Je, asili ya majini ni ipi?

Wewe acha gonjera mzee.quran hii ndio inatanabaisha uhusiano wa waislam na majini.na wakristo sisi tunawaeleza hivyo, ni jukumu lako kukataa kwa fact.

Uko unaandika article ndefu ndefu,kwamba ibilisi sio jini ila wana asili moja ya kuumbwa kwa moto,huyu ibilisi alipewa nafasi ya kumsujudia adam akagoma hapa ndipo ugomvi ulipoanzia akashushwa chini.lakini hawa majini hatujaambiwa wao ni wakati gani walikubari kumsujudia adam ila tunaambiwa walikuja baadae wakasilimu, pamoja na kusilimu bado kwenda mbinguni ilikuwa haiwezekani kwao walizuiwa, kwanini wakati wao ni tofauti na ibilisi?????
 
Na kwa kuongezea hapo mkuu, hilo neno Satan au ibilis kama yatumikavyo kwa pamoja si jina halisi la kiumbe, ni jina litokanalo na kitendo, "upinzani na uhasi " lakini Bible imemtaja huyu kuwa malaika wa Mungu wa nuru Lux -ER. Nyongeza tu. Atakaye jua zaidi aende kwa etymology ya maneno hayo ya kiebrania.
 
Kwani neno pepo kwa kingereza linaitwaje? Huu hauwezi kuwa mjadala, mantiki ndogo tu ni viumbe vya kiroho vyenye utendaji visivyoonekana kufananika na upepo, ugumu uko wapi hapo?
 
