Mate sio kilainishi sahihi wakati wa tendo la ndoa na ni hatari kwa afya ya Mwanamke

Kiungonguli

Member
Jul 26, 2015
60
96
Wakati matumizi ya mate yakiwa maarufu kwa wengi wakati wa kujamiiana, hasa yanapotumika kama aina fulani ya kilainishi hasa ukeni na hivyo kuleta ladha ya tendo, habari si njema sana kwa watumiaji wa mate hayo wanapoburudika, hasa kwa wanandoa.

Wataalamu wa afya wamesema kuna ongezeko la magonjwa yanayosababishwa na maambukizi ya fangasi na bakteria katika via vya uzazi vya mwanamke, huku chanzo kikubwa kikitajwa kuwa ni mate.

Uzoefu unaonyesha baadhi ya wanaume wamekuwa wakiyatumia mate kama kilainishi wakati wa tendo, hivyo wanawake kupata magonjwa hayo ambayo huwasababishia kutokwa uchafu na harufu mbaya ukeni.

Hali hiyo imewafanya wanawake wengi kusaka tiba mitandaoni wakitafuta dawa za kutibu matatizo hayo kwa kusafisha uke kwa njia mbalimbali, ikiwemo kujifukiza na kuweka vitu mbalimbali ukeni kwa lengo la kutibu fangasi na bakteria.

Hata hivyo, wataalamu wameenda mbali zaidi na kudai kuwa magonjwa hayo ambayo huonyesha dalili mbalimbali yasipotibiwa kwa wakati husababisha bakteria na virusi hao kushambulia zaidi uke na kupanda taratibu mpaka katika via vya uzazi vya mwanamke na kusababisha ugonjwa wa maambukizi katika via vya uzazi (PID).

Mkuu wa Kitengo cha magonjwa na kinamama na uzazi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Nathanael Mtinangi alisema kitendo cha matumizi ya mate wakati wa tendo hakishauriwi na hakikubaliki kisayansi.
“Sana sana ni kusababisha na kusambaza magonjwa. Haikubaliki,” anassema.

Sayansi inaeleza kuwa kinywa cha binadamu kimeundwa na mamia ya bacteria ‘oral micro flora’ ambao ni rafiki kwa afya ya kinywa, hata hivyo wana madhara iwapo wataenda ukeni.

Pia katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kuna aina ya bacteria ‘lactobuciluss’ pamoja na fangasi ‘candida albicans’ ambao ni rafiki kwa mfumo wa uzazi wa mwanamke, lakini sayansi inasema hawa wana madhara iwapo wataenda mdomoni.

Maambukizi yanavyotokea
Baadhi ya madaktari bingwa wa magonjwa ya uzazi walithibitisha kuwa magonjwa yanayosababishwa na fangasi na bakteria kwa wanawake yamekuwa yakiongezeka hivi sasa, licha ya kwamba yamekuwepo kwa kipindi kirefu.

Daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa uzazi na wanawake kutoka Hospitali ya Aga Khan, Jane Muzo, alisema unapochukua mate na kuyaweka katika uke wa mwanamke unahamisha bakteria wanaopatikana katika mdomo na kuwaleta katika uke.

“Kumbuka hao ni aina tofauti ya bakteria, hivyo hawawezi kuishi pamoja, matokeo yake hukinzana na husababisha wageni au wenyeji kudhoofika.

“Wenyeji wanapodhoofika husababisha bakteria wageni kutawala eneo hilo na kwa kuwa bakteria hao sio eneo husika kwao kuishi huanza kuleta madhara makubwa katika uke na kusababisha aina mbalimbali za maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke,” alisema.

Alisema bakteria hao wakati mwingine huzoeana na kuzaa bakteria chotara wanaoweza kuwa wapole au wakali. Iwapo watakuwa wakali husababisha saratani ya kizazi, uvimbe na magonjwa mengine ya mfumo wa uzazi.

Daktari bingwa wa magonjwa ya uzazi na wanawake kutoka hospitali ya Salaaman iliyopo Temeke, Abdul Mkeyenge alieleza kuwa kwenye kinywa cha binadamu kuna bakteria ambao makazi yao ni huko, hivyo wanaotumia mate kama kilainishi wanakosea.

“Kisayansi mate hatuyatumii kama kilainishi katika kufanya tendo la ndoa kwa kuwa kwenye kinywa kuna bakteria tofauti, hivyo unapotumia mate kama kilainishi kuna faida ya wakati huohuo, lakini utakuwa unawahamisha wale bakteria kuja ukeni, kwa hiyo madhara yake ni maambukizi,” alisema Dk Mkeyenge.

Alisema bakteria anapoingia huanza kushambuliana na bakteria rafiki wa ukeni na mara nyingi bakteria wa ukeni huishiwa nguvu.

“Wale bakteria wanaanza kutoka pale kwenye uke wanapanda mpaka kufikia pale juu kwenye via vyote vya uzazi, hapo mwanamke anaweza kuja kupata ‘bacterio vaginosis’ ataanza kupata dalili za uchafu unaotoka na harufu, lakini kitaalamu inaitwa kisamaki samaki,” alisema.

Alisema pia mwanamume anaweza kuwa na maambukizi ya fangasi au bakteria wengine kwenye kinywa hivyo anavyoyatoa mate mdomoni na kuyapeleka ukeni ni rahisi kumsabababishia mwenzi wake akapata maambukizi ya fangasi sehemu za siri.

Alisema wamekuwa wakitibu wagonjwa wengi wa marudio ambao wanaugua fangasi mara kwa mara.

“Wanawake wanalalamika wanapata fangasi zisizoisha kila siku anatibiwa hospitali hajajua sababu ni nini, kumbe huwa anafanyiwa hivyo na mpenzi wake badala ya kupona inazidi kuendelea.

“Mwingine kwenye kinywa anaweza kuwa na virusi wengine wengi, akipaka mate anatoa maambukizi mwenzake anapata vipele, wengine hunyonyana sirini ni rahisi kupata maambukizi ya bakteria, fangasi au virusi katika mfumo wa uzalishaji,” alisema.

Alisema wapo wanawake wanaopata madhara makubwa zaidi, ikiwemo kutokwa na maji machafu wakati wa tendo na hivyo kupoteza thamani yao na kuonya kwamba asipopata matibabu kwa wakati tatizo huwa kubwa zaidi.

Alitaja madhara mengine ya bakteria hao kuwa ni pamoja na mwanamke kupata maambukizi katika via vya uzazi, yaani PID.

“PID hii tunaita ni maambukizi katika via vya uzazi. Hawa bakteria wakishashamiri ukeni wataanza kuleta haya madhara madogo madogo lakini wanapozidi kupanda juu husababisha maambukizi katika via vya uzazi ambayo ndiyo PID,” alisema.

Aliyataja madhara ya PID kuwa ni pamoja na kupata ugumba, uvimbe, ujauzito kutunga nje ya kizazi, kuwa na mkusanyiko wa usaha katika sehemu za nyonga na madhara mengine.

Nini kifanyike?
Dk Mkeyenge alisema wanaume wanatakiwa kuwaandaa wenza wao wakati wa kufanya tendo la ndoa.

“Wengi wanapokuwa na wenza hawawaandai vizuri, baadaye wakati wa tendo unakuta anakuwa mkavu hajapata ule ute ambao ndiyo kilainishi kutoka mwilini.

“Ukimwandaa vizuri kuna majimaji ambayo anaweza kuyatoa ndiyo yanayosaidia kulainisha sehemu za siri, hata baadaye ukija kumwingilia hatahisi maumivu yoyote wala karaha...

“Wanaume wengi hawawaandai wenza wao ipasavyo, hivyo baadae wanapata michubuko na wanaumia, hapo ndipo mwanaume anatafuta suluhisho la haraka wanatumia mate kama kilainishi lakini kiafya haitakiwi,” alisema Dk Mkeyenge.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Dare, Dk Lilian Mwakyosi, alisema maandalizi ya tendo hupaswa kufanyika kwa kipindi kirefu kila mmoja kumuandaa mwenzake kisaikolojia, hasa mwanaume kumwandaa mwanamke ili kuepuka msuguano.

“Msuguano unaweza kusababisha maumivu kwa mwanamke, kukosa hamu ya tendo, damu wakati wa tendo na maambukizi ya magonjwa mbalimbali, ikiwemo virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine ambayo huambukizwa kwa njia ya ngono,” alisema.

Utafiti
Utafiti uliochapishwa kwenye jarida la bailojia la PLoS Agosti 2020 ulithibitisha kuwa tendo la ndoa kwa kutumia kinywa kunaweza kusababisha mazingira ya maambukizi ukeni.

Utafiti ulibaini wanawake wenye ugonjwa huo, huenda wasioneshe dalili lakini wengine hutoa harufu mbaya.

Pia unaonesha aina fulani ya bakteria inayopatikana kwenye mdomo, ikihusishwa na magonjwa ya kwenye ufizi na utando wa meno, unavyoweza kuchangia kupata ugonjwa huu.

Bakteria wa mdomo ‘Fusobacterium nucleatum’ walionekana kusaidia ukuaji wa bakteria wengine kwenye tatizo la kuwashwa kwenye uke.

