Jay Moe, rudi kwenye gemu!

fareed simwelewagi vizuri, ila jmo a.k.a mchopanga anasomeka vya kutosha.!!


simu yangu ni soo
Kuishika mtu sikubali,
Hata niwe na Demu wangu simu yangu ntaiweka mbali.
Na sichelewi kuizima nkaiwasha nikiachana nae, najua ikiwa hewani nitagombana nae

Simu yangu inakuwa Daftari la kuhifadhia mistari, una create Folder kama msg za Siri, wapendao kubip hapa mtaliwa Dola pembeni natumia Beeper chunga ntakutia hasara, sinunui Simu Dukani simu zangu zote mazabe, yenye Ndogo thamani ili machizi wasiibe
Wameiba 6210 Sasa niko na blue 1, wamentoa Finland sasa niko Japan...

Juma Juma Juma ama kwa hakika wewe ni mbarikiwa Alhaj
 
hapa akiwepo Jay Moe pembeni akakaa super producer Majani, basi ngoma inayotokea hapo ni noma kweli..
The man knows to write and to flow but I wonder why hanaga bahati. Nimemiss team ya wanamziki wa kweli wa zamani
 
Kama unaubongo mdogo lazima umdis Fid Q huku J.moe mwenyewe anamkubali Fid. Ni jambo la kumshukuru Mungu Fid na J.moe wako Bongo hawa jamaa wanajua
 
More technic, mteule , mbakiaji ninamkubali sana pia,na huyu dogo mwingine huyu wa elimu mtaani .com
 
nimeanza na nyumba sina mpango na corola
makonda mi wana hivyo nasafiri kisela

hii kitu yupo na mims never be me!!
 
Hawa waache wapotee na wataendelea kupotea sana tu, na wasiojuwa lolote kwenye muziki wataendelea kupiga Bingo ndefu kwa awamu, mtu anaimba tu Mama kidoti mamaa, mama sepetu mamaa, Mama Duaimond Mamaa, ushuzi mtupu na ndio wanaoingiza pesa.

Sugu aliwaonesha mapema namna ya kupambana na mfumo kandamizi na akandaa Hip Hop Summit akawaleta na jamaa zake kutoka USA lakini ilikuwa ni kazi bure. sintokaa niwaurumie watu wasiokuwa na umoja hata chembe, wanapitwa hata na Bongo Movie wenye vyama vyao vya kisanii sanii?
 
Juma mchopanga level ingine.... Huwa nikisikiliza Unforgetable aliyoshirikishwy na Nako 2 Nako inanifanya nizidi kumpigia salute jamaa..... Siku hizi kila nyimbo ni mapenzi, Mipasho, Na sifa za kipuuzi. Jay mo kwangu anabaki kati ya walio bora kabisa.......
 
Jamaa mkal sana.... Nasikia yupo kwa majani anatengenesha ngoma mpya.....
Naamini itabamba kama zilizopita..... sijawahi kuchoka kumsikiliza jay mo....
 
yupo uholanzi

Acha stori za ghahawa,juzi tu alikuwa na show Tegeta pamoja na Mansu Li.

ENEWEI
Huyu ndo MC nnayemkubali zaidi TZ.Ile Albam yake ya kwanza ya ULIMWENGU NDO MAMA ilikuwa balaa,jamaa ana uwezo mkubwa wa kuandika,kuflow na ana idea za kipekee e.g Bishoo,kama unataka dem,story3,mvua na jua,Maisha ya Boarding,kimyakimya,etc.
Me huwa nashangaa jinsi watu wanavyomsifia FID eti ndo no1 mc in TZ.Yaan wabongo bwana,m2 akitunga nahau na misemo ndo wanamuona mkal
 
..Watanzania bana, eti mnasema Jay Mo hana bahati wakati hamjawahi hata kununua kazi zake!!!, mtu hajawahi kununua CD yake, hajawahi kulipa kwenda shows zake, anaishia kusema oooh Jay Mo hana bahati. Tatizo sio bahati tatizo ni sisi waTZ.
Hebu tujiulize kwanini wasanii wa Uganda wanafanya vizuri!!!!?
Bado naendelea kuunga mkono zile harakati za Mh Sugu na Vinega, Anti-Virus ila siasa ndo iliiua hizo harakati, tumerudi kule kule, industry ya muziki hapa Bongo imeshikwa na kikundi cha watu wachache tena matajiri, wao ndio wenye hakimiliki ya nani atoke na kwa wakati gani, tuachane na Story eti Jay Mo hana bahati.
 