Shetani Ni Nani?
Sisi hatujamwona Shetani ana kwa ana lakini ametolewa habari zake na wahyi. Kwa hivyo ni wajibu kusadiki kuwa yupo, na si wajibu kujua alivyo.
Mwenyezi Mungu (S.W) amemtaja katika Qur’an kwa sifa ya kupoteza watu na kuwaepusha na twaa ya Mwenyezi Mungu na amali ya heri. Kwa hiyo kila wazo linalokupitia moyoni au mtu anayejaribu kukuhadaa kukuweka mbali na twaa na kheri ya Mwenyezi Mungu, kukuhadaa kuasi sharia na kuuvika uovu na ubatilifu nguo ya uongofu, basi huyo ni Shetani wa hisia au wa kimaana.
Jambo la kushangaza ni kuwa “mashetani watu” nao wanaomba walindwe na shetani, hali wao wenyewe ni mashetani lakini hawajijui. Ni sawa na mtu anayesoma Qur’an na huku inamlaani mwenyewe; kama ilivyoelezwa katika hadith.
Qur’an inamlaani mwongo aliye haini. Kwa hivyo huyo mwongo anapoisoma huwa amejitamkia laana yeye mwenyewe.
Mwenyezi Mungu anasema:
ﺃُﻭﻟَٰﺌِﻚَ ﺟَﺰَﺍﺅُﻫُﻢْ ﺃَﻥَّ ﻋَﻠَﻴْﻬِﻢْ ﻟَﻌْﻨَﺔَ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﻭَﺍﻟْﻤَﻠَﺎﺋِﻜَﺔِ ﻭَﺍﻟﻨَّﺎﺱِ ﺃَﺟْﻤَﻌِﻴﻦَ {87}
“Hao malipo yao ni kushukiwa na laana ya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.” (3:87)
Hukumu
Kusoma Au’dhu... kabla ya kusoma Qur’an ni sunna, wala si wajib; ni kama vile kuosha mikono na kusoma Bismillah kabla ya kula. Lau hiyo Au’dhubillahi ingelikuwa ni wajibu ingeliwajibishwa katika swala, mahali pa fatiha na Sura. Wanavyuoni wote wamesema kuwa si wajib.
Mwenye Miftaahul-Karaama amesema:”Hawakuhitalifiana katika hilo isipokuwa Ibn al-Junaid ambaye mafakihi wamemwita: ‘aliyejitenga’.”
Mantiki Ya Iblis
Kwa mnasaba wa Au’dhu (kujilinda na Shetani) nitadokeza vigano alivyonasibishwa navyo Ibilisi.
Kwa sababu ingawaje ni vigano, lakini vina picha wazi kwa watu wengi wa zama hizi; hasa wale wanaotaka kujinufaisha bila ya kuangalia maslahi ya wengine, kwa kufanya mbinu za kujaribu kila njia ya kucheza na maneno na kuficha haki.
Tutayaonyesha hayo kwa matamko tu; bila ya kudhihirisha madhumuni.
Inasemekana kuwa Ibilisi alimwambia Mwenyezi Mungu (s.w.t): “Haijuzu kuniadhibu kwa kuacha kumsujudia Adam.” Mwenyezi Mungu akamuuliza, “Kwa nini?”
Akajibu: “Kama ungelitaka hasa nimsujudie ungenifanyisha kwa nguvu.”
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akamuuliza: “Wakati gani ulijua kwamba sikukutaka umsujudie Adam? Je ulilijua hilo baada ya kukuamrisha na kuasi amri yangu? Au kabla ya kukuamrisha kusujudu?”
Akasema: “Ni baada ya kuniamrisha”.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Akasema: “Basi umejishinda. Kwa sababu ulihalifu kabla ya kujua kuwa Mimi niliyataka yale uliyoacha kuyafanya. Zaidi ya hayo kama ningekufanyisha kwa nguvu, basi isingelikuwa amri.”
Utaona katika mantiki ya Ibilisi sura iliyo wazi kwamba Mwenyezi Mungu hawafanyishi wenye kuwajibikiwa na sharia kama vile anavyofanya katika kuumba kwa njia ya “kun fayakun” (kuwa, ikawa). Isipokuwa anawafanyisha kwa njia ya kuongoza matakwa ya mtu kwa sharia inayoelezwa ya kuamrisha mema na kukataza mabaya.
Inasemekana kuwa siku moja Ibilisi alikutana na Mtume Muhammad (s.a.w.) akamwambia: “Hakika Mwenyezi Mungu amekusifu kwa jina la kiongozi, na mimi amenisifu kwa jina la mpotezaji. Lakini uongozi na upotezaji vyote vinatokana na Yeye, kwa hiyo wewe na mimi hatuna chochote.”
Mtume akasema: “Hapana! Mimi hubainisha batili na kuikataza na kuitolea kiaga kibaya; hali wewe una unafiki na hadaa ya ubatilifu; na mtu ana uwezo, upambanuzi na hiyari. Kwa hivyo mwenye kufanya hiyari nzuri (akaongoka) anajifanyia mwenyewe, na mwenye kuifanya mbaya (akapotea) pia anajifanyia mwenyewe.”
Imesemekana kuwa Ibilisi alimwendea Nabii Isa (a.s.) akamuuliza: “Si unadai kuwa wewe una daraja kubwa kwa Mungu? Basi hebu jitupe kutoka juu tuone, je atakuokoa?”
Masihi akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anayemjaribu mja wake na sio mja kumjaribu Mola wake.” Imesemekana kuwa baada ya gharika na kukauka maji, Ibilisi alimwendea Nuh (a.s.) akamwambia: “Hakika wewe umenisaidia, kwa hiyo ninataka kukulipa.”
Nuh (a.s.): Akasema: “Mungu apishe mbali! kumsaidia na kiumbe kama wewe.”
Akasema Ibilisi: “Ndio hivyo.”
Nuh (a.s.): Akasema “kwa nimekusaidia nini?
Akasema Ibilisi:“Umewaapiza watu wako ili waangamie wakaangamia, na nilikuwa nikijishughulisha usiku na mchana kuwapoteza kwa muda huo. Baada ya kuaangamizwa watu wako, sina kazi ya kufanya; sipati wa kumpoteza.”
Nuh (a.s.) akasema: “Utanilipa nini?
Akasema: “Ninakunasihi usikasirike, kwa sababu hasira ya mtu inarahisisha kunifuata. Wala usihukumu kati ya watu wawili. Kama ukifanya hivyo, basi mimi nitakuwa wa tatu wenu. Wala usikae faragha na mwanamke kwani mimi hukuvutia kwake na yeye humvutia kwako.”
Kutokana na mantiki hii ya kishetani, inaonyesha kuwa Shetani ndiye mchochezi, na kwamba yeye huzipongeza silaha zenye kuangamiza.
Inasemekana kwamba Mtume (s.a.w.) na sahaba zake walimpitia mtu mmoja akirukuu na kusujudu kwa unyeyekevu. Wakasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni uzuri ulioje wa swala ya mja huyu!” Mtume akasema: “Huyu ndiye aliyemtoa baba yenu peponi.”
Lengo la hekaya hii ni kuwa haifai mtu kughurika na kuhadaika kwa zuhudi na ibada ya dhahiri.
Inasemekana kuwa Nabii Musa (a.s.) alikuwa akienda kuzungumza na Mola wake, ikatokea kukutana na Ibilisi, akamwambia “Unakwenda wapi ewe uliyezungumza na Mwenyezi Mungu?”
Nabii Musa (a.s.) akasema: “Ninakwenda kwa Mola wangu kupokea maneno kutoka kwake na niko tayari kukuombea akusamehe kama utaniahidi kuung’oa upotevu wako.”
Ibilisi akasema: “Mimi sina haja ya kuombewa na wewe wala mwingine, bali ni juu Yake Yeye Mungu kutaka radhi yangu.” (Mungu apishe mbali).
Musa (a.s.) akamwambia: “Kafiri mkubwa we Mwenye laana!”
Ibilisi Akasema: “Kwani nina dhambi gani mimi? Mungu alinitaka nimsujudie Adam, na mimi kwa iIkhlas yangu, siwezi kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Sasa tangu lini Ikhlas ikawa ni dhambi?”
Musa (a.s.) akamjibu: “Hii ni kuchezea maneno tu nako hakuwezi kukufaa wewe hata chembe, utaona yatakayokupata Kesho (Kiyama).” Ibilisi akasema: “Na wewe utaona nitakavyofanya kesho.”
Akasema: “Utafanya nini?”
Ibilisi akajibu: “Nitamtaka Mwenyezi Mungu atimize ahadi Yake na nitamtolea hoja kwa kauli Yake:
ﻭَﺭَﺣْﻤَﺘِﻲ ﻭَﺳِﻌَﺖْ ﻛُﻞَّ ﺷَﻲْﺀٍ ۚ {156}
“Na rehema yangu hukienea kila kitu.” (7:156)
“Nami ni ‘kitu,’ kwa hiyo ni wajibu rehema Yake inipate (inienee). Kama mimi si chochote, basi sitahisabiwa wala kuadhibiwa.”
Akasema Musa (a.s.): “Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu inamwenea yule mwenye mwelekeo nayo, na wewe uko mbali sana nayo.”
Ibilisi akasema: “Basi nitafanya njia nyingine. Nitawaita wafuasi wangu waliopotea na nitamtaka Mwenyezi Mungu (s.w.t.) naye awaite wafuasi Wake waumini, halafu ipigwe kura. Hapo atajulikana nani mshindi mwenye sauti ya wengi. Kama Mwenyezi Mungu akikataa kura, nitafanya maandamano makubwa mpaka nipate ninayotaka.”
Kigano hiki kina lengo la kwamba watu wa batili ni wengi zaidi kuliko watu wa haki, kwa sababu haki ni nzito na batili ni nyepesi; kama alivyosema Amirul Muminin, Ali (a.s.): “Yapasa mwenye akili kutoangalia wingi kuwa ni kipimo cha haki, wala uchache kuwa ni kipimo cha batili.”
Katika Nahjul-Balagha, amesema: “Hakika kundi kubwa ni watu wa batili hata wakiwa wengi; na kikundi kidogo ni watu wa haki hata wakiwa wachache.”
Qur’an tukufu nayo inasema: “Na wengi wao ni wenye kuchukia haki.”( 23:70)
ﻭَﻟَٰﻜِﻦَّ ﺃَﻛْﺜَﺮَ ﺍﻟﻨَّﺎﺱِ ﻟَﺎ ﻳَﻌْﻠَﻤُﻮﻥَ {21}
“Lakini watu wengi hawajui.” (12:21)
ﻭَﻟَٰﻜِﻦَّ ﺃَﻛْﺜَﺮَ ﺍﻟﻨَّﺎﺱِ ﻟَﺎ ﻳَﺸْﻜُﺮُﻭﻥَ {38}
“Lakini watu wengi hawashukuru.” (12:38)
ﻭَﺃَﻛْﺜَﺮُﻫُﻢْ ﻟَﺎ ﻳَﻌْﻘِﻠُﻮﻥَ {103}
“Na wengi wao hawatumii akili.” (5:103)
ﺑَﻞْ ﺃَﻛْﺜَﺮُﻫُﻢْ ﻟَﺎ ﻳُﺆْﻣِﻨُﻮﻥَ {100}
“Bali wengi wao hawaamini.” (2:100)
Kuna Hadith inayosema: “Wakikutana wasaidizi wa Ibilisi wanaweza kujaza Mashariki na Magharibi.”
Ni kwa madondoo haya, na mengineyo mengi, ndipo Shia wakasema: Khalifa wa Mtume ni kama Mtume; huchaguliwa na Mwenyezi Mungu; siye yule anayechaguliwa na watu.
Huyo anayechaguliwa na watu ni Mfalme wa watu; si Khalifa wa dini. Ama mkuu wa dini, kwa Shia, ni yule mwenye sifa zilizoelezwa. Sio yule anayechaguliwa na watu wala si yule anayewekwa na kiongozi wa kidunia.
Na kwa nini isiwe hivyo? Je, watu wenye matamanio ya dunia wanaweza kuaminika kuongoza dini ya Mwenyezi Mungu? Basi kama ni hivyo na wawachague na kuwapigia kura Mitume, na walifaradhishe hilo kwa Mwenyezi Mungu. Ametakata kabisa Mwenyezi Mungu na yale wayasemayo madhalimu.
Natija ya kimantiki ni kwamba Khalifa wa Mtume hawi, na hatakuwa, isipokuwa kwa usimulizi unaotokana na Mtume mwenyewe, na kwamba mkuu wa dini ni yule mwenye sifa zilizosimuliwa.
Mwenye kujipachika ukuu wa dini bila ya kuwa na sifa zilizotajwa, basi atakuwa amemzulia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na ameruka patupu mwenye kuzua.
Kwa hivyo basi, yote hayo yanafahamisha kuwa suala lolote haliwezi kuwa la kweli mpaka liwe limefuata haki; na kwamba mbinu za kucheza na maneno, haziwezi kuifanya batili iwe haki, au haki iwe batili, wala kisichoingia akilini kiingie akilini; hata kama hizo mbinu zitakuwa za hali ya juu kiasi gani.
Tutakalolifahamu ni kuwa mwenye mbinu hizo ni mwanafunzi hodari wa Ibilisi katika kuificha haki, na kuifunika na moshi wa hadaa.
Assalaam alaykum
 
