Je alichotabiri Nyerere tayari kinatokea sasa?

Kwani Nyerere alikuwa Mungu mtu?
GT, You better take care of your Nyererephobia!! Upende usipende ,Mwalimu alikuwa kiongozi mwenye maono ya mbali na alikuwa anaongoza nchi kwa kumuogopa mwenyezi Mungu tofauti na wengine waliomfuata ambao imedhihilika kuwa ni mafisadi wao wenyewe na wapambe wao.
 
Mkandara:

Nchi inaongozwa na katiba sio maonyo ya Nyerere. Mpaka sasa mnanukuu tu alichosema Nyerere, wakati alichosema sio mwongozo wa nchi. Na Ujamaa sio mwongozo wa nchi.

Dola yoyote ambayo haina check and balance itakuwa na matatizo kama aliyopo sasa Tanzania. Na shukrani zote za kuwa na katiba isiyojali check and balance zinamwendea Mzee Julius kwa sababu alibadilisha katika hili ajilundikie madaraka.

Hivyo sioni sababu ya kusifia utabiri wake wakati ukiangalia katiba ya Tanzania, unaona wazi itatokea wakati watu watatumia madaraka yao vibaya.

Ukisoma decralation of independency (USA), ukisoma constitution (USA), utaona kuwa aliyotosema Utabiri wa Nyerere, yalishaonwa miaka zaidi ya 200 iliyopita na ni miongozo ya nchi.

Ukisoma Agano jipya si kuna sehemu inayosema kuwa kutatokea manabii wa uongo, watakaoponyesha na kutoa miujiza kwa jina la Yesu. Usemi huu si unafanana na aliyotabiri Nyerere?

Kutomhusisha Nyerere na matatizo ya sasa ni kuikana historia yetu na haitotusaidia kupata ufumbuzi.

Mwanzo ya yote haya ni pale alipopora madaraka ya Bunge na kuyahamishia kwenye chama chak, Chama kushika hatamu. Watetezi wa hatamu za nchi kushikwa na wananchi kupitia Bunge lao kina Mwakitwange and co walionyeshwa mlango.

Kukosoa mapungufu aliyokuwa nayo Nyerere ambayo yanatuathiri hadi sasa haina maana watu wanaofanya hivyo wananchukia, la hasha tutapotoka tukiwa na mtazamo huo.
 
Mnamlaumu Mwalimu kwa lipi? Je hicho alichokisema si ndicho kinatokea sasa?

Palipo na haki na uongozi wa sheria huwa hapatokei vurugu; kinachotokea sasa ni kwasababu viongozi tulio nao hawatoi haki sawa kwa watu wote na sheria za nchi hazifuatwi.

Mwalimu alikuwa kichwa kweli kweli!

Lakini hakuwa kiongozi mzuri.
 
Zakumi,
Ukisoma Agano jipya si kuna sehemu inayosema kuwa kutatokea manabii wa uongo, watakaoponyesha na kutoa miujiza kwa jina la Yesu. Usemi huu si unafanana na aliyotabiri Nyerere?
Mkuu wewe unaamini Ubepari na mimi naamini Ujamaa hivyo haiwezi tukawa na Nabii wa kweli au Uongo mmoja..
Naposoma agano la kale nalielewa tofauti na wewe kwa sababu imani zetu tofauti.. Hivyo inategemea huyo Nabii wa Uongo anakuja na hoja gani..
Kifupi sote hatujaipata pepo, Tanzania bado ni maskini na inazidi kushuka daraja kila mwaka.. Nchi nyingine zinapiga hatua wakati sisi tunashuka.. Leo hii tupo katika kumi bora za Umaskini duniani.. hatukuwepo wakati mwalimu au Mwinyi walipokuwa madarakani.. for the first 25 Yrs Tanzania tulikuwa maskini lakini sii maskini hivi..

Hivyo hata hawa waliopo ni manabii wa Uongo..Mungu wanayemtangaza ni kujipa wao Uungu.. Sawa na yale mafundisho yayonambia kwamba Yesu ni Mungu..Hawa ndio Manabii wa uongo Yesu hakuwahi kusema wala kudai kuwa yeye ni Mungu. Na Nyerere pia hakusema kuwa yeye ndiye muumba...
 
Unitendei haki mkuu. Quote post yote ama sivyo tutakuwa kwenye play-offs.
 
Zakumi,
Mkuu Nimekuelewa...kumbe hukuwa na maana Nyerere ni Nabii wa uongo isipokuwa maneno yake yanafanana na utabiri wa Yesu!.. loh samahani..
Mkuu wangu Yesu hakuwa anatabiri, alijua wazi kuwa watakuja Manabii wa Uongo..Kwa mfano, wewe unapotegemea mgeni kuja nyumbani kwako ukamtaarifu mke na watoto, hapo hufanyi utabiri ila unafahamu ujio wa mtu huyo.. nikiwa maana kuwa, Yesu hakutabiri ila alifahamu kuwa manabii wa uongo watakuja...

Quote zote zilizopo ktk Constitution zinalenga matatizo yaliyopo au ujio wa matatizo ambayo yanawekewa ufumbuzi mapema kabla hayajatokea na kutusambaratisha... Ni kwamba yapo au yanakuja ndio maana katiba mara zote inatakiwa kutazama mambo yaliyopo na yanayotegemewa kutokea ili kuimarisha haki na amani wala sii utabiri..
Utabiri mara nyingi ni tahadhali, kinaweza kutokea au kisitokee na zote huwa ni kitu nje ya alama (sign)zote..Ni sisi tu Wadanganyika mara zote huchukulia utabiri kama ni 100% ya tukio..Hata Sheikh Yahya akikosea utabiri wake watu husema sana waka m-diss..bila kujua kwamba huo ni utabiri.

Nyerere alisema haya sii kwamba yeye ni mjuzi kuliko sote lakini kinachotangulia ni kwamba aliweza kututahadhalisha mapema na swali linakuja ..Kichwa cha mada ni swali au hoja fupi kabisa..Je, Ule utabiri wa Nyerere ndio umetimia?..Jibu rahisi kabisa, umetimia au haujatimia na sababu zipi?... tumamaliza.
Lakini badala yake naona watu wanataka kumzungumzia yeye kama Kiongozi na makosa ya kuwachagua Mwinyi na Mkapa..Jamani hata Yesu alimchagua Petro ambaye alikuja mkana.. lakini bado waumini wote tuna imani na mafundisho ya Yesu..Mzigo wa Petro anaubeba yeye mwenyewe Petro na sii kumlaumu Yesu..

Mkapa na Mwinyi hawa wote sii walikuwa viongozi wetu.. Kuna Utabiri upi walioufanya zaidi ya kusubiri matokeo!..Mwinyi alidai kwamba kuondoka kwake - Tutakuja mkumbuka yeye!..Haya huyo Mkapa katuita sisi wote wajinga, tumejaa wivu na kadhalika...Kikwete yeye anasema Kelele za mlangoni hazimzuii kulala...ina maana wakati watu mpo nje mlangoni mkipiga makelele ya Umaskini mwenzetu ndio kwanza anatafuta usingizi...
Hapa ndipo tulipopoteza haki na sheria! siku zote haki na sheria sii lazima iwe kwa mtazamo wako au wangu.. Hata Hitler alisisitiza haki na sheria kusimamishwa ili kuliweka taifa ktk umoja waliokuwa nao..
 
Mkandara:

Nchi inaongozwa na katiba sio maonyo ya Nyerere. Mpaka sasa mnanukuu tu alichosema Nyerere, wakati alichosema sio mwongozo wa nchi. Na Ujamaa sio mwongozo wa nchi.

Mkuu Zakumi, nchi haiongozwi na Katiba. Nchi inaongozwa kwa Katiba. Nchi zote duniani zinatakiwa kuongozwa na wanadamu kwa kutumia Katiba. Katiba ni kifaa cha maongozi, ni program inayotoa muongozo. Katiba zote hutungwa na wanandamu, hivyo hubadilishwa na wanadamu kila inpobidi. Katiba inaweza kutumiwa na viongozi na vile vile inaweza isitumiwe na viongozi hao hao. Inapotokea kuwa viongozi wanaacha kutumia Katiba, wananchi wakiwa na uwezo wa kutosha, wanaweza kuilaumu/kuishitaki/kutoichagua na wakati mwingine hata kuipindua serikali iliyopo madarakani.

Tukirudi kwenye mchango wako mzuri uliotanguliwa na maneno hayo hapo juu, ni wazi kuwa Katiba aliyoitumia Nyerere na Katiba inayotumiwa hivi sasa zina tofauti kubwa (baada ya mabadiliko ya 1992). Wakati wa Nyerere, hakukuwa na vyama vingi vya siasa, na vile vile Muungano ulidumishwa kwa namna ya tofauti na sasa.

Katiba hii, ambayo ndio muongozo wetu, inaweza kubadilishwa wakati wowote na kuchukua sura tofauti kabisa kama viongozi wenye dhamana ya kufanya hivyo wakiamua kuchukua hatua za kufanya hivyo.

Mimi naamini kwa dhati kabisa kuwa Nyerere hana mkono wake katika yanayotokea hivi sasa nchini (japokuwa viongozi wetu wanataka tuamini kuwa wanamuenzi Nyerere katika kuendesha nchi).
 
Invicible,
He was the best of the best. You can quote me 200 years from now.

Jasusi:

Nyerere alikuwa mpigania uhuru tu. Kwenye masuala mengine aliboronga BIG TIME. Katika anga za kupigania uhuru, tumeshamaliza kazi. Hivyo hatatokea mpigania uhuru kama yeye na ataendelea kuwa the best of the best.

Katika anga za elimu, maendeleo ya jamii na mambo mengine we are still looking for our Joshua to lead us to our promised land. Hivyo basi we won't quote you now or 200 years from now.

Don't close the door, the best is yet to come.
 
Mkuu Zakumi, nchi haiongozwi na Katiba. Nchi inaongozwa kwa Katiba. Nchi zote duniani zinatakiwa kuongozwa na wanadamu kwa kutumia Katiba. Katiba ni kifaa cha maongozi, ni program inayotoa muongozo. Katiba zote hutungwa na wanandamu, hivyo hubadilishwa na wanadamu kila inpobidi. Katiba inaweza kutumiwa na viongozi na vile vile inaweza isitumiwe na viongozi hao hao. Inapotokea kuwa viongozi wanaacha kutumia Katiba, wananchi wakiwa na uwezo wa kutosha, wanaweza kuilaumu/kuishitaki/kutoichagua na wakati mwingine hata kuipindua serikali iliyopo madarakani.

Tukirudi kwenye mchango wako mzuri uliotanguliwa na maneno hayo hapo juu, ni wazi kuwa Katiba aliyoitumia Nyerere na Katiba inayotumiwa hivi sasa zina tofauti kubwa (baada ya mabadiliko ya 1992). Wakati wa Nyerere, hakukuwa na vyama vingi vya siasa, na vile vile Muungano ulidumishwa kwa namna ya tofauti na sasa.

Katiba hii, ambayo ndio muongozo wetu, inaweza kubadilishwa wakati wowote na kuchukua sura tofauti kabisa kama viongozi wenye dhamana ya kufanya hivyo wakiamua kuchukua hatua za kufanya hivyo.

Mimi naamini kwa dhati kabisa kuwa Nyerere hana mkono wake katika yanayotokea hivi sasa nchini (japokuwa viongozi wetu wanataka tuamini kuwa wanamuenzi Nyerere katika kuendesha nchi).

Naona sasa tupo kwenye masuala ya syntax na semantic. Katiba ya sasa haina tofauti kubwa na ya wakati wa chama kimoja.

Labda kama unazungumzia katiba ya CCM.
 
Zakumi,
Mkuu Nimekuelewa...kumbe hukuwa na maana Nyerere ni Nabii wa uongo isipokuwa maneno yake yanafanana na utabiri wa Yesu!.. loh samahani..
Mkuu wangu Yesu hakuwa anatabiri, alijua wazi kuwa watakuja Manabii wa Uongo..Kwa mfano, wewe unapotegemea mgeni kuja nyumbani kwako ukamtaarifu mke na watoto, hapo hufanyi utabiri ila unafahamu ujio wa mtu huyo.. nikiwa maana kuwa, Yesu hakutabiri ila alifahamu kuwa manabii wa uongo watakuja...

Quote zote zilizopo ktk Constitution zinalenga matatizo yaliyopo au ujio wa matatizo ambayo yanawekewa ufumbuzi mapema kabla hayajatokea na kutusambaratisha... Ni kwamba yapo au yanakuja ndio maana katiba mara zote inatakiwa kutazama mambo yaliyopo na yanayotegemewa kutokea ili kuimarisha haki na amani wala sii utabiri..
Utabiri mara nyingi ni tahadhali, kinaweza kutokea au kisitokee na zote huwa ni kitu nje ya alama (sign)zote..Ni sisi tu Wadanganyika mara zote huchukulia utabiri kama ni 100% ya tukio..Hata Sheikh Yahya akikosea utabiri wake watu husema sana waka m-diss..bila kujua kwamba huo ni utabiri.

Nyerere alisema haya sii kwamba yeye ni mjuzi kuliko sote lakini kinachotangulia ni kwamba aliweza kututahadhalisha mapema na swali linakuja ..Kichwa cha mada ni swali au hoja fupi kabisa..Je, Ule utabiri wa Nyerere ndio umetimia?..Jibu rahisi kabisa, umetimia au haujatimia na sababu zipi?... tumamaliza.
Lakini badala yake naona watu wanataka kumzungumzia yeye kama Kiongozi na makosa ya kuwachagua Mwinyi na Mkapa..Jamani hata Yesu alimchagua Petro ambaye alikuja mkana.. lakini bado waumini wote tuna imani na mafundisho ya Yesu..Mzigo wa Petro anaubeba yeye mwenyewe Petro na sii kumlaumu Yesu..

Mkapa na Mwinyi hawa wote sii walikuwa viongozi wetu.. Kuna Utabiri upi walioufanya zaidi ya kusubiri matokeo!..Mwinyi alidai kwamba kuondoka kwake - Tutakuja mkumbuka yeye!..Haya huyo Mkapa katuita sisi wote wajinga, tumejaa wivu na kadhalika...Kikwete yeye anasema Kelele za mlangoni hazimzuii kulala...ina maana wakati watu mpo nje mlangoni mkipiga makelele ya Umaskini mwenzetu ndio kwanza anatafuta usingizi...
Hapa ndipo tulipopoteza haki na sheria! siku zote haki na sheria sii lazima iwe kwa mtazamo wako au wangu.. Hata Hitler alisisitiza haki na sheria kusimamishwa ili kuliweka taifa ktk umoja waliokuwa nao..

Worshiping dictators is a pain in the a$$. Now unaanza kusema Hitler alivyosisitiza. Lakini si unajua destruction aliyoleta.

Kwanini usilinganishe Tanzania na Botswana? waAfrica hata siku moja hamtoi pongezi kwa Rais wa kwanza wa Botswana kwa jitihada zake za kujenga democratic institutions kwanza na baadaye ku-tackle issue za maendeleo.

Siku zote mnawaenzi second class dictators, kwa sababu ya elimu za bure.
 
"Dola lazima isimamie sheria ili kulinda haki na kuhifadhi amani. Wajibu huu usipozingatiwa, wataibuka manabii wenye kuihubiri haki kwa kuwahukumu wengine. Hamtabaki salama mkifikia hapo"

J.K. Nyerere

Mi nakubaliana na principle hii ya Mwalimu. Ni sawa kabisa! Dola ndiyo yenye wajibu na haki ya kusimamia sheria (halali) ili kulinda haki ya kila mwananchi. Na hili likishafanyika, basi kutakuwa na amani kati ya wananchi. Dola ikishindwa kufanya hii kazi, basi kila raia atajichukulia sheria mkononi. Wataibuka manabii, yaani "viongozi" wa kujiteua wenyewe na kuwasemea wengine. Hawa mara nyingi hawatafuata sheria bali watatumia vipimo vyao binafsi kukabili matatizo ambayo yalipaswa kukabiliwa na dola. Kwa kuwa watakuwa wanafanya kazi isiyo yao na mara nyingi bila kufuata utaratibu wa sheria, basi wanaishia kuvunja sheria na kuwatendea isiyo haki wale wanaoonekana ni chanzo cha matatizo ya kweli ambao dola ilipaswa kuwashughulikia. Kwa hiyo, katika kutetea haki ya wengi kunaweza kukawa na uvunjaji wa haki.

Sasa suala hapa si Mwalimu alifanya nini. Bali je, KANUNI yake hii ina ukweli? Mi nasema "ndiyo ina ukweli".
Mfano mdogo tu: angalia yanayotokea kule Arumeru ambako wananchi wameleta uharibifu mkubwa wakidai kwamba yale maeneo ni yao na alipewa mhe. Kimaro kwa njia zisizo halali, na kwamba walishalifikisha suala lao kwa wakubwa wa serikali mara nyingi. Kwa kuwa serikali haikufanya chochote (kusimamia sheria ili haki itendeke) wameamua kujichukulia sheria mkononi. Kwao ndiyo haki. Lakini ujue ni "haki" inayopitiliza kwani haina kipimo cha sheria. Na hawa watu hawakukurupuka tu wakaanza kujichukulia "Haki" bali lazima kuna manabii waliowahubiri (viongozi wao) na kutoa hukumu ya kitu gani kifanyike.
Je, kwa mwendo huu tutafika kweli kwenye maisha bora kwa kila mtanzania? Dola ifanye kazi yake bana!
 
Mnatoa mfano wa Arumeru ku-validate maneno yako. Lakini wakati wa Nyerere matatizo kama hayo yalitokea.

Mbona wakurya walikuwa wanajichukulia sheria mikononi mwao. Miaka ya 1982, 83, 84, wasukuma na wanyamwezi walianzisha majeshi ya jadi ya sungusungu. Majeshi haya yalikuwa ni ya wananchi kujichukulia sheria mikononi baada ya serikali kushindwa kutoa ulinzi na usalama.

Kama suala la Arumeru ni kushindwa kwa dola, hata wakati wa Mchonga dola iliboronga.
 
Worshiping dictators is a pain in the a$$. Now unaanza kusema Hitler alivyosisitiza. Lakini si unajua destruction aliyoleta.

Kwanini usilinganishe Tanzania na Botswana? waAfrica hata siku moja hamtoi pongezi kwa Rais wa kwanza wa Botswana kwa jitihada zake za kujenga democratic institutions kwanza na baadaye ku-tackle issue za maendeleo.

Siku zote mnawaenzi second class dictators, kwa sababu ya elimu za bure.

Wasomi wa siku hizi bwana! Eti tuilinganishe Tanzania na Botswana! Population ya Botswana ni nusu ya population ya Dar es Salaam. Ka-nchi kenyewe ukubwa wake ni sawa na kisiwa cha Madagascar, ina wilaya tisa tu tena ndogo ndogo! Botswana wana dhahabu, almasi nasikia hata uranium wanayo. 'Wasomi' ndani ya JF wanataka tuifananishe Botswana na Tanzania na tumpongeze Rais wa kwanza wa Botswana kwa kujenga democratic institutions na tumponde na kumkejeli Rais wetu wa kwanza kwamba hakuna la maana aliloifanyia nchi hii!

Hizo democratic institutions zinamsaidiaje mwananchi wa kawaida ambaye, tangu 1966 Uhuru wa Botswana ulipopatikana mpaka sasa, anaisha kwa kipato cha dola moja na ushei kwa siku? Kwa utajiri wote uliopo Botswana ukilinganisha na udogo wa nchi hiyo tungetegemea wenzetu wangelikuwa wanaishi kama wako peponi!

Ni ninyi 'wasomi' wa nchi hii ambao mumeachiwa madini na 'dictator' Mjamaa ambaye hakutaka kujitajirisha yeye na kwa udikteta wake aliwapiga vita sana viongozi wenziwe wasithubutu kujitajirisha. Kaenda Mbinguni kawaachieni madini yamelala ardhini mnashindwa kuwasaidia Watanzania wenzenu ili madini hayo yatumike kwa manufaa ya Taifa. Hivi sasa karibu mtaanza kutoana roho na kuwatoa roho wananchi wasio na hatia kutokana na kutokuzingatia maadili mema aliyokuwa akijaribu kufundisha 'dikteta' Nyerere!

Mnauponda Ujamaa lakini ndio huo uliotuelimisha sie watoto wa wakulima wa vijijini na watoto na wajukuu zetu wanaendelea kufaidi matunda ya sisi kusoma kwetu bureeeee kwa ajili ya Ujamaa mnaouponda. Wakulima vijijini na kizazi chao wana matumaini gani?

Mkiendelea kulaumu Marehemu wa jana badala ya kuangalia ya leo, mengi tu aliyofundisha na aliyotabiri Mwalimu yatatokea.
 
Back
Top Bottom