Wastaafu wapewe 25% na inayobaki wapewe 80% ya mshahara wao kila mwisho wa mwezi

Dec 13, 2018
30
140
WASTAAFU WAPEWE 25% NA INAYOBAKI WAPEWE 80% YA MSHAHARA WAO KILA MWISHO WA MWEZI.

Leo 13:15pm.

Kanuni iliyotangazwa na mamlaka ya usimamizi wa Sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA) inasema mstaafu atalipwa asilimia 25% ya mafao yake baada ya ukomo wa ajira na kiasi cha fedha kinachobaki,mstaafu huyo atalipwa kama mshahara kwa miaka 12 ijayo.

Vifo vya Mapema kwa wastaafu na pengine msongo wa mawazo,presha ndio msingi wa hoja ya kupewa 25% na kila mwisho wa mwezi wapokee 80% ya uliokuwa mshahara wao.Na hii ni research imefanywa kwa muda wote ambao Wazee wetu wamekuwa wakipata mafao.

Wengine wameishia kupotea na milioni 100 wakirudi Nyumbani wamebakiwa na milioni 25 na ndio kwanza ana miaka 15 ya kuishi mbeleni kama life expectancy inavyosema na bado anahitaji kujenga nyumba ya kuishi.

Bwana Odindo anauliza,kumnyima mstaafu hela yake kwa mkupuo mmoja na kumpangia atumieje, kwani pensheni mmiliki wake ni mfanyakazi au Serikali!?

Nikujibu tu hiyo pension ni Mali ya mfanyakazi ila duniani kote hakuna mtu anayepewa mafao yake kwa mkupuo, kama ungekuwa ni Chadema ningekwambia muulize Lissu kama pale Ubelgiji wanapewa kwa mkupuo fedha zote,

Serikali zote duniani zinatunza fedha za wastaafu kwa kuwalipa mwisho wa mwezi sawa sawa na kiwango ulichokuwa unalipwa mshahara,

Hapa kwetu Tanzania kudai fedha yote Pengine ni tamaa mbaya na mwishowe ugeuka kuwa majanga kwao ama ni kutaka kutapanya fedha na mwishowe kuja kuituhumu Serikali kutojali wastaafu wake,

Huku wakiwa wameshalipwa mafao yao na wengine kutapanya pesa ama kudhulumiwa,kuibiwa na wengine kutojua matumizi sahihi ya kufanyia pesa hizi, hii ni research imefanywa na kutoka na suluhisho hilo kwa faida ya maisha bora ya Wastaafu wetu na wazee wetu.

Bado jambo hili ni Utata wa kizazi cha kibeuzi,na kimajira na kimpambazuko,nasema ni majanga ya kileo,na majanga ya kileo ni dhahama ya kesho, Ni utata wa kimajanga.Na itachukua muda kueleweshwa kwa mkokotenge huu hata watu wakauelewa pasipo kuupotosha, kama ifanywavyo sasa kwa Mama aliyelia ofisi za mfuko wa pensheni akililia kulipwa pesa yote kwa mkupuo mmoja, pengine inahitajika semina elekezi kwa kila mstaafu Mtarajiwa.

Marekani wastaafu wanalipwa mwisho wa mwezi na wakiendelea kuzeeka akina Mange Kimavi wanaajiliwa kwenda kuwatawaza na kuwafuta ngozi na Spirit kama kuna vijibacteria viweze kufa na kila mwisho wa mwezi ama baada ya miezi mitatu watahitajika kufika barazani kwa afisa utumishi wa eneo walilopo kwa ajili ya kusalimiana kujuliana hali na maendeleo binafsi na kusaini kwamba wapo fit na wanafurahia namna Serikali inavyowajali, hawana tamaa ya kuchukua mipesa halafu wakaitapanye na kesho waanze kutilia huruma na kuwapa watu shida.

Nchini Norway mwajiri anakata kila mwezi kuingiza kwenye mfuko wa pension . Serikali kwa kila mtoto au mtu aliyeandikishwa kuishi Norway anakatiwa bima ya Taifa.

Hii bima ndio inakupatia "matibabu" na kupewa fedha za kujisetiri wakati huna kazi. Wakati wa kustaafu kwa wale waliofanya kazi watapata pension kutoka mifuko hiyo miwili ila malipo yote yanapitia serikalini na kulipwa kama mshahara mwisho wa mwezi.

