Je, CC za engine pekee ndio zinaamua ulaji wa mafuta wa gari?

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,328
Kuna baadhi ya watu huyakataa magari kwa kuangalia Cc za engine(Engine capacity). Lakini huenda kuna watu wameacha magari mazuri kwa sababu ya kigezo hiki. Hebu tuangalie baadhi ya mambo mengine ambayo yanaweza kuchangia ulaji wa mafuta kwenye gari.

1. Aina ya gearbox iliyotumika
Aina ya gearbox iliyotumika inaweza kuamua gari itumie vipi mafuta. Kwa mafano manual gearbox zinafanya gari itumie mafuta sana ukilinganisha na Traditional Automatic gearbox. Hata kwa Automatic Gearbox, DSG ambayo inatumiwa na VW na Audi inaongoza kwa kuwa na matumizi mazuri ya mafuta ikifuatiwa na CVT na mwisho ndio zinakuja Traditional Automatic Gearbox. Kwa kifupi engine yenye Cc2000 halafu ina gearbox ya CVT au DSG inaweza kwenda umbali sawa na engine yenye Cc1500 halafu ina tradional gearbox kwa kiasi cha mafuta kinachofanana. Mfano engine ya HR16DE yenye Cc1600 ambayo imefungwa kwenye Nissan Dualis ikiwa katika hali nzuri inaweza kwenda 18Km kwa lita moja kwa sababu ya gearbox ya CVT. Hiki kitu huwezi kukipata kwa gari yenye engine kama hiyo halafu inatumia gearbox ambayo ni Traditional AT.

2. Aina ya mafuta
Engine za diesel zina ufanisi zaidi na zinatumia mafuta kidogo ukilinganisha na engine za petrol. Kwa mfano sehemu ambayo kwenye gari ya petrol unaweza kutumia Lita 10 gari ya diesel unaweza kutumia lita 8. Na hapo pia itategemea ni aina gani ya gearbox unatumia. Pia bei ya Diesel ni ndogo ukilinganisha na bei ya petrol.

3. Mfumo unaotumika kuingiza mafuta kwenye engine
Mfumo unaotumika kuingiza mafuta kwenye engine unaweza kuchangia sana kwenye utumiaji wa mafuta wa engine yako. Siku za nyuma kwenye magari kulikuwa na Carburator ambayo watengenezaji wa magari waliamua kuachana nayo na sababu mojawapo ya kuiacha ilikuwa ni upotevu wa mafuta. Mfano pia 1AZ FSE na 1 AZ FE ni engine za familia moja lakini zimetofautiana kidogo sana kwenye ulaji wa mafuta na nguvu inazalishwa hii ni kwa sababu 1AZ-FSE inamwaga mafuta moja kwa moja kwenye combustion chamber wakati 1AZ-FE inamwaga mafuta nyuma ya intake valves.

4. Uwepo wa mifumo mbalimbali kwenye engine mfano EGR, VVT n.k
Exhaust Gas Recirculation (EGR) inasaidia kwa kiasi fulani kupunguza ulaji wa mafuta kwenye gari kwa kiasi fulani. Ukichukua engine mbili za aina moja ambazo moja ina EGR na nyingine haina, yenye EGR inakuwa na ufanisi mzuri kwenye matumizi ya mafuta ukilinganisha na ambayo haina EGR. The same kwa upande wa VVT. VVT inasaidia mafuta kuchomwa kwa wakati. Kuna muda muda mafuta yanatakiwa kuchomwa mapema(Ignition Advance) na kuna muda mafuta yanatakiwa kuchomwa kwa kuchelewa (Ignition Retard).

5. Undeshaji wako wa gari
Mnaweza kutoka hapa watu wawili wenye magari yanayofanana kila kitu na mkawekewa kiasi sawa cha mafuta kinachofanana. Kunaweza kuwa na utofauti mkubwa wa umbali ambao magari yenu yatazima kulingana na uendeshaji wa kila mmoja.

6. 4WD au AWD
Gari ambazo ni partial 4WD na AWD zinatumia mafuta mengi hasa muda ambao 4WD inapokuwa ON kwa maana nguvu kubwa zaidi inatumika kuzungusha tairi zote 4. Kama eneo unalokaa halina ulazima wa kuchukua AWD chukua tu gari ambayo ni 2WD itakupunguzia kiasi gharama za mafuta.

7. Gari kuwa Hybrid
Gari za Hybrid zinaweza zinatumia mafuta kidogo kutokana na kwamba kuna muda utaachana na engine na utatumia mfumo mwingine uliopo kama Umeme n.k. Mfano Nissan Fuga 2012 version ambayo ni Hybrid ikiwa na engine ya VQ35HR ambayo ina Cc 3500 tena ni petrol inaweza kwenye 19Km kwa lita moja. Yaani kwa lugha rahisi mafuta ya 100,000/= yanaweza kukutoa Dar mpaka Mbeya na yakabaki.


*************##############************


KAMA UNAHITAJI GATI USED IWE MKONONI AU YARD TUWASILIANE, TUKUTAFUTIE GARI ZURI.


*************############***************


PIA KWA WENYE MATATIZO MBALIMBALI YA MAGARI, TUNAFANYA:


1. FULL SYSTEMS DIAGNOSIS (GHARAMA NI TSH. 40,000/= TU KWA GARI HIZI, TOYOTA, NISSAN, SUZUKI, SUBARU, JEEP NA FORD).


2. ENGINE DIAGNOSIS KWA BRAND YOYOTE YA GARI. GHARAMA NI TSH. 20,000/= TU.


3. KUREKEBISHA MATATIZO KAMA GARI KUKOSA NGUVU, ENGINE KUMISI, KUWASHA TAA YA CHECK ENGINE, MATATIZO YA AUTOMATIC GEARBOX N.K.


***************##############***************
 
Nakubaliana na wewe hasa Kwenye fuel consumption nakumbuka nilikuwa naweka mafuta ya tsh 10000 Kwenye Carina Ti asubuh maeneo ya Chamazi na nikifika Kariakoo taa inawaka lakini sikuhizi natumia tsh 10000 ya mafuta Kwenye rumion naenda Kariakoo narudi tena full kipupwe na taa haiwaki hata kidogo.

Engine kama 5A ya Carina Ti inakula mafuta mengi tofauti na VVTi
 
Nakubaliana na wewe hasa Kwenye fuel consumption nakumbuka nilikuwa naweka mafuta ya tsh 10000 Kwenye Carina Ti asubuh maeneo ya Chamazi na nikifika Kariakoo taa inawaka,lkn sikuhizi natumia tsh 10000 ya mafuta Kwenye rumion naenda Kariakoo narud tena full kipupwe na taa haiwaki hata kidogo....
engine kama 5A ya Carina Ti inakula mafuta mengi tofauti na VVTi

Kilichoongezeka kwenye Rumion ni hiyo VVT na hiyo gearbox ya CVT. So far gari nyingi wanafunga CVT kwa sababu ya fuel efficient.
 
Shukrani sana kaka!Hivi mkuu kuna faida gani na hasara gani za kuwa na gari inayotumia deasel?Kwa nini watu wengi hawapendi gari zinazotumia deasel?

1. Gari ya diesel inauzwa gharama kuliko gari ya petrol. Hata kwenye calculator ya TRA gari za diesel zina kodi kubwa ukilinganisha na gari ya petrol.

2. Kufanya service gari ya diesel ni gharama kuliko gari ya petrol. Injector nozzle moja ya Engine ya V8 ya toyota ambayo ni ya Diesel inauzwa siyo chini ya milioni moja tena hapo ni refurbished.

3. Diesel ziko vulnerable sana na mafuta mabaya. Ukizoea kuweka kidebe kwenye gari yako ya diesel utaipaki siku si nyingi. Ukiweza kulitunza utaenjoy.

Zipo sababu nyingi. Ila ukiweza kuziovercome gari ya diesel ni nzuri kuliko ya petrol kiupande fulani.

1. Engine za diesel zinadumu sana kuliko za petrol.

2. Engine za diesel zina nguvu sana kama unavuta kitu.

3. Ulaji wa mafuta mdogo. Ile 20% less kuliko petrol mimi nimeandika tu lakini inaweza fika mpaka 30%.
 
Unapatikana wapi?

Naomba gharama za kuduplicate Key ya gari (Gari ni push to start)

Gari yangu ina CVT gear box. Ni auto manual ina gia saba. lakini naona zinaingia gia sita tu.

Pia kuna muda nakanyaga mafuta RPM inapanda tuu bila gari ku accelerate na baadae nikiachia mguu kidogo RPM inashuka na gia kuingia
 
Nakubaliana na wewe hasa Kwenye fuel consumption nakumbuka nilikuwa naweka mafuta ya tsh 10000 Kwenye Carina Ti asubuh maeneo ya Chamazi na nikifika Kariakoo taa inawaka,lkn sikuhizi natumia tsh 10000 ya mafuta Kwenye rumion naenda Kariakoo narud tena full kipupwe na taa haiwaki hata kidogo....
engine kama 5A ya Carina Ti inakula mafuta mengi tofauti na VVTi
Gari za VVTi zinakula vizuri sana mafuta hasa mfumo wake ukiwa uko vizuri bila ubovu wowote kwenye sensors na spark plugs. Bila shaka rumion yako ni 1500cc
 
Ivi mnataka gari ambazo hazili mafuta mengi, mnataka wazalishaji wa hayo mafuta wale mawee au sioo eeeh
Gari ile mafuta ila ikujali na uchumi wako aisee. Imagine uweke mafuta ya laki moja almost 50+ litres kisha utembelee siku 3 is it worth it? Uende kazini na kurudi tu siku tatu gari ikuzimikie kabla hujafika kwako? Utafurahia hilo?

Thus why Carburetor ikatupiliwa mbali. Sasa kuna VVT-i ila nayo soon tunaiacha tutahamia HYBRiD kisha full EV. Gari imekuwa ni kitu cha lazima so lazma kuimiliki kusiwe chanzo cha mateso.
 
Back
Top Bottom