Juma mchopanga a.k.a mbakiaji. Mkimuona mwambieni arudi kwenye game watu tumemic mistari. Toka am so famous na producer bora kuliko wote africa mashariki, p funk, hatujamsikia.
Mkimuona mwambie arudi, kwani eti ney wa mitego naye anaimba hip hop. Chid benz naye anatamba!
Hadi zola d eti naye anaimba! Moe rudi mjomba. Masikio ya hiphop yana njaaa
Daaaaaaaah nimemis sana mistari ya Moe mshkaji ni mkali:lying:
 
Hawa waache wapotee na wataendelea kupotea sana tu, na wasiojuwa lolote kwenye muziki wataendelea kupiga Bingo ndefu kwa awamu, mtu anaimba tu Mama kidoti mamaa, mama sepetu mamaa, Mama Duaimond Mamaa, ushuzi mtupu na ndio wanaoingiza pesa.

Sugu aliwaonesha mapema namna ya kupambana na mfumo kandamizi na akandaa Hip Hop Summit akawaleta na jamaa zake kutoka USA lakini ilikuwa ni kazi bure. sintokaa niwaurumie watu wasiokuwa na umoja hata chembe, wanapitwa hata na Bongo Movie wenye vyama vyao vya kisanii sanii?

Umesema vyema mkuu,Wasanii wa hiphop ndio wepesi kurubuni kuliko hata bongo fleva!!
Mabingwa wa kulalama pembeni akijtokeza mtu mbele ili wapigane pamoja wanarubuniwa show mbili za fiesta wanatosa wenzao!!
Wajiulize wanatofauti gani kimaisha na maskini jeuri kama Mapacha a.k.a maunjanja supplier?
Badala ya kusimama kupigania sera bora za sanaa na haki zao kwenye vyombo vya habari vyote wanamuachia Ruge awaamulie!!
Ndio maana daima namuheshimu Sugu kwa misimamo yake toka e
 
Juma mchopanga a.k.a mbakiaji. Mkimuona mwambieni arudi kwenye game watu tumemic mistari. Toka am so famous na producer bora kuliko wote africa mashariki, p funk, hatujamsikia.
Mkimuona mwambie arudi, kwani eti ney wa mitego naye anaimba hip hop. Chid benz naye anatamba!
Hadi zola d eti naye anaimba! Moe rudi mjomba. Masikio ya hiphop yana njaaa

Mi naamini wasanii wetu wangekuwaa na mshikamano, umoja na upendo isiingekuwa shida kwa wasanii wakogwe kusikika, the only thing ninachokiona ni kuwapo kwa gap kubwa mno kati ya wasanii walio kwenye chart sasa na wale waliovuma zamani mfano Jaymo!

Lkn hili gap linatokaana na wasani walovuma zamani kutokukubali kazi za wasanii wanaovuma sasa, naamini kuwa Jaymoe akishirkiana na msanii anayeimba (sio kuchana) kama ommy dimpoz, Diamond, Ben Paul, vanessa Mdee, walter hata master bro na wengine wa aina hy wote wanaweza kuwa tite kwenye game na wakafanikiwa kwa maana ya kuuza sana muziki huo wa corabo, the only thing mdudu anaewamaliza baadhi ya wasanii wetu ni ubinafsi!

Binafsi napennda sana muziki na nam-feel sana Jaymo hasa akifanya featuring na mwanamuziki anayeimba R&B gerne!
Naamini kama kuna wakati wasanii wataacha roho ya ubinafsi na kuwa na uwezo wa kupembua mambo wataweza shirikiana na hatimaye wote ufanikiwa!

Kwa kuanza Binamu yangu (mwanaFA) fanya feat na Vanessa Mdee, aisee i wish nisikie hiyo track coz itabamba sana, is like naisikia sasa masikioni wangu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom