Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Kama kawaida, kila nikipata fursa ya kuandika, huwa naandika mfululizo wa makala hizi ziitwazo "Kwa Maslahi ya Taifa" zenye lengo la kuhamasisha uzalendo miongoni mwa Watanzania, ambazo huandikwa kwa mfumo wa maswali na huchapishwa katika gazeti la Habari Leo, kila siku za Jumatano. In near future makala hizi zitandamanana na vipindi vya TV, TV Series, ambapo taratibu za udhamini zikikamilika, vipindi vya vitaonekana kwenye TV.
Kwa wiki hii nazungumzia umuhimu wa Umoja na Mshikamano kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, ndio siri pekee ya mafanikio ya vita yoyote duniani. Swali ni "Jee Hili Janga la Corona ni Vita?. Jee sisi Watanzania, serikali yetu, CCM, Wapinzani, bila kuwa wamoja, kusimama pamoja kwa upendo, mshikamano na ushirikiano wa kupigana kwa pamoja kwa lengo moja, kwa nguvu moja, kwa sauti moja, jee tutaweza kweli kushinda vita hii?!.
Janga la Corona ni vita, ili tushinde vita yoyote ni lazima sisi Watanzania, kuanzia serikali yetu, CCM, wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla wetu, tuwe kitu kimoja, tuwe wamoja, tusimame pamoja kwa upendo na mshikamano kwa kufanya kila kitu kwa pamoja, kwa ushirikiano na kuwa kitu kimoja, kwa kuunganisha nguvu zetu zote ziwe ni nguvu moja ya pamoja, tupaze sauti zetu zote ziwe ni sauti moja, na tupambane bega kwa bega kwa mshikamano wa nguvu moja, sauti moja na lengo moja la ushindi, ndio tutashinda vita hii!. Tukiendelea kuipigana vita hii kwa hivi hivi tunavyokwenda sasa, kwa kila mtu kusema lwakwe...
Tukipambana na Corona bila kusimama pamoja, huku kila mtu amesimama kivyake, anasema lake, kama hali ilivyo sasa, rais kusema hili, serikali kusema hili, Waziri Mkuu kusema lile, Waziri wa Afya kusema lake, CCM kuifananisha Corona na Wapinzani, Wapinzani kusema Serikali inaficha takwimu, wananchi kuruhusiwa kutumia barakoa za vitambaa, wataalamu kusema yao, wananchi kuruhusiwa kutumia tiba asili na tiba mbadala ikiwemo kujifukiza, wataalamu wa afya kupishana, mbuzi na hadi papai kukutwa na virusi vya Corona, kiukweli ni mchanganyiko mkubwa, kunatuchanganya sisi Watanzania tusijue tufuate lipi, tumwamini nani, kuna msemo usemao miluzi mingi humpoteza mbwa mwelekeo, humchanganya asijue afuate lipi aache lipi na mwisho hubaki ameduwaa asijue la kufanya!.
Ili tushinde vita hii, ni lazima kwanza viongozi wetu wazungumze kwa lugha moja na kutoa kauli moja thabiti ili sisi Watanzania tufuate moja, tusimame pamoja kwa upendo na mshikamano as as one, tupigane pamoja, kwa nguvu moja, sauti moja na lengo moja, ndio tutashinda vita hii.
Tangu kuanza kwa vita hii, mpaka hapa tulipo, Watanzania tumegawanyika, hivyo hatua ya kwanza ni kwa baba mwenye nyumba wetu, rais Magufuli kutuleta pamoja sisi watoto wake wote wa nyumba yake kuanzia yeye mwenyewe kama Baba, serikali yake, CCM, Wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla, atulete pamoja, tuwe wamoja, kitu kimoja, tuongee kwa lugha moja, sauti moja, nguvu moja na lengo moja la kushinda vita, ndio tutashinda vita hii.
Hili litafanyikaje?, hili litafanyika hatua kwa hatua,
Namalizia kwa lile swali langu la wa mwanzo wa bandiko hili, hivi hili janga la Corona ni vita kweli ya wote au ni vita ya serikali pekee?. Kama ni vita ya wote, mbona hatujashirikishwa kikamilifu ipasavyo?. Mbona karibu kila kitu ni kama ni serikali tuu?. Jee tunaweza tushinde vita hii bila sisi Watanzania, kuanzia serikali, CCM, wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla wetu, kushirikishwa kikamilifu, tuwe wamoja?, tusimame pamoja kama kitu kimoja, kwa kuunganisha nguvu zetu zote kwa pamoja chini ya umoja ni nguvu, ziwe ni nguvu moja kuu, tupaze sauti zetu zote ziwe ni sauti moja, na tumbambane kwa mshikamamo, bega kwa bega kwa lengo moja?.
Its Only Pamoja Tutashinda!.
Nawatakia Jumanne Njema.
