Tetesi: JayRutty kusitisha mkataba na Simba mwisho wa msimu huu

Ni ngumu sana kwa tajiri kama MO kutishwa na maneno ya kwenye khanga. Hayo maneno ni kwa ajili ya maskini siku iende!
Tatizo nchi hii mmejaa machawa, mtu akiwa na kipato anakupangia hata namna ya kufikiri.
Mo atatoka kisheria. Mashabiki wa Simba wanaoumia wako wengi ikiwemo viongozi waliopo serikalini.
Siku zote mo amekuwa akilalamika kupata hasara mbona haondoki.
 
Taarifa za uhakika ni kwamba boss Mo kaamua kukita mizizi pale msimbazi kiasi kwamba mzabuni wajezi kaona hakuna future nzuri.

Atavunja mkataba kwa gharama zake na yuko tayari kulipa fedha ya fidia kwa Simba ili aondoke.

Genius Mangungu unaupiga mwingi.
Ikiwa hivyo ni sawa tu. Licha ya changamoto za kiuongozi zilizopo Simba, ila Jayrutty ndio anaivuruga Simba kwa kutumia 'chawa' wake.

Napata hisia atakuwa ameside na Mangungu katika kuleta hizi chokochoko.

How come 'chawa' wake walalamike kutopostiwa ishu ya kuchangia sijui 'Ex-factor' kwenye mitandao ya klabu?! wakati hilo ni jambo lililo chini ya kampuni yake?

Alivyoahidi kusajili mchezaji mkubwa kila dirisha, alitegemea kitu gani?
 
Tatizo nchi hii mmejaa machawa, mtu akiwa na kipato anakupangia hata namna ya kufikiri.
Mo atatoka kisheria. Mashabiki wa Simba wanaoumia wako wengi ikiwemo viongozi waliopo serikalini.
Siku zote mo amekuwa akilalamika kupata hasara mbona haondoki.
Umesema kweli. MO atatoka kisheria na sio kwa maneno ya kwenye khanga! Ushanfahamu!!?
 
Kwa dalili zilizopo tunapoelekea hata bila Jayrutty kuhusika Mo asipokuwa makini anakwenda kuondoka kwa aibu kubwa sana na atapoteza mtaji wake wote aliowekeza pale Simba kwa miaka mingi. Zamani wanasimba wote walikuwa hawaoni wala hawasikii likifika suala la Mo. Ukimgusa kidogo tu Mo utashukiwa kama mwewe itabidi utafute pa kutokea. Lakini nilichokiona kwa siku za karibuni ni kama wanasimba ambao wanampinga MO mitandaoni na hata huku mitaani wameamza kuongezeka kwa kasi ya ajabu na hii ni kutokana na matokeo mabovu uwanjani hasa anapokutana na mtani wake.

Wanachama, mashabiki na wapenzi wengi wa Simba wameanza kukata tamaa na MO kutokana na mambo yaliyotokea hivi karibuni ikiwemo suala la Mwalimu kuchukuliwa kibabe na Yanga kwenye kambi ya Simba wakati wanajiandaa na derby. Ile ni "scandal" kubwa sana ni sawa na adui yako aje nyumbani kwako wakati umelala amchukue mkeo uliyetamba kijiweni kuwa umeshamlipia mahari na kumtumia tiketi na wenzako wamemuona akiingia kwako usiku halafu kesho alfajiri anaibukia kwa adui yako. Maana yake mwenzako kalala naye usiku kucha!. Na mbaya zaidi Simba wakaenda kutandikwa kwenye derby kwa hiyo hapo maumivu kwa wanasimba yakawa mara mbili zaidi.

Suala lingine litakalosababishwa Mo kung'olewa ni sajili zisizoeleweka zinazoifanya Simba ishindwe kutamba kwenye ligi ya ndani na hata kimataifa kama zamani. Imefika mahali hata Singida inaweza kusajili wachezaji wenye viwango vikubwa kuliko hata Simba. Na kinachowasikitisha wanasimba wengi ni pale wanapoona mchezaji wa kawaida sana mwenye kiwango kidogo kasajiliwa halafu dau linalotangazwa ni kubwa. Pia kitendo cha wanasimba kufika uwanjani kuangalia mpira halafu hata mechi ndogo tu za kawaida wanashika roho mkononi wakiwa hawana uhakika wa matokeo kinawatesa sana na mara nyingine hata wakiwa wanaoongoza wanatamani mpira uishe haraka waondoke na matokeo chanya.

Kitendo cha kufika mahali wanasimba kuanza kumuoan Jayrutty kama mkombozi wao hii ni dalili mbaya kubwa kwa Mo kuwa mambo yameshaanza kuchemka. Utajiri alionao Jarutty ni mdogo kulinganisha na Mo lakini tabia yake ya kutimiza kila analoliahidi huu ni mwiba mchungu kwa Mo. Kila mwaka Mo anaahidi kuleta kombe la Afrika Tanzani lakini maajabu kila mwaka Simba inazidi kuporomoka kwenye viwango vya CAF kutoka namba tano mpaka sasa imefikia kuwa ya kumi na moja. Na yote hii imesababishwa na sajili mbovu za hivi karibuni.

Mwisho kabisa atakayesababisha zoezi la Mo kuandoka pale Simba litokee haraka ni yule kiongozi ambaye yeye mwenyewe Mo anamwita kuwa mshauri wake wa karibu pale Simba. Huyo jamaa amempeleka chaka sana MO kwa kusajili wachezaji wa ajabu ajabu. Kinachoshangaza ni pale ambapo Mo mweyewe hashtuki kabisa wakati kila msimu ukiisha analipa fidia za kuvunja mikataba na wachezaji wengine wanapelekwa kwa mkopo kwenye vilabu vingine. Halafu mwamba anachukua tena hela anaanza tena kusajili magalasa yake. Ikifika mwisho wa msimu mzunguuko ni ule ule halafu anatamba kabisa kuwa Simba haidaiwi na haipelekwi FIFA kwa madai ya usajili wakati yeye kashatia hasara na MO ndio analipa. Halafu mwamba hataki kabisa watu wenye weledi na utaalamu wa mpira na wanaofahamu fitina na siasa za mpira wa kibongo wapeleke uzoefu wao klabuni na hata kumfikia Mo.

Anyway kwa hali inavyoenda hivi sasa Mo akiendelea kushupaza shingo na kumkumbatia huyo anayemwita mshauri wake wa karibu muda si mrefu watang'oka pamoja pale Simba. Pona pona ya MO ni kumtosa huyo jamaa na kuanza upya kwa kushirikisha makundi yote bila ubaguzi kama alivyofanya mzee Dalali wakati anachukua uongozi.

Ni mtizamo tu.

Ni mtizamo tu
 
Upo sahihi mo akiendelea kung'ang'ania kuwepo peke yake wakati katiba imeshasema mabadiliko yanayotakiwa hizi pesa anazotoa zitakula kwake, pia watu wengi hawamtaki keshapoteza support hata mitandaoni, nimeona Aggy Simba na Tunu Shemkome wakishambuliwa kwenye page zao kisa wamemsifia.
Hata Dalali naye amempinga kitendo cha kusema Simba ina laana kwa kubadilisha logo yake ni wazi hakubaliani na matendo ya mo.
 
Shida kubwa kwa MO ni kumwamini mwamba wakati anampeleka chaka. Na wanasimba wengi sasa hivi wanakereka kuona Yanga inazidi kupaa wakati wao timu yao inazidi kushuka. Na kuna uwezekano mkubwa Yanga kwa kikosi alichonacho sasa hivi akaenda kufyeka kile kichaka kule CAF na hapo kama MO hajashtuka na kufanya marekebisho haraka sana hili nalo linakwenda kumuathiri pale Simba

Na kibaya zaidi katiba mpya imemkalia vibaya sana Mo. Wapinzani wake wanataka kupitia huko huko kwenye katiba mpya wamchomoe na yeye bado hajasanuka kwa sababu mwamba kampumbaza. Kilichokuwa kinambeba ni timu kufanya vizuri walau kimataifa. Sasa hivi kutokana na sajili mbovu hata huko kimataifa huenda Simba ikafanya vibaya na hapo ndio itakuwa majanga kwake.
 
Back
Top Bottom