Je, Corona ni vita? Watanzania, Serikali yetu, CCM, Wapinzani bila umoja na mshikamano wa nguvu moja, lengo moja na sauti moja, tutaweza kushinda?

Ni kweli mkuu acha sisi wengine tubaki home tukisaidiana na watoto,vitani wanapaswa kwenda wapiga nyungu wa ukweli Kama wewe.Kuhusu hiyo tweet ya Lissu naomba kabla ya kumshutumu msikilize tena Magufuli? Je huwa anasema yeye ni mwanasayansi au huwa anasema tuna wanasayansi wengi pale anapoponda juhudi za watu wengine? Magufuli ameshajipambanua kuwa yeye anaweza kila kitu,yeye ndo anajua kila kitu,yeye ndo anajua vipi na yeye ndo anajua dawa ni ipi na inapatikana wapi,yeye ndo anajua mbinu za kupambana na corona na hawezi copy and paste.Sasa wewe ni nani unayetaka watu waungane nae wakati yeye hataki?
Kwa hiyo ndugu mzalendo, kwa kuwa raisi hashauriki na anajiona anayejua kila kitu ndiyo mnaamua kuombea tupoteze hii vita! Narudia, Magufuli na ccm wakipoteza hii vita ni taifa zima limepoteza. Acheni uzalendo wa kinafiki. Mjue kutofautisha vita za kitaifa na vita za kivyama. Unaweza ombea miradi kama SGR na JNHPP ifeli "nikakuelewa". Ila ukiombea tupoteze kwenye mapambano na corona eti kwa kuwa raisi hajachukua maoni yako nakuona kama mzalendo uchwara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo ndugu mzalendo, kwa kuwa raisi hashauriki na anajiona anayejua kila kitu ndiyo mnaamua kuombea tupoteze hii vita! Narudia, Magufuli na ccm wakipoteza hii vita ni taifa zima limepoteza. Acheni uzalendo wa kinafiki. Mjue kutofautisha vita za kitaifa na vita za kivyama. Unaweza ombea miradi kama SGR na JNHPP ifeli "nikakuelewa". Ila ukiombea tupoteze kwenye mapambano na corona eti kwa kuwa raisi hajachukua maoni yako nakuona kama mzalendo uchwara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Some of us have nothing to lose,maana tu wasindikizaji tu
 
Sasa mkuu paschal, unakwenda vitani na unabeba askari wenye mentality kama hizi halafu unategemea ushindi. Ni lini raisi alisema nchi ina akiba ya kuendesha nchi for 6 months? Wakati wa vita akili kama hizi unaziacha nyumbani zisaidiane na watoto na akina mama kuandaa vyakula kwa ajili ya wapambanaji.

Nchi hii haiwezi kwa sasa kuwa na akiba za kuendesha nchi kwa miezi sita bali huwa inakuwa na akiba ya kuweza "kuagiza bidhaa kutoka nje" kwa kipindi hicho. Kuweza kuagiza bidhaa kutoka nje ni kitu kimoja na kuweza kujiendesha ni kitu kingine.

Kimsingi simshauri raisi kusikiliza upinzani ambao kwao jang hili ni fursa ya kujitutumua na kuonesha namna gani CCM na Magufuli siyo watawala sahihi kwa nchi hii. Wakati wa mambo hayo si wakati wa majanga ambapo taifa zima lina common enemy.

Juzi hapo nimesoma twitter post ya Tundu Lissu akimnanga raisi kuwa vita hii itamshinda. Tafsiri ya kushindwa vita dhidi ya corona ni taifa zima kuangamia na kufutika kabisa! Sasa askari kama huyo kuchukua ushauri wake siyo kuamua kupoteza vita kwa kukusudia kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huez kushirikiana na jeshi ambalo halikutaki.

Vita hii naifananisha na vita ya Syria
Serikali ina jeshi lake,kuna waasi wana vikosi vyao kuna IS ukiangalia kila mtu anapigana kwa maslahi yake.
Serikali haitaki kushirikiana na waasi lakini wote wanapigana na IS na waasi hawataki kushirikiana na serikali sababu hawajaitwa kushirikiana. Corona ni adui wa kila mtu kama serikali imeshindwa kuwaunganisha wapiganaji bas kushindwa lazma.

Sioni kosa la wapinzani kwa sababu wao wenyewe wanapigana lakini serikali imedharau nguvu yao.
 
Kwa hiyo ndugu mzalendo, kwa kuwa raisi hashauriki na anajiona anayejua kila kitu ndiyo mnaamua kuombea tupoteze hii vita! Narudia, Magufuli na ccm wakipoteza hii vita ni taifa zima limepoteza. Acheni uzalendo wa kinafiki. Mjue kutofautisha vita za kitaifa na vita za kivyama. Unaweza ombea miradi kama SGR na JNHPP ifeli "nikakuelewa". Ila ukiombea tupoteze kwenye mapambano na corona eti kwa kuwa raisi hajachukua maoni yako nakuona kama mzalendo uchwara.

Sent using Jamii Forums mobile app
:D🤣
 
Watafuta kiki katika siasa nguvu zao wakizielekeza katika vita dhidi ya CORONA hakika sehemu kubwa tutashinda.
 
Huyu Paskali na wasukuma wengine wengi wapo katika kundi la gwajiboy. Na wanaambizana ujinga kwamba hakuna kum-criticize Magufail kwa chochote. Haya ndio matokeo yake. Anatuletea ... humu ndani, akiungwa mkono na wasukuma wengine na misukule ya pale lumumba.
Duh...!, karibu huku auangalie tunavyosifu!.
Japo Serikali inafanya hatua mbalimbali za utekeleza kukabiliana janga hili, hazitoshi, more needs to be done, naiomba serikali yetu iwe sikivu, isishupaze shingo kwa kujifanya yenyewe ndio inajua kila kitu, usikilize maoni ya wadau, wakiwemo wapinzaia, mfano hoja ya partial lockdown, kwenye mikusanyiko ya ibada, Mungu ni Omnipresent, hakaini kanisani kwenye nyumba za ibada tuu yupo popote na watu wanaweza kusalia popote, kama Vatican kwenye shina la Ukatoliki, na Saudi Arabia kwenye shina la Uislamu, wao wamefunga, kitendo alichokifanya Baba Askofu Severin Niwemugizi. Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, la kuepusha waumini wake na janga la Corona kwa kufunga ibada kwenye jimbo lake ni kitendo cha kupigiwa mfano, unless kama ibada nayo ni uzalishaji mali za kanisa na nchi!. Rais wetu asiwabeze viongozi wa dini kwa kutumia maneno ya ushetani, maana you never know inawezekana wanaoepusha misongamano ndio mpango wa Mungu halafu watete wa misongomano isiyo ya lazima kama ibada ndio mpango wa shetani.
Paskali
P
 
Wanabodi,
.Japo Serikali inafanya hatua mbalimbali za utekeleza kukabiliana janga hili, hazitoshi, more needs to be done, naiomba serikali yetu iwe sikivu, isishupaze shingo kwa kujifanya yenyewe ndio inajua kila kitu, usikilize maoni ya wadau, wakiwemo wapinzaia, mfano hoja ya partial lockdown, kwenye mikusanyiko ya ibada, Mungu ni Omnipresent, hakaini kanisani kwenye nyumba za ibada tuu yupo popote na watu wanaweza kusalia popote, kama Vatican kwenye shina la Ukatoliki, na Saudi Arabia kwenye shina la Uislamu, wao wamefunga, kitendo alichokifanya Baba Askofu Severin Niwemugizi. Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, la kuepusha waumini wake na janga la Corona kwa kufunga ibada kwenye jimbo lake ni kitendo cha kupigiwa mfano, unless kama ibada nayo ni uzalishaji mali za kanisa na nchi!. Rais wetu asiwabeze viongozi wa dini kwa kutumia maneno ya ushetani, maana you never know inawezekana wanaoepusha misongamano ndio mpango wa Mungu halafu watete wa misongomano isiyo ya lazima kama ibada ndio mpango wa shetani.
Nawatakia Jumanne Njema.
Paskali
Pole yake Pasco Mayalla,na huu uteuzi umrmpita licha ya juzi kuramba miguu kupitia 🌟 tv
P
 
Wanabodi,

Kama kawaida, kila nikipata fursa ya kuandika, huwa naandika mfululizo wa makala hizi ziitwazwa "Kwa Maslahi ya Taifa" zenye lengo la kuhamasisha uzalendo miongoni mwa Watanzania, ambazo huandikwa kwa mfumo wa maswali na huchapishwa katika gazeti la Habari Leo, kila siku za Jumatano, hivi makala hizi huandamanana na vipindi vya TV, TV Series, ambapo taratibu za udhamini zikikamilika, vipindi vya vitaonekana kwenye TV. Kwa wiki hii nazungumzia umuhimu wa Umoja na Mshikamano kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, ndio siri pekee ya mafanikio ya vita yoyote duniani. Swali ni "Jee Hili Janga la Corona ni Vita?. Jee sisi Watanzania, serikali yetu, CCM, Wapinzani, bila kuwa wamoja, kusimama pamoja kwa upendo, mshikamano na ushirikiano wa kupigana kwa pamoja kwa lengo moja, kwa nguvu moja, kwa sauti moja, jee tutaweza kweli kushinda vita hii?!.

Janga la Corona ni Vita, ili tushinde vita yoyote ni lazima sisi Watanzania, kuanzia serikali yetu, CCM, wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla wetu, tuwe kitu kimoja, tuwe wamoja, tusimame pamoja kwa upendo na mshikamano kwa kufanya kila kitu kwa pamoja, kwa ushirikiano na kuwa kitu kimoja, kwa kuunganisha nguvu zetu zote ziwe ni nguvu moja ya pamoja, tupaze sauti zetu zote ziwe ni sauti moja, na tupambane kwa mshikamamo, bega kwa bega kwa nguvu moja, sauti moja na lengo moja la ushindi, ndio tutashinda vita hii!, tukiendelea hivi hivi tunavyokwenda sasa, kwa kila mtu kusema lwakwe...

Tukipambana na Corona bila kusimama pamoja, huku kila mtu amesimama kivyake, anasema lake, kama hali ilivyo sasa, kwa serikali kusema hili, rais kusema hili, Waziri Mkuu kusema lile, Waziri wa Afya kusema lake, CCM kuifananisha Corona na Wapinzani, Wapinzani kusema Serikali inaficha takwimu, wananchi kuruhusiwa kutumia barakoa za vitambaa, wataalamu kusema yao, wananchi kuruhusiwa kutumia tiba asili na tiba mbadala ikiwemo kujifukiza, wataalamu wa afya kupishana, mbuzi na hadi papai kukutwa na virusi vya Corona, kiukweli ni mchanganyiko mkubwa, kunatuchanganya sisi Watanzania tusijue tufuate lipi, tumwamini nani, kuna msemo usemao miluzu mingi humpoteza mbwa mwelekeo, humchanganya asijue afuate lipi aache lipi na mwisho hubaki ameduwaa asijue la kufanya!.

