Je alichotabiri Nyerere tayari kinatokea sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je alichotabiri Nyerere tayari kinatokea sasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanzania, Jun 4, 2009.

 1. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  "Dola lazima isimamie sheria ili kulinda haki na kuhifadhi amani. Wajibu huu usipozingatiwa, wataibuka manabii wenye kuihubiri haki kwa kuwahukumu wengine. Hamtabaki salama mkifikia hapo"

  J.K. Nyerere
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ndugu yangu wewe hujipendi!
   
 3. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mtanzania:

  Fortune favours the brave. Remember that.

  Mambo mengine waliyopangwa kwenye dola ya watanzania ni imagination ya viongozi waliopita na sio experience ya watanzania wenyewe.

  Hivyo wache watu wakanyagane na wajenge experience. Matatizo yakizidi watatokea washindi na mashujaa wa kuiandika historia.
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Kwani Nyerere alikuwa Mungu mtu?
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Huyu mzee kuna mazuri na mapungufu aliyoyafanya, kwangu moja ya pungufu kubwa la Mwalimu, ilikuwa kutoheshimu utawala wa sheria na ndilo tatizo kubwa linalotula Tanzania sasa hivi, tumedumaa kiuchumi, kielimu, kisiasa ni kwa sababu ya kutojua kuheshimu sheria wala haki, mbegu za matatizo ya kisheria na hali tuliyonayo sasa aliyapanda yeye mwenyewe no wonder alijua kuwa kuna siku hatutabaki salama,

  - Alimuona kwa macho yake Salmin akiiba uchaguzi, akanyamaza akidai eti ameongea na Salmin amemuahidi kuwa ataunda serikali ya mseto, serikali ya mseto my foot! ndio maana leo huko Visiwani hakuna salama, sasa how can one call huu kuwa ni utabiri?

  - Utabiri of what wakati ni wewe mtabiri unayeyapanda hayo hayo matatizo yatakayokuja kuleta matatizo halafu you turn arround na kutabiri kwamba matatizo uliyoyapanda yatakuja kuleta matatizo? I do not get it!

  Respect.

  FMEs!

   
 6. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Inawezekana uko sahihi lakini tulitaraji walioomba uongozi (isomeke utawala) kurekebisha hayo. Ni uhawayani uliopindukia kuendelea kumlaumu mfu. Tuwaache wafu wawazike wafu wenzao.
   
 7. mohammedzahor

  mohammedzahor Member

  #7
  Jun 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka yangu wewe tatizo la mwalimu ni kumuangalia dr. Salmini tu. Mimi nadhani tatizo unalo wewe zaidi mana umetoka nje ya mada.
  Wazee wanasema kama hujafanya utafiti huna haki ya kusema, hivyo ni vyema unyamaze kimya ili usidhihirishe ujinga wako kwa umma.
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Uhayawani utakuwa kutotafuta ukweli wa matatizo yetu yalipo na yalipotokea, huwezi tatua tatizo ambalo hujui kuwa unalo na limekutokea wapi, kutafuta ukweli sio kumlaumu mfu ni kutafuta nothing but the truth, uhayawani wa juu na wa ajabu utakua ni kuwalamumu wanafunzi wa muanzishaji bila ya wananchi ambao walikuwepo wakati matatizo yanapandwa!

  Respect.

  FMEs!
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Matatizo ya sheria na haki Tanzania yapo kila mahali, lakini kuna yanayozidi mipaka kama yale ya mauaji ya Pemba, yasingetokea kama kule kungekuwepo na sheria, je ile sheria ilianza kuvunjwa na nani?
  - Hapa chini naona mkuu uko kwenye mada, binafsi sioni faida yake kwa taifa kwa hiyo nakuachia mwenyewe! na wala hayanihusu!

  Respect.

  FMEs!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Tizama sheria zetu za sasa alizozipanda Mwalimu!

  Respect.

  FMEs!
   
 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Unaweza rekebisha jambo likupalo mlo kwa mlango wa KIA( Chai Maharage)?
  Uovu haupatilizwi nusu nusu. Kabla ya kupatilizwa uovu ni lazima ujae katika kipimo chake kisha ufurike ndipo ghadhabu ya upatilizo itakapo inuka na kuwachanganya wote, waliokuwemo na wasiokuwemo.
   
