Je daraja la Kigamboni kuitwa daraja la Mwalimu Nyerere ni sahihi?

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,292
Hayati Mwalimu Nyerere ni Muasisi wa Taifa hili, ni raisi wa kwanza na ameifanyia makubwa nchi hii,.
Lakini Yeye mwalimu si muasisi pekee wa nchi hii na wala hakuijenga peke yake.
leo hii Mwalimu ameenziwa kwa vitu vingi, ukiwemo uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, Vyuo, barabara, Conference center.
Je kulikuwa kuna haja tena ya kuendelea kutumia jina lake kwenye daraja?
Nadhani nchi hii ina haja ya kuwakumbuka watoto wake walioipa heshima, wapo mababu zetu kina Kinjekitile, Abushiri, Mwinyikheri, Abdulwahid Sykes, Dr Kyaruzi, Dossa Aziz na waasisi mbalimbali.
kwa nini vitu vingi viitwe jina la Mwalimu Nyerere?.
yatupasa kuenzi mashujaa wetu kwa haki.
 
Kuna tatizo kubwa kwa viongozi wakati wa kuenzi thamani zetu ukiwemo utamaduni

Wengi wanadhani Nyerere ndiye alianzisha utamaduni ' mbovu' in fact hakupendelea sana.
Akiwa Sumbawanga, alikataa uwanja usiitwe kwa jina lake, badala yake uitwe Mandela

Hakuna doubt Nyerere ni ''iconic'' na hivyo atatokea maeneo mengi, ikiwemo nchi za nje pengine kuliko viongozi wengine. Hata hivyo, kwa hapa nyumbani kuna jambo tunakosea.

Kwa mfano, tunadhani kuita majina ya Nyerere mara nyingi ndiko kumuenzi, Makosa!!

Nyerere anaweza kutajwa sehemu moja tu ikawa katika hadhi anayostahili
Uwanja wa ndege unaitwa kwa jina lake, hadhi ya uwanja ilingane na ukubwa wa jina
Barabara ya Nyerere inatoka uwanja wa ndege kuingia mjini, iwe katika hadhi hiyo

Ukumbi wa mikutano down town haukuwa na sababu za kuitwa tena au daraja
Nyerere mwenyewe alithamini sana values na tradition zetu.

Princess Margaret akaiita Muhimbili, wodi zikapewa majina ya Kibasila , Mwaisela, Sewa Haji, Makuti n.k. Daraja la Kigamboni halikuapaswa kuitwa tena Nyerere

Kama ningepewa nafasi ya maoni, daraja hilo ningeshauri liitwe Mzizima

Dar imeanzia maeneo hayo ya Mzizima. Wangapi wanajua jina hilo na maana yake?
Kule Feri wanaita Feri bila kujua ndiyo Mzizima yenyewe. Mzizima inapotea

Kwanini kusiwe na public consultations kupata maoni?

Ni akina nani hawa wanaoamua tu regardless of history, tradition or values?
 
Nadhani mko sahihi katika hili kulikuwa hakuna haja ya kuliita daraja la kigamboni kuwa ni la Nyerere. Tungetafuta watu wengine wa kuwapa heshima hiyo waliotoa mchango mkubwa kwa taifa letu
 
Nadhani kwenye hili jina la daraja inafaa kutoka kwenye mjadala mwembamba na kuutanua.

Jina la daraja limeshatolewa. Ila kutakuwa na vitu vingine huko mbeleni.

Kazi ya kutafuta majina ya miundombinu na kumbukumbu iwe mojawapo ya majukumu ya wizara ya Nape. Kuwe na kitengo maalum cha kimkakati cha kuhakikisha vitu fulani havisahauliwi. Itengenezwe waiting list iliyotokana na utafiti.
 
Nadhani kwenye hili jina la daraja inafaa kutoka kwenye mjadala mwembamba na kuutanua.

Jina la daraja limeshatolewa. Ila kutakuwa na vitu vingine huko mbeleni.

