Je ataweza kuningojea??Najiuliza Sana.

Je ataweza kuningojea??Najiuliza Sana.

Sawa mkuu asante,lakini nafahamu kua sio kila principle is applicable in life.
mf. Aliyeko juu mngoje chini utangoja weeee,watu wanazidi kwenda juu tu.
Kuteleza sio kuanguka, wapo wanaoteleza nakuanguka kimoja.
as I said, its my principle.. lakin ipo siku utakuja kukubaliana na mimi.., viumbe hawa ni wa ajab sana. huwez kujua ni kitu gan wanataka.
 
suala kubwa hapo ni uaminifu ndugu,hayo maneno ati fimbo ya mbali haiui nyoka humjia mtu akiwa amepoteza tumain."Muamin Nae atakuamin'
 
Kumpenda na Kumuamini ni vitu viwili vinavyotegemeana. Hauwezi kumpenda usiyemuamini na pia hauwezi kumuamini usiyempenda.

Inavyoonyesha Haumpendi ila unalailazimisha nafsi iamini kuwa unampenda.

Mkuu,unakajua aka kasemo "Never Trust a Woman except your Mom". but Nampenda huwezi pima.
 
C'mmon,mkuu are u serious??

Ni ushauri mzuri huo mkuu kinachotakiwa ni kuupima maana inawezekana ukaamua kusoma hapa hapa nchini, kama ungeleta uzi mapema kabla ya kuondoka tungekushauri uoe kabla ya kuondoka maana hata na yeye kichwani atakuwa anawaza kuhusu pata potea
 
umngoje ye amekua nani bwana,we fanya yako na yy afanye yake,..kamwe usingojee kinachosimama,chenyewe kpo tu,ss utakingoja vp
 
Kaka situation yako inasikitisha.


Mwanamke akiwa mwenyewe anapata sana vishawishi. Ex-boyfriends, mabosi etc.

Ila mwanamke anaweza kumudu hali hii iwapo TU, anampenda kwa DHATI mpenzi wake. Hii hata iweje piga ua msichana ataendelea kusubiri TU.

Kama sivyo basi kama ana marafiki wa kike wanaweza kumuinfluence na matokeo yake akakutana na njemba zikachukua kimoja.

Social networks zinaongoza kwa kutongozwa wanawake. FACEBOOK!!

Ila pia hata wewe ulipo huko unaweza kushawishika kumuacha solemba mwenzi wako. Group discussion na akina dada usiku hatari sana.

CHA KUFANYA

Sijui mpenzi wako mnaishi vipi kwenye ukweli, uwazi na mawasiliano ila nakushauri yafuatayo:

1. Mpenzi wako asiwe kabisa FACEBOOK

2. Mawasiliano kati ya wewe na mpenzi wako yawe ni ya kila saa/kila baada ya muda/kila siku. Hakuna ubusy kwenye mawasiliano. Mimi hapa nilipo ungejua niko wapi lakini nawasiliana na mke wangu KILA wakati. Kwa siku mara 50+ labda.

3. Mkeep busy awe anawasiliana na ndugu zako, dada, mama, kaka, shangazi, etc. Maana umesema ilikuwa mfunge ndoa so anafahamika

4. Jaribu pia kufahamu muda gani anakuwa free/fahamu ratiba yake(nadhani unafahamu). Mfano kama anafanya kazi unajua kabisa kuanzia labda saa mbili mpaka muda fulani(lunch) atakuwa busy. Unaweza kumtumia message moja mbili ukamuacha aendeleze taifa. Unafahamu anarudi saa ngapi, anarudi na usafiri gani etc. Kama ilikuwa karibu mfunge ndoa vyote hivi unafahamu

5. Punguza wivu utadata. Kuwa na wasiwasi tu iwapo unaona si kawaida kutowasiliana nawe. Jaribu kuwaza labda simu kwenye charge au chochote kingine. Wanawake si rahisi kucheat kama wako IN LOVE

6. Mpe majukumu mengine labda kufuatilia harusi fulani, kiwanja, biashara etc.

7. HAKIKISHA kutokuwepo kwako inakuwa ni PHYSICAL TU ila MENTALLY uko nae. Unajua amekula nini, amevaa nini amefika kazini saa ngapi, amekutana na challenges gani. Pia na wewe share nae unayojifunza.

