Jay Moe atamba kusoma na Rais wa DRC Joseph Kabila

Kwahiyo hayo maisha ya kishua aliyokuwa akiishi ndio alikuwa hatembei kabisa maana jiji hili hasa miaka hiyo kurudi nyuma nyumba za udongo zilikuwa sio za kutafuta sana kuanzia msasani,mwananyamala,magomeni,ilala,ubungo,manzese na maeneo kibao zilikuwa nyingi tu
Ukienda kariakoo mtaa Tandamti bado zipo nyumba za udongo
 
Msanii wa Bongo Fleva, Jay Moe ameeleza changamoto alizokumbana nazo shule hadi kupelekea kutoa albamu ya Ulimwengu Ndio Mama, licha ya hiyo kuna vitu ambavyo anajivunia ikiwemo kusoma shule moja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Joseph Kabila.

Rapper huyo amesema kutokana na kukulia katika maisha ya kishua hadi unafika wakati ambao anaenda boarding school alikuwa hajui kama kuna nyumba za udongo nchini zaidi ya kuziona kwenye movie za Vietnam.

Ameeleza kuwa wakati anaenda Mbeya kuanza form one mwaka 1993 ndipo alianza kuona nyumba za udongo kitu kilichomfanya kuanza kulia lakini baba yake na ndugu zake walipomueleza kuwa amekua hivyo hana budi kuachana na mambo ya kitoto na kupambana.

“Siku ya kwanza nilipofika Irambo (secondary) jamaa wameniibia begi la mamisosi, kwa hiyo kule ndipo nilipojifunza maisha kiasi kwamba nilipofika form three mzee wangu alitaka anihamishie Dar es Salaam lakini nikamwambi hapana mimi nabaki, nimeshazoea ingawa maisha ni magumu,” Jay Moe amekiambia kipindi cha The Play List cha Times FM.

“Kingine kinacho-inspire image mimi nimesoma na Joseph Kabila ambaye ni Rais wa Congo, nimesoma na Cesi, nimesoma na Clara ambao wote ni watoto wa mzee Kabila. Mimi nikiwa form two Jose ndio anamaliza form six na alikuwa kaka mkuu wa shule, kwa hiyo nilijifunza kama huna mama basi, kuna ulimwengu ambao utakufunza kama mama,” amesema Jay Moe.

By Peter Akaro
Huyu chinga ina maana Tangu azaliwe mpk anaanza form 1 hakuwahi kwenda kwa bibi na babu huko kwao lindi?

wamakonde wenzangu wanazidi kuniabisha asee,juzi harmonize kasema haipendi ngozi nueusi na hataki watoto wake wawe weusi,leo Mchopanga nae anasema hakuwahi kujua kama kuna Nyumba za udongo,wakatikwa miaka ya 90 kurudi nyuma msasani na mikocheni pale chama ile mitaa ya kina babuu wa kitaa nyumba za udongo zilikua kibao.
 
brazameni kidole huyo amesema amezaliwa sinza ss late90s nyumba za udongo sinza dar nzima c kibao t!
 
Kwahiyo hayo maisha ya kishua aliyokuwa akiishi ndio alikuwa hatembei kabisa maana jiji hili hasa miaka hiyo kurudi nyuma nyumba za udongo zilikuwa sio za kutafuta sana kuanzia msasani,mwananyamala,magomeni,ilala,ubungo,manzese na maeneo kibao zilikuwa nyingi tu
NDIO UJUE WATU WENGINE HAWAJUI KUDANGANYA. YAANI DAR MOAKA BAGAMOYO KIGAMBONI KUNA NYUMBA KIBAO ZA MBAVU ZA MBWA. HALAFU YEYE ASEME AMEZIONA AKIWA ANENDA MBEYA
 
Ni kweli hata mie kabila nilimkuta Irambo kuna Arthur mwambene Javan bway shehiza wote walisoma pale
 
Huyo dada yake kabila(Cesi) anaishi na mshkaji mmoja beach boy,,, wanapiga hela za madini ya Congo ni nouma ,,,,,,jamaa alikuwa choka mbaya,,ila nowadays yupo njema
 
Back
Top Bottom