Kazi ya kutafuta majina ya miundombinu na kumbukumbu iwe mojawapo ya majukumu ya wizara ya Nape. Kuwe na kitengo maalum cha kimkakati cha kuhakikisha vitu fulani havisahauliwi. Itengenezwe waiting list iliyotokana na utafiti.
Kwenye hili la daraja, ni mfamo mzuri wa jinsi tusivyopjipanga na tusivyo na vyombo husika. Tukilipanua ni vema

Fikiria ,unateremka uwanja wa Mwalimu Nyerere, unapitia barabara ya Nyerere, kisha daraja la Nyerere kulekea chuo cha Nyerere, unaamkia mkutano ukumbi wa Nyerere

Kwa watu wanaojua kuenzi na kupanga miji hii ina chosha na kutoa picha isiyo nzuri kwamba Taifa hili ima halina au linaupungufu wa 'mashujaa' au thamani zake za vitu

Tena uwanja wa ndege ungeitwa Nyerere Inter Aiport inge sound vizuri sana kuliko jina Mwalimu Julius Nyerere. Halitamkiki vema hasa kwa wageni wasiojua kiswahili

Daraja la Rufiji limeitwa Mkapa.
Nini nafasi ya watu wa Rufiji katika ukombozi wa Taifa hili?
Je, hatutambui maji maji ilipigwana sana maeneo hayo? Akina Kinjeketile wapo wapi?

Kilimanjaro inter aiport ipo Arusha Zaidi ya Kilimanjaro. Kwa mkakati kabisa ikaitwa Kilimanjaro kwasababu ya Mlima na hivyo kuwa sehemu ya kutangaza kivutio hicho.

Mtu anaye google Kilimanjaro mara nyingi hukutana na K'njaro airport.
Hivyo ndivyo tunaheshimu thamani zetu

Kwasababu mambo haya yanafanywa na wanasiasa wasiojua lolote bali kujipendekeza, leo hakuna anayejua Kichwele au mzizima na kuna kosa gani kwa majina kama hayo?

Wanasiasa wamebadilisha Bagamoyo Rd yenye historia inayotukuka na sasa ni Kibaki. Wamebadilisha ocean Road na sasa ni Obama.

Kwanini Ocean road isiitwe Dr Robert Coch Rd? Huyu ni mwanasayansi aliyetafiti ugonjwa wa TB duniani. Nani anajua kuwa Robert alifanya kazi Ocean Rd?

Je, haikuwa jambo jema ili kuamsha fikra za vijana wa leo kutambua thamani na umuhimu wa maeneo?

Kwa nchi za wenzetu zipo kamisheni maalumu za kutafiti na kutoa majina tena kwa vigezo kadhaa. Si kwamba ni kamisheni za watu kukaa wakisubiri, bali ikibidi watu hao huitwa kutokana na nyadhifa zilizopo.

Mfano, mkurugenzi wa makumbusho(museum), wasomi wa historia, wachambuzi wa masuala ya kijamii, viongozi wa taasisi muhimu za kitaifa n.k.

Hapa sikubaliani na kuwakabidhi akina Mh Nape. Hawa ni viongozi wanapita tu, kinachotakiwa ni kamisheni inayotokana na nyadhifa za watu katika muda uliopo

Kama ni kumuenzi mwalimu, Chuo cha Kivukoni ingekuwa taasisi moja kubwa na pengine kuitwa Nyerere center of excellence.

Ingetosha kuendeleza legacy yake kwa heshima kuliko kutawanya jina lake tuu bila kuwa na maana halisi ya kumuenzi mwalimu

Ukiwauliza waliotoa jina la uwanja wa ndege wa Dar, barabara ya Pugu, daraja la Kigamboni, chuo cha kigamboni na ukumbi wa mikutano kwanini wametoa jina la Nyerere , hakuna atakayeweza kusimama na kutetea kwa hoja na mantiki

Jibu rahisi utasikia ni Rais wa kwanza.
Hakuna anayeweza kutetea jina hilo, huku wakijifanya wana muenzi.

Ndio, wanajifanya kwasababu hawana sababu za kutushawishi wala matinki.
 
Hili la Obama kupewa jina la barabara inayokatiza ikulu inanitatiza kidogo.
 
Hili la Obama kupewa jina la barabara inayokatiza ikulu inanitatiza kidogo.
Hatuna utaratibu ulioainishwa kuhusu namna gani majina yanatolewa

In fact hiyo haikuwa kazi ya Ikulu, ilikuwa jukumu la serikali za mitaa
Inapobidi kama tungekuwa na kamisheni maalumu, hali isingefikia mahali ambapo watu wanakaa katika chai na kuamua tu bila kuwa na vigezo
 
Zamani ili kujenga mshikamano wa kitaifa mitaa katika miji mikubwa iliitwa majina ya mikoa mbalimbali, au vitu vya humuhumu nchini kwa mfano mtaa wa tanga, mtaa wa bukoba, mtaa wa Arusha hii ni mitaa inayopatikana ilala Dar es salaam.