Ili tushinde vita hii, ni lazima kwanza viongozi wetu wazungumze kwa kauli moja thabiti, ili sisi Watanzania tufuate moja, tusimame pamoja kwa upendo na mshikamano as as one, tupigane pamoja, kwa nguvu moja, sauti moja na lengo moja, ndio tutashinda vita hii.

Tangu kuanza kwa vita hii, mpaka hapa tulipo, Watanzania tumegawanyika, hivyo hatua ya kwanza ni kwa baba mwenye nyumba wetu, rais Magufuli kutuleta pamoja sisi watoto wake wote wa nyumba yake kuanzia yeye mwenyewe kama Baba, serikali yake, CCM, Wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla, atulete pamoja, tuwe wamoja, kitu kimoja, tuongee kwa lugha moja, sauti moja, nguvu moja na lengo moja la kushinda vita, ndio tutashinda vita hii.

Hili litafanyikaje?, hili litafanyika hatua kwa hatua,
  1. Hatua ya Kwanza ni Ushirikishwaji - japo Corona ni vita, na tangu kutangazwa kwa vita hii, Amiri Jeshi wetu Mkuu, amechukua vikosi vyake vya kiserikali tuu na kutangaza vita. Bahati nzuri wakati wa vita vya Kagera, japo nilikuwa mdogo, lakini tayari nilikuwa shule ya msingi, kabla ya kutangaza vita, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alituhamasisha, tukahamasika kwa uzalendo, ndipo alilihutubia taifa na kusisitiza uzalendo, kujitoa, umoja, na mshikamano wa Watanzania wote na kuitoa ile hotuba maarufu ya " Nia, Sababu na Uwezo". Lakini kwa hapa Tanzania kwenye vita hii, tangu janga hili limeanza, serikali ndio imehodhi ukamanda na wapiganaji wa vita hii, kwa kuunda kamati 3 za kiserekali za kushughulikia, Kamati ya Mawaziri, Kamati ya Wakatibu Wakuu na Kamati ya Wataalamu. Mawaziri ni ya serikali, Makatibu Wakuu ni wa Serikali, hao wataalamu ni kina nani?, hapa kunahitajika uwazi na ushirikishwaji umma, hivyo sasa uindwe kamati ya kitaifa, kwa serikali kuomba ushirikishwaji wa Watanzania wote wenye mawazo yoyote chanya ya kusaidia, wakiwemo wa Diaspora, wayalete on line, out of mawazo hayo, inaundwa kamati shirikishi ya kitaifa ambayo itajumuisha sekta zote, sio hali ilivyo sasa, vita hii inaweza kuwa inaongozwa na kama kama Goliati, akitegemea nguvu zake na serikali yake pekee, kumbe kuna akina Daudi wengi tuu wapo na wangeweza kusaidia sana kama wangeshirikishwa lakini wamejinyamazia tuu kimya kwa sababu hawajashirikishwa!.
  2. Korona ni Janga, Ni Vita, Vita Ikiisha Tangazwa, Amri ni Moja, Umoja, Mshikamano, Ushirikiano Ndio Siri ya Ushindi!-Korona ni janga, ni vita, vita ikiishatangazwa, ili tushinde vita hii ni lazima viongozi wetu wa serikali, wanasiasa, wapinzani, wataalamu, wote tuzungumze kwa lugha moja, sauti moja na kauli moja iliyooka. Amiri Jeshi Mkuu au serikali ikiishasema jambo fulani, mfano idadi ya waliokufa ni idadi fulani, sheria ya kivita inatumika, waliokufa ni idadi hiyo hiyo iliyotangazwa!, hata kama mtu umeona na kushuhudia kwenye mitandao ya kijamii miili 100 inazikwa!, bado una wajibu wa kuisema ile idadi tuu iliyotangazwa rasmi na serikali. Haiwezekani tuko vitani, leo Waziri Mkuu akatutangaza idadi ya vifo ni kadhaa, halafu kesho wewe kwasababu ni kiongozi wa chama cha upinzani, ukaitisha press conference, na kuituhumu serikali kuwa haisemi kweli! na badala yake unaleta idadi ya vifo vya mitandaoni!, what does this mean?!. Tutawachanganya Watanzania!, hizi idadi za kwenye mitandao, waachiwe watu wa mitandaoni, kwenye hili lazima serikali, wapinzani mzungumze kwa lugha moja na kauli moja kwa maslahi ya taifa!, kama ushirikishwaji ungefanyika mwanzo, nimemshuhudia Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli, akitusisitiza Watanzania wote kuwa hii vita ni yetu sote, CCM, Wapinzani, na Watanzania wote kuweka pembeni tofauti zetu na kushikamana pamoja, kuunganisha nguvu ya pamoja na kupigana kwa pamoja, tutashinda. Haiwezekani Waziri Mkuu ataje idadi ya vifo, halafu kesho yake waziri mkuu kivuli kuibuka na kusema serikali inasema uongo. Ile kanuni ya a collective responsibility inakuwa applicable kwenye hili la Corona tuongee kwa kauli moja, sauti moja na kupigana kwa nguvu moja na lengo moja... Tutashinda.
