Je, CDF na IGP wakifikisha miaka 60 wanaweza kuongezewa muda au lazima wastaafu?

Mabeyo atakuwa na 60+ years

Nilisoma mahali yeye Ni class of 79 monduli amesoma na mwakibolwa mwaka mmoja hapo monduli

Mwakibolwa kashastaafu yeye yupo
Taratibu za maofisa wakubwa wa jeshi na kustaafu zinategemea umekaa katika ngazi fulani kwa miaka mingapi, na ukashindwa kupanda cheo kifuatacho kwa sababu umeshindwa kupita mitihani ya kukupandisha. Hii ndiyo inatokea unakuta vijana wadogo tu kwenye ngazi za major, Lt. Colonel na Makanali wanastaafu kabla ya kufika miaka ya kustaafu ile ya uraiani. Ingawaje sikumbuki kikamilifu ni miaka mingapi, lakini unatakiwa kukaa kwenye ngazi miaka fulani, usipopanda unapumzika (unastaafu).
 
Sio lazima CoS ndio achaguliwe kuwa CDF wakati Mboma anateuliwa kuwa CDF wala hakuwa CoS na wala Waitara wakati akiteuliwa CDF hakuwa CoS na isitoshe wakati Gen.Mboma anastaafu walistaafu pamoja CoS Gideon Sayore wala rais hakusubiri eti kwanza aanze kustaafu Sayore amteuwe CoS mwingine eti baadaye ndio aje kuwa CDF kumbukumbu zangu katika miaka ya karibuni ni Gen.Mwamunyange na Gen.Mabeyo tu ndio walianza kuwa CoS na baadaye kuwa CDF na hata polisi kuwa Kamishna pale makao makuu sio kigezo kwamba ndio ateuliwa kuwa IGP mfano mzuri ni Mahita aliteuliwa kuwa IGP akitokea Arusha kama RPC.
Sahihisho: RPC siyo ngazi/cheo cha polisi, bali nafasi ya kiutawala. Inawezekana alikuwa RPC lakini mwenye cheo kikubwa. Kumbuka wakuu wote wa police wa mkoa hawalingani vyeo. Kuna wengine ni Commissioners, Deputy Commissioners, Senior Assistant Commissioners, Assistant Commissioners, na kuna wakati hata Senior Superintendents wanakuwa RPC. Mahita anaweza kuwa alikuwa na cheo kikubwa kipolice lakini ni RPC.
 
Sio lazima rais kushauriana na mtu yeyote katiba inampa mamlaka rais kufanya anavyoona yeye yaani rais akae na mamejor general ashauriane nao kuhusu uteizi wa cdf uliona wapi hiyo
Theoretically uko sahihi lakini pia inaonekana hujui kuwa rais hupata ushauri kutoka jeshini kabla ya kuteua majenerali hata kama katiba inamruhusu; hata wakati anampandisha Mbuge papo kwa papo pale Dodoma bado alikiri hadharanai kuwa tayari alishashauriana na uongozi wa jeshi. Zamani ilikuwa ni rahisi kufanya hivyo lakini sasa jeshi limeshakuwa kubwa sana na kuna transparency kubwa kiasi kuwa Rais hawezi kujiamulia kumteua kamanda bila kuwa na support ya jeshi.

Sikiliza hotuba hii vizuri jinsi anavyoianza

Theoreticall uko sahihi lakini pia inaonekana hujui kuwa rais huwa huwa hupoata ushauri kutoka jeshini kabla ya kuteua majenerali hata kama katiba inamruhusu; hata wakati anampandisha Mbuge papo kwa papo pale Dodoma bado alikiri hadharanai kuwa tayari alishasharuriana na uongozi wa jeshi. Zamani ilikuwa ni rahisi kufanya hivyo lakini sasa jeshi limeshakuwa kubwa sana na kuna transparency kubwa kiasi kuwa Rais hawezi kujiamulia kumteua kamanda bila kuwa na support ya jeshi.

Sikiliza hotuba hii vizuri jinsi anavyoianza

Kwa miaka ya sasa ambayo watu wamekwenda mafunzo mbalimbali ya kijeshi na kiutawala, mtu akichafika cheo cha kanali au brigedia ana uwezo wa kushika vyeo vyovyote vilivyobakia vya kijeshi na kwa ufanisi mzuri tu. Vyeo vilivyobaki vinarudiarudia mambo yaleyale ya kiutawala, tofauti kubwa ni scale.
 