Paskali

- Hatua ya Kwanza ni Ushirikishwaji - japo Corona ni vita, na tangu kutangazwa kwa vita hii, Amiri Jeshi wetu Mkuu, amechukua vikosi vyake vya kiserikali tuu na kutangaza vita. Bahati nzuri wakati wa vita vya Kagera, japo nilikuwa mdogo, lakini tayari nilikuwa shule ya msingi, kabla ya kutangaza vita, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alituhamasisha, tukahamasika kwa uzalendo, ndipo alilihutubia taifa na kusisitiza uzalendo, kujitoa, umoja, na mshikamano wa Watanzania wote na kuitoa ile hotuba maarufu ya " Nia, Sababu na Uwezo". Lakini kwa hapa Tanzania kwenye vita hii, tangu janga hili limeanza, serikali ndio imehodhi ukamanda na wapiganaji wa vita hii, kwa kuunda kamati 3 za kiserekali tuu za kushughulikia, Kamati ya Mawaziri, Kamati ya Wakatibu Wakuu na Kamati ya Wataalamu wa serikalini. Mawaziri ni ya serikali, Makatibu Wakuu ni wa Serikali,kwa nini hao wataalamu ni wa serikali tuu?!. Hapa kunahitajika uwazi na ushirikishwaji umma, hivyo sasa uindwe kamati ya kitaifa, kwa serikali kuomba ushirikishwaji wa Watanzania wote wenye mawazo yoyote chanya ya kusaidia, wakiwemo wana Diaspora, wayalete on line, out of mawazo hayo, inaundwa kamati shirikishi ya kitaifa ambayo itajumuisha sekta zote, sio hali ilivyo sasa, vita hii inaweza kuwa inaongozwa na kamanda kama Goliati, akitegemea nguvu zake na serikali yake pekee, kumbe kuna akina Daudi wengi tuu wapo na wangeweza kusaidia sana kama wangeshirikishwa lakini wamejinyamazia tuu kimya kwa sababu hawajashirikishwa!.
- Korona ni Janga, Ni Vita, Vita Ikiisha Tangazwa, Amri ni Moja, Umoja, Mshikamano, Ushirikiano Ndio Siri ya Ushindi!-Korona ni janga, ni vita, vita ikiishatangazwa, ili tushinde vita hii ni lazima viongozi wetu wa serikali, wanasiasa, wapinzani, wataalamu, wote tuzungumze kwa lugha moja, sauti moja na kauli moja iliyooka. Amiri Jeshi Mkuu au serikali ikiishasema jambo fulani, mfano idadi ya waliokufa ni idadi fulani, sheria ya kivita inatumika, waliokufa ni idadi hiyo hiyo iliyotangazwa!, hata kama mtu umeona na kushuhudia kwenye mitandao ya kijamii miili 100 inazikwa!, bado una wajibu wa kuisema ile ile idadi tuu iliyotangazwa rasmi na serikali. Haiwezekani tuko vitani, leo Waziri Mkuu anatutangaza idadi ya vifo ni kadhaa, halafu kesho wewe kwasababu ni kiongozi wa chama cha upinzani, ukaitisha press conference, na kuituhumu serikali kuwa haisemi kweli! na badala yake unaleta idadi ya vifo vya mitandaoni!, what does this mean?!. Tutawachanganya Watanzania!, hizi idadi za kwenye mitandao, waachiwe watu wa mitandaoni, kwenye hili lazima serikali, wapinzani mzungumze kwa lugha moja na kauli moja kwa maslahi ya taifa!, kama ushirikishwaji ungefanyika mwanzo, nimemshuhudia Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli, akitusisitiza Watanzania wote kuwa hii vita ni yetu sote, CCM, Wapinzani, na Watanzania wote kuweka pembeni tofauti zao za kisiasa na kuwa kitu kimoja kwa kushikamana pamoja, kuunganisha nguvu ya pamoja na kupigana kwa pamoja, tutashinda. Haiwezekani Waziri Mkuu ataje idadi ya vifo, halafu kesho yake waziri mkuu kivuli kuibuka na kusema serikali inasema uongo. Ile kanuni ya a collective responsibility inakuwa applicable kwenye hili la Corona tuongee kwa kauli moja, sauti moja na kupigana kwa nguvu moja na lengo moja... Tutashinda.
- Watanzania Wenye Uwezo Kusaidia, Wasaidie, Serikali Pekee Haiwezi Kila Kitu. - kama zilivyo vita nyingine zote, umoja ni nguvu, hatuwezi kuiachia serikali kufanya kila kitu, serikali pekee haiwezi, hivyo kufanyike resources mobilization kwa kila Mtanzania kujitolea kuchangia kwa uwezo wake kama nilivyoshauri hapa wakiwemo wenye uwezo wa ziada na uzoefu wajitokeze, waitwe, washirikishwe, wakiwemo ma veterani wa utatibu na wa kila fani, huitwa kwenye kupanga mikakati, sisi ma veterani kwenye sekta ya media tupo, tuitwe, tushirikishwe, miongoni mwetu kuna mabingwa wa utoaji elimu kwa umma, tuwe recalled turudi newsrooms tukawasaidie hawa vijana wa sasa suala zima la utoaji wa elimu ya umma, hili lingefanyika tangu mwanzo, tungewasaidia sana Watanzania, ila hadi hapa tulipo, hatujachelewa!. Media zetu hazina uwezo wa utoaji elimu, hivyo media ziwezeshwe, maveterani tuitwe turudi newsroom tusaidie.