  3. Watanzania Wenye Uwezo Kusaidia, Wasaidie, Serikali Pekee Haiwezi Kila Kitu. - kama zilivyo vita nyingine zote, umoja ni nguvu, hatuwezi kuiachia serikali kufanya kila kitu, serikali pekee haiwezi, hivyo kufanyike resources mobilization kwa kila Mtanzania kujitolea kuchangia kwa uwezo wake kama nilivyoshauri hapa wakiwemo wenye uwezo wa ziada na uzoefu wajitokeze, waitwe, washirikishwe, wakiwemo ma veterani wa utatibu na wa kila fani, huitwa kwenye kupanga mikakati, sisi ma veterani kwenye sekta ya media tupo, tuitwe, tushirikishwe, miongoni mwetu kuna mabingwa wa utoaji elimu kwa umma, tuwe recalled turudi newsrooms tukawasaidie hawa vijana wa sasa suala zima la utoaji wa elimu ya umma, hili lingefanyika tangu mwanzo, tungewasaidia sana Watanzania, ila hadi hapa tulipo, hatujachelewa!. Media zetu hazina uwezo wa utoaji elimu, hivyo media ziwezeshwe, maveterani tuitwe turudi newsroom tusaidie.
  4. Japo Serikali inafanya hatua mbalimbali za utekeleza kukabiliana janga hili, hazitoshi, more needs to be done, naiomba serikali yetu iwe sikivu, isishupaze shingo kwa kujifanya yenyewe ndio inajua kila kitu, usikilize maoni ya wadau, wakiwemo wapinzaia, mfano hoja ya partial lockdown, kwenye mikusanyiko ya ibada, Mungu ni Omnipresent, hakaini kanisani kwenye nyumba za ibada tuu yupo popote na watu wanaweza kusalia popote, kama Vatican kwenye shina la Ukatoliki, na Saudi Arabia kwenye shina la Uislamu, wao wamefunga, kitendo alichokifanya Baba Askofu Severin Niwemugizi. Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, la kuepusha waumini wake na janga la Corona kwa kufunga ibada kwenye jimbo lake ni kitendo cha kupigiwa mfano, unless kama ibada nayo ni uzalishaji mali za kanisa na nchi!. Rais wetu asiwabeze viongozi wa dini kwa kutumia maneno ya ushetani, maana you never know inawezekana wanaoepusha misongamano ndio mpango wa Mungu halafu watete wa misongomano isiyo ya lazima kama ibada ndio mpango wa shetani.
  5. Redefining Roles za Upinzani Wqkati wa Vita. Upinzani unaitwa opposition kumaanisha kupinga, lakini japo ni jukumu lake kupinga na kukosoa, lakini sio lazima kupinga tuu kila kitu, linapokuja suala la maslahi kwa taifa lenye national interests, CCM na Wapinzani wanapaswa kuweka tofauti zao pembeni na kuwa kitu kimoja, hivyo kwenye mazuri ya CCM kwa maslahi ya taifa, Wapinzani msione aibu kuiunga mkono CCM na kuipongeza, na CCM nayo pia inapokutana na hoja za upinzani zenye maslahi kwa taifa mfano inapokopy hoja nzuri au sera mzuri za wapinzani na kuzitekeleza, isione aibu kuwapongeza wapinzani kama hoja ya katiba mpya, elimu bure etc, lakini inapotangazwa vita, role ya upinzani changes, hakuna tena kupinga kitu chochote!, zinatumika martial laws, sheria za kijeshi, amri ni moja tuu, ama kuunga mkono, ama kunyamaza kimya!. Haiwezekani Amiri Jeshi Mkuu au serikali ikasema kitu fulani, halafu akatokea kiumbe mwingine akakohoa kuipinga serikali!. Hili ni jambo la ajabu sana!. Hii itakuwa sio vita bali ni kusemazana, kwenye vita hakuna kusemezani ni amri tuu, ikitolewa kauli yoyote rasmi ya serikali ni amri!.
  6. Kwa vile mpaka sasa Corona haina kinga wala tiba, naunga mkono juhudi zote zinazochukuliwa na serikali yetu kukabiliana na janga hili, tuendelee kufuata ushauri wote wa kitaalamu unaotolewa katika kukabiliana na janga hili, na kwa vile Corona ni adui asiyejulikana, tutumie silaha zote za ki sasa za hospitali za kiimali, tiba asili, tiba mbadala, na hata akitokea mtu akaoteshwa chochote, tusidharau, na hata kama ni kweli uchawi upo, na wachawi wapo, waruhusiwe kuiloga Corona ife iishe tuendelee na maisha yetu bila kusahau kumtanguliza Mungu, maana bila YEYE sisi binaadamu pekee, Hatuwezi.
Hitimisho.
Namalizia kwa lile swali langu la wa mwanzo wa bandiko hili, hivi hili janga la Corona ni vita kweli ya wote au ni vita ya serikali pekee?. Kama ni vita ya wote, mbona hatujashirikishwa kikamilifu ipasavyo?. Mbona karibu kila kitu ni kama ni serikali tuu?. Jee tunaweza tushinde vita hii bila sisi Watanzania, kuanzia serikali, CCM, wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla wetu, kushirikishwa kikamilifu, tuwe wamoja?, tusimame pamoja kama kitu kimoja, kwa kuunganisha nguvu zetu zote kwa pamoja chini ya umoja ni nguvu, ziwe ni nguvu moja kuu, tupaze sauti zetu zote ziwe ni sauti moja, na tumbambane kwa mshikamamo, bega kwa bega kwa lengo moja?.
Its Only Pamoja Tutashinda!.

