Je alichotabiri Nyerere tayari kinatokea sasa?

Amen.
Najua Vijana wataanza kunicharukia kwa bahati ya kwenda kutibiwa bure! Karibu Prof. Mwakyusa atawaletea Apollo pale mlimani ili sote tufaidi matunda ya tiba ya uhakika. Mwakyusa - a product of Ujamaa wa Nyerere!
 
Hali ya uongozi Tanzania ipo hivi: Vipofu milioni kadhaa (milioni 40 kwa sasa) wanatawaliwa na chongo wachache. Hivi ndivo hali ilivyokua awamu zote zilizopita, ya sasa na zitakazo kuja kwa miaka mingi sana.

Tofauti pekee kati ya awamu ya kwanza na zilizofuatia ni kwamba Nyerere na wasaidizi wake wa karibu kabisa hawakuwa walafi.

Naweka msistizo uhusiano kati ya mtawala na mtawaliwa kuwa kama wa chongo na kipofu.
 
Wasomi wa siku hizi bwana! Eti tuilinganishe Tanzania na Botswana! Population ya Botswana ni nusu ya population ya Dar es Salaam. Ka-nchi kenyewe ukubwa wake ni sawa na kisiwa cha Madagascar, ina wilaya tisa tu tena ndogo ndogo! Botswana wana dhahabu, almasi nasikia hata uranium wanayo. 'Wasomi' ndani ya JF wanataka tuifananishe Botswana na Tanzania na tumpongeze Rais wa kwanza wa Botswana kwa kujenga democratic institutions na tumponde na kumkejeli Rais wetu wa kwanza kwamba hakuna la maana aliloifanyia nchi hii!

Hizo democratic institutions zinamsaidiaje mwananchi wa kawaida ambaye, tangu 1966 Uhuru wa Botswana ulipopatikana mpaka sasa, anaisha kwa kipato cha dola moja na ushei kwa siku? Kwa utajiri wote uliopo Botswana ukilinganisha na udogo wa nchi hiyo tungetegemea wenzetu wangelikuwa wanaishi kama wako peponi!

Ni ninyi 'wasomi' wa nchi hii ambao mumeachiwa madini na 'dictator' Mjamaa ambaye hakutaka kujitajirisha yeye na kwa udikteta wake aliwapiga vita sana viongozi wenziwe wasithubutu kujitajirisha. Kaenda Mbinguni kawaachieni madini yamelala ardhini mnashindwa kuwasaidia Watanzania wenzenu ili madini hayo yatumike kwa manufaa ya Taifa. Hivi sasa karibu mtaanza kutoana roho na kuwatoa roho wananchi wasio na hatia kutokana na kutokuzingatia maadili mema aliyokuwa akijaribu kufundisha 'dikteta' Nyerere!

Mnauponda Ujamaa lakini ndio huo uliotuelimisha sie watoto wa wakulima wa vijijini na watoto na wajukuu zetu wanaendelea kufaidi matunda ya sisi kusoma kwetu bureeeee kwa ajili ya Ujamaa mnaouponda. Wakulima vijijini na kizazi chao wana matumaini gani?

Mkiendelea kulaumu Marehemu wa jana badala ya kuangalia ya leo, mengi tu aliyofundisha na aliyotabiri Mwalimu yatatokea.

BN:

Umejuaje kama mimi ni msomi? au ni matunda ya Nyerere. Ujamaa nauponda kwa sababu hakukuelimisha. Hizo ni fikra za potofu. Mipango ya elimu ya Tanzania ilitegemea na inaendelea kutegemea vitu viwili: mfumo wa elimu ya mkoloni na misaada ya wahisani.

Bila misaada, Ujamaa usingeweza kuwa na hata shule za chini ya mbuyu. Na bila misingi ya elimu ya mkoloni, elimu isingekuwepo.

Kuhusu Botswana, nitaendelea kusema Worshiping dictators is a pain in the a$$. Democratic institutions hazitegemei ukubwa au idadi ya nchi. Ni maamuzi tu ya viongozi wa mwanzo.
 
Amen.
Najua Vijana wataanza kunicharukia kwa bahati ya kwenda kutibiwa bure! Karibu Prof. Mwakyusa atawaletea Apollo pale mlimani ili sote tufaidi matunda ya tiba ya uhakika. Mwakyusa - a product of Ujamaa wa Nyerere!

Kwa mtaji huo Nyerere ni product ya mkoloni. Hivyo tushukuru wakoloni kwa kutusomeshia watu wa mfano wake.
 
Wasomi wa siku hizi bwana! Eti tuilinganishe Tanzania na Botswana! Population ya Botswana ni nusu ya population ya Dar es Salaam. Ka-nchi kenyewe ukubwa wake ni sawa na kisiwa cha Madagascar, ina wilaya tisa tu tena ndogo ndogo! Botswana wana dhahabu, almasi nasikia hata uranium wanayo. 'Wasomi' ndani ya JF wanataka tuifananishe Botswana na Tanzania na tumpongeze Rais wa kwanza wa Botswana kwa kujenga democratic institutions na tumponde na kumkejeli Rais wetu wa kwanza kwamba hakuna la maana aliloifanyia nchi hii!

Hizo democratic institutions zinamsaidiaje mwananchi wa kawaida ambaye, tangu 1966 Uhuru wa Botswana ulipopatikana mpaka sasa, anaisha kwa kipato cha dola moja na ushei kwa siku? Kwa utajiri wote uliopo Botswana ukilinganisha na udogo wa nchi hiyo tungetegemea wenzetu wangelikuwa wanaishi kama wako peponi!

Ni ninyi 'wasomi' wa nchi hii ambao mumeachiwa madini na 'dictator' Mjamaa ambaye hakutaka kujitajirisha yeye na kwa udikteta wake aliwapiga vita sana viongozi wenziwe wasithubutu kujitajirisha. Kaenda Mbinguni kawaachieni madini yamelala ardhini mnashindwa kuwasaidia Watanzania wenzenu ili madini hayo yatumike kwa manufaa ya Taifa. Hivi sasa karibu mtaanza kutoana roho na kuwatoa roho wananchi wasio na hatia kutokana na kutokuzingatia maadili mema aliyokuwa akijaribu kufundisha 'dikteta' Nyerere!

Mnauponda Ujamaa lakini ndio huo uliotuelimisha sie watoto wa wakulima wa vijijini na watoto na wajukuu zetu wanaendelea kufaidi matunda ya sisi kusoma kwetu bureeeee kwa ajili ya Ujamaa mnaouponda. Wakulima vijijini na kizazi chao wana matumaini gani?

Mkiendelea kulaumu Marehemu wa jana badala ya kuangalia ya leo, mengi tu aliyofundisha na aliyotabiri Mwalimu yatatokea.
Umeongea vizuri sana bibi. Mi nnakuunga mkono asilimia 100. Tufanye kazi! Marehemu alifanya nafasi yake. Na kweli wengi wetu tumesoma kwa sababu ya huo Ujamaa. Bila Ujamaa huo sijui wangapi tungekuwa na mapesa ya kwenda shule. Tuwe na shukrani
 
Kwa mtaji huo Nyerere ni product ya mkoloni. Hivyo tushukuru wakoloni kwa kutusomeshia watu wa mfano wake.
Nakubaliana na wewe kuwa Nyerere ni product ya mkoloni kwa maana kwamba ndiyo waliomsomesha na alisoma wakati wa mkoloni. Lakini Mwalimu hakuwa kasuku wa kumeza ujinga wote wa mkoloni. Hakukubali kuwa indoctrinated. Pamoja na kupata elimu ya mkoloni aliweza kujikomboa kifikra, kuondokana na kasumba ya mkoloni. Ndiyo maana alikuwa "jeuri" kwa hao jamaa. Hakuwaogopa hata kidogo kwenye masuala ya ukweli.
Lakini cha zaidi ni kwamba alitufundisha watanzania pia kuondokana na kasumba ya ukoloni. Unakumbuka maneno aliyotamka mwalimu baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar kugoma miaka ya 60 wakisema afadhali enzi za mkoloni?
Kutokana na fikra za Mwalimu watanzania tuko huru kwa kiasi kikubwa kutokana na kasumba ya ukoloni kuliko - naamini - mataifa mengi jirani zetu.
 
Naona sasa tupo kwenye masuala ya syntax na semantic. Katiba ya sasa haina tofauti kubwa na ya wakati wa chama kimoja.

Labda kama unazungumzia katiba ya CCM.

Mkuu Zakumi, Katiba ya sasa ina mabadiliko mengi sana ukilinganisha na Katiba ya wakati wa Nyerere. Kuna vifungu vilivyofutwa na vingine vilivyoongezwa. Kwa mfano,
1. Katiba ya chama kimoja haikuwa na Tume ya uchaguzi
2. Katiba ya chama kimoja haikuwa na vyama vingi
3. Katiba ya chama kimoja ilimsema Makamu wa Rais kuwa ni Rais wa Zanzibar

Na kadhalika. Ukitanua wigo huo hapo juu tu, utagundua kuwa Katiba imebadilika sana.

Ila ni kweli kuwa Katiba hii ya sasa inakipendelea zaidi chama tawala.
 
Ni ninyi 'wasomi' wa nchi hii ambao mumeachiwa madini na 'dictator' Mjamaa ambaye hakutaka kujitajirisha yeye na kwa udikteta wake aliwapiga vita sana viongozi wenziwe wasithubutu kujitajirisha. Kaenda Mbinguni kawaachieni madini yamelala ardhini mnashindwa kuwasaidia Watanzania wenzenu ili madini hayo yatumike kwa manufaa ya Taifa. Hivi sasa karibu mtaanza kutoana roho na kuwatoa roho wananchi wasio na hatia kutokana na kutokuzingatia maadili mema aliyokuwa akijaribu kufundisha 'dikteta' Nyerere!

Mnauponda Ujamaa lakini ndio huo uliotuelimisha sie watoto wa wakulima wa vijijini na watoto na wajukuu zetu wanaendelea kufaidi matunda ya sisi kusoma kwetu bureeeee kwa ajili ya Ujamaa mnaouponda. Wakulima vijijini na kizazi chao wana matumaini gani?

Mkiendelea kulaumu Marehemu wa jana badala ya kuangalia ya leo, mengi tu aliyofundisha na aliyotabiri Mwalimu yatatokea.

Nimesoma kwa makini sana ulichokiandika. Nilichoshindwa ni kuelewa msimamo wako katika issue nzima inayozungumziwa.

Kwanza umemsema Dikteta Mjamaa Nyerere na vita yake dhidi ya utajiri. Baadae ukaongelea faida za dikteta huyo huyo kwa watoto wa wakulima wa vijijini waliopata elimu na kusababisha wajukuu zetu kufaidika nayo. Je, ni Dikteta huyo huyo mwenye kutoa haki namna hiyo?
 
Ndugu zangu, hivi bado hamjatambua kwamba TANZANIA ya sasa haifuati misingi ya utawala bora na ustawi wa haki na sheria? Hapa tuna kitu kimoja tu! Matabaka! Tabaka la WATAWALA dhidi ya WATAWALIWA.

Wanaotawaliwa wanawaona WATAWALA kama Miungu Watu, hivyo kuwaogopa. Wanaotawala wanajiona kama Miungu Watu, hivi kuwaona walio chini yao kama wapagazi na watumwa kwao.

Wanatarajia (wameshaonja asali...) kutawala milele. Si utabiri wangu, lakini nakumbuka kwa mbali Mwalimu akisema "itafika siku mtu asiye nacho atashika panga na kumtafuta aliye nacho na kumwambia ampe sehemu ya hicho alicho nacho, la sivyo..."

Mwenye kusikia asikie. Mwenye kuona aone. Mwenye kutamka atamke.

Tunakoelekea ni kubaya zaidi kuliko tulikotoka. Lakini tuwaambie hawa WANAOTUTAWALA kwamba hila zao tumezitambua, mwaka 2010 tuzifanyie kazi.

WATAWALA wataiba kura mpaka lini? WATAWALA watanunua shahada za kupiga kura za WATAWALIWA fukara mpaka lini? Kama una ndugu yako Biharamulo, mwambie ASIUZE shahada yake ya kupiga kura, kwani, licha ya kwamba ni kosa la jinai, ni sawa na yeye mwenyewe kuuza UTU wake. Umaskini wetu usituponze tukauza UTU wetu kwa WATAWALA mafisadi!

Najipenda, lakini siogopi kusema.

./Mwana wa Haki
 
Nimesoma kwa makini sana ulichokiandika. Nilichoshindwa ni kuelewa msimamo wako katika issue nzima inayozungumziwa.

Kwanza umemsema Dikteta Mjamaa Nyerere na vita yake dhidi ya utajiri. Baadae ukaongelea faida za dikteta huyo huyo kwa watoto wa wakulima wa vijijini waliopata elimu na kusababisha wajukuu zetu kufaidika nayo. Je, ni Dikteta huyo huyo mwenye kutoa haki namna hiyo?

Recta,
Kwa ubongo wangu wa ndege ni kuwa umeshindwa kumwelewa Bibi Ntilie alivyotumia neno dictator. angalia alivoliweka katika ya hizo mark. Bila shaka alikusudia kusema kama mnamwita dictator au ni huyohuyo dictator. Ni uandishi tu. Au wakati mwingini ni sarcasm. Upo mkuu hapo mkuu wa seminary?
 
Nakubaliana na wewe kuwa Nyerere ni product ya mkoloni kwa maana kwamba ndiyo waliomsomesha na alisoma wakati wa mkoloni. Lakini Mwalimu hakuwa kasuku wa kumeza ujinga wote wa mkoloni. Hakukubali kuwa indoctrinated. Pamoja na kupata elimu ya mkoloni aliweza kujikomboa kifikra, kuondokana na kasumba ya mkoloni. Ndiyo maana alikuwa "jeuri" kwa hao jamaa. Hakuwaogopa hata kidogo kwenye masuala ya ukweli.
Lakini cha zaidi ni kwamba alitufundisha watanzania pia kuondokana na kasumba ya ukoloni. Unakumbuka maneno aliyotamka mwalimu baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar kugoma miaka ya 60 wakisema afadhali enzi za mkoloni?
Kutokana na fikra za Mwalimu watanzania tuko huru kwa kiasi kikubwa kutokana na kasumba ya ukoloni kuliko - naamini - mataifa mengi jirani zetu.

No offense. Lakini inaonyesha kuwa unafikiri watu waliosoma wakati wa ukoloni walikuwa makasuku. Huo sio ukweli.

Wakati wa mkoloni, wanafunzi DSM waliandamana kupinga mabadiliko yaliwanyima wanafunzi nafasi za kuendelea.

Wakati wa mkoloni wafanyakazi kama vile bandarini walikuwa wanagoma na kudai haki zao.

Wakati wa mkoloni kulikuwa na mgogoro mkubwa wa ardhi huko Arumeru.

Wakati wa mkoloni kulikuwa na vyama vya ushirika.

Kuna mifano mingi inayoonyesha watu hawakupokea elimu kama kasuku na msitake kupotesha umma hapa.

Migomo ya miaka ya 60 ilikuwepo kwa sababu, mzee mzima alianza kuingilia masuala ya academy kwa mtazamo wake. Alitaka watu waende JKT.

Miaka ya mwisho kabla mkoloni kuondoa, mkoloni alitoa liberty kwa wanafunzi na tulipopata uhuru tu liberty hiyo ikaanza kupotea. Hiyo ndio sababu kubwa ya migomo miaka ya 60.
 
Umeongea vizuri sana bibi. Mi nnakuunga mkono asilimia 100. Tufanye kazi! Marehemu alifanya nafasi yake. Na kweli wengi wetu tumesoma kwa sababu ya huo Ujamaa. Bila Ujamaa huo sijui wangapi tungekuwa na mapesa ya kwenda shule. Tuwe na shukrani

Cha ajabu shukrani ya kusomeshwa kwenu ni wizi, na uzembe makazini.
 
Recta,
Kwa ubongo wangu wa ndege ni kuwa umeshindwa kumwelewa Bibi Ntilie alivyotumia neno dictator. angalia alivoliweka katika ya hizo mark. Bila shaka alikusudia kusema kama mnamwita dictator au ni huyohuyo dictator. Ni uandishi tu. Au wakati mwingini ni sarcasm. Upo mkuu hapo mkuu wa seminary?

Nakushukuru sana Mkuu. Umenifumbua macho. Sikuiona kwa upande huo.

Nadhani maelezo yake sasa yametulia. Hongera sana Bibi Ntilie.
 
Mkuu Zakumi, Katiba ya sasa ina mabadiliko mengi sana ukilinganisha na Katiba ya wakati wa Nyerere. Kuna vifungu vilivyofutwa na vingine vilivyoongezwa. Kwa mfano,
1. Katiba ya chama kimoja haikuwa na Tume ya uchaguzi
2. Katiba ya chama kimoja haikuwa na vyama vingi
3. Katiba ya chama kimoja ilimsema Makamu wa Rais kuwa ni Rais wa Zanzibar

Na kadhalika. Ukitanua wigo huo hapo juu tu, utagundua kuwa Katiba imebadilika sana.

Ila ni kweli kuwa Katiba hii ya sasa inakipendelea zaidi chama tawala.

Katiba ya Tanzania haikubadilika. Mabadiliko ya katiba ya sasa ni sawa kamati ya olimpiki duniani kufuta olimpiki ya walemavu. Na baadaye kuwashauri wanariadha walemavu (vyama vya upinzani) na kushiriki kwenye olimpiki proper pamoja na wanariadha wasio walemavu (CCM).
 
Zakumi,
Mkuu wewe kiboko yaani umezungukwa na watu woten hawa bado unahema... ama kweli mwenzangu Bepari.. sijui kama unaujua ubepari maanake kila naposoma unamlaumu Nyerere na unashindwa kuelewa maelezo ya watu wengine..

Mkuu wangu nimemtumia Hitler kuonyesha jinsi haki na sheria inavyoweza kutafsirika iwe kwa mabaya au mazuri kinachotakiwa ni kusimamisha ili kulinda haki na amani ya wananchi wako. Na nimesema wazi kwamba kosa la Hitler ni pale alipotaka kuitawala dunia lakini within Germany huyu Hitler alionekana kuwa kiongozi bora kama kina Churchill, Washington, Lincoln,Trudeau, Mao tse tung na hata huyo wa Botswana..Kila mmoja wao alichofanya ni kusimamisha sheria iwe ya Kidikteta au Demokrasia lakini wote ktk mitazamo wayo ni ktk malengo ya kusimamisha haki na amani baina ya watu. wake. Umeona mwenyewe Saadam ambaye alikuwa dikteta na uchafu wqote aliofanya lakini sasa hivi nchi imewashinda.. Demokrasia imeshindwa kufanya kazi kabisa...

Nitarudia tena kukwambia kwamba Huwezi kumlinganisha Nyerere na rais wa Botswana hata kidogo... Mimi nimekaa pale Gabarone ni mji mdogo kuliko hata mji wowote wa mikoa ya Tanzania. Nchi nzima ina watu wasiozidi millioni mbili tena wanaishi ktk robo ya eneo la nchi hiyo sehemu zingine zote ni jangwa..
Sasa ikiwa nchi inaingiza mara tatu ya kipato cha tanzania na una population ya watu wa wilaya ya Temeke utashindwa vipi kuiendeleza nchi hiuyo.. Kifupi wWabotswana wanaibiwa vibaya sana kuliko sisi, mabillioni kwa mabillioni yanaibiwa na hawa viongozi wao kila mwaka.. kwa sababu uchumi wa nchi hiyo ni ziada kila siku ya Mungu..Yaani raia wao anaweza kugawa dollar millioni kwa kila raia na fedha ikabakia..That's how rich they are!..Lakini ukweli ni upi?.. Botswana bado wapo bado ktk nchi maskini! ni miaka ya hivi karibuni tu ndio kidogo unaweza kuona mabadiliko hata Gabarone penyewe na sii ya hivyo ukalinganisha na Dubai au Kuwait..

Kuhusiana na katiba, Mkuu sheria ya vyama vingi imeandikwa kabla ya vyama kuzinduliwa hivyo huwezi kusema ni Olimpiki ya walemavu wakati hapakuwepo na walemavu kabla ya.. Ni matusi makubwa sana unayatumia hapa.. na yote haya yanatokana na kushindwa kupata jawabu la matatizo tuliyokuwa nayo. Unachofanya ni kutafuta mchawi... yaleyale ya Miafrika ndivyo tulivyo!.. hapa Unaua albinos tu...
 
"Dola lazima isimamie sheria ili kulinda haki na kuhifadhi amani. Wajibu huu usipozingatiwa, wataibuka manabii wenye kuihubiri haki kwa kuwahukumu wengine. Hamtabaki salama mkifikia hapo" J.K. Nyerere

Dola ya Tanzania imeshindwa kusimamia sheria na kulinda haki na matokeo yake wameibuka mafisadi na sasa mwananchi wa kawaida hayuko salama. Huu ndiyo ukweli na CCM lazima ibebe hii lawama na bado kidogo tu tutahakikisha hukumu tulizozitoa kwa hawa zinatekelezwa - hiyo ndio salama yetu.
Chuo Cha Mafisadi (CCM), sasa lazima kifutwe.
 
Katiba ya Tanzania haikubadilika. Mabadiliko ya katiba ya sasa ni sawa kamati ya olimpiki duniani kufuta olimpiki ya walemavu. Na baadaye kuwashauri wanariadha walemavu (vyama vya upinzani) na kushiriki kwenye olimpiki proper pamoja na wanariadha wasio walemavu (CCM).

Zakumi, inaelekea umesoma Katiba moja tu (ya chama kimoja , kabla ya 1992), au umesahau moja ya Katiba (ya awali) ama hujasoma zote mbili (ya chama kimoja na ya vyama vingi - 1992). Nakushauri ujaribu kutafuta muda uzisome zote mbili halafu uje kujenga hoja hapa.

Mimi sioni lolote linalohusiana na mwongozo wa Nyerere katika utawala wa nchi yetu tangu tuvunje Azimio la Arusha na maazimio mengine yote, tangu turekebishe Muungano (kikatiba), tangu tubadilishe mwelekeo wa kiuchumi wa Taifa na tangu tuanze sera mpya za ubinafsishaji, biashara huria na kuingia kichwa kichwa kwenye globalization (bila kuielewa kwa kina na kuiandalia makao yake katika jamii yetu).

Zakumi, nchi hii haiyumbi kwa kuwa Nyerere aliamua hivyo. Nchi hii ilikuwa imara wakati wake. Sheria zilikuwa msumeno, viongozi walikuwa waadilifu zaidi na wananchi walikuwa na usawa wa wastani kuliko sasa. Sera zozote zilizokuwepo zilitekelezwa bila kujali eneo, rangi ya watu, uwezo n.k. WaTanzania walikuwa waTanzania wa kweli japo masikini.

Hivi sasa tumebadili mwelekeo kiasi kwamba, ili tuweze kurudi hadi pale alipotuachia Nyerere, tunahitaji kupigania uhuru upya. Na ni baada ya kufanya hivyo ndipo tunaweza kujiendeleza tena na kufika kwenye ustaarabu tunaoutaka. Kuna njia panda ambayo tulikosea kuchagua upande wa kupita na sasa tumepotea. Lakini tatizo letu si kukosea njia tuliyopita baada ya kufika njia panda, bali ni kuendelea kujidai hatujapotea na kuendelea na safari yetu hadi tutakapopotea zaidi na kushindwa kurudi tulipotoka.

Hilo ndilo linalotia hofu kuu.
 
Zakumi,
Mkuu wewe kiboko yaani umezungukwa na watu woten hawa bado unahema... ama kweli mwenzangu Bepari.. sijui kama unaujua ubepari maanake kila naposoma unamlaumu Nyerere na unashindwa kuelewa maelezo ya watu wengine..

Mkuu wangu nimemtumia Hitler kuonyesha jinsi haki na sheria inavyoweza kutafsirika iwe kwa mabaya au mazuri kinachotakiwa ni kusimamisha ili kulinda haki na amani ya wananchi wako. Na nimesema wazi kwamba kosa la Hitler ni pale alipotaka kuitawala dunia lakini within Germany huyu Hitler alionekana kuwa kiongozi bora kama kina Churchill, Washington, Lincoln,Trudeau, Mao tse tung na hata huyo wa Botswana..Kila mmoja wao alichofanya ni kusimamisha sheria iwe ya Kidikteta au Demokrasia lakini wote ktk mitazamo wayo ni ktk malengo ya kusimamisha haki na amani baina ya watu. wake. Umeona mwenyewe Saadam ambaye alikuwa dikteta na uchafu wqote aliofanya lakini sasa hivi nchi imewashinda.. Demokrasia imeshindwa kufanya kazi kabisa...

Nitarudia tena kukwambia kwamba Huwezi kumlinganisha Nyerere na rais wa Botswana hata kidogo... Mimi nimekaa pale Gabarone ni mji mdogo kuliko hata mji wowote wa mikoa ya Tanzania. Nchi nzima ina watu wasiozidi millioni mbili tena wanaishi ktk robo ya eneo la nchi hiyo sehemu zingine zote ni jangwa..
Sasa ikiwa nchi inaingiza mara tatu ya kipato cha tanzania na una population ya watu wa wilaya ya Temeke utashindwa vipi kuiendeleza nchi hiuyo.. Kifupi wWabotswana wanaibiwa vibaya sana kuliko sisi, mabillioni kwa mabillioni yanaibiwa na hawa viongozi wao kila mwaka.. kwa sababu uchumi wa nchi hiyo ni ziada kila siku ya Mungu..Yaani raia wao anaweza kugawa dollar millioni kwa kila raia na fedha ikabakia..That's how rich they are!..Lakini ukweli ni upi?.. Botswana bado wapo bado ktk nchi maskini! ni miaka ya hivi karibuni tu ndio kidogo unaweza kuona mabadiliko hata Gabarone penyewe na sii ya hivyo ukalinganisha na Dubai au Kuwait..

Kuhusiana na katiba, Mkuu sheria ya vyama vingi imeandikwa kabla ya vyama kuzinduliwa hivyo huwezi kusema ni Olimpiki ya walemavu wakati hapakuwepo na walemavu kabla ya.. Ni matusi makubwa sana unayatumia hapa.. na yote haya yanatokana na kushindwa kupata jawabu la matatizo tuliyokuwa nayo. Unachofanya ni kutafuta mchawi... yaleyale ya Miafrika ndivyo tulivyo!.. hapa Unaua albinos tu...

Mkandara:

Sio kwamba naupenda ubepari, lakini siwezi kukubali upuuzi wa kuwa ujamaa ni alternative ya ubepari. Na vilevile sikubali kuwa Tanzania inaweza kuwa welfare state kwa kutumia Ujamaa.

Makabila yetu mengi hayajapitia hata feudalism. Basi itakuwaje turuke steps zote ambazo ni muhimu katika maendeleo ya jamii?

Watanzania tunaEngineer maendeleo na tunatakiwa kutumia njia zote zinazofaa ziwe za kutoka East or West.

Kuhusu Botswana: Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi. Watanzania mliamini kuwa Ujamaa utashinda. Na ukishinda utakuwa mfano kwa nchi zingine za kiAfrika kufuata. Na vilevile watanzania watakuwa makuhani wa kueneza Ujamaa barani Africa. Tuliiweka Tanzania katika nafasi isiyostahili. Leo ujamaa umeshindwa, many of you haven't come to terms with the demise of Ujamaa. Kilichobakia ni wivu tu. Kenya wakifanya vizuri kidogo, mnasema mkoloni aliwaacha pazuri. Botswana akifanya vizuri, mnasema nchi ndogo.

Kuhusu sheria na katiba ya vyama vingi. Wabunge wa CCM (chama kimoja) ndio waliotunga sheria ya kuanzisha vyama vingi. Hapa ni sawa na Yanga kutunga taratibu za kuendesha mashindano ya ligi ya soka Tanzania.
 
Zakumi, inaelekea umesoma Katiba moja tu (ya chama kimoja , kabla ya 1992), au umesahau moja ya Katiba (ya awali) ama hujasoma zote mbili (ya chama kimoja na ya vyama vingi - 1992). Nakushauri ujaribu kutafuta muda uzisome zote mbili halafu uje kujenga hoja hapa.

Mimi sioni lolote linalohusiana na mwongozo wa Nyerere katika utawala wa nchi yetu tangu tuvunje Azimio la Arusha na maazimio mengine yote, tangu turekebishe Muungano (kikatiba), tangu tubadilishe mwelekeo wa kiuchumi wa Taifa na tangu tuanze sera mpya za ubinafsishaji, biashara huria na kuingia kichwa kichwa kwenye globalization (bila kuielewa kwa kina na kuiandalia makao yake katika jamii yetu).

Zakumi, nchi hii haiyumbi kwa kuwa Nyerere aliamua hivyo. Nchi hii ilikuwa imara wakati wake. Sheria zilikuwa msumeno, viongozi walikuwa waadilifu zaidi na wananchi walikuwa na usawa wa wastani kuliko sasa. Sera zozote zilizokuwepo zilitekelezwa bila kujali eneo, rangi ya watu, uwezo n.k. WaTanzania walikuwa waTanzania wa kweli japo masikini.

Hivi sasa tumebadili mwelekeo kiasi kwamba, ili tuweze kurudi hadi pale alipotuachia Nyerere, tunahitaji kupigania uhuru upya. Na ni baada ya kufanya hivyo ndipo tunaweza kujiendeleza tena na kufika kwenye ustaarabu tunaoutaka. Kuna njia panda ambayo tulikosea kuchagua upande wa kupita na sasa tumepotea. Lakini tatizo letu si kukosea njia tuliyopita baada ya kufika njia panda, bali ni kuendelea kujidai hatujapotea na kuendelea na safari yetu hadi tutakapopotea zaidi na kushindwa kurudi tulipotoka.

Hilo ndilo linalotia hofu kuu.

Kuhusu katiba hakuna mabadiliko yoyote ya maana na ndio maana CCM wanashinda tena kisheria kwa kutumia bajaji wakati CHADEMA wanatumia Helikopta.

Kuhusu sheria wakati wa Nyerere I beg to differ. Kama sheria zilikuwa zinafuatwa kwanini waandishi wa habari hawakuwa huru au hatukuwa na uhuru wa kufanya tunavyotaka?

Kuhusu kupigani uhuru upya. Hiyo kazi Nyerere alimaliza na is the best of the best katika hiyo nyanja. Labda tu kama unataka kuvunja record zake. Tatizo kubwa ni wewe na wenzako mko Paranoia tu kwa sababu mnashindwa ku-influence maendeleo kama mnavyotaka nyinyi na mmebanwa na ndugu zenu waliosomeshwa bure na Ujamaa.

Lakini hata kama mtafanikiwa kuupata huo uhuru mpya, likehood ya wewe kurudi makosa ya sasa ni kubwa kwa sababu za kiutamaduni.
 
Zakumi,

Mkuu hata sikuelewi kabisa.. unaposema makabila yetu hayakupitia feudalism una maana gani?. Kwani hao kina Mkwawa, Mirambo, Mengi Sina na wengine wote walitawala vipi sehemu zao..Ni step zipi ambazo zilirukwa ikiwa tuliweza kuunganisha tawala hizi na kuunda chama cha TAA chini ya mwenyekiti ambaye hakuwa mtawala wa makabila..ebu nifahamishe vizuri.

Na kuhusu Botswana hakuna aliyesema ukubwa wa pua ni wingi wa makamasi ila nimesema makamasi mengi toka pua ndogo..huwezi kujikamua jipua lako kubwa ukafikiri ni sifa wakati huna makamasi..Wewe ndiye unataka kulinganisha pua hizi kupata wingi wa makamasi..Utafananishaje Tanzania na Botswana nchi yenye maendeleo eneo lisilozidi mkoa mmoja wa Tanzania..Barabara ya Pugu road peke yake ni highway ya Botswana mwanzo hadi mwisho..Kama uliwahi kuona ile sinema ya Gods must be crazy, basi hiyo ndio hali halisi ya mazingira na makazi ya watu huko vijijini (3/4 ya nchi hiyo).
Mkuu wangu tunajipima maendeleo yetu kutokana na uwezo wetu, waswahili wanasema cha mtu mavi..Usitegemee yaliyoko Botswana au Dubai yanawezekana au yaigwe yataboresha maisha ya WaTanzania..wala Kuiga kunywa kwa Tembo kwa sababu tu Unayaona maendeleo toka Marekani basi nasi tunaweza kuwa kama wao... tutapasuka msamba..

Mkuu hawa jamaa wametoka mbali sana na nikufahamishe tu kwamba Ujamaa ulianzwa hatra nchi hizo.. Marekani, Ufaransa na hata Uingereza walipitia Ujamaa kufika hapa walipo na hadi leo hii wana vitu kibao viko chini ya serikali wanaviuza (privatise) taratibu kulingana na wakati..Sio sisi tuliokuja uvamia Ubepari kwa sababu tu IMF imezungumza wakati tukijua fika walitaka kuingia na Ukoloni mamboleo tukashindwa hata kuweka guard zetu sawa.
 
Back
Top Bottom