Je, CHADEMA hawaelewi maana ya Lockdown?

Kama nchi, Pesa tunazo, na uwezo tunao...

Serikali yetu sikivu ya awamu ya tano haiwezi shindwa ikitoke total lockdown...

Usipotoshe raia na kuifanya serikali yetu ionekane haiwezi... wakati tunajua inaweza...



Cc: mahondaw
 
Unashauri watu kama wachuuzi, bodaboda, wavuvi, mamantilie n.k wakigoma kukaa ndani njia gani itumike kuwafanya wakae ndani?
Tuna serikali inayokusanya matirioni ya shillingi kwa mwezi ,haiwezkusustain watu wake hata kwa mwezi mmoja,au yenyewe ni serikali ya madaraka,ndege,flyover,SGR na vitu vingine vinavyofanana na hivyo?
 
Rais alisema ana pesa za kuendesha nchi kwa miezi mitano, Sasa iweje lockdown ya miez miwil iwe tatizo,

Suala ni kwamba waache uongo na kujimwambafai, haya Sasa kumetokea janga tekeleza Ile kauli uliyosema nchi ina pesa za kuitosha miezi mitano, alafu lawama zinapelekwa kwa wapinzani ajabu
 
Tuna serikali inayokusanya matirioni ya shillingi kwa mwezi ,haiwezkusustain watu wake hata kwa mwezi mmoja,au yenyewe ni serikali ya madaraka,ndege,flyover,SGR na vitu vingine vinavyofanana na hivyo?
Sawa, twende hatua inayofuata.
Nieleweshe njia gani ya distribution/ mgawanyo itumike kwa hicho kinachokusanywa kwa yale makundi niliyoyataja pale mwanzo.
 
Unajua maana yake?

Freeman karantini imemshinda kakimbilia posho mjengoni.......wewe kapuku si ndio utafia nyumbani kwa wazazi kabisa!
 
Kuna tofauti kati ya kuendesha nchi na kuwalisha wananchi bwashee.
 
Well said!
 
Rwanda wamepelekewa msaada wa chakula na Bakhresa wa Tanzania.

Kenya juzi wananchi walitaka kuuwana kwa kugombea chakula cha msaada!
 
Unafahamu mass testing gharama yake? Je, unavyo vifaa kwa kazi hiyo?

Mkuu, argument yako ni ya kipumba.vu. Hizo ulizozitoa ndio sababu hasa za kwanini tumekuwa hatuna lockdown. Yaani tumeacha ugonjwa uchukue wengine wakati wengine maisha yao yaendelee.

So, waambieni watu “hatutachukua hatua za lockdown kwa sababu hatuna uwezo na lockdown italeta shida kubwa kuliko corona”. Then mkae na mtulie. Hauna tofauti na wale wanaosema “tutumie lugha ya kiswahili elimu ya juu” sababu zao hasa sio kwa sababu kiingereza hakina manufaa, bali ni kwa sababu kiingereza kimewashinda!!

Kuweni wa kweli. Msiseme lockdown haina maana. Semeni hatuna uwezo nayo na turuhusu corona ichukue inaotaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…