Nawatakia Jumanne Njema.

Paskali
Wandugu, hapa nafanya tuu follow up ya Corona nikipitia kujikumbusha niliwahi kuandika nini au kusema nini kuhusu Corona na hiki kinacho endelea sasa. Corona is real tusifanye masihara, tujilinde kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi , Star TV, huwa ninakuwa live kwenye kipindi cha TV cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho huwa kinatangwa live na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi, kwa Jumamosi ya kesho, mgeni wetu ni Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe tukijadili kuhusu athari za Corona kwenye sekta ya Habari, nini kifanyike.

Ukipata nafasi karibu utufuatilie.

P
 
Viongozi wa Dini, Imani, Waheshimiwe na Viongozi wa Siasa. kama Vatican kwenye shina la Ukatoliki, na Saudi Arabia kwenye shina la Uislamu, wao wamefunga, kitendo alichokifanya Baba Askofu Severin Niwemugizi. Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, la kuepusha waumini wake na janga la Corona kwa kufunga ibada kwenye jimbo lake ni kitendo cha kupigiwa mfano, unless kama ibada nayo ni uzalishaji mali za kanisa na nchi!. Nakuomba Rais wetu Magufuli asiwabeze hawa viongozi wa dini au wa kiimani kwa kutumia lugha na maneno ya ushetani, viongozi wengine wa dini za ukweli za Mungu wa kweli are very powerful, kama alivyokuwa akielezwa Sheikh Baramia wa Bagamoyo. Nyerere aliwaheshimu viongozi wa dini zote, wakiwemo masheikh na Maaskofu, sikuwahi kumsikia Mwinyi, Mkapa na Kikwete kupishana popote kauli na viongozi wa dini, hivyo kama ni kweli rais wetu Magufuli amepishana kauli na Askofu NiweMugizi wa jimbo lake kutokana na Askofu huyo kufanya lockdown huku rais Magufuli akiwa Chato, maana you never know inawezekana wanaoepusha misongamano ndio mpango wa Mungu halafu watete wa misongomano isiyo ya lazima kama ibada ndio mpango wa shetani, then tunamshauri rais Magufuli akamwangukie Askofu wake. Enzi za Nyerere, mimi nilikuwa nasali St. Peters, rais Nyerere alikuwa anapiga magoti kupokea Ekaristi Takatifu, kama ni kweli rais Magufuli kuna kauli anezitoa kumpinga Askofu wake, asione shida kujishusha na kwenda kumpigia goti Askofu wake aombe msamaha, maana hawa watu wa Mungu hawa...
Paskali
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Katika bandiko hili la mwezi April, 2016, kuna mstari nilizungumzia kitu kinachoitwa karma ya watumbuliwa ambao hawakutumbuliwa kwa haki.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Katika bandiko hili la mwezi April, 2016, kuna mstari nilizungumzia kitu kinachoitwa karma ya watumbuliwa ambao hawakutumbuliwa kwa haki.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
Mkuu naona unaplace shifting gear....Sawa bwana.

Pumzika kwa amani JPM.
 
Ndio naaga aga kwa kufunga The Magufuli chapter, akiisha pumzishwa tumuache apumzike kwa amani.

P
Akizikwa mazuri yote (kama alikuwa nayo) atazikwa nayo na kusahaulika mara moja badala yake yataibuka mabaya yake yote ambayo ni mengi sana na yaliwaathiri wengi ambao watayakumbuka muda mrefu ujao mpaka nao wazikwe. Tenda wema nenda zako, Pascal!
 
Wanabodi,

Kama kawaida, kila nikipata fursa ya kuandika, huwa naandika mfululizo wa makala hizi ziitwazo "Kwa Maslahi ya Taifa" zenye lengo la kuhamasisha uzalendo miongoni mwa Watanzania, ambazo huandikwa kwa mfumo wa maswali na huchapishwa katika gazeti la Habari Leo, kila siku za Jumatano. In near future makala hizi zitandamanana na vipindi vya TV, TV Series, ambapo taratibu za udhamini zikikamilika, vipindi vya vitaonekana kwenye TV.

Kwa wiki hii nazungumzia umuhimu wa Umoja na Mshikamano kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, ndio siri pekee ya mafanikio ya vita yoyote duniani. Swali ni "Jee Hili Janga la Corona ni Vita?. Jee sisi Watanzania, serikali yetu, CCM, Wapinzani, bila kuwa wamoja, kusimama pamoja kwa upendo, mshikamano na ushirikiano wa kupigana kwa pamoja kwa lengo moja, kwa nguvu moja, kwa sauti moja, jee tutaweza kweli kushinda vita hii?!.

Janga la Corona ni vita, ili tushinde vita yoyote ni lazima sisi Watanzania, kuanzia serikali yetu, CCM, wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla wetu, tuwe kitu kimoja, tuwe wamoja, tusimame pamoja kwa upendo na mshikamano kwa kufanya kila kitu kwa pamoja, kwa ushirikiano na kuwa kitu kimoja, kwa kuunganisha nguvu zetu zote ziwe ni nguvu moja ya pamoja, tupaze sauti zetu zote ziwe ni sauti moja, na tupambane bega kwa bega kwa mshikamano wa nguvu moja, sauti moja na lengo moja la ushindi, ndio tutashinda vita hii!. Tukiendelea kuipigana vita hii kwa hivi hivi tunavyokwenda sasa, kwa kila mtu kusema lwakwe...

Tukipambana na Corona bila kusimama pamoja, huku kila mtu amesimama kivyake, anasema lake, kama hali ilivyo sasa, rais kusema hili, serikali kusema hili, Waziri Mkuu kusema lile, Waziri wa Afya kusema lake, CCM kuifananisha Corona na Wapinzani, Wapinzani kusema Serikali inaficha takwimu, wananchi kuruhusiwa kutumia barakoa za vitambaa, wataalamu kusema yao, wananchi kuruhusiwa kutumia tiba asili na tiba mbadala ikiwemo kujifukiza, wataalamu wa afya kupishana, mbuzi na hadi papai kukutwa na virusi vya Corona, kiukweli ni mchanganyiko mkubwa, kunatuchanganya sisi Watanzania tusijue tufuate lipi, tumwamini nani, kuna msemo usemao miluzi mingi humpoteza mbwa mwelekeo, humchanganya asijue afuate lipi aache lipi na mwisho hubaki ameduwaa asijue la kufanya!.