Watafiti, Dk Amanda Lewis kutoka chuo cha California na wafanyakazi wengine, wanasema kuwa utafiti huo unaonyesha matumizi ya mdomo kwenye tendo la ndoa yanavyoweza kuchangia ugonjwa wa kuwashwa kwenye uke.

Kuhusu mate
Dk Mkeyenge alisema mate yametengenezwa au yanaundwa na vitu vitatu, ikiwemo uteute, majimaji na kimeng’enya kinachofahamika kama ‘salivary amylase au ptyalin’.

Kazi ya maji yaliyo katika mate ni kuyeyusha chakula kinywani, kulainisha chakula kiwe rahisi kumeza, kimeng’enya (salivary amylase) ni kubadili wanga / kabohaidrete kuwa sukari rahisi ‘maltose’ hivyo kufanya kazi kubwa ya mate kuwa ni kimeng’enya chakula.

Alisema hivyo vitu kazi yake ni kulainisha chakula kinapoingia kwenye kinywa kiwe tayari kwa kumezwa na kulainishwa na enzymes ina kazi ya kuvunja vunja chakula kutoka kwenye wanga kwenda kuwa sukari.

Hata hivyo, alisema mate hayo huishi kwenye kinywa cha binadamu na huwa kuna muunganiko wa bakteria zaidi ya mmoja ambao wakiwa mdomoni hawana madhara yoyote, kwani wapo ili kulinda kinywa.

“Kwenye mwili wa binadamu kuna bakteria wengi sana na hawa wote hawana madhara, waliopo kwenye ngozi hawana madhara isipokuwa wakiingia wataleta madhara kwenye tishu kwa kutengeneza usaha na tishu itaoza kutakuwa na kidonda ambacho kitakuwa kinatoa usaha,” alifafanua.

Wasemavyo wanaume, wanawake
Baadhi ya wanaume waliozungumza na Mwananchi, walisema wamekuwa wakitumia mate kutokana na baadhi ya wanawake kukosa hisia wakati wa tendo la ndoa.

“Zamani wanawake ukishakuwa nao tu hampati shida, lakini siku hizi tunalazimika kutumia mate sababu ndiyo kilainishi pekee, hata kama anatumia bia au mvinyo wameshakuwa sugu, hivi vitu havisaidii,” alisema Side Musa, mkazi wa Dar es Salaam.

Baadhi yao walisema wamekuwa wakipata shida hiyo kwani wanawake wengi hawana hamu ya tendo hivyo wanashindwa kulainika mapema.

“Wengi siku hizi wanawaza pesa, sasa hapo unadhani inakuwaje, wapo wanaowaza marejesho ya vikoba mpo eneo la tukio lakini yeye mawazo yake yapo mbali kabisa, utamwandaa hadi utachoka yupo tu,” alisema Kelvin Mushi.

Hata hivyo, baadhi ya wanawake walisema hali hiyo haiingiliani na kile ambacho wanaume wanakisema bali ni matokeo ya kimaumbile.

“Mwanamume anaweza kuwa amerudi amechoka, lakini ukajua hatakuwa na uhitaji na wewe akili yako ukaielekeza kwingine, baadaye unashangaa ana uhitaji na wewe haupo tayari kwa wakati huo,” alisema Mama Imran, mkazi wa Kimara Korogwe.

Mkazi wa Arusha, Ashura Mushi alisema kuna ukweli kwamba baadhi ya wanawake wanakosa hamu, hali inayochangia mate kutumika.

Source: Mwananchi
 

hydroxo

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
2,248
3,747
IMG-20220715-WA0006.jpg
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
33,838
75,698
Uzi huu umekaa kibaguz mno,
Wao mbona hutulamba uume wanapotuandaa (almaarufu blowjob)
 

Amazon2

JF-Expert Member
Jul 31, 2019
3,917
6,627
kupaka mate kwenye kichwa Cha uume kunaongeza stimu ya mapenzi,

Ni kama vile unavompiga kibao kalioni wkt wa doggy style
Sio kwamba tunapenda kupaka mate, kuna wanawake kei zao kavu kama jangwa.
Ukilazimisha kuingiza bila kulainisha kidogo unamchubua.

Kumwandaa???
Hata umwandae masaa 3 kwake hakunaga kuteleza
 

Aaliyyah

JF-Expert Member
Mar 20, 2022
8,615
20,133
Sio kwamba tunapenda kupaka mate, kuna wanawake kei zao kavu kama jangwa.
Ukilazimisha kuingiza bila kulainisha kidogo unamchubua.

Kumwandaa???
Hata umwandae masaa 3 kwake hakunaga kuteleza
Khe masaa matatu
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Top Bottom