Mkuu, ibilisi si jina la kiumbe. Huyu kiumbe aliitwa Lucifer, nyota ya asubuhi, kitendo chake kikampa hilo jina la ibilisi au shetani, mpinzani na muhasi. Vitabu vilivyoitangulia Quran vimefundisha hayo.
 
Ipi ni akili salama na ipi timamu? Timamu nadhani imekamilika. Salama sijui unamaanisha nini hapa na sijui iliyokamilika isiwe salama, sa kukamilika kwake kukoje hapa.
 
We hivi majini yamezuiwa kwenda mbinguni? Hii dini ina mashaka ya wazi sana, sijui kiaje hawa waungwana hawayaoni. Mi nadhani Lucifer ni bonge la smartest kiumbe. Ukizubaa lazima akupoteze mazima, ujue hata Yesu aliwekwa kwenye kona mbaya, mpango wote wa Mungu ulitakiwa ushindwe kule.

Muhammad alifanya kosa kuoa, nadhani naye angemshinda tu, alizibaini hizi hila mapema sana. Mmmmmmhhh! Hapana nawaza tu kwa maandishi, sijasema kitu hapa.
 

Kaka natamani ungekuwa unaandika mambo ya kweli hata kidogo,naamini tungeenda sawa.Nakuuliza swali nani aliyekuambia kama jini ni malaika muasi ? Siku ya sita hapo sijaelewa embu nifafanulie kidogo.

Nilichokigundua kwako huzungumzii mambo kielimu bali unayazungumzia mambo kihisia na kimantiki kama unavyo likariri tamko hilo.Hapa nakupa elimu kidogo.Mantiki ni elimu kwayo hutumia akili kuutafuta ukweli.Kwa kutumia akili peke yake huwezi kuupata ukweli.

Unaposema UPENDO tamko hili hulipi haki yake,upendo si huruma tu mzee,upendo ni kuongoza,kuonya,kukataza na kuadabisha.Hukumu ni imekuwepo ili kuilinda sheria na watu waishi kwa upendo na amani bali kwa adabu.Hata leo hii mzazi kamwe hawezi kushuhudia ujinga ukifanywa na watoto wake,pasi na kuwakanya na kuwaadabisha.

Kila mitume walitumwa kwa watu hao na mahitaji ya watu,bali walitumwa na miujiza yao kama sababu ya wale wanaowafikishia ujumbe wapate kuamini na Allah mlezi angetaka kuwafanya waamini bila miujiza angeweza,lakini kamwe huwezi kukuta katika mwenendo wa Allah ni wenye kubadilika.Yaani nidhamu aliyoiweka kwa viumbe vyake haibadiliki.

Pia kaka nimeona unalalamika sana.Sisi Mola wetu tunayemuabudu ni mwingi wa huruma,huruma ambayo ni ya dhati yake yeye tu kwa maana hakuna mwenye huruma kuliko yeye.Wasio kuwa waislamu kutokana na matukio au chuki na ujinga wao juu ya uislamu wanaiona dini ya kiislamu ayinganii juu ya upendo,huo ni uongo uliopetuka mipaka.

Katika uislamu ni makosa kukubali kudhulumiwa wala kuona nduguyo anadhulumiwa na ni wajibu kumpa yeyote haki yake hata kama ni adui yako.Hivi kuna upendo gani kuliko kumpa mtu haki yake ? UPENDO mnaouzungumzia nyinyi ni upendo wa zwazwa bali si upendo halisi.

Halafu katika jambo la kijinga ulilo liongea ni hili la namba.Kaka mantiki ya namba saba iwe itakavyo kuwa na uchache wako wa elimu unalinganisha siku na siku hizi,ni baina ya mashariki na magharibi.Kadhalika kwetu sisi waislamu jumapili ni siku ya kwanza na jumamosi ni siku ya saba,hilo liko wazi na tunaiita "Yawmul sabt".Je una cha ziada juu ya siku ya sabato ?

Halafu kaka namba saba ni namba tu,Mathalani leo hii Mola ametuwekea usiku na mchana ili tupate kudhibiti miaka na mahesabu,na kuhusu siku na namba zake alitueleza ili tujue yaani kutupa habari.Na Allah anajua zaidi.

Kaka waislamu tumefunzwa kuhoji mzee na Allah ameshatuambia ya kuwa kama hatujui jambo tuwaulize wanao jua,na mkifikiwa na habari kutoka kwa mtu muovu basi ichunguzeni ili msije kufikwa na madhila kutokana kutokuujua ukweli. Kaka wakiristo walipotea sababu walikuwa ni vichwa mchunga na mpaka leo mpo vile vile na mayahudi walipotea sababu ya kukithirisha kwao kuuliza uliza.

Nikumbushe mtume alipotoka Jabal Hiraa alimwambia nini mke wake ?
 
Mkuu, ibilisi si jina la kiumbe. Huyu kiumbe aliitwa Lucifer, nyota ya asubuhi, kitendo chake kikampa hilo jina la ibilisi au shetani, mpinzani na muhasi. Vitabu vilivyoitangulia Quran vimefundisha hayo.
Ibilisi ni jina la nani ? Usiandike "Muhasi" sahihi ni muasi.aomba unitajie hivyo vitabu vilivyoitangulia Qur'an kwa majina,kisha niambie vimesemaje kuhusu hilo.
 
1. Ni kitu gani majini?
Majini ni viumbe miongoni mwa viumbe vya Allah (SWT) wanatofautiana na binadamu na vile vile malaika . Lakini kuna sehemu kadhaa ambapo hushirikiana na binadamu katika sifa, sifa ya uhuru na uwezo wa kuchagua ‘baina ya haki na batili, makosa na usahihi, kheri na shari’. Tofauti iliyopo kati yao na binadamu ni ya kile kinachojulikana kama asili ya maumbile kwani maumbile ya majini yanatofautiana na maumbile ya binadamu.
2. Ni mada ipi walioumbiwa nayo majini?
Allah (SWT) ametufahamisha ya kuwa amewaumba majini kutokana na moto na hiyo ni katika aya tofauti mfano, Neno lake Allah ( S W T): "Na majini tumewaumba hapo mwanzo kutokana na moto wa upepo wenye joto kubwa" , Al- Hajar 27 . Na akasema katika aya nyingine katika sura ya Ar-Rahman, aya ya 15:
"Na akaumba majini kutokana na ( ncha ) ya ulimi wa moto" .
Vilevile Mtume (SAW) ameeleza kuhusu namna walivyoumbwa majini wakati aliposema: "Wameumbwa malaika kutokana na nuru, wakaumbwa majini kutokana na ulimi wa moto. Na wameumbwa binadamu kutokana na namna mlivyoelezwa." Hadithi hii imetolewa na Muslim kutokana na Bi Aisha (RA)
Hivyo basi asili ya kuumbwa majini kwa mujibu ya maelezo yaliyomo ndani ya Qur-an na Sunna za Mtume Muhammad (SAW) ni kwamba wameumbwa kwa moto. Hivyo jinni kwa asili yake ni moto. Lakini wameondoka kweye ile asili yao ya moto kama vile mwanadamu asili yake ni udongo, lakini mwanadamu alivyo si udongo, isipokuwa asili tu ndio udongo. Hivyo, majini nao wana asili tu ya moto lakini si moto wenyewe, kwani kuna ushahidi wa hadithi ya Mtume (SAW) ambayo inafahamisha kwamba majini si moto kama tunavyofahamu wa kuunguza isipokuwa ile ilikuwa tu asili ya maumbile yao. Na kuthibitisha kwamba majini hawapo tena katika yale maumbile yao ya asili ( moto ) ni tamko lake Mtume (SAW): "Hakika adui wa Allah (SWT) Ibilisi, alinitokezea na kijinga cha moto ili anichome nacho katika uso wangu." Imepokewa na An-Nasaiy. Vilevile Imam Ahmad amepokea kutokana na Mtume (SAW) kwamba kuna mtu alimuuliza Abdur-Rahman bin Khanbash: “Nini alifanya Mtume (SAW) wakati alipojiwa na mashetani?”. Alisema: “ Mashetani walimjia Mtume (SAW) kutokea majimbo fulani, wakamteremkia kutoka majabalini huku akiwepo Shetani na kijinga cha moto kwa ajili ya kumchoma nacho Mtume (SAW), akasema: 'Alitishika'. Jaabir akasema: 'Nami nilihisi hivyo hivyo ( kwamba .Mtume (SAW) atatishika )'. Akasema: 'Akawa anarudi nyuma'. Akasema: 'Akamtokezea Jibril (AS) akasema: 'Ee Muhammad sema', Mtume (SAW) akauliza,'niseme nini?' Akamwambia, 'Sema: Najilinda kwa maneno ya Allah (SWT) yaliotimia, maneno ambayo hafui dafu yeyote juu ya maneno hayo ikiwa ni mwema, mbaya kutokana na shari ya alichokiumba, na kudhurika na shari ya kinachoteremka kutoka mbinguni na shari ya kinachopanda. Na shari ya fitna za usiku na mchana. Na shari iliyopo ardhini na ile itokayo ardhini, Ee Rahman.' Na hapo ukazimika moto wa mashetani kwa uwezo wa Allah ( S W T)."
Hivyo basi tunapata kuelewa kutokana na hadithi hii kwamba lau kama majini wangekuwa wapo katika yale maumbile yao ya asili ( moto ) na kwamba wao wanaunguza, isingehitajika mmoja kati ya hao mashetani kubeba kijinga cha moto. Kwani ingetosha tu kuwa mkono wa shetani au kiungo chake chochote kinatosha kumunguza binadamu kama vile ambavyo mwanadamu huchomwa na moto akiugusa. Hivyo inaonyesha dhahiri kwamba ule moto walioumbiwa Majini umetapakaa katika maeneo yote ya umbile la majini na kuwa ni viumbe ambao hawaunguzi isipokuwa wao pia huungua kwa moto. Na bila shaka yoyote, Majini huwa wanakula na kunywa kama tulivyo sisi. Pia hukua kimaumbile kama akuavyo mwanadamu kwa kula na kunywa. Na katika vyakula vyao kuna ambavyo ni vya baridi na vya moto. Na kutokana na kuzaana kumewageuza wao kutoka kwenye ile mada ya moto walioumbiwa mwanzo na kuwa na sifa nne: (1) Joto (2) Baridi (3) Majimaji (4) Ukavu.
3. Ni lini yaliumbwa majini ?
Kuna kauli nyingi zinazozungimzia kuhusu hasa ni lini Allah (SWT) aliwaumba Majini, lakini kauli zote hizo hazina ushahidi wa Qur-an au Sunna za Mtume (SAW) hivyo sisi hatutozizungumzia . Hivyo tunaweza tu kusema kwamba, Majini waliumbwa kabla ya kuumbwa mwanadamu na hivyo ni kutokana na kauli yake Allah (SWT) aliposema, "Na tulimuumba mwanadamu kwa udongo mkavu unatoa sauti ( unapogongwa ), unaotokana na matope mepesi meusi yaliyovunda, na majini tuliwaumba kabla , kwa moto wa upepo wenye joto ( kubwa kabisa )", Al - Hijr 26 - 27 . Hivyo ameweka wazi Allah (SWT) katika aya hizi kwamba Majini yaliumbwa kabla ya mwanadamu.
4. Ni aina ngapi za majini?
Majini yapo aina tatu kama ilivyokuja katika hadithi za Mtume (SAW) ambapo imetajwa na Ibun Aby Dunia katika kitabu cha "Makaidish - Sheitaan" kutokana na Abud - Dardaa, kwamba Mtume (SAW) amesema: "Allah (SWT) amewaumba majini ya aina tatu: Aina ya kwanza ni majoka , nge na wadudu wa ardhini. Aina ya pili ni kama upepo hewani. Na aina ya tatu ni wale watakaohesabiwa kwa mabaya yao na mazuri yao."
1. Je majini wana miili?
Kwa wale wenye ujuzi na elimu ya maisha yao wametofautiana katika pande mbili kwa kauli mbili tofauti.