 12. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I stand by what I said. Kama ingekuwa hakuna kujifunza kutoka kwa waanzilishi bila shaka hadi leo dunia ingekuwa ina ndege zilizotengenezwa na wana ndugu Alright .
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Nadhani wewe ndo umedandia UDA ya Rangi Tatu safarini kwenda Ubungo.
  Hilo tatizo lilisemwa ni mfano mmoja wa kulea Mapimbi Tanzania.
  Kuna matatatizo ya kuwaacha Watanzania wajiju huku yeye akishughulika na Ukombozi kusini mwa Afrika.
  Kuna Matatizo ya kunyang'anya watu ardhi mika ya 70 leo wanauziwa wageni.
  Kuna Tatizo la kujenga siasa ambayo hata yeye mwenyewe hakuwahi ianisha wazi wazi kiuchumi.
  Kuna Tatizo la kuibana sekta ya Elimu ngazi ya Sekondari na vyuo.
  Kuna tatizo la Kuhusudu na kuabudu jembe la mkono.
  Yako mengini.

  Ukivuna Bangi maana yake ulipanda Bangi.
   
 14. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sawa sawa lakini kudhani kuwa Nyerere anawezakusaidia kwenye hali tuliyomo kunanipa shia kuelewa. The man not only is dead but also decomposed. Tukae kusema tu huyu ndiye aliyetusababishai haya na hivyo tumekwisha? Ngekuwepo tungemwambia kama wanavyofanya wanaodai kusafishwa wanapokashfiwa na wahariri. Kwa kiwango na ukurasa sawa ulivyotoa habari hiyo nitake radhi. Tungemwambia nyerere kwa kiwango kile kile ulichotufikisha huku sahihisha.
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  What is the meaning of history?

  history is anything that is past recorded, weather about culture, food or people.

  History is also about all the remaining facts of past time that is extincted to this day. plenty of people use history.

  - I am not moving, kwamba mtabiri hatakiwi kuwa mshiriki wa kutengeneza utabiri anao utabiri maana utakuja kutokea tu kama yanayotupata sasa ya kutokuwa na utawala wa sheria na haki!

  Respect.

  FMEs!
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Jun 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu FMEs,
  Hakika mwalimu alikuwa mwalimu kweli.. ebu soma tena maneno yako hapo juu kisha vuta maneno ya mwalimu hapa chini

  "Dola lazima isimamie sheria ili kulinda haki na kuhifadhi amani. Wajibu huu usipozingatiwa, wataibuka manabii wenye kuihubiri haki kwa kuwahukumu wengine. Hamtabaki salama mkifikia hapo"

  J.K. Nyerere

  Mkuu ni exactly alichosema mwalimu na kinaleta maana kabisa.. Hapa tunazungumzia maneo ya mwalimu ili tuyapime na hali iliyopo, tayari watu wamekwisha ibuka manabii wanaotaka kumhukumu mwalimu...

  Mkuu tafadhali, unajua fika kwamba Salmin alipoingia Ikulu ya Zanzibar ni mwaka 1990, mwenyekliti wa CCM alikuwa Mwinyi, iweje leo kweli tuanze kumzungumzia mwalimu ambaye aling'atuka kwa kila makosa ambayo yametokea..Hivi kweli tunaweza kumlaumu Mkapa kwa chaguzi zote za Kikwete kwa sababu tu alikuwa rais kabla ya Kikwete!..

  Haya maswala kudumaa kielimu na Kisiasa kweli umeyafanyia utafiti au?.. mkuiu ulikuzwa na mwalimu na tunayaona matunda yake wewe ukiwa mfano mzuri wa somo la mwalimu...inakuwaje leo unaanza na habari kama vile sii wewe mwandishi...Nitakukumbusha tena kuwa hapa JF bado naamini kabisa wanafunzi wa mwalimu ndio shina la elimu zote tunayopata humu....

  Mwalimu had power, yes hilo linafahamika lakini mwaka 1990, ni mwaka ambao Mwinyi alianza kuchukua mwelekeo wake..

  Kweli yawezekana mwalimu hafuati sheria lakini sii yeye aliyeanzisha vyama vingi na akapingwa na viongozi na wananchi wengi..Je, leo hii kutofanikiwa kwa demokrasia nchini tunaweza kumlaumu kweli Nyerere ati kwa nini alipindisha sheria na matakwa ya wananchi kutokuwa na vyama vingi isipokuwa CCM..

  Hivi kweli kama sii kuwepo kwa vyama vingi leo hii mzee wangu FMES ungeweza kusema haya unayoyasema hapa..watu kama Mbowe, Dr. Slaa, Zitto, Mwakyembe, Mama Kilango hawa wote ni matunda ya mwalimu tena basi kama unakumbuka bunge la mwaka 1995 jinsi lilivyokuwa na upinzani wenye nguvu sidhani kama ungefikia kusema haya yote.....

  Lau kama kile chama cha NCCR kilichowaunganisha wanasiasa wakongwe kingeendelea kuwepo hadi leo sidhani kama CCM ingekuwa madarakani....sidhani...Lakini tumekuja vuruga sisi wenyewe kwa kugombania hizo ruzuku na posho.. Na CCM wajanja wameweka kiwango kikubwa cha posho na ruzuku za Wabunge ili muuane wenyewe..

  Kinachotokea leo sii unabii bali ni manabii wa Uongo, wagombea ruzuku na posho za serikali kwani wenye uchungu husimama imara hata kama wanapingwa na bunge zima.. Na tunawajua!
   
 17. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sema wewe Mkandara kiazi nikisema mimi muhogo nitaambiwa ni mzizi
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Bob, hapa tunaongea simple politics, unasema Mwalimu alikuwa hana nguvu by 1990, sasa alianzishaje vyama vingi huku akiwa hana nguvu? Wakati wa uhuru si vyama vingi vilikuwepo, and then vilipotelea wapi? Hivi kweli sio Mwalimu aliyemshauri Mrema kugombea ubunge na kusahau urais? hivi kweli mkuu wangu bado huoni kuwa Mwalimu alikuwa na mapungufu ya kutopenda sheria na ndiyo tumeyarithi as a nation, na ndio maana tumekwama?

  - Mambo ya rais wetu kuwa na kofia mbili ndiyo yaliyokuwa chanzo cha kuharibu utawala wa sheria, akaanzisha tabia za kuwapeleka CCM wavunja sheria za jamhuri tabia ambayo tumeirithi mpaka leo, badala ya kuwafikisha kwenye mkono wa sheria, fate ya Lowassa na Richimonduli inaenda kujadiliwa CC na NEC badala ya Kisutu, halafu unashangaa kwa nini hatuna sheria na haki?

  - Mwalimu was the greatest hilo halina ubishi, lakini kwenye sheria alikuwa na mapungufu makubwa sana na ametuachia matatizo makubwa sana ambayo huenda hiki kizazi yakatushinda kuya-overcome, wa-Tanzania hatujui sheria, hatujui ukweli, na hatujui haki ukweli ni kwamba hatujui! Ndio maana na Sokoine naye akaanza kumuiga Mwalimu na kuwa na sheria yote mikononi mwake, Mrema naye akajaribu akiwa waziri kuwa na sheria zote mikononi mwake, ndio maana tumekwama na sio rahisi kujinasua maana viongozi karibu wote tulionao leo ni wanafunzi wake na wao sheria ndio hakuna kabisaa! ujanja ujanja tu ambao in the end ni temporary tu huku taifa linadidimia na wote tunadidimia!

  Respect.

  FMEs!
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkulu Bob, tizama maneno ya a sitting Waziri Mkuu wetu, masikini ya Mungu hajui hata power alizonazo kisheria kwamba sisi wananchi tunamtegemea yeye kusimamia sheria na kama anashindwa anamfikishia rais wa jamhuri, kama sheria hazitoshi anatakiwa kwenda bungeni kuomba ammendment ili apewe sheria imara za kusimamia taifa kwenye rushwa na ufisadi,

  - yeye anaenda kuwalilia wachungaji wa Dini, ooooh! Mungu ibariki Tanzania! Akitoka huko anaenda CC na NEC kulalamikia sheria siku imeisha na yeye anaweza kuwa Waziri Mkuu kwa term mbili pia kama Sumaye!


  - Respect.

  FMEs!
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jun 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  FMES,
  Mkuu swala la kuanzisha vyama vingi halihusiani na nguvu ya mtu bali nguvu ya hoja..Tunamlaumu Nyerere kwa makosa yetu wenyewe ikiwa ni pamoja na kumpendekeza kwake Mkapa....Mijitu mijinga tukamchagua kwa kura kibao...

  Umesema tena Nyerere alimshauri Mrema kutogombea Urais! - ALIMSHAURI....Then, what mbona Mrema aligombea Urais na kidogo achukue kiti cha Ikulu!..Nguvu ya kumzuia mtu na ushauri au hoja ni vitu viwili tofauti kabisa..Ni huyo huyo Nyerere msaafu aliyewaita Mrema na Sharrif Hamad na kuwapongeza kama Wapinzani, Mwinyi akamtumia watu wa Usalama wa taifa huko Butiama..Hii ndio nguvu ya mtawala.
   
Loading...