8. Si vibaya ukijitutumua ukamtumia kinauli akaja kukutembelea au wewe ukarudi likizo. Miaka miwili ni mingi ingawa narudia tena kama ANAKUPENDA ATASUBIRI TU.

Yako mengi sana sana sana ila mimi ninajitahidi kudeal na long distance relationship na honestly namshukuru Mungu naimudu.

Kaka hii shule uliyotoa hapa nimeipenda sana. Safi sana.
 
Sasa unacheka nini Mr. Wise? Mkuu Wi-Fi anakuambia wewe kuwa, pamoja na na kuwa uko abroad, kesho asubuhi kwa saa za Bongo, si ajabu tukawa nawe hapa hapa jukwaani tukijadili mada yako wakti weye ungekuwa umelala kwa saa za uko kwenu abroad! Get it right?

Hivi Abroad ni wapi??!! Maana nashindwa kuelewa kwa nini baadhi ya watu mnadhani kuwa, abroad maana yake ni tofauti ya masaa lukuki. Kwa mfano Moscow na Dar kuna tofauti ya saa moja tu. Kwa hiyo kulala na kuamka kwa watu wa Moscow na Dar kunaweza kuwa sawa kabisa. Acheni kukariri bwana, au ndio vijana wa Mulugo??!!
 
Mkuu naona unajribu kusubiri Boat ya Zanzbar Ubungo Terminal
 
Same here. The only woman who deserve my trust, unconditional uncompromise love and my full attention is my mother. the rest can knock themselves out to hell, anytime/

Dada zako pia hawana maana??!!!
 
Mkuu kumegewea muhimu wala usifikirie kuhusu hilo cha umuhimu usikute kaolewa au kuzalishwa tu.

Na bora umalize kwanza chuo then ndo uje mfanye mipango ya ndoa kuliko ungeolea watu we umeondoka zako,,maana kusaidiwa mke inauma aisee bora mchumba.
 
Hivi Abroad ni wapi??!! Maana nashindwa kuelewa kwa nini baadhi ya watu mnadhani kuwa, abroad maana yake ni tofauti ya masaa lukuki. Kwa mfano Moscow na Dar kuna tofauti ya saa moja tu. Kwa hiyo kulala na kuamka kwa watu wa Moscow na Dar kunaweza kuwa sawa kabisa. Acheni kukariri bwana, au ndio vijana wa Mulugo??!!

Mkuu
Mi nataka kuanzisha Tution ya Geography O-Level Humu;....Twende
1. Angalia nyuzi za longtude za maeneo husika kama ni East or West then note down
2. Tafuta tofauti ya nyuzi za maeneo husika
3. Chukua ile tofauti ya nyuzi uliyoipata kisha Gawanya kwa 15
4. Namba uliyoipata ndio tofauti ya masaa kwa maeneo hayo usika
5. Kumbuka eneo lilopo East sana kupita eneo jingine ndio litakua liko mbele kwa masaa uliyoyapata
Mfano: London,UK is 0' and Dar es salaam,Tanzania is 45' East
Then, the difference in degrees (45'-0' = 45' )
the difference in hours 45/15 = 3hrs
But Dsm iko East ya London, that means Dar es imeizidi London kwa masaa ma 3.

Now NATUMAI WA TZ WENZANGU HAWATACHANGANYIKIWA NA NENO ABROAD TENA
 
Mkuu kumegewea muhimu wala usifikirie kuhusu hilo cha umuhimu usikute kaolewa au kuzalishwa tu.

Na bora umalize kwanza chuo then ndo uje mfanye mipango ya ndoa kuliko ungeolea watu we umeondoka zako,,maana kusaidiwa mke inauma aisee bora mchumba.

Mkuu iyo KUMEGEWA MUHIMU kwako wewe tu!mi ikitokea napiga chini/naachana nae.
 
Back
Top Bottom