Huu ni wakati muafaka wa kuiweka historia ya Tanzania na Jiografia yake katika enzi ya vitu vya thamani tunavyovijenga. Pale South Afrika kuna uwanja wa ndege wa Oliver Tambo, Tambo ni mpigania uhuru lakini hajawahi kuwa raisi wa South Afrika, hata hivyo ameenziwa kwa ule uwanja ulioko Jo' berg. Sisi Kila kitu ni Nyerere! Aaaaaah Jamani Comeon!
 
Mada hii inaweza kuonekana ni rahisi pengine haina mantiki.
Ukweli ni kuwa hii mada ni muhimu sana kwa Taifa letu.

Nasema hayo kwasababu tatizo tunalolijadili ni kubwa kuliko linavyoonekana.

Sote tunafahamu maana ya alama za Taifa ziwe katika maumbo au majina.
Kwa mfano, ule mnara wa askari pale Posta unaweza kuonekana kama sanamu tu.

Uzuri wa uwepo wake ni kuamsha udadisi 'curiosity' kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Unaweza kumsikiliza mbunge wa bunge la JMT katika video hapo chini ukaona kwanini tuna tatizo. Msikilize mwenyewe kisha utafakari

VIDEO: Mbunge aliyempongeza Diamond Platnumz
 
Zamani ili kujenga mshikamano wa kitaifa mitaa katika miji mikubwa iliitwa majina ya mikoa mbalimbali, au vitu vya humuhumu nchini kwa mfano mtaa wa tanga, mtaa wa bukoba, mtaa wa Arusha hii ni mitaa inayopatikana ilala Dar es salaam.

Huu ni wakati muafaka wa kuiweka historia ya Tanzania na Jiografia yake katika enzi ya vitu vya thamani tunavyovijenga. Pale South Afrika kuna uwanja wa ndege wa Oliver Tambo, Tambo ni mpigania uhuru lakini hajawahi kuwa raisi wa South Afrika, hata hivyo ameenziwa kwa ule uwanja ulioko Jo' berg. Sisi Kila kitu ni Nyerere! Aaaaaah Jamani Comeon!
Kikwete tumpe nini?
 
Ni kweli hata mimi natatizika kila kitu tunapachika jina la Nyerere wakati wapo watu wengi waliostahili kupewa heshima.
Tuna tatizo kubwa sana na halitandoka hadi tuwe na kamisheni maalumu ya kutangaza au kutoa majina ya maeneo au sehemu muhimu za Taifa letu

Tunaongozwa na chuki na hisia za kisiasa ili kufuta historia hata kama ndivyo ilivyo.

Kwa mfano, wapi jina la mwisho la gavana aliyetoa uhuru kwa Tanganyika?

Ni mkoloni, lakini historia ndivyo inavyosema na inapaswa tuienzi kama ilivyo

Kule Polanda kambi za mauaji ya wayahudi zipo. Gold cost kuna point of no return, ikionyesha uchungu mkubwa sana wa utumwa.

Leo akina Obama wanakwenda kujionea madhila hata kama ilikuwa na machungu kiasi gani. Ndiyo historia, haiandikwi wala kufutwa ipo kama ilivyo

Wapi kuna alama ya Jina la Tanganyika?

Hata kama halitakiwi kwasababu za kisiasa, kwasababu za kihistoria haliwezi kufutwa kamwe. Nyerere alipewa Tanganyika si Tanzania

Tunataka vijana wetu wakalisikie jina hilo katika vipindi vya 'Jeopardy' kweli

Hatuwezi kukataa ukweli kuwa Mzizima ndiyo Dar . Na hapa naomba kuwa biased, wakazi wa Dar hatujawapa heshima ya mji wao kama inavyostahili.

Jina la Mzizima halipaswi kufutwa, ndiyo Dar yenyewe. Afrika kusini leo wanakumbuka 'Polkwane' kama sijakosea ambayo ni Pretoria. Haibadilishi kitu lakini ina maana sana

Viongozi wetu hawana maono, kila anayeibuka anataka umaarufu tu na njia ya mkato ni kupitia jina la Nyerere.

Well, lazima tuwe na kitu kinacholingana na hadhi yake, si kila structure Nyerere tu.

Hatuna thamani zingine au mashujaa kama Taifa kweli!
 
Back
Top Bottom