- Japo Serikali inafanya hatua mbalimbali za utekeleza kukabiliana janga hili, hazitoshi, more needs to be done, namuomba rais wetu Magufuli na serikali yetu iwe sikivu, isishupaze shingo kwa kujifanya yenyewe ndio inajua kila kitu, usikilize maoni ya wadau, wakiwemo wapinzani, mfano hoja ya partial lockdown, kwenye mikusanyiko ya ibada, Mungu ni Omnipresent, hakai kanisani kwenye nyumba za ibada tuu yupo popote na watu wanaweza kusalia popote.
- Viongozi wa Dini, Imani, Waheshimiwe na Viongozi wa Siasa. kama Vatican kwenye shina la Ukatoliki, na Saudi Arabia kwenye shina la Uislamu, wao wamefunga, kitendo alichokifanya Baba Askofu Severin Niwemugizi. Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, la kuepusha waumini wake na janga la Corona kwa kufunga ibada kwenye jimbo lake ni kitendo cha kupigiwa mfano, unless kama ibada nayo ni uzalishaji mali za kanisa na nchi!. Nakuomba Rais wetu Magufuli asiwabeze hawa viongozi wa dini au wa kiimani kwa kutumia lugha na maneno ya ushetani, viongozi wengine wa dini za ukweli za Mungu wa kweli are very powerful, kama alivyokuwa akielezwa Sheikh Baramia wa Bagamoyo. Nyerere aliwaheshimu viongozi wa dini zote, wakiwemo masheikh na Maaskofu, sikuwahi kumsikia Mwinyi, Mkapa na Kikwete kupishana popote kauli na viongozi wa dini, hivyo kama ni kweli rais wetu Magufuli amepishana kauli na Askofu NiweMugizi wa jimbo lake kutokana na Askofu huyo kufanya lockdown huku rais Magufuli akiwa Chato, maana you never know inawezekana wanaoepusha misongamano ndio mpango wa Mungu halafu watete wa misongomano isiyo ya lazima kama ibada ndio mpango wa shetani, then tunamshauri rais Magufuli akamwangukie Askofu wake. Enzi za Nyerere, mimi nilikuwa nasali St. Peters, rais Nyerere alikuwa anapiga magoti kupokea Ekaristi Takatifu, kama ni kweli rais Magufuli kuna kauli anezitoa kumpinga Askofu wake, asione shida kujishusha na kwenda kumpigia goti Askofu wake aombe msamaha, maana hawa watu wa Mungu hawa...
- Redefining Roles za Upinzani Wakati wa Vita. Upinzani unaitwa opposition kumaanisha kupinga, lakini japo ni jukumu la upinzani kupinga na kukosoa, lakini sio lazima kupinga tuu kila kitu na kila wakati. Linapokuja suala la maslahi kwa taifa lenye national interests, CCM na Wapinzani wanapaswa kuweka tofauti zao pembeni na kuwa kitu kimoja, hivyo kwenye mazuri ya CCM kwa maslahi ya taifa, Wapinzani msione aibu kuiunga mkono CCM na kuipongeza, na CCM nayo pia inapokutana na hoja za upinzani zenye maslahi kwa taifa mfano inapokopy hoja nzuri au sera mzuri za wapinzani na kuzitekeleza, isione aibu kuwapongeza wapinzani kama hoja ya katiba mpya, elimu bure etc, lakini inapotangazwa vita, role ya upinzani changes, hakuna tena kupinga kitu chochote!, zinatumika martial laws, sheria za kijeshi, amri ni moja tuu, ama kuunga mkono, ama kunyamaza kimya!. Haiwezekani Amiri Jeshi Mkuu au serikali ikasema kitu fulani, halafu akatokea kiumbe mwingine akakohoa kuipinga serikali!. Hili ni jambo la ajabu sana!. Hii itakuwa sio vita bali ni kusemazana, kwenye vita hakuna kusemezani ni amri tuu, ikitolewa kauli yoyote rasmi ya serikali ni amri!.
- Kwa vile mpaka sasa Corona haina kinga wala tiba, naunga mkono juhudi zote zinazochukuliwa na serikali yetu kukabiliana na janga hili, tuendelee kufuata ushauri wote wa kitaalamu unaotolewa katika kukabiliana na janga hili, na kwa vile Corona ni adui asiyejulikana, tutumie silaha zote za ki sasa za hospitali za kiimali, tiba asili, tiba mbadala, na hata akitokea mtu akaoteshwa chochote, tusidharau, na hata kama ni kweli uchawi upo, na wachawi wapo, waruhusiwe kuiloga Corona ife, iishe tuendelee na maisha yetu bila kusahau kumtanguliza Mungu, maana bila YEYE sisi binaadamu pekee, Hatuwezi.