Je, anaweza kufunga tumbo lake?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, anaweza kufunga tumbo lake??

Discussion in 'JF Doctor' started by Mbavu za Mbwa, Jun 14, 2011.

 1. M

  Mbavu za Mbwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 45
  Imekuwa ni kawaida sana kwa mzazi(mwanamke) aliyejifungua kulifunga tumbo lake kwa mkanda au kitambaa ili kulifanya lirudi katika hali yake ya kawaida. Hii inafanyikaa sana kwa akina mama ambao hujifungua kwa njia ya kawaida. Swali langu ni hili: mke wangu alijifungua kwa njia ya kupasuliwa miezi 7 iliyopita. kutokana na kupasuliwa huko, hakuwahi kulifunga tumbo hilo na sasa limekuwa kubwa na linampotezea shepu yake halisi. je, anaweza kulifunga kwa sasa? Au kuna madhara pindi atakapofanya hivyo ukizingatia kuwa ana mshono. Kama si kufunga anaweza kutumia njia gani mbadala iliyo salama ili kupunguza tumbo? Naombeni msaada wenu
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mbavu za mbwa...njia sahihi zaidi ya kurudisha tumbo baada ya kujifungua, hasa baada ya miezi kadhaa (mfano 7 kwa case ya mkeo) ni kufanya mazoezi ya kurudisha tumbo na sio kulifunga. Kufunga huwa hakusaidii sana hivyo usisikitike sana kwamba sababu alikuwa na kidonda hakuweza kufunga. Kufunga huwa kunaongeza presha ya tumbo na kufanya kizazi (uterus) kicontract haraka na kurudi kwenye hali yake ya udogo. hii husaidia kupunguza uwezekano wa kumwaga damau baada ya kujifungua, na pia kuharakakisha kutoka kwa yale maji maji baada ya kuzaa (lochia) ambayo hutoka kwa takribani wiki 3 hadi 6 baada ya kujifungua. Lakini kufunga hakusaidii kurudisha tumbo la nje ambalo mara nyingi ukuzwa na mlundukano wa mafuta kwenye ukuta wa tumbo.

  Ushauri: Muone mtaalamu wa mazoezi ya viungo au ajiunge gym, apewe mazoezi specifically ya kupunguza tumbo na litarudi kama ilivyokuwa mwanzo, labda inaweza isiwe exactly, but to a larger extent.
   
 3. giningi

  giningi Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuu maana na mimi nina tatizo hilo nitakwenda gim
   
 4. C

  Chiku Dunia New Member

  #4
  Feb 13, 2015
  Joined: Feb 11, 2015
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sijazaa lakini tumbo ni kubwa,nmetumia Mkanda mwezi mzima haujanisaidia,je naweza kufanyaje ili tumbo liishe,hapa nilipo hakuna gym
   
 5. R

  Rayd JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2015
  Joined: Jan 7, 2015
  Messages: 281
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwa Mazoez Ya 2mbo We N Rahs Sana, Riwa Akuelekeze Wik Yako Moja Utakua Vzur,
   
 6. Mshikemshike

  Mshikemshike JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2015
  Joined: Dec 29, 2012
  Messages: 314
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Kweli nakubaliana na ww Mi nimefunga 4 month baada ya kujifungua lakini alijarudi kbs
   
 7. mean girl

  mean girl Member

  #7
  Feb 17, 2015
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kufunga tumbo kuna faida zake,pale tu utakapojifungua langu lilirudi kwa sababu ya kufunga hata uende gym wakati wa zoezi unatakiwa uwe umefunga kurahisisha tumbo kurudi katika shepu yake ya awali
   
 8. SiimaK

  SiimaK JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2015
  Joined: Jan 12, 2015
  Messages: 341
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kufunga tumbo wakati umetoka kujifungua haisaidii kurudisha tumbo hata kidogo, kwanza watu tuna maumbile tofauti wengine hata kabla ya kupata huja uzito tayari wana matumbo makubwa, akija kuzaa ndio kabisa linaongezeka na mavyakula ya uzazi wanakula sana vyakula vya wanga na mafuta kwa hiyo wanaongezeka mwili na tumbo, inabidi kufanya mazoezi ya tumbo ili akaze nyama za tumbo na madaktali wengi hawapendi mwanamke kufunga tumbo au kutumia maji moto baada ya kujifungua kwani inalemaza vijimishipa vidogo vidogo vya kwenye tumbo. Njia rahisi ya kutoa uchafu wakati umejifungua ni kunjwa vitu vya moto moto.
  Kuna wanawake ambao asili yao hawana matumbo makubwa hawa hata wasipofunga tumbo wakati wamejifungua hubaki hivyo likiwa dogo, kama mimi nimezaa watoto 3 sijawahi kufunga tumbo wala kujikanda na maji moto lakini ukiniona tumbo langu kama sijawahi kuzaa pia sipendelei sana vyakula vyenye mafuta sana na vyakula vya wanga nakula kiasi, kama ni ugali nakula size ya ngumi yangu ya mkono, na chakula cha usiku saa 11 jioni ndio nakula.
  Nakushauri mkeo afanye mazoezi na mtoto akiacha kunyonya ajibangie muda wa kula, sio anakula na kupanda kitandani, atanenepa ajishangae.
   
 9. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #9
  Feb 17, 2015
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Me la kwangu lilirudi vizuri tu baada kama 2 weeks likawa flat kabisa ila kusema ukweli nlikua sipendi hilo jambo la kufungwa....na kila mda ulipita linazidi kupungua na pia ukiwa unanyonyesha inasaidia sana tumbo kurudi haraka
   
 10. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #10
  Feb 17, 2015
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Ulichelewa kuanza kufunga ungelifunga siku chache baada ya kujifungua
   
 11. KikulachoChako

  KikulachoChako JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2015
  Joined: Jul 21, 2013
  Messages: 14,095
  Likes Received: 11,582
  Trophy Points: 280
  Mwanamke mwenye tumbo la wastani huwa anavutia sana....
   
 12. NIMPENDENANI

  NIMPENDENANI JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2015
  Joined: Nov 2, 2014
  Messages: 5,684
  Likes Received: 3,776
  Trophy Points: 280
  Lina rudi mrembo Sema Mie walikua wananikazaje, na kunyonyesha Twins wakiume lazima lirudi, nilipo maliza 40 nikaanza gym , na vyakula pia nilikua nakimbia sana supu Za kutwa mara 2 sijui wali wa maji ...
   
 13. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #13
  Feb 17, 2015
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Hahahaha hilo la kukazwa lilinikuta ndio mana nkawa sipendi kufungwa alafu wakati wa kulala ati nsilifungue hahaha nlikua nashindwa kwa kweli
   
 14. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2015
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  My sisters...no short cuts...you want that body you are dying to have...fanya diet and hit the gym! Funga mikanda sijui kumeza midonge, hazijawahi kuwa njia za uhakika za kurudisha miili yenu iwe kabla hamjajifungu..tatizo kudeka na uvivu tu....Heidi Klum, Vicky Posh Beckham, Beyounce, Kim K and sooooo many other hot chics hawakufunga mikanda..waliingia gym na trainers wao..miezi miwili tu baada ya kuzaa wanahit runways na bikinis!
   
 15. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #15
  Feb 17, 2015
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280

  Ahsante sana tutajitahidi

  Alafu ati kuna uwezekano wa kuondoa tumbo bila ya ku loose weight?
   
 16. NIMPENDENANI

  NIMPENDENANI JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2015
  Joined: Nov 2, 2014
  Messages: 5,684
  Likes Received: 3,776
  Trophy Points: 280
  mie nilikua naona kama sipumui,wakati wa kula,halafu tumbo linawashaaaa mpaka basi,na kuna ile dawa wanachanganya asali,uwatu,pilipili manga,habasoda yani inakua mchanganyiko unakunywa asubuhi kabla ya chai na jioni,jamani inatiajoto inaniwasha mpaka viganjani wanasema inasafisha lakin kweli manake week moja unajiona mzima na maziwa yanatoka kama bomba..
   
Loading...