Ili tushinde vita hii, ni lazima kwanza viongozi wetu wazungumze kwa lugha moja na kutoa kauli moja thabiti ili sisi Watanzania tufuate moja, tusimame pamoja kwa upendo na mshikamano as as one, tupigane pamoja, kwa nguvu moja, sauti moja na lengo moja, ndio tutashinda vita hii.

Tangu kuanza kwa vita hii, mpaka hapa tulipo, Watanzania tumegawanyika, hivyo hatua ya kwanza ni kwa baba mwenye nyumba wetu, rais Magufuli kutuleta pamoja sisi watoto wake wote wa nyumba yake kuanzia yeye mwenyewe kama Baba, serikali yake, CCM, Wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla, atulete pamoja, tuwe wamoja, kitu kimoja, tuongee kwa lugha moja, sauti moja, nguvu moja na lengo moja la kushinda vita, ndio tutashinda vita hii.

Hili litafanyikaje?, hili litafanyika hatua kwa hatua,
  1. Hatua ya Kwanza ni Ushirikishwaji - japo Corona ni vita, na tangu kutangazwa kwa vita hii, Amiri Jeshi wetu Mkuu, amechukua vikosi vyake vya kiserikali tuu na kutangaza vita. Bahati nzuri wakati wa vita vya Kagera, japo nilikuwa mdogo, lakini tayari nilikuwa shule ya msingi, kabla ya kutangaza vita, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alituhamasisha, tukahamasika kwa uzalendo, ndipo alilihutubia taifa na kusisitiza uzalendo, kujitoa, umoja, na mshikamano wa Watanzania wote na kuitoa ile hotuba maarufu ya " Nia, Sababu na Uwezo". Lakini kwa hapa Tanzania kwenye vita hii, tangu janga hili limeanza, serikali ndio imehodhi ukamanda na wapiganaji wa vita hii, kwa kuunda kamati 3 za kiserekali tuu za kushughulikia, Kamati ya Mawaziri, Kamati ya Wakatibu Wakuu na Kamati ya Wataalamu wa serikalini. Mawaziri ni ya serikali, Makatibu Wakuu ni wa Serikali,kwa nini hao wataalamu ni wa serikali tuu?!. Hapa kunahitajika uwazi na ushirikishwaji umma, hivyo sasa uindwe kamati ya kitaifa, kwa serikali kuomba ushirikishwaji wa Watanzania wote wenye mawazo yoyote chanya ya kusaidia, wakiwemo wana Diaspora, wayalete on line, out of mawazo hayo, inaundwa kamati shirikishi ya kitaifa ambayo itajumuisha sekta zote, sio hali ilivyo sasa, vita hii inaweza kuwa inaongozwa na kamanda kama Goliati, akitegemea nguvu zake na serikali yake pekee, kumbe kuna akina Daudi wengi tuu wapo na wangeweza kusaidia sana kama wangeshirikishwa lakini wamejinyamazia tuu kimya kwa sababu hawajashirikishwa!.
  2. Korona ni Janga, Ni Vita, Vita Ikiisha Tangazwa, Amri ni Moja, Umoja, Mshikamano, Ushirikiano Ndio Siri ya Ushindi!-Korona ni janga, ni vita, vita ikiishatangazwa, ili tushinde vita hii ni lazima viongozi wetu wa serikali, wanasiasa, wapinzani, wataalamu, wote tuzungumze kwa lugha moja, sauti moja na kauli moja iliyooka. Amiri Jeshi Mkuu au serikali ikiishasema jambo fulani, mfano idadi ya waliokufa ni idadi fulani, sheria ya kivita inatumika, waliokufa ni idadi hiyo hiyo iliyotangazwa!, hata kama mtu umeona na kushuhudia kwenye mitandao ya kijamii miili 100 inazikwa!, bado una wajibu wa kuisema ile ile idadi tuu iliyotangazwa rasmi na serikali. Haiwezekani tuko vitani, leo Waziri Mkuu anatutangaza idadi ya vifo ni kadhaa, halafu kesho wewe kwasababu ni kiongozi wa chama cha upinzani, ukaitisha press conference, na kuituhumu serikali kuwa haisemi kweli! na badala yake unaleta idadi ya vifo vya mitandaoni!, what does this mean?!. Tutawachanganya Watanzania!, hizi idadi za kwenye mitandao, waachiwe watu wa mitandaoni, kwenye hili lazima serikali, wapinzani mzungumze kwa lugha moja na kauli moja kwa maslahi ya taifa!, kama ushirikishwaji ungefanyika mwanzo, nimemshuhudia Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli, akitusisitiza Watanzania wote kuwa hii vita ni yetu sote, CCM, Wapinzani, na Watanzania wote kuweka pembeni tofauti zao za kisiasa na kuwa kitu kimoja kwa kushikamana pamoja, kuunganisha nguvu ya pamoja na kupigana kwa pamoja, tutashinda. Haiwezekani Waziri Mkuu ataje idadi ya vifo, halafu kesho yake waziri mkuu kivuli kuibuka na kusema serikali inasema uongo. Ile kanuni ya a collective responsibility inakuwa applicable kwenye hili la Corona tuongee kwa kauli moja, sauti moja na kupigana kwa nguvu moja na lengo moja... Tutashinda.
  3. Watanzania Wenye Uwezo Kusaidia, Wasaidie, Serikali Pekee Haiwezi Kila Kitu. - kama zilivyo vita nyingine zote, umoja ni nguvu, hatuwezi kuiachia serikali kufanya kila kitu, serikali pekee haiwezi, hivyo kufanyike resources mobilization kwa kila Mtanzania kujitolea kuchangia kwa uwezo wake kama nilivyoshauri hapa wakiwemo wenye uwezo wa ziada na uzoefu wajitokeze, waitwe, washirikishwe, wakiwemo ma veterani wa utatibu na wa kila fani, huitwa kwenye kupanga mikakati, sisi ma veterani kwenye sekta ya media tupo, tuitwe, tushirikishwe, miongoni mwetu kuna mabingwa wa utoaji elimu kwa umma, tuwe recalled turudi newsrooms tukawasaidie hawa vijana wa sasa suala zima la utoaji wa elimu ya umma, hili lingefanyika tangu mwanzo, tungewasaidia sana Watanzania, ila hadi hapa tulipo, hatujachelewa!. Media zetu hazina uwezo wa utoaji elimu, hivyo media ziwezeshwe, maveterani tuitwe turudi newsroom tusaidie.
  4. Japo Serikali inafanya hatua mbalimbali za utekeleza kukabiliana janga hili, hazitoshi, more needs to be done, namuomba rais wetu Magufuli na serikali yetu iwe sikivu, isishupaze shingo kwa kujifanya yenyewe ndio inajua kila kitu, usikilize maoni ya wadau, wakiwemo wapinzani, mfano hoja ya partial lockdown, kwenye mikusanyiko ya ibada, Mungu ni Omnipresent, hakai kanisani kwenye nyumba za ibada tuu yupo popote na watu wanaweza kusalia popote.
  5. Viongozi wa Dini, Imani, Waheshimiwe na Viongozi wa Siasa. kama Vatican kwenye shina la Ukatoliki, na Saudi Arabia kwenye shina la Uislamu, wao wamefunga, kitendo alichokifanya Baba Askofu Severin Niwemugizi. Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, la kuepusha waumini wake na janga la Corona kwa kufunga ibada kwenye jimbo lake ni kitendo cha kupigiwa mfano, unless kama ibada nayo ni uzalishaji mali za kanisa na nchi!. Nakuomba Rais wetu Magufuli asiwabeze hawa viongozi wa dini au wa kiimani kwa kutumia lugha na maneno ya ushetani, viongozi wengine wa dini za ukweli za Mungu wa kweli are very powerful, kama alivyokuwa akielezwa Sheikh Baramia wa Bagamoyo. Nyerere aliwaheshimu viongozi wa dini zote, wakiwemo masheikh na Maaskofu, sikuwahi kumsikia Mwinyi, Mkapa na Kikwete kupishana popote kauli na viongozi wa dini, hivyo kama ni kweli rais wetu Magufuli amepishana kauli na Askofu NiweMugizi wa jimbo lake kutokana na Askofu huyo kufanya lockdown huku rais Magufuli akiwa Chato, maana you never know inawezekana wanaoepusha misongamano ndio mpango wa Mungu halafu watete wa misongomano isiyo ya lazima kama ibada ndio mpango wa shetani, then tunamshauri rais Magufuli akamwangukie Askofu wake. Enzi za Nyerere, mimi nilikuwa nasali St. Peters, rais Nyerere alikuwa anapiga magoti kupokea Ekaristi Takatifu, kama ni kweli rais Magufuli kuna kauli anezitoa kumpinga Askofu wake, asione shida kujishusha na kwenda kumpigia goti Askofu wake aombe msamaha, maana hawa watu wa Mungu hawa...
  6. Redefining Roles za Upinzani Wakati wa Vita. Upinzani unaitwa opposition kumaanisha kupinga, lakini japo ni jukumu la upinzani kupinga na kukosoa, lakini sio lazima kupinga tuu kila kitu na kila wakati. Linapokuja suala la maslahi kwa taifa lenye national interests, CCM na Wapinzani wanapaswa kuweka tofauti zao pembeni na kuwa kitu kimoja, hivyo kwenye mazuri ya CCM kwa maslahi ya taifa, Wapinzani msione aibu kuiunga mkono CCM na kuipongeza, na CCM nayo pia inapokutana na hoja za upinzani zenye maslahi kwa taifa mfano inapokopy hoja nzuri au sera mzuri za wapinzani na kuzitekeleza, isione aibu kuwapongeza wapinzani kama hoja ya katiba mpya, elimu bure etc, lakini inapotangazwa vita, role ya upinzani changes, hakuna tena kupinga kitu chochote!, zinatumika martial laws, sheria za kijeshi, amri ni moja tuu, ama kuunga mkono, ama kunyamaza kimya!. Haiwezekani Amiri Jeshi Mkuu au serikali ikasema kitu fulani, halafu akatokea kiumbe mwingine akakohoa kuipinga serikali!. Hili ni jambo la ajabu sana!. Hii itakuwa sio vita bali ni kusemazana, kwenye vita hakuna kusemezani ni amri tuu, ikitolewa kauli yoyote rasmi ya serikali ni amri!.
  7. Kwa vile mpaka sasa Corona haina kinga wala tiba, naunga mkono juhudi zote zinazochukuliwa na serikali yetu kukabiliana na janga hili, tuendelee kufuata ushauri wote wa kitaalamu unaotolewa katika kukabiliana na janga hili, na kwa vile Corona ni adui asiyejulikana, tutumie silaha zote za ki sasa za hospitali za kiimali, tiba asili, tiba mbadala, na hata akitokea mtu akaoteshwa chochote, tusidharau, na hata kama ni kweli uchawi upo, na wachawi wapo, waruhusiwe kuiloga Corona ife, iishe tuendelee na maisha yetu bila kusahau kumtanguliza Mungu, maana bila YEYE sisi binaadamu pekee, Hatuwezi.
Hitimisho.
Namalizia kwa lile swali langu la wa mwanzo wa bandiko hili, hivi hili janga la Corona ni vita kweli ya wote au ni vita ya serikali pekee?. Kama ni vita ya wote, mbona hatujashirikishwa kikamilifu ipasavyo?. Mbona karibu kila kitu ni kama ni serikali tuu?. Jee tunaweza tushinde vita hii bila sisi Watanzania, kuanzia serikali, CCM, wapinzani na Watanzania wote kwa ujumla wetu, kushirikishwa kikamilifu, tuwe wamoja?, tusimame pamoja kama kitu kimoja, kwa kuunganisha nguvu zetu zote kwa pamoja chini ya umoja ni nguvu, ziwe ni nguvu moja kuu, tupaze sauti zetu zote ziwe ni sauti moja, na tumbambane kwa mshikamamo, bega kwa bega kwa lengo moja?.
Its Only Pamoja Tutashinda!.