Kundi la mwanzo limeonelea kwamba hawa viumbe majini hawana maumbile kama tunavyofahamu miili ilivyo, bali ni mada iliyopo katika hali aliyoiumba Allah (SWT).
Kundi la pili linaonelea kwamba majini wana maumbile ya aina fulani fulani na wenye kauli hii nao wametofautiana. Kuna wanaosema kwamba maumbile yao ni kama kioo, 'transparent' ( ambapo ukiangalia unaweza kuona upande wa pili ), au ni maumbile yanayobadilika kuchukua sura mbali mbali na vile vile yawezekana pia kuwa wapo katika hali kama ya hewa ( hewani ).
Na kuna waliosema kwamba miili yao ni laini 'soft' mno kiasi kwamba si rahisi kuonekana na macho yetu, kutokana na udhaifu wa kuona tuliokua nao. Kwani Allah (SWT) angeweza kutupa uwezo wa kuwaona tungeliwaona. Na kile kinachofahamisha ulaini wa maumbile yao ni ushahidi uliopo katika Qur-an Tukufu katika neno lake Allah (SWT) aliposema: "Hakika yeye ( shetani ) pamoja na kabila lake wanakuoneni, hali ya kuwa ninyi hamwaoni" , Al-A'raaf 27. Haya ni baadhi ya maoni na ushahidi uliopokelewa. Hivyo sote tunatosheka na ushahidi kwamba macho yetu hayakupewa uwezo wa kuwaona, lakini wao wanatuona.
2. Je majini wana majina mengine?
Jawabu ni ndio; majini wana majina mbali mbali katika lugha ya kiarabu tutataja baadhi yake:
( a ) Jinni : Anapokusudiwa jinni tu. Na maana ya neno jinni ni kitu kisichoonekana au kilichofichika.
( b ) Aamir : Anapokusudiwa yule anaishi katika majumba ya watu.
( c ) Shetani : Anapokuwa na shari
( d ) Rauhaan : Yule anaewatokezea watoto
( e ) Afriit : Anapokuwa na nguvu za kupindukia
3. Je majini wana uwezo wa kujibadilisha?
Majini wana uwezo huo, tena uwezo mkubwa mno wa kujigeuza katika maumbile tofauti kama vile kuwa kama majoka, nge, farasi, ng'ombe, ngamia, kondoo na ndege. Na pia wana uwezo wa kujigeuza katika maumbile va kibinadamu.
4. Uwezo wa majini
Majini wana uwezo na nguvu ambazo ni zaidi ya alizonazo binadamu na miongoni mwa nguvu zao hizo ni ule uwezo wao mkubwa wa kusafiri. Na mfano wa haraka haraka ambao tungependa kuutoa ni ule wa ahadi ya mmoja kati ya Majini wenye nguvu, Afriit, alipomwahidi Nabii Suleyman (AS) katika baraza lake, kwamba angeweza kumletea kiti cha enzi cha Malkia wa Yemen kutoka huko mpaka pale walipo ambapo ni Palestina kabla ya Nabii Suleyman (AS) kuvunja kikao chake. Allah (SWT) amesema katika suratun - Naml aya ya 38, 39: "( Suleyman akakusanya mawaziri wake akasema): 'Enyi wakuu! Ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajakuja kwangu, hali ya kuwa wamekwisha silimu?' Mjasiri mmoja wa majini akasema: 'Mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako hapo na mimi hakika ninazo nguvu na uwezo wa hilo na ni mwaminifu'" . Miongoni mwa nguvu zao pia ni ule uwezo wa kupaa mbali mbinguni kusikiliza habari. Na hiyo ilikuwa kabla ya kuja Mtume Muhammad (SAW).
5. Je majini hufa?
Hilo halina shaka kwani nao wanajumuishwa kwenye tamko la Allah (SWT) katika Qur-an, suratur- Rahman 26, 27: " Kila kilichoko juu yake ( ardhi na mbingu ) kitatoweka; na inabaki dhati ya Mola wako ( tu Mwenyewe ) Mwenye utukufu na heshima ". Na Mtume (SAW) amesema katika dua: "Najilinda kwa utukufu wako, ambapo hapana mwingine apasaye kuabudiwa kwa haki isipokua wewe ambaye hufi, lakini majini na watu wote wanakufa" , imepokewa na Bukhari. Hivyo, kutokana na ushahidi uliotangulia majini hufa kama wanavyokufa viumbe wengine lakini Iblisi yeye amepewa muda mrefu wa kuishi mpaka siku ya kiyama, kama inavyoeleza Qur-an Tukufu, Al-A'raaf 14, 15: "Akasema ( Shetani ), 'Nipe muda ( nisife ) mpaka siku watakapofufuliwa ( viumbe )'. Akasema( Allah SWT ), 'utakua ni miongoni mwa waliopewa muda ( lakini si mpaka wakati ulioutaja ).'"
6. Ni vipi wanavyotembea mashetani?
Katika hili Mtume (SAW) anatufundisha kwa kusema:
"Yeyote kati yetu asitembee na kiatu kimoja kwani shetani hutembea na kiatu kimoja."
7. Ni muda gani ambao wanatapanyika mashetani?
Wanatapanyika wakati unapoingia usiku na hiyo ni kutokana na uthibitisho wa hadithi ya Mtume (SAW) aliposema, "Unapoingia usiku au linapoingia giza wazuieni watoto wenu ndani, kwani mashetani hutapanyika wakati huo, litakapopita lisaa limoja baadaye muachilie, na fungeni milango na mumtaje Allah (SWT), kwani hakika shetani hafungui mlango uliofungwa." Imepokewa na Bukhari.
8. Wapi kipo kiti cha enzi cha Iblis?
Kiti cha enzi cha Iblis kipo baharini. Imepokewa na Imam Ahmad kutoka kwa Jabir kwamba Mtume (SAW) amesema, "Hakika Iblisi ameweka kiti chake cha enzi kwenye maji, kisha hutuma majeshi yake."
9. Mayoe ya Iblisi
Ametoa mayoe Iblisi mara nne:
( a ) Kapiga yoe wakati alipolaaniwa
( b ) Wakati alipotolewa kwenye pepo
( c ) Wakati alipopewa utume Mtume Muhammad (SAW)
( d ) Wakati ilipoteremshwa Suratul - Fatihah
10. Mambo aliyotangulia kufanya Iblisi kabla ya binadamu
( a )Iblisi ndiye aliyetangulia kulia kwa sauti
( b )Iblisi ndiye aliyetangulia kulinganisha ubora wa viumbe, yaani yeye ndiye wa mwanzo kujilinganisha na mwanadamu na kujiona bora.
( c )Naye ndiye aliyeanzisha nyimbo na kuimba

Je Iblisi alikuwa ni miongoni mwa majini au alikuwa ni Malaika?
Tamko ( Jinni ) limekaririwa katika Qur-an Tukufu mara ishirini na mbili. Hivyo, limetajwa pekee neno ( Jinni ) pasi na kuambatanisha na neno ( Insi ) mwanadamu mara nane katika sehemu tofauti, kuhusiana na kuambatanishwa kwa neno ( Insi ) mwanadamu na neno ( Jinni ) limetajwa mara kumi na tano ndani ya Qur-an Tukufu.

Iblis (LAA)
1. Je Ibilisi ni katika majini au malaikah?
Iblisi ni katika majini, kwani neno la Allah (SWT) katika suratul Baqarah, aya 34 , " isipokua Iblisi" linafahamisha kwamba alikua si Malaikah isipokuwa yeye alikua pamoja na Malaikah wakati ilipotolewa amri ya kumsujudia Adam (AS).
Kuna rai nyingi nyingine zinazodai kwamba Iblisi ni katika Malaikah, lakini zote hazina nguvu mbele ya neno lake Allah (SWT) aliposema: "isipokuwa Iblisi alikua ni katika majini akaiasi amri ya Mola wake." Al-Kahf 50. Vile vile ushahidi mwingine wa kuthibitisha ya kwamba Iblisi ni katika majini ni neno lake yeye Mwenyewe Iblisi alipokua akizungumza na Allah (SWT) aliposema :
"Umeniumba kutokana na moto, na kumwumba yeye ( Adam A S ) kutokana na udongo." Al 'Araf 12.
Na vile vile Iblisi ana watoto kinyume na malaika, na kwamba malaikah wao wapo kama vile walivyoelezea na Allah (SWT): "Hawamwasi Allah katika amri zake na wanatekeleza kila wanaloamrishwa." At-Tahrim 6. Izingatiwe kwamba malaikah wameumbwa kutokana na nuru, lakini majini wameumbwa kutokana na moto. Hivyo basi Iblisi ni katika majini wala si malaikah
2. Ni vipi anatakiwa mwislam kuamini kuhusiana na majini?
( a ) Wao ( Majini ) ni viumbe wa Allah (SWT), kama ambavyo Allah (SWT) aliumba malaika vile vile aliumba majini na watu
( b ) Qur-an Tukufu haikuelezea namna ya sifa ya ndani ya maisha ya majini isipokua tu vile walivyoumbwa kwa moto, na namna ya kuongea kwao na sisi kuongea nao na kuwasiliana nao
( c ) Lakini la kuzingatia mno ni kwamba Qur-an kwa nguvu zote inakataza watu kutaka msaada kutoka kwa majini au kuwategema, kuwaogopa n.k kwani atakaye wafanya kuwa ni wapenzi wasaidizi, na kuomba kinga kutoka kwao kinyume na Allah (SWT), Allah (SWT) atamdhalilisha huyo atakayefanya hivyo.
Majini ni viumbe miongoni mwa viumbe wa Allah (SWT) ambao wamepewa majukumu ya kiibada kama alivyopewa mwanaadam.
 