Taratibu za maofisa wakubwa wa jeshi na kustaafu zinategemea umekaa katika ngazi fulani kwa miaka mingapi, na ukashindwa kupanda cheo kifuatacho kwa sababu umeshindwa kupita mitihani ya kukupandisha. Hii ndiyo inatokea unakuta vijana wadogo tu kwenye ngazi za major, Lt. Colonel na Makanali wanastaafu kabla ya kufika miaka ya kustaafu ile ya uraiani. Ingawaje sikumbuki kikamilifu ni miaka mingapi, lakini unatakiwa kukaa kwenye ngazi miaka fulani, usipopanda unapumzika (unastaafu).
Sidhani Kama hii Ina apply Tanzania

Labda marekani

Huku mbona tunawaona wazee Wana staafu maluteni na makapteni
 
Najua vizuri na kuna mtu aliuliza na nimemjibu kwamba wakati huo Mahita alikuwa SACP,nijuavyo kwa miaka kadhaa sijawahi sikia CP kuwa RPC wala SSP kuwa RPC nijuavyo watu kama Tibaigana,Kova na Sirro hawa kwa wakati tofauti walikuwa na vyeo vya CP wakiwa ni makamanda wa kanda maalum ya DSM ambapo ndani yake kuna ma-RPC wa mikoa mitatu ya kipolisi Ilala,Kinondoni na Temeke wakiwa chini yao na SSP's angalau wapo walioweza kuwa RCO japo kwa sasa sina uhakika kama yupo RCO mwenye cheo cha SSP
Sahihi kabisaaaa...
 
RCO wenye vyeo vya ssp ni wengi tu..RTO ndio unawakuta mpaka ASP kutegemea na ukubwa wa mkoa husika.
 
Utoke ubrigadier general yani one star general, uwaluke major generals,luteni generals afu uwe general haiwezekani...vyeo vya kijeshi hupanda kwa ngazi wanaomrithi cdf ni ma general ambao ni three star generals (luteni jenerali) yani lazima ufike cheo cha uluteni jenerali ndipo uwe cdf....huwez tu ukatoka ubrigadier au major general uwe cdf bila kuwa luteni general
General Mboma alipopandishwa cheo kuwa General na kuwa CDF hakuwa Lt. General bali alikuwa Major General. Aliwaruka wengi waliokuwa senior wake aliwemo Lt. General Martin Mwakalindile ambaye baadaye alipepelekwa Maputo Mozambique kuwa balozi.
 
Hujaelewa! Chagonja alianza kupanda cheo hadi CP, nadhan kwa akili zake,alijua he is the next IGP baada ya Mwema! Matokeo yake akapata Mangu na kua IGP, Chagonja alipokosa U IGP akawa ana muhujumu Mangu,ndiyo maana Magu aliwatoa wote pale,alianza na Chagoja akampa RAS sijui mkoa gani huko,then kwa heshima akampa ubalozi Mangu huko Rwanda
Kama ilivyo sasa kati ya Sirro na Mambo sasa, kuna clip Sirro anamnanga hadharani kabisa...
 
Pengine mazoea tu na tabia za watu

Ila afisa JWTZ maslahi manono sana hamna wa kuwalinganisha serikalini
Mbona ndugu yangu mmoja alistaafu akiwa na nyota 3 lakini alikuwa kawaida sana, hata gari hakuwa nalo?? Nyumba ya kawaida sana tuu
 
Mbona ndugu yangu mmoja alistaafu akiwa na nyota 3 lakini alikuwa kawaida sana, hata gari hakuwa nalo?? Nyumba ya kawaida sana tuu
Hakuwa bloodie huyo angekuambia vizuri maslahi yake ,mbona hata vyuo mishahara mikubwa mikubwa lakini wanastaafu wanapanda daladala

Ingekuwa mmoja ameoa afisa JWTZ labda akawa anatoa info ndio watu wangeelewa sema ishu za viapo vya usiri wa kazi za jeshi , uafisa wa jeshi unaambatana na umahiri wa usiri mkubwa

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom