio kwamba hizi zilizopo zingepunguzwa zibaki chache halafu ziboreshwe, na kule kwingine kwenye nguvu zetu nyeusi nako pia paboreshwe
 
Naandika haya nikiwa kitandani nagonjeka.. Mwili wote unauma sana!

Ni wazi maisha yamebadilika sana, dunia imebadilika sana na wanadamu nao wamebadilika sana, vitu karibia vyote vimerahisishwa mno, yaliyokuwa ya sirini mengi yamewekwa bayana...
Inafikirisha sana hii. Wengine hapa tunaamini kuwa kuna Super natural being ambaye ametuumba na kututaka tuishi kwa matendo mema tu (Good deeds) but hakuleta dini kama hizi!! Wala hana haja na mambo hayo.

Anyways, kila mtu na lake
 
Chini ya hili jua hakuna kipya kitakachokuja kuwa tofauti na hivi tunavyoviona katika maisha yetu.

Haya tunayoyaona na mengine mengi ambayo bado hatujayaona yalikuwepo tangu enzi hizo,yaani kama ni movies tunaweza kusema maisha tunayoishi...
fcc4f7e0a0c38334588edd1a65f2eb57.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dini mpya? Mbona tayari dunia inayo dini mpya? Mpira umeteka mioyo ya watu wengi duniani na umewaunganisha. Angalia viwanja vinavyojaa dunia nzima. Mpira umepekekwa mpaka nchi za kiislam na wameupokea kisawasa kiasi cha kuachana na uislam wao kama dini. Uislam umebaki kama kabila tu duniani kote. Mzungu unaanzaje kumhubiri habari za dini akuelewe zaidi ya mpira? Ulaya ndiyo wametia fora kwa kuachana na dini. Hii dini mpya haiitwi dini inaitwa soka. Hii soka ina madhehebu yake ambayo ni michezo mbalimbali ya kimataifa
 
Umefundishwa kuna Mungu na umemmjua,mahusiano yako na yake hayahitaji kanisa wala msikiti ila wewe kuwa mwema kwa watu kwa namna yoyote utakayoweza.

Maisha yalipofikia ukitaka uige kutoka kwa watu kila kitu utajikuta sehemu mbaya sana.
ulikoanzia ukristo kuna wapuuzi kibao wanafanya mambo kinyume nao,ulikoanzia uislam nako hali ni hiyo hiyo.
mimi kama mkristo nakumbushwa kushika nilicho nacho,nisibabaike hata kidogo vinginvyo kwisha habari yangu.

by the way dini mpya tayari iko imeweka mpaka mifumo yake na inaandaa sheria zake.
 

Je, Dunia ilianzia Mashariki ya Kati?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Padri mmoja aliulizwa na kijana mmoja kuhusu uwepo wa Mungu akajibu hata yeye hajui kama yupo. Kuna dini imekuwa na misimamo mikali ya kutokubadilika tangu kale nayo imeanza kumomonyoka, ni suala la muda tu waumini wake wataachana nayo na kujua kuwa ilikuwa ni uongo na ulaghai tu.

Nachunguza hamasa kwenye dini mbalimbali zinazoonekana ni smart naona hakuna tena mahudhurio makubwa kama zamani, watu wako bize na mambo yao ya shughuli zao. Haya mambo yalitabiriwa hayana budi kutokea. Ni muelekeo wa zama za mpangilio wa ulimwengu mpya
 

Je, Dunia ilianzia Mashariki ya Kati?

Sent using Jamii Forums mobile app
Fuvu la mtu wa kale liligunduliwa Tanzania liliishi miaka zaidi ya milioni 2 , story ya adamu haina miaka 10000, apa kuna mtu na binadamu🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom