Je, asili ya majini ni ipi?

Oh my goodness! Pumbaa tupu na uzezeta!!
 
Afu hawa watu sijui huwa wanataka nini tu yaan nabii wao anaitwa issa lakin kila saa yesu jaman wafuas wa lucifer nyie nabii wenu ni issa bin mariam yesu ni mungu achaneni naye hawahusu nyie bakini na issa wenu kwan shida iko wapi arifu


Link Halima Mdee amjibu Rais Magufuli kuhusu madawa ya kulevya

Link2 Je, asili ya majini ni ipi?

Link3. Was Jesus a Muslim?

Link4. Was Jesus a Muslim?
 
Soma upate faida
 
Imani siyo supernatural power. You don't know what you talking about!
Hivi kuna Binadamu yeyote ambaye ameshaenda Motoni,halafu akarudi Duniani kuelezea jinsi kulivyo? Au ni Imani tu za Binadamu kuwa ukifa unaenda Motoni au Peponi.
 
Hivi kuna Binadamu yeyote ambaye ameshaenda Motoni,halafu akarudi Duniani kuelezea jinsi kulivyo? Au ni Imani tu za Binadamu kuwa ukifa unaenda Motoni au Peponi.
Swala la motoni au peponi si imani ya binadamu tu bali ni mafundisho ambayo yamo katika biblia na Quran.
Biblia ina mention juu ya moto, lakini sito kwenda kiundani sana juu ya hilo. Fundisho la moto katika biblia ni symbolical. Biblia inapo ongelea moto ina maanisha "kukatiliwa mbali" kwa maana ya kwamba Mungu akikuukumu kwa kutotii huto exist tena. That makes sense kwamba Mungu hawezi kukuchoma milele wakati umeishi miaka si zaidi ya 80 na kufanya dhambi baada kufika miaka 15 alafu uchomwe milele!? Kwa kweli hapo hamna haki! Lakini Quran inafundisha tofauti kwamba siku ya kiama mtenda dhambi anapata mateso milele!

Hii issue ya kuamini hivi vitabu vya imani inategemea na kitu gani ndani ya maandiko yamekusukuma kuamini. Binafsi baada ya kuisoma biblia nikaona kuna maandiko mengi ambayo si rahisi mwanadamu kujua pasipo taarifa kutoka kwa Mungu. Kwa mfano, biblia iliandika more than 4000 years ago kwamba dunia ni duara na hiko katika anga la mbingu pasipo kushikiliwa na kitu. Kwahiyo sasa kama biblia ingesema vingine nisinge kuwa na imani nayo.

Kwa mfano, unajua mtu una amini kwamba mtu fulani ni baba yako kutokana na ushaidi fulani uliyo kuwapo ingawa hukushuhudia wao wakifanya matendo ya procreation! Bali imani inakuwepo kutokana na baadhi ya evidence zilizokuwepo kama kufanana, DNA, upendo wa wazazi na kadhalika. Haiwezekani mtu ufanane na baba yako alafu ukatae kwamba siyo baba yako hata kama hukushuhudia kile kitendo.
Ni sawa sawa na Biblia kuna mambo mengi yamethibitishwa kuwa kweli na binadamu kwa hivi sasa, na yaliongelewa siku nyingi kabla ya advances technology kuwepo.
 

Link Halima Mdee amjibu Rais Magufuli kuhusu madawa ya kulevya

Link2 Je, asili ya majini ni ipi?

Link3. Was Jesus a Muslim?

Link4. Was Jesus a Muslim?[/QUOTE]
Mmmhhh toa ushahid
 
Nachangia tu.

Waislamu wanakitabu chao ambacho ndo mwongozo wao na kina mafundisho yake
Kwa hiyo wako sahihi wanachosema kama Qurani inavyosema.

Wakristo nao wana vitabu vyao wanavyo viamini, kama vile Torati, Manabii, Wafalme, Zaburi, Injili, ambavyo wameviweka pamoja na kuviita Biblia, vinatoa mwongozo na mafundisho ambayo wanapo yasema wako sahihi.

Kila dini iko sahihi kutokana na mwongozo wake.
Ziko imani nyingine nyingi tu kama Wabudha, Wahindu, Wa rastafari nk.
Nao wana vitabu vyao na wako sahihi wanapofata mafundisho yake.

Tatizo

Linatokana na swali

Je imani gani au dini gani ndiyo inayofuata maagizo ya Mungu aliyeumba mbingu na nchi na inatumia kitabu gani ?

Hapo kila dini au imani inasisitiza kuwa wao ndo wako sahihi

Kama ndo hivyo basi kila watu wabaki na imani yao au dini yao kwani wameisoma na kuielewa na wako tayari kupewa zawadi waliyo ahidiwa na Mungu wao.

Kama kutatokea wadadisi watakaotaka kuzisoma imani zote kwa hekima ili wamtafute Mungu wa kweli yupo katika imani au dini gani, basi wanaweza kubadilisha imani zao na kujiunga kwenye imani watayoiona ni sahihi

Hapo ndipo tunaposikia, Bwana Josefu amesilimu na kuwa Muislamu, au ustadh kilemile sasa ni Mkristo nk.

Bila hivyo kila mtu aheshimu imani ya mwenzake na ndo anavyoamini.

Huwezi kumbadilisha mtu ghafla katika imani yake au kumwaminisha mtu haraka juu ya imani nyingine na wengine hawako tayari kujaribu kuisoma kwa umakini imani nyingine ili kujua kuwa wapo sahihi au la.

Lazima mjue ukweli huu la sivyo
Mtabishana kutwakuchakuchakutwa, msifikie muafaka

Nasilisha.
 
Hivi kuna Binadamu yeyote ambaye ameshaenda Motoni,halafu akarudi Duniani kuelezea jinsi kulivyo? Au ni Imani tu za Binadamu kuwa ukifa unaenda Motoni au Peponi.
Ili kupata jibu la swali lako ni wewe mwenyewe unatakiwa kujiuliza je una akili? Je doctor gani alishawah kukufanyia operation ya kichwa kisha akathibitisha kuwa unazo au hauna??

Je unaweza kututhibitishia kuwa wewe una akili?

Utakapo tafakari jibu la haya maswali ndipo utakapo pata jibu la hilo swali lako!!

Sio kila kitu huthibitishwa kwa kuona
 
Naona wengi badala ya kukupa majibu wamehamia ktk malumbano ya kidini.

In shaa Allah nitajitahidi kukujibu walau kwa uchache Kama ifuatavyo : Swali lako la kwanza ni:

1)NANI ALIYE WAUMBA MAJINI?

Jibu: majini wameumbwa na Mwenyezi Mungu. Uthibitisho ni Qur 51:56 Allah aliposema:

"Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu mimi "

Pia 7:54 Qur an
" .... Fahamuni : kuumba (ni kwake tu Mwenyezi Mungu) na amri zote ni zake (Mwenyezi Mungu), ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote".

Pia Qur 30:26 inasema
"Na vyote vilivyopo mbinguni na ardhini humtii yeye.

Bila shaka huu ni ushahidi tosha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye ALIYE WAUMBA MAJINI NA VITU VYOTE UVIONAVYO ULIMWENGUNI.

2)
umeuliza WAMEUMBWAJE?
Jibu: wameumbwa kwa Moto. Ushahidi: quran 7:12

".....Akasema (iblisi) : mimi ni bora kuliko yeye, (mimi) umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo. "

Pia Qur 55:15
" Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto ".

Kwa hiyo MAJINI waliumbwa kwa moto.

3)
KWA NINI HAWAONEKANI
Jibu:
Ameitwa Jinni kwa sababu ya kutoonekana kwake na watu, hii ni kwa sababu kila kisichoonekana kwa jicho la binadamu ktk lugha ya kiarabu jina lake (hutoholewa) hutokana na herufi hizi (JIYM) na (NUUN).

Kwa mfano :bustani huitwa 'janna' kwa sababu ya kuzungukwa kwake na majani kila upande pasiweze kuonekana ndani.

Mfano wa pili. :Elimu ya uzazi huitwa 'Ilmul ajinna' kwa sababu ya kutoonekana kwake kile kilichokuwemo tumboni mwa mzazi.

Na majinni nao wamepewa hilo jina kwa sababu ya kutoonekana kwao kwa macho ya binadamu.

Ukichunguza hayo maneno 'JANNA' 'AJINNA ' na' JINNI' yana herufi ya JIYM na NUUN ndani yake.

4)
WANATAJWA WAPI KTK VITABU VYA DINI?

Jibu: Hawa majini wametajwa ktk Qur an na ktk biblia. Ktk Qur an wametajwa sehem tofaut tofaut na pia ipo sura inyowaelezea kwa kirefu, sura ya 72.

Pia ktk biblia wametajwa katika maeneo tofauti tofauti.
Mfano 1wafalme 13:17 walihusishwa na ujenzi wa nyumba ya nabii suleyman.

Pia ktk yuda 1:6-na 2kornto 11:14-15 biblia inawatambua majini km malaika waovu.
Ila ikumbukwe kuwa malaika waliumbwa kwa nuru na majinni kwa moto

Yuda 1:9 imemtaja kwa jina la "IBLIS" Kama alivyo tajwa ktk quran. Yuda 1:9 "lakini malaika mkuu alipo shindana na ibilisi na kuhojiana naye...."
Pia ufunuo 20:10 inasema ibilisi mwenye kuwadanganya watu atatupwa kwenye shimo la moto.
Hata ukisoma quran 6:128 inasema hao majini waovu na wafuasi wao wa kibinadamu wataingia Motoni.

(5)
NAMNA YA KUWADHIBITI
Jibu: kuwadhibiti kwake ni kwa kuisoma quran. Ukiisoma ayatul kursiy asubuh basi unajilinda nao tangu hiyo asubuh mpaka jioni yake.

Na pia Ukiisoma tena kwa hiyo jioni basi utajilinda dhidi yao mpaka asubuh yake.

kwa kifupi pendelea kuisoma hii ayatul kursiy In shaa Allah Mwenyezi Mungu atakuepusha nao.

(6)
MAUMBILE YAO HALISI
Jibu: Mtume (swalla Allahu 'Alayhi wa sallam) amesema:
"majini wako namna tatu, namna moja wana mabawa wanaruka na (namna) nyingine majoka na ng' e na hawapendi kuashiria mahala pamoja na hupenda kuhama".

Atw-twabraaniy na Al-haakim na Al-Bugharary.

(7)
WANAAMINI MUNGU GANI?
Jibu: miongoni mwao wapo walio silimu na walio Baki kwenye ukafiri ambao ndio huwapotosha binamu ili waende nao Motoni siku ya mwisho .

Quran 72:14 "nasi wapo miongoni mwetu walio silimu, na wamo miongoni mwetu walio kengeuka. Walio silimu hao ndio Walio tafuta uongofu

Kwa hiyo ktk wao majini wapo miongoni mwao walio silimu na waka mwamini Mwenyezi Mungu huyu tunaye mwamini wanadamu. Nao wakitenda mema basi watalipwa Kama watakavyo lipwa wanadamu watendao mema. Na wale waovu nao watalipwa Kama ilivyo kwa wanadamu watendao waovu.

(8)
WATAADHIBIWA ADHABU GANI?
Jibu: Majini waovu wataadhibiwa adhabu ya moto. Uthibitisho ni quran

6:128 "Na ile siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya Majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi Katika wanadamu.

Na marafiki zao katika wanadamu waseme: Mola wetu! Tulinufaishana sisi na wao, na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea

Basi Mwenyezi Mungu atasema: moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako niwenye hekma na mwenye kujua.

Pia rejea Ufunuo 20:10
"Na Yule ibilisi mwenye kuwadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti alimo Yule mnyama na Yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku Hata milele na milele "

(9)
JE WANAWEZA KUZAA NA BINADAMU
Jibu : Ndio quran 18:50 inaonyesha kuwa ana kizazi chake (generation) pia quran 17:64 yaonyesha kuwa anauwezo wa kuzaa na mwanadamu

Rejea visa vya majini mahaba
Utapata kuelewa zaidi Juu ya hili.
Yangu ni hayo, km kuna sehemu nimeenda wrong basi wataalam watanisahihisha
 

soma vizuri hayo uliyoandika ndipo utakapoona uijui elimu ya waislamu juu ya majini usitake kueleza kitu ambacho huna elimu nacho, waachie wenyewe waislamu wajieleze na nawe jielezee kwa upande wako ili sote tupate faida kwa swali hili zuri.
 
Majini/mapepo = malaika waasi!
Wakristo walio na Roho Mtakatifu tu ndo wanaifahamu siri hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…