Je CCM imemsindikiza Arcado Ntagazwa kwenda Chadema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je CCM imemsindikiza Arcado Ntagazwa kwenda Chadema?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Richard, Aug 17, 2010.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Kada wa muda mrefu wa CCM Arcado Ntagazwa ameamua kujiunga rasmi na chama cha Chadema.

  Mzee Ntagazwa amewahi kuwa waziri katika awamu ya kwanza na ya pili ya serikali ya Tanzania.

  Katika mahojiano yake na BBC mzee Ntagazwa amesema kwamba sababu kubwa yeye kujiunga na Chadema ni kwamba chama hicho kinatekeleza maudhui ya mwaka 1975 ambayo chama cha TANU kilikuwa nayo na baadae CCM ya hayati mwalimu Nyerere na sasa CCM haifuati maudhui hayo.

  Maudhui hayo ni pamoja na swala la kupinga rushwa na kukata kabisa mizizi yake.

  Hivi karibuni makamu mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa alisikika akisema kwamba CCM itakuwa tayari kuwasindikiza wale wote ambao wataamua kujiengua na chama hicho na ikibidi kuwasindikiza kwenda huko kwenye vyama vingine.

  Swali je CCM imemsindikiza mzee Ntagazwa ambae nnamwona kwamba ni mmoja wa "heavyweight" au "sepremo" katika siasa?
   
 2. M

  MC JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ndugu,Ukiandika habari ukimnukuu Msekwa wa sasa inabidi pia ukumbuke kuwa 'ameajiri wapuuzi/wahuni wengi na yeye mwenyewe anashauliwa aache upuuzi/uhuni' Kama hujanielewa Angalia Gazeti la Raia Mwema toleo namba 146 Raia Mwema - Muungwana ni Vitendo
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  URAIA WA NTAGAZWA............mtujuvye....! je ni MTANZANIA????
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama kila mtu akija na kusema siyo raia basi kila mtu siyo raia wa Tanzania ndugu yangu
   
 5. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Alishawahi kuvuliwa utanzania,sasa anataka yajirudie!
   
 6. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,946
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Kwani wengine si unajua wanavyozeeka hata akili inakuwa kwishne,na hasa pale anapokuwa hana kazi ya kufanya zaidi ya kupiga porojo hapo CCM,na mtu safi hawezi kvumilia uchafu uliopo CCM,kwanza huyu mzee bado tunamdai alitapeli pesa ya serikali kwa kumlipia matibabu eti mwanawe ambaye naye ni mwajiriwe serikalini ,tena ana ajira iliyotakata pale Ubalozi wa Tz Uingereza
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mbona unapiga mbwa aliyekwisha kufa? Hii kesi si aliisha shinda?

  Amandla......
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Aug 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Msekwa anaongea Upuuzi, amezungukwa na wapuzi, na anaemtilia maanani anaangukia kwene fikra za wapuuzi.
   
 9. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Moja ya mambo nnayokumbuka ni pale mzee Pius Msekwa - mzee wa siku nyingi katika siasa za Tanzania , alipotoa kauli kuhusu vurugu za Tarime kwenye uchaguzi mdogo mwaka 2008, kwamba "angezungumza na raisi Kikwete" ili kupeleka majeshi wilayani Tarime kuwadhibiti na kuwapa fundisho wapiga kura wa Tarime.

  Ilikuwa ni kauli ya ajabu sana.
   
 10. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Kuna kipindi posts za Hesabu hazitofautiani na MS.
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Aug 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ndo maana Jenerali Ulimwengu , alimlima kwa makala nzuuri wiki jana, rejea raia Mwema la J5 WIKI JANA.
   
 12. M

  Mutu JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mu-Iran kama Rostam ahaaaaaaaaaaaaaaaaa

  Unaaja kujadili mambo unajadili vijimabo
   
 13. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  kwenye makambi ya wakimbizi kuna ndugu zake...mjomba n.k...! je ni RAIA HUYU?
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280

  Hatujui babu wa babu yangu alitokotokea kwa vile Tanzania haikuwapo wakati huo. Kwa hali hiyo nina wasiwasi sana na uraia wangu, huenda mimi siyo mtanzania.

  Nadhani kuwa, kimantiki, watu wote waliozaliwa kabla ya mwaka 1964 siyo watanzania halisi!
   
 15. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mzee Ntagazwa asisahau kwamba mwaka 2005 alikwishajulikana kwamba ana nia ya kwenda Chadema kwahio kwa sasa sijui atawaambia vipi wananchi au ndio ilikuwa premature?

  Ntagazwa vows to sue 'lying' newspaper

  2005-08-27

  By Lydia Shekighenda

  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]
  Arcado Ntagazwa [​IMG]

  Cabinet minister Arcado Ntagazwa said yesterday that he was planning to sue a Kiswahili weekly which claimed that he had defected to the opposition.

  Ntagazwa told a news conference in Dar es Salaam that the paper published a story on its front page on August 18, claiming that he had joined Chadema after his defeat in CCM preferential polls earlier this month.

  ''I'm currently consulting my lawyer before suing the reporter, publisher and owners of the newspaper,'' he said.

  The Minister of State in the Vice-President's Office (Environment) said the newspaper did not bother to contact him before running the story.

  ''Even if it was a party official who gave them the information, they were supposed to trace me and find out what I have to say. They didn't do this,'' Ntagazwa said.

  He added that he had no intention of leaving CCM despite his defeat in the nominations.

  Ntagazwa also slammed CCM Kibondo district officials for attempting to make political capital out of the death of his wife.

  Ntagazwa was among four ministers and deputy ministers beaten in the CCM nominations.

  Others are Energy and Minerals minister Daniel Yona, Deputy Minister of Agriculture and Food Security Pius Mbawala and Deputy Minister of Foreign Affairs and International Co-operation Abdulkadir Shareef.


  SOURCE: Guardian
   
Loading...