Ni hivi,
Taratibu zinaelekeza kuwa, wenye vyeo sawa ndiyo waoane. Yaani, afisa kwa afisa na private kwa private.
Lakini, afisa wa Kiume anaweza kumuoa private wa kike. Lakini afisa wa kike hawezi kuolewa na private wa kiume. Hivyo, muolewaji anapaswa kuwa chini kicheo kuliko muoaji. Endapo kuna ambaye atataka kuolewa nje ya masharti, basi mmoja aache kazi au figisu zihusike.
Lakini, kuolewa na raia ni ruksa na wala hakuna shida. Ijapo, kuna sheria mpya inataka kuanzishwa kuwa Mwanajeshi wa kike haruhusiwi kuolewa na raia. Sijajua kama imeshapita na itaanza kutumika lini.