Nawatakia Jumanne Njema.

Paskali


Pascal you are very right!
 
Akizikwa mazuri yote (kama alikuwa nayo) atazikwa nayo na kusahaulika mara moja badala yake yataibuka mabaya yake yote ambayo ni mengi sana na yaliwaathiri wengi ambao watayakumbuka muda mrefu ujao mpaka nao wazikwe. Tenda wema nenda zako, Pascal!
Kama ambavyo Nyerere anakuwa landmark ya ukombozi barani Afrika, nadhani na mwendazake itachukua muda kumsahau.

Kuna mabaya huenda alifanya na kuna mema mengi pasi shaka alifanya.

Moja ya wema ambao upo ni kujenga ukuta wa mererani ili Tz ipate haki yake ya udhibiti wa vito vya Tanzanite ili kuweza kupata kodi.

Juzi madam President kazundua kiwanda cha police ambacho uniforms zinashonwa, itachukua muda kumbukumbu hiyo kufutika.

Alizindua kiwanda cha viatu Arusha, utachukua muda kumbukumbu hiyo kufutika.

Aliwapcha changamoto wana CCM kwa kuhoji, inakuwaje taasisi CCM isiwe na fedha zake kujiendeshea mambo yake ikiwao uchaguzi; 2020 CCM haikutembeza bakuli kwa "matajiri"

Alihoji kwanini tume ya chaguzi ipewe fedha na nchi zingine then hao watoa hela wewe masharti namna gani uchaguzi ufanyike na wao kuwa wenye kipimo cha uchaguzi;

Alihoji nchi hii watu wasombe dhshabu tu na kuweka fedha huko kwao hivi haiwezekani serikali kuwa shareholder wa mali za Watanzania, sio haba akapata hisa 16% na Tz kuingia kwenye management na board.

Huyu mzee, kwanini China apewe kila mradi, kwanini wasishindanishwe na wengine; eventually akapata fair deal kwa kujenga SGR toka Turkey na JNHP toka Egypt

Ardhi kupimwa na hati kutolewa kila mkoa badala ya kanda; huyu mzee hakuna wa mchezo.

Ujenzi wa vituo vya afya kila kata na walau kila wilaya kuwa na hospotali; hii kufutika labda kizazi cha hawa wafe wote na waje ambao watasoma kwenye vitabu.

Wanachuo kutogoma kwa kucheleweshewa boom kwa miaka 5,
Majambazi na upigaji kufungwa break, haya kusahaulika mmmh.

ATC toka kuwa na ndege ya kukodi mpaka Twiga kurejea hewani na si haba, kuna trip za China, India na baadhi ya nchi za SADC; JPM was simply exceptional to forget him as a doer and a man after deliverables.

Well; tujitahidi kufanya makubwa kwa Watanzania na kwa haki pasi kuonea mtu na pasi upendeleo ili misingi ya wema wowote kama upo basi ukuzwe na ubaya wowote uachwe ili Watanzania tuendelee kujivunia nchi yetu.
 
Corona siyo vita ni changamoto ya upumuaji tu. Nyungu kidogo, malimau na tangawizi zinatosha kuirejesha ilipotoka huko kwa mabeberu. Tusitishane!
 
Wanabodi,

Kama kawaida, kila nikipata fursa ...
  1. Redefining Roles za Upinzani Wakati wa Vita. Upinzani unaitwa opposition kumaanisha kupinga, lakini japo ni jukumu la upinzani kupinga na kukosoa, lakini sio lazima kupinga tuu kila kitu na kila wakati. Linapokuja suala la maslahi kwa taifa lenye national interests, CCM na Wapinzani wanapaswa kuweka tofauti zao pembeni na kuwa kitu kimoja, hivyo kwenye mazuri ya CCM kwa maslahi ya taifa, Wapinzani msione aibu kuiunga mkono CCM na kuipongeza, na CCM nayo pia inapokutana na hoja za upinzani zenye maslahi kwa taifa mfano inapokopy hoja nzuri au sera mzuri za wapinzani na kuzitekeleza, isione aibu kuwapongeza wapinzani kama hoja ya katiba mpya, elimu bure etc, lakini inapotangazwa vita, role ya upinzani changes, hakuna tena kupinga kitu chochote!, zinatumika martial laws, sheria za kijeshi, amri ni moja tuu, ama kuunga mkono, ama kunyamaza kimya!. Haiwezekani Amiri Jeshi Mkuu au serikali ikasema kitu fulani, halafu akatokea kiumbe mwingine akakohoa kuipinga serikali!. Hili ni jambo la ajabu sana!. Hii itakuwa sio vita bali ni kusemazana, kwenye vita hakuna kusemezani ni amri tuu, ikitolewa kauli yoyote rasmi ya serikali ni amri!
Paskali
Corona ni vita, ikitangazwa amri ni moja tuu.
Sasa chanjo imeletwa, natoa wito Watanzania, tukachanje!.
P
 
Back
Top Bottom