Ipi ni akili salama na ipi timamu? Timamu nadhani imekamilika. Salama sijui unamaanisha nini hapa na sijui iliyokamilika isiwe salama, sa kukamilika kwake kukoje hapa.
Akili iliyo salama ni akili iliyosalimika kutokana uchafu wa kupandikizwa kwa fikra potofu,ujinga,matamanio ya nafsi na chuki za kijinga.
 
Uoga kwakuwa tunasema uongo au? Huwa huosomi Quran Mkuu au? Huoni kwamba mafundisho yake ni yakujifanananisha kwa kwenda kinyume na Ukristu? Mfano, wakristu wanasema Yesu ni mwana wa Mungu, Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa, wao hufanya vile ninyi fanyeni hivi nk
 
Haya mafundisho yana mushkeli sana, hayajanyooka.
 
Kwenye biblia Yesu alishawahi kumwita mtu ni shetani.
 
Embu tumia akili sasa.

Binadamu ni malaika!!!, binaadam akikosa anapewa nafasi ya kutubu kwa gharama yoyote.

Malaika muasi hana nafasi hiyo, na kwa kujua hilo akaahidi kupoteza binaadam.
Petro alivyoitwa shetani na Yesu je,Yesu alikuwa ana maana Petro ni malaika?
 
Duh! Kwanza umeniambia mi muongo, ila nimecheka sana. Halafu sina elimu, hapa nadhani ulimaanisha ya kidini, inawezekana, lakini niyanenayo hayatoki kwa vitabu na imani zenu?

Halafu, nawe kuwa huru kidogo. Si kila nitakachoambiwa na kufundishwa eti kwakuwa wengi wanakiamini nami nisiwe huru kukihoji, hapana. Hata hizi dini, kuna kanuni na misingi mingine iliwekwa na wanadamu kabisa kama mm, akina maswahaba na watakatifu (ktk ukatoliki) akna St. Augustine,.

Unapohisi nimeongea la uongo nielekeze hapo. Kuhusu saba, sidhani kama ni namba tu. Imetumika mahali pengi na jamii nyingi hata ambazo hazikuwa na mahusiano. Mfano ma ibrahimists wote wamezitumia, wahindu, budha, lakini hata wale waamerika kusini ambako walitengwa na dunia ya vitabu hivi vya dini wana kaimani juu ya namba saba.

Pia, huku kwetu Afrika hii ni namba muhimu sana ktk imani, utabibu, uchawi nk au ndo unayasikia haya. Najua ushawahi sikia misemo zunguka mbuyu, unajua ni mara ngapi? Kunde au nafaka mganga wa kienyeji ktk kuchemsha dawa huziweka ngapi? Na mengineyo mengi. Kuna namba mfano 40 pia haiko tu. Quiz, itafakari saba, utaijua sita.

Kuhusu maneno ya Mtume alipotoka pangoni, wewe ni muislamu unaijua vyema, we itolee tu ufafanuzi. Sa sijui ni upi utakaoutoa ubishane na mtume mwenyewe aliyekutwa na huo mkasa.

NB: Usihofu lolote, kwangu kuwa huru kabisa, nena lolote juu ya lolote. Sema labda humu si huru sana. Nifundishe chochote ukiaminicho ila nawe funguka kupokea mapya. Then, sisi kama binadamu tumekamilika kabisa, kwahiyo usijidharau na kujiona labda una mapungufu fulani ukijilinganisha na binadamu mwingine aliyewahi kuishi hapa duniani, Yesu amefundisha hilo pia.
 
Binadamu hajakamilika.Hujabatilisha uongo wako.Kanusha kama wewe si muongo mzee.Ila vitu virahisi sana.
 
Unaweza kunitajia hata misingi iliyowekwa katika uislamu na binadamu,kama ulivyotolea mfano maswahaba wa mtume alayhisalaamu.Uislamu ni elimu,tena elimu pana sana,mimi kuwa muislamu haimaanishi naujua uislamu wote,ndio maana nikakwambia niambie mtume alipatwa na nini katika huo mkasa na alimwambia nini mkewe...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…