Wakati mwingine makampuni hufa lakini haki yako imetunzwa na serikali. Wasio kuwa kazini watapata kutoka kwenye mfuko huo mmoja wa taifa tu. Kiwango cha pension kwa ujumla hutegemea kwanza miaka mingapi umefanya kazi na ukubwa wa mshahara wako wa mwisho.

Kwa wale ambao hawakufanya kazi huwa wana pata kiwango cha chini. Kwa sasa ni karibu 100000NOK kwa mwaka. Wote hulipwa kwa mwezi hadi kufa. Hakuna anayepewa mkupuo wa hela.Hii kwa mkupuo wanaotaka watu hapa Tanzania ni "fraud" ama matumizi mabaya ya fedha ya mafao kwa mstaafu.

Ukifanya research utagundua wastaafu wa Afrika haswa Tanzania, wanachakaa ama kufa upesi baada ya kustaafu na sababu kubwa ikiwa ni msongo wa mawazo, lakini zipo pia sababu nyinginezo.

Nadhani kwa kutafuta suluhisho pengine, Serikali iendelee kuwalipa mshahara hata baada ya kustaafu, lakini je umelisaidiaje Taifa ungali na nguvu zako.

Kama ilivyo Ulaya na Marekani, Wazee wanapaswa kujaliwa ili waweze kuishi maisha marefu, ukichukua suluhisho la research uliyofanya kuhusu wastaafu kuchakaa ama kufa kutokana na msongo wa mawazo, utagundua ama walitumia vibaya pesa ya mafao au waliibiwa na ndugu, jamaa, ama marafiki ama walikosa idea ya nini cha kufanya na pesa yao ya mafao, hivyo basi nami ningependa wapewe kidogo kidogo mwisho wa mwezi.

Mimi kwa maoni yangu ningependekeza wapewe 25% na zinazobaki wapewe 80% ya mshahara wao kila mwisho wa mwezi, hii ni kwa faida ya uhai na afya ya Wazee wetu wastaafu.

Pengine haya yangekuwa majibu jadidi kwa mpambazuko wa kimkakati katika utata wa kizazi cha kibeuzi kumkomboa Mzee mstaafu.

Kuna wakati miaka ya 1998-2002 Argentina iliwahi kuwa inawapa wastaafu kabichi na karoti badala ya pesa kila mwisho wa mwezi, pengine hili ndilo la kuhofia lakini naamini kamwe haliwezi kutokea hapa Tanzania.

Ni kweli pesa ni halali ya mfanyakazi lakini huwa hazitolewi kama *lump sum*(mkupuo) ni pesa inatolewa kwa mwezi kulingana na sheria ya mfuko,Pengine hii sheria ya lump sum 25% inahitaji marekebisho kidogo ili iweze kumfaa vyema mstaafu.

Ndugu Watanzania tutake kujua huu mfumo wa wastaafu kupewa bulungutu la pesa kwa mkupuo lilianza lini?

Nijuacho binafsi wastaafu hulipwa asilimia fulani ya pesa kidogo,kidogo, wakishastaafu mpaka watakapozimaliza au wakifa bado hawajazimaliza zinarudi serikalini sawa na social security kama zina misingi bora ya kusaidia wastaafu.

Na wakati wa Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Mwinyi hayakuwepo haya ya mstaafu kulipwa bulungutu kama bahati nasibu! Sasa je yalianza lini haya? Naona Bunge hata kama Spika Ndugai kakataa lakini liko sahihi labda implementation katika calculation ya hizo pesa iwe na dosari za hapa na pale ila ulipwaji ndio huwa vile tangu zamani.

Pengine uanzishwaji wa mifuko uliokuwepo ulitunga sheria za ajabu ajabu ili kuwavutia watu wajiunge hii ndio inawatokea puani baada ya kukutana na "Moment of Truth "Ni muda wa mfuko kujipanga upya,na kuacha ya enzi zile ya watu kujikopesha kiholela kinyume na sheria na mifuko ilijiingiza kwenye miradi ya ajabu ajabu ambayo imeshindwa kujijipa, Awamu hii ya tano, ni muda wa kuweka mambo sawa kuita "A Spade, a Spade and not a spoon,kama Mwalimu Mfaume alivyotufundisha kwenye General studies enzi hizo pale St Peters.

Niwatakie yaliyo mema wastaafu wetu, pamoja na Mama yangu,Mwalimu Mloka ambaye amestaafu muda si mrefu, Